Financial Intelligence
Senior Member
- Sep 29, 2023
- 112
- 248
Kwamara nyingine Matokeo yakionesha benki hii imevunja rekodi kwa mwaka mwingine tena baada ya kupata mafanikio ya kihistoria.
NMB Tanzania imefanikiwa kuongeza Jumla ya mapato ya Benki na kufikia Shilingi Trilioni 1.4 ikiwa ni ongezeko 18% ukilinganisha na FY2021|22
Jambo bora zaidi ni uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato uliboreshwa zaidi hadi kufikia 39% hii ni sawa na kusema wanakusanya zaidi na wanatumia kiduchu.
Wakati huohuo uwiano wa mikopo chechefu umeshuka hadi kufikia 3.2.% Takwimu hizi zote ni chini ya ukomo wa kikanuni wa Benki Kuu wa 55% na 5% mtawalia.
Kutokana na ufanisi huu, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kwa 26% hadi TZS 775BL huku Faida baada ya Kodi ikifikia TZS 542BL ikiwa ni ongezeko la 26%. kwa mwaka.
Mizania ya Benki imeendelea kukua na kufikia jumla ya mali ya Shilingi Trilioni 12.2 ikiwa ni ukuaji wa asilimia 19 kwa mwaka.
Tuliendeleza ajenda ya ujumuishaji wa kifedha kwa kufungua akaunti mpya za wateja zaidi ya milioni 1.2, na kufanya jumla ya akaunti za wateja wetu kufikia zaidi ya akaunti milioni 7.1. Hii ni idadi kubwa zaidi ya wateja kwa taasisi moja ya fedha nchini.
NMB iliwekeza zaidi ya TZS 6BL kwenye elimu, afya na mazingira, ikiwa sehemu ya dhamira yetu ya kujitolea kusaidia jamii inayotuzunguka.
Akiwasilisha Taarifa ya Fedha ya Mwaka 2023, Afisa mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ms Ruth Zaipuna amewashukuru wateja wote, wanahisa, wafanyakazi pamoja washirika wote wa Benki,
Zaidi sana ameishikuru Serikali kupitia Benki Kuu na Watanzania wote kwa mchango wao thabiti na imani waliyonayo kwa Benki ya NMB Tanzania.
Mtakumbuka katika mwaka wa 2023 jumla ya faida kwa mabenki yóte ilifikia shilingi Trilioni moja hivyo faida hii ya NMB inakuwa ni sawa na 78% ya faida yote katika robo ya tatu ya Mwaka uliokwisha.
Ningumu kuzungumzia mafanikio haya bila kumzingimzia Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NMB PLC Ms Ruth Zaipuna na Bodi nzima ya Benki hiyo chini ya Dkt Edwin Mhede.