Financial Manager wa Unilever auawa na majambazi

Mkimbizi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
222
34
Habari zilizotufikia punde zinasema kuwa Financial manager wa Unilever Company MR.LUGANO ELIA ameuawa na majambazi usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake kimara.

Habari zaidi zinasema kuwa majambazi yalimfuatilia alipokuwa anatoka ofisini saa tano usiku na kumlazimisha awape pesa na simu yake yenye thamani ya zaidi ya millioni 1.
Mungu ailaze roho yake mahali pepa peponi..
 
Dah! haya majambazi bado yanatamba tu!? au ni visasi ivyo....may the almighty god Rest his soul in Peace...pole sana kwa wafiwa
 
Kwa kweli itakuwa kuna kitu kafanya kwa mtu na analipa kisasi. Wamuue kwa pesa na simu tu!! si kweli...
 
Kikwete na Saidi Mwema wako zuia basi mauaji haya ya raia, manake ya uchumi na mengine yamekushinda. Ujeshi jeshi si ndio zako Kanali, na ulikuwa ofisa wa usalama and all, fanya kweli basi hapa, tunamwagishwa damu watu wako Mheshimwa, come on man! Painful times.
 
Hawa majambazi kwakweli yanatikisa sana Mbezi pamoja na Kimara na maeneo mengine pia, inawezekana sio kisasi labda alibishana nao maana wale ukiwabishia basi ni kukulipua. Inasikitisha sana, Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen.
 
Unajua POLICE wanalala sana maeneo ya Kimara home haipiti wiki majambazi yanatanua tu na kuchukua pesa zao sasa hivi tumesha zoea yaani haipiti wiki mtu kapigwa risasi mtu kajeruhiwa mara tumelazwa chini yaani tabu tupu........polisi amkeni mnakula dili nini???
 
Hebu tupe data zaidi, ukiangalia issue hii inafanana na ya mtangazaji mmoja wa zamani sikumbuki jina lake aliuwawa on the same grounds
 
Nawapa pole wafiwa
Kianachonisikisha zaidi ni huu utambaji wa viongozi wa Polisi hasa wanaokuja Mkoa wa Dar es Salaam, utadhani wao ndio muarobaini wa jinai zote jijini. Huyu wa sasa anatamba mpaka leo kuwa majambazi, vibaka na wapiga debe wakae mkao wa kula. leo ni siku mia moja tangu afike lakini majambazi wapo, vibaka kibao na wapiga debe wamejazana vituoni. Polisi wenye pikipiki wapo lakini kazi ni kufukuzia maroli yaliyopakia mizigo barabarani.
 
Unajua POLICE wanalala sana maeneo ya Kimara home haipiti wiki majambazi yanatanua tu na kuchukua pesa zao sasa hivi tumesha zoea yaani haipiti wiki mtu kapigwa risasi mtu kajeruhiwa mara tumelazwa chini yaani tabu tupu........polisi amkeni mnakula dili nini???

Wataachaje kulala ikiwa Kamanda wao anashabikia siasa MARA ana acha kufanya kazi yake ipasavyo.
 
Nawapa pole wana familia na wote walioguswa na msiba huo.
Mweyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema.AMINA
 
Bongo inatisha! Mungu ailaze pema roho ya marehemu na awape faraja familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu katika kipindi hiki kigumu kwao.
 
Jamani inatisha sana.MUngu ailaze roho yake mahali pema.SASA umefikati wa wa jeshi kulinda usalama maana wanakaa tu hawana kazi wanakula mshahara bure tu,hakuna vita tz .tunawaomba watusaidie kwa kulinda wananchi jamani,nchi kama ethiopia ukipita barabarani ni wajeshi kila mahali na hao viongozi wanaona sijui wanataka mpaka waombwe mana wakija hapa addis wanaona walivyojaa njian na sio tu wakati wa viongozi hawa jamaa ni full time security.Nhata mwema alikuwepo hapa wiki iliyopita kaona sasa sijui kwa nini wanashindwa kushauriana na wenzao wa jeshi
 
Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi na kuwafariji aliowaacha.

JK asipoangalia nchi, Dar au nchi nzima inaweza kuwa sawa na Johannesburg. Kama tumefikia kuua kwa sababu ya pesa chache za kwenye waleti na celifoni, basi tunakoelekea ni pabaya sana.
 
Back
Top Bottom