Financial Manager wa Unilever auawa na majambazi

Toa pole kwanza, ndio uulize. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali panapostahili. Amen

Inavyoelekea wewe huenda msibani badala ya kulia kivyako unaangalia watu gani hawalii. Mimi nimechanganyikiwa hadi nikasahau kutoa pole kwa mjane na watoto, ndugu na marafiki wa marehemu. Mwenyezi Mungu aipokee roho ya marehemu pema peponi, Amen.
 
Unilever ni Kampuni gani hiyo?

Ni ile inayotengeneza Blue Band, Omo, Geisha n.k. Iko Pugu Road karibu na Mantrac na Kiwanda cha gesi (TOL) Unamkumbuka yule mama wa Kiingereza alikuwa ananakuja sana hapa Tanzania wakati wa Mkapa, alikuwa waziri wa Uingereza wakati wa Tonny Blair. (Nadhani ni Lynder Cholker lakini sina uhakika na jina). Ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hii iliyo na makao makuu Uingereza na matawi mengi third world (Malawi, Kenya, Tanzania n.k)
http://en.wikipedia.org/wiki/Lynda_Chalker
 
Nawapa pole wafiwa
Kianachonisikisha zaidi ni huu utambaji wa viongozi wa Polisi hasa wanaokuja Mkoa wa Dar es Salaam, utadhani wao ndio muarobaini wa jinai zote jijini. Huyu wa sasa anatamba mpaka leo kuwa majambazi, vibaka na wapiga debe wakae mkao wa kula. leo ni siku mia moja tangu afike lakini majambazi wapo, vibaka kibao na wapiga debe wamejazana vituoni. Polisi wenye pikipiki wapo lakini kazi ni kufukuzia maroli yaliyopakia mizigo barabarani.

Wameshindwa. Kero zikizidi, wanayo mbinu moja wanayoipenda sana, nayo ni kutangaza vita dhidi ya ujambazi. This technique is very effective kupunguza joto ya jiwe.... kwa muda.

.
 
pole kwa ndugu na jamaa. mola aiweke mahali pema peponi
roho ya marehemu.
 
Ndo maana mi Bongo nshaamua ntakuja kutembea tu lakini siwezi rudi kuishi, yani watu wanakuwa victims of their own success, haka ka gari kangu ninakoendesha huku mamtoni ndio kanaweza kakawa msiba wangu huko, hiki ki selula changu kitakuwa ndio chanzo cha mauti yangu, nikiwa na drive kurudi home litakuja jitu na mgari wake lina leseni ya kununua halafu limelewa bwii na kuniparamia, nikienda hospital hata kama nina hela zangu naambiwa dawa hakuna na kama zipo kuna uwezekanio zikawa fake! no! no! no! sirudi ng'oooooo!
Pole sana wafiwa, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
 
Haya Kova shughuli hiyo umenijibodoa sana kuwa ujambazi na uhalifu umepungua ndani ya siku 100 toka ulipoingia ofisini. Jamaa wana beep hao kwenye ile namba uliyotoa je utapiga?
 
Profession ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu imepoteza mmoja kati ya wawakilishi wake mahiri. Rest in peace mhasibu! poleni wafiwa wote!
 
Raha ya Milele umpe Ndugu Lugano Elia Ee Mungu; na Mwanga wa Milele umuangazie. Apumzike kwa Amani. Amen.
 
Ndo maana mi Bongo nshaamua ntakuja kutembea tu lakini siwezi rudi kuishi, yani watu wanakuwa victims of their own success, haka ka gari kangu ninakoendesha huku mamtoni ndio kanaweza kakawa msiba wangu huko, hiki ki selula changu kitakuwa ndio chanzo cha mauti yangu, nikiwa na drive kurudi home litakuja jitu na mgari wake lina leseni ya kununua halafu limelewa bwii na kuniparamia, nikienda hospital hata kama nina hela zangu naambiwa dawa hakuna na kama zipo kuna uwezekanio zikawa fake! no! no! no! sirudi ng'oooooo!
Pole sana wafiwa, Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Mkuu! Huko majuu hawauawi watu kwa ajili ya simu tu? Mbona nasikia ukimwangalia mtu vibaya tu (ukim'dis') wanakuondoa! Mbona nasikia wakitamani raba zako tu, umeondoka! Au jaketi! Au hawaipendi tu sura yako! Si kwetu tu, sehemu nyingi kuko hivyo.

Tatizo kwetu wakuu wameona kero ni changudoa na machinga! Majambazi wameachiwa sungusungu!

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Na awafariji na kuwapa nguvu wafiwa.
 
Roho ya marehemu ipumzike mahala pema peponi.Poleni wafiwa wote.Mungu awe faraja yenu na nguzo yenu.
 
Bongo longolongo nyingi, polisi wanajisifu badala ya kusifiwa na wananchi wanaowatumikia!.

Nimeambiwa hao majambazi walitumia pistol kutoa roho ya Ndg Lugano, na hawakuchukua chochote!

Inawezekana ni chuki binafsi, au kweli walikuwa na nia ya kuiba ila hawakufanikiwa, maana naambiwa wamempiga risasi mbele za watu wengi! Kazi kwenu Polisi, tunataka muwakamate hao wauwaji hatutaki yaani yaani!

Mungu amrehemu Lugano na awape subira ndugu na jamaa wote waliokuwa karibu siku za uhai wake! Amen
 
BUBU MSEMAOVYO
Unilever ni producers wa households and consumer utilities the like of OMO NA VITU KAMA HIVYO.Ni kampuni kubwa sana kuanzia Marekani na duniani kote.INAUZA SHARE ZAKE NEW YORK STOCK EXCHANGE MARKET.
 
Nawapa pole wafiwa
Kianachonisikisha zaidi ni huu utambaji wa viongozi wa Polisi hasa wanaokuja Mkoa wa Dar es Salaam, utadhani wao ndio muarobaini wa jinai zote jijini. Huyu wa sasa anatamba mpaka leo kuwa majambazi, vibaka na wapiga debe wakae mkao wa kula. leo ni siku mia moja tangu afike lakini majambazi wapo, vibaka kibao na wapiga debe wamejazana vituoni. Polisi wenye pikipiki wapo lakini kazi ni kufukuzia maroli yaliyopakia mizigo barabarani.

Mkuu Congo,
Ninakubaliana na mawazo yako kwa upande mmoja, lakini vilevile hali ikifikia hapa, inabidi tujiulize na sisi kama wanajamii tunamchango gani katika kuhakikisha tunapambana kwa nia ya kupunguza uhalifu katika maeneo yetu tunayoishi?
Iko haja ya jamii kuangalia ni maeneo gani wao wanaweza wakashirikia kwa ajili ya kujiletea maendeleo yao na kupunguza kero zinazowakabili.
Mimi hapa ninapoishi, pamoja na mambo mengine, wakazi wa eneo hili wanajihusisha vilivyo katika masuala ya kijamii kuanzia shule, maji, usalama nk. Hali hii inafanya eneo hili kufanya kazi kwa ukaribu, urahisi na ufanisi mzuri na taasisi zinazohusika na maeneo ambayo wao wanayasimamia pia.
Kwa mfano kuna mkazi ambaye kama kuna tatizo katika uzoaji takataka, basi wakazi huweza kumtaarifu na yeye hufuatilia na kujua kulikoni.
Kwahiyo wakati ambapo tunapiga kupiga kelele za kushambuliwa na majambazi, si vibaya tukatafakari zaidi na zaidi!
 
Mmimi naona hata kama kuna sababu gani ama za mapenzi kudhulumiana hakuna haja ya jf kusupport mauaji kama haya!!!!kamwe forum haita kubali unyama huu na vyombo vya sheria vikamate mkondo wake
 
Bongo longolongo nyingi, polisi wanajisifu badala ya kusifiwa na wananchi wanaowatumikia!.

Nimeambiwa hao majambazi walitumia pistol kutoa roho ya Ndg Lugano, na hawakuchukua chochote!

Inawezekana ni chuki binafsi, au kweli walikuwa na nia ya kuiba ila hawakufanikiwa, maana naambiwa wamempiga risasi mbele za watu wengi! Kazi kwenu Polisi, tunataka muwakamate hao wauwaji hatutaki yaani yaani!

Mungu amrehemu Lugano na awape subira ndugu na jamaa wote waliokuwa karibu siku za uhai wake! Amen

Nilichosikia kinafanana na ulichoeleza. Inadaiwa alivamiwa nje ya geti la kuingia kwake na kwamba walitoweka bila kuchukua chochote. Kuhusu vitu vilivyoibwa, inawezekana ni vibaka waliofika eneo la tukio muda mfupi baadae.

.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom