FikraPevu: Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

Nasikitika hata kabla ya ripoti ya mtaalam wa mabomu haijajoka tayari vyombo vya habari vimekuwa vikiandika kwamba marehemu alilipuliwa na bomu la machozi.

Ikumbukwe mtutu uliyotumiwa kwenye tukio lile huweza kutumiwa kufyatulia mabomu ya aina tofauti ili mradi iwe ni bomu lenye kipenyo cha 40mm

Kuna bomu lingine la 40mm ambalo ni la kivita Low Velocity High Explosive Airburst Grenade.

Bomu hilo lina linafyatuliwa mithili ya risasi kwenye kitako cha gamba lake lina primer kama ile ya risasi. Baada ya kufyatuliwa kichwa cha hilo bomu ambacho ndiyo chenye madhara makubwa hulipuka kinapogongana na target

Kwa maneno mengine kama target ni laini mfano kwenye theluji(snow) linaweza lisilipuke mpaka litakapokanyagwa

Kuna uvumi kwamba marehemu alifyatuliwa bomu kisha likawa mwilini na kulipuka pale alipojikunja

KIWANGO CHA USAMBARATISHWAJI WA MWILI WA MAREHEMU KINANIFANYA NITAFUTE UWEZEKANO WA KUKATA RUFAA KAMA MATOKEO YA UCHUNGUZI YATASEMA LILIKUWA NI BOMU LA MACHOZI

Haki itakuwa haijatendeka kama hatutaelezwa ni mtaalam yupi aliyechunguza hilo bomu na kwa vigezo vipi amefikia kuhitimisha kwamba lilikuwa bomu la machozi

Wasiwasi wangu ni kwamba IGP Mwema ataendelea kupeta pamoja na Kamuhanda kuendelea kuua. Bomu la machozi hapo litashift blame kwa mtunguaji. Na itachukuliwa kama manslaughter tu

Kuna huyu JF member mwingine ana mtizamo kama wangu na anaonekana hata kumfahamu kwa undani mmoja wa watuhumiwa. Ni jitihada za huyu jamaa kumsafisha mtuhumiwa hapa JF zimenitia shaka. Jisomee mwenyewe hapa;
...good observation Mkuu, it makes sense, ukizingatia ni Wa-pot wa marehemu...

...Kimsingi nadhani mauaji yamefanywa na yule kijana mwembamba aliyeelekeza bunduki ya kulipulia mabomu ya machozi akiwa takribani mita 0.5 kutoka kwenye tumbo la marehemu, ifahamike kuwa bomu la machozi linapaswa kupigwa kwenye umbali wa takriban mita 100 ili lisiwe na madhara na shurti lisielekezwe direct kwenye mwili wa binadamu...

...Kosa la huyo dogo,kama hakutumwa basi ni kichwa cha bangi, alilenga mwili na alikuwa karibu mno kinyume na utaratibu wa matumizi ya mabomu haya, na mbaya zaidi nadhani badala ya kutumia bomu la machozi lenye kizibo cha njano yeye alitumia bomu la mlipuko ambalo lina kizibo chekundu japo yote yana rangi ya jungle green,kosa kubwa...

...Bomu la mlipuko likipigwa na kugonga kitu kigumu(kama uti wa mgongo kwenye kesi hii) linalipuka na kutoa kishindo kizito, naamini ndicho kilichotokea na kuusambaratisha mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi...

N.B poti kwa lugha ya kijeshi hapa Tanzania ni "homeboy" inaonekana mwenzetu anamjua mtuhumiwa mwenye bastola na nguo za kiraia, kwamba ni mnyakyusa kama marehemu Mwangosi
 
..na mbaya zaidi nadhani badala ya kutumia bomu la machozi lenye kizibo cha njano yeye alitumia bomu la mlipuko ambalo lina kizibo chekundu japo yote yana rangi ya jungle green,kosa kubwa...

...Bomu la mlipuko likipigwa na kugonga kitu kigumu(kama uti wa mgongo kwenye kesi hii) linalipuka na kutoa kishindo kizito, naamini ndicho kilichotokea na kuusambaratisha mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi...

Huo mtizamo hapo, dah!
 
Asante kwa uchambuzi na ufafanuzi murua, tusubiri hiyo ripoti ya tume iliyoundwa japokuwa dunia na watanzania tayari walishauona ukweli kwa macho yao ya nyama.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza kama askari aliyemfyatua Mwangosi (RIP) alikuwa na akili timamu au alikuwa ametumia sigara kubwa. Ninashangaa kwa askari ambaye amehudhuria mafunzo kuamua kukoki silaha yake na kumuelekezea mtu ambaye hana hatia. Mi nakumbuka tukiwa JKT tulifundishwa kuwa kumuelekezea mwenzio silaha hata kama haina risasi ni kosa na adhabu yake ni kali. Silaha muelekezee adui ambaye naye anakuattack. Na ninafikiri kwa polisi sheria ni kali zaidi maana wao kazi yao kubwa ni kukamata na sii kuua hata kama ni adui.

Sasa najiuliza huyu askari aliona Mwangosi tayari yuko chini ya ulinzi. Kilichomfanya amuelekezee silaha nini nini? Kama alikuwa anamtisha, kilichomfanya aikoki ni nini? Hizi si Bangi?

Hata kamanda aliyeamuru askari wafanye fujo naye anastahili apimwe.

Hivi huko polisi huwa hawa askari hawawapimwi kama wanatumia madawa ya kulevya? Kama hawapimwi, ni kutokujua kuwa kuna wanaovuta au ni kudharau. Au je, huwa wanavutishwa kwanza?

Ni vyema sasa askari wote wakaanza kupimwa kama wanavuta la sivyo wataanza kutufanyia vitendo vya kutukata viungo kama walivyofanya askari wa Sankoy au wanavyofanya wa Kony baada ya kuvutishwa bangi.
 
Mkuu yule siyo Askari ni wale vijana wa CCM ambao wapo kwenye zile kambi zao.......maswali yao yanatosha kuprof weledi wa huyo askari wa kichina
 
Back
Top Bottom