FikraPevu: Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
POLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu limefahamishwa.

Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.

Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.

Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.
Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.

Source: Fikra Pevu | Kisima cha busara!
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.
 
Hapo ndiyo litakapozimwa jambo hili la kuuzunisha. Wakati watawala (Serikali na viongozi wa CCM) wakiwatupia lawama mojakwamoja vyama vya upinzani, pasi tusitegemee jipya hapo.
 
asishtakiwe kwa mauaji pekee bali ashtakiwe kwa kumjeruhi askari mwenzake maana hilo nalo ni kosa..ila mahakama zetu najua ataachiwa huru tu for lack of evidence
 
Kama kweli serikali inataka kutenda haki katika hili Polisi wote waliohusika katika kumpiga mwandishi wahusishwe katika kesi hiyo pamoja na wote waliotoa maagizo ya kufanya hivyo. na ni vizuri Picha na majina yao yakawekwa hadharani tuwatambue.
 
Usanii mtupu,WATAKUWA WAMEMKODISHA ASKARI TOKA KIVU DRC aje kula mema magereza kuliko kusota chaka kule nothern kivu kama walivyomkodi kushtakiwa yule MUNGIKI WA ULIMBO,hapa RPC IRINGA,IGP NA NCHIMBI wastep aside..ful stop.serikali Dhaifu hii inatufanya mabwege.
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.
Mmesahau ya Imran Kombe!
 
Nani mwenye ubavu wa kutoa hukumu ya mtu aliyeamriwa kutawanya mkusanyiko wa watu waliokusanyika kwa amani katika tawi la chama chao?

Je nikweli hukumu itakuwa free and fair?

Kama Nchimbi hashangai kuuliwa kwa mwadishi kwa bomu bali anaona msg ya Slaa ni tatizo je huoni hilo ni tatizo?

Kukamatwa kwake ni kwania ya kutuliza hasira za wanahabari au lengo lao ni kuonyesha uwajibikaji wa dharura wa jeshi la polisi?

Tutarajie nini?the new movie on market!Buy your copy now.
 
Sasa hizo tuhuma za haraka haraka za akina Nchimbi, Nape, Tendwa, na wengineo dhidi ya Chadema zinatoka wapi? Hizo tume walizojiundia haraka haraka wakati kila kitu kiko wazi walitaka kuficha nini au kwa malengo gani?

Muuaji hakuwa peke yake bali syndicate fulani na wote tulishuhudia idadi ya wale askari (more than six) kila mmoja akirusha ama kirungu, teke, au mkono wake kumpiga mwandishi - hawa wote kwa namna moja au nyingine walichangia kifo cha Mwangosi hivyo wote wakamatwe na kushtakiwa kwa kosa la mauaji otherwise huu ni mkakati wa kujaribu kuficha kombe mwanaharamu (CCM) apite.

Ilitokea kwa kudra za Mwenyezi Mungu kwenye tukio pakawa na "manabii" walifanikiwa kupata picha; je, hawa wasingekuwepo ingekuwaje - tusingeishia kwenye hadithi za "KITU KIZITO"?

Ni wananchi wangapi wanauwawa katika mazingira tatanishi kama haya lakini kelele za watanzania zimebakia kuwa "kilio cha samaki"?

Jemedari Mkuu, Mh. Rais wetu stuka, kuna kitu kisicho cha kawaida kinaendelea katika himaya yako baba. Hali si shwari.
 
wanajaribu kuwafumba macho watanzania...wanataka watu wahame kutoka kwenye kutafuta ukweli kwa kina wahamie kwenye mvutano wa kesi ya huyo mtu mahakamani huku wakijipanaga kuzima moto...
 
Sasa kama askari aliyetekeleza mauaji anafahamika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani, huo msururu wa tume za uchunguzi wa kazi gani? Hata hivyo natarajia kuona washitakiwa katika kesi hii ya mauaji ni pamoja na RPC wa Iringa.
Au tume zinalazimika kuwa nyingi ili kufanya cover up ya wahusika wakuu waliotoa amri ya kuzuia mikutano ya Chadema na kuua raia asiyekuwa na hatia.

Mkuu wangu, kama hujapata picha ni kwamba, Tume hyo inakazi maalumu kuonyesha uhusika wa CDM katika "mauaji" hayo, ili itoe mapendekezo yake na hatimaye ndoto za Tendwa na wanaomtuma zitekelezwe na baadae waje kutunga hyo sheria ya kubana shughuli za siasa katika mda usio wa uchaguzi....
Kazi za shetani hufanyakazi kwa uwazi sana huku wao wakidhani ni siri mno.
 
Sasa hizo tuhuma za haraka haraka za akina Nchimbi, Nape, Tendwa, na wengineo dhidi ya Chadema zinatoka wapi? Hizo tume walizojiundia haraka haraka wakati kila kitu kiko wazi walitaka kuficha nini au kwa malengo gani?

Muuaji hakuwa peke yake bali syndicate fulani na wote tulishuhudia idadi ya wale askari (more than six) kila mmoja akirusha ama kirungu, teke, au mkono wake kumpiga mwandishi - hawa wote kwa namna moja au nyingine walichangia kifo cha Mwangosi hivyo wote wakamatwe na kushtakiwa kwa kosa la mauaji otherwise huu ni mkakati wa kujaribu kuficha kombe mwanaharamu (CCM) apite.

Ilitokea kwa kudra za Mwenyezi Mungu kwenye tukio pakawa na "manabii" walifanikiwa kupata picha; je, hawa wasingekuwepo ingekuwaje - tusingeishia kwenye hadithi za "KITU KIZITO"?

Ni wananchi wangapi wanauwawa katika mazingira tatanishi kama haya lakini kelele za watanzania zimebakia kuwa "kilio cha samaki"?

Jemedari Mkuu, Mh. Rais wetu stuka, kuna kitu kisicho cha kawaida kinaendelea katika himaya yako baba. Hali si shwari.

huyo mkuu yupo kwenye 40 ya meles zenawi.
 
Hahaha na atafungwa unknown jail....Tanzania ni zaidi ya uijuavyo na hamruhusiwi kuingilia mahakama kuanzia wote mfunge midimo yenu muwachie mahakama ifanye kazi yake.....
 
Askari alikuwa na bomu kwa ajili ya shughuli za kufungua tawi!!?? Askari aliiba bomu hilo wapi??? Na aliyesahinisha hilo bomu ali akatekeleze amri ya wakubwa ni nani!! Ilikuwa alitumie kwa kiongozi gani ambaye ni adui wa CCM na serikali kwa ujumla???
 
Future tense haisaidii, wamkamate kwanza na ashitakiwe ndio kidogo nitaWAELEWA.
 
askari alikuwa na bomu kwa ajili ya shughuli za kufungua tawi!!?? Askari aliiba bomu hilo wapi??? Na aliyesahinisha hilo bomu ali akatekeleze amri ya wakubwa ni nani!! Ilikuwa alitumie kwa kiongozi gani ambaye ni adui wa ccm na serikali kwa ujumla???
mkuu sijakuelewa, hebu nifafanulie vizuri.
Kumbuka tunazungumzia bomu la machozi.
 
jina la huyi askari pamoja na cheo chake bila kusahau namba yake vipo wazi au ndio changa la macho?
 
Back
Top Bottom