fikra, misimamo ya kisiasa na mustakabli wetu

Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
59,221
79,513
Ndugu wana JF,

Katika muendelezo wa kumshambulia Dr Kitila tunapaswa kurudi nyuma kidogo na kufahamu mambo kadha wa kadha. Kwanza siasa ni nini haswa? na siasa ina mirengo/mielekeo ya aina zipi? na pia chama cha siasa ni nini haswa? na kinaongozwa na nini? na dira ya chama cha siasa ni nini? Maana hapa ninavyoona mimi kuna udhaifu wa watu kutojua kwamba fikra zinaweza kuwa tofauti na hii upelekea pia misimamo tofauti kidogo katika kusimamia sera za chama bila ya kuleta mvurugano wa chama husika!

Mbali ya misimamo tofauti, msingi wa misimamo hiyo huwa katika kutekeleza sera za chama husika kiufanisi. Ndo maana humu duniani tunapata kusikia wanasiasa wenye mrengo wa kati, wa kushoto na kulia au tunasikia majina kama mlibelari na pia mradikali kadhalika kwa kizungu hizi aina zote zinaangukia katika kitu kinaitwa "political orientation" nathani Bwana Kitila inapaswa uanzishe somo hili humu ndani! watu wasichanganye madesa na pia hizi fikra na misimamo tofauti haiwezi epukika na chama husika kinapaswa kukirimu tofauti hizo ndogo ambazo hutokana haswa na approach ya wahusika katika kutafuta majawapu ya utekelezaji wa sera za chama husika!

Kwa kuanzia tu ningependa tujaribu kutoa mifano hai kwa kuwaelezea wanasiasa maarufu na waliojijengea majina kama Dr Slaa, Mh Mbowe, Mchungaji Mtikila, Mh Zitto, Mh Tundu Lissu, Mh Jussa (
:playball:), Raila Odinga, Maalim Seif, Dr Mwakyembe na Mh Sitta (:fear:inanibidi aisee ) misimamo yao kisiasa! Na pia ningependa Mwana Kijiji ausike pia katika kuelezea watu hawa. Wakati mwingine watu wanakuwa na misimamo tofauti katika utekelezaji ili kusukuma gurudumu la ukombozi haraka na kwa ufanisi zaidi. Ninaamini thread hii itasaidia kuondoa shuku wasiwasi juu ya watu fulani kwa vile tu wana msimamo/fikra tofauti na tunayoyasadiki katika muelekeo watu wa kisiasa. Na pia ikumbukwe misimamo pia ina kikomo chake na haipaswi kukinzana na misingi mama inayosimamia chama na kama misimamo ikizidi sana kukinzana basi huaribu maana halisi ya mtu kuwa kwenye chama fulani.

Nakaribisha michango yenu woote humu ndani haswa haswa ya magwiji wa kiswahili, katika kuweka mambo sawa na kujaribu kutoa ile dhana ya usaliti inayojengeka kwa kasi dhini ya wanasiasa wetu pindi wanapotofautiana kidogo hata kama bado wanaheshimu, kuziamini na kuzitumikia sera za chama...
 
Nape na Mwigulu ni wanasiasa tumbo, hawajui maana ya siasa. Siasa sawa na mahakama, mawakili hupingana kwa hoja kizimbani, kesi ikiisha, wanakunywa pamoja
 
Back
Top Bottom