Figisu figisu Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa

Kwa hiyo uchaguzi wa chama unaenda sambamba na kura za maoni za urais???
Naam. Na hii ndiyo inaleta utulivu ndani ya CCM na hupunguza gharama. Kuna wakati Lowasa akiwa CCM alipendekeza kutenganishwe Urais na Uenyekiti. Kwamba ikiwa Magufuli atakuwa Rais, Lowasa awe Mwenyekiti. Hoja hii pia ilisimamiwa sana na akina Kingunge. CCM wakashtuka kwani wangeweza kumfukuza uanachama Rais kwa vile tu wao wana nguvu kwenye chama
 
Baada ya kumchangia aliyemtukana Rais sasa Mheshimiwa Ephata Nanyaro anatoa fedha kwa makada wa CCM! Hata hivyo, kila chama kina demokrasia yake. CCM wanachuja sana wakati wa kumpata mgombea Urais ndipo anapatikana mtu ambaye automatically anakuwa Mwenyekiti wao. Mfumo huu ni mzuri sana kwani unaondoa ukiritimba ndani ya chama tofauti na kwetu ambapo Mwenyekiti anaweza kubadili katiba muda wowote ili aendelee kubaki madarakani. Kikwete anatamani sana kuendelea na Uenyekiti ila desturi ya chama inamuondoa kinyemela.
We jamaa una akili sana, tatizo upo uliko siko mkuu.
 
Back
Top Bottom