Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,319
- 33,125
Bi Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma warejea C.C.M 17/10/2010
Wakongwe wawili wa siasa za vyama vingi visiwani Zanzibar Mheshimiwa Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma wamerudisha kadi zao za uanachama wa Civic United Front (CUF) na kuchukua za Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo jimboni Kawe, Dar es Salaam na kuahidi wenzao wengi toka CUF watafuata nyayo zao.
Alisema tangu historia ya vyama vingi ianze Tanzania, kila wakati wa uchaguzi wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hulazimika kukimbia visiwani humo kwa kuhofia hali ya kutokuwa na usalama katika kipindi hicho.
"Lakini sasa napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Kikwete kwa kurudisha heshima ya nchi yetu duniani kwani mwaka huu wa kampeni, hakuna hata mmoja aliyehama visiwani humo kukimbia uchaguzi" alimaliza Juma Othman akishangiliwa na umati mkubwa wa wana CCM waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Mama Fatma Maghimbi amewahi kuwa waziri kivuli wa Katiba na Sheria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama mbunge wa Chama Cha Wananchi CUF. Naye Juma Othman Juma amewahi kuwa muanzilishi wa Chama Cha Siasa visiwani kabla ya kujiunga na Chama cha Wananchi CUF.
Kikwete akielezea mpango wa Serikali wa kujenga Fly-overs jijini Dar kupunguza msongamano wa magari.
Kikwete akielezea mpango wa Serikali yake wa kujenga fly-overs Dar kupunguza msongamano wa magari
wananchi wa Kawe wakichukua viti ili kukaa wakati wa mkutano wa kampeni za Kikwete/CCM
Msanii wa Bongo Fleva Diamond akitumbuiza leo Kawe kwenye mkutano wa kampeni wa Kikwete/CCM
Kikwete akimnadi Bw. Othman mgombea udiwani kata ya Kawe
Kikwete akimnadi Mama Kizigha, mgombea ubunge wa CCM jimbo la Kawe
from: Bi Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma warejea C.C.M -
Wakongwe wawili wa siasa za vyama vingi visiwani Zanzibar Mheshimiwa Fatma Maghimbi na Juma Othman Juma wamerudisha kadi zao za uanachama wa Civic United Front (CUF) na kuchukua za Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo jimboni Kawe, Dar es Salaam na kuahidi wenzao wengi toka CUF watafuata nyayo zao.
L-R: Juma Othman Juma na Fatma Maghimbi
Akielezea sababu zake za kurudi CCM, Juma Othman Juma amesema ameguswa kwa kazi kubwa aliyofanya Mheshimiwa Kikwete Tanzania Bara na Visiwani hususan aliporejesha amani na utulivu visiwani Unguja na Pemba kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Alisema tangu historia ya vyama vingi ianze Tanzania, kila wakati wa uchaguzi wananchi wengi wa visiwa vya Unguja na Pemba hulazimika kukimbia visiwani humo kwa kuhofia hali ya kutokuwa na usalama katika kipindi hicho.