FATAKI; Hivi ni akina baba tu au hata akina Mama?

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Kuna tangazo ambalo linalenga kuwaepusha akina dada (hasa wale wenye umri mdogo) na uchu wa akina baba wapenda ngono. Binafsi sina tatizo sana na ujumbe uliomo kwenye matangazo haya, tatizo langu ni kwamba mbona wanaandamwa akina baba tu? Je, hakuna akina Mama ambao ni FATAKI??????
 
Naomba utu elimishe sisi tusio jua. Fataki ni nini hapa kwa unavyo maanisha wewe?
 
Naomba utu elimishe sisi tusio jua. Fataki ni nini hapa kwa unavyo maanisha wewe?

Kwa mujibu wa matangazo hayo, ni kwamba baba mtu mzima/mwenye adhi/uwezo wa kifedha na ambaye anahisiwa kuwa muathirika wa ukimwi (tafsri yangu binafsi kutokana na ninavyolielewa tangazo hilo) anamlaghai mtoto mdogo kwa vizawadi vidogovidogo na chips ili akafanye naye tendo la ngono. Huyu ndiye anaitwa Fataki kwa mujibu wa tangazo hilo linalosikika kwenye vituo vya Redio takribani viwili.

Sasa swali langu ni kwamba, je, hakuna hakina mama wa aina hii ambao nao huwalaghai wavulana wadogo kwa kuwafadhili ktk masuala madogomadogo kwa lengo hilo hilo? Kama wapo, ni kwanini tangazo hili linakuwa selective?
 
Kashaija, na mimi nashare the same concerns, hilo tangazo limekaa kiupande mmoja mno! Kuna masugar mummy inabidi na wenyewe wawekwe hewani
 
tena hilo tangazo linanichefua wakinamama wanawarubuni vijana wa kiume hilo hawalioni mbaya zaidi wakina mama wenyewe wamefiwa na waume zao na kilicho waua hakijulikani,sorry siyo wote
 
Kwa mujibu wa matangazo hayo, ni kwamba baba mtu mzima/mwenye adhi/uwezo wa kifedha na ambaye anahisiwa kuwa muathirika wa ukimwi (tafsri yangu binafsi kutokana na ninavyolielewa tangazo hilo) anamlaghai mtoto mdogo kwa vizawadi vidogovidogo na chips ili akafanye naye tendo la ngono. Huyu ndiye anaitwa Fataki kwa mujibu wa tangazo hilo linalosikika kwenye vituo vya Redio takribani viwili.

Sasa swali langu ni kwamba, je, hakuna hakina mama wa aina hii ambao nao huwalaghai wavulana wadogo kwa kuwafadhili ktk masuala madogomadogo kwa lengo hilo hilo? Kama wapo, ni kwanini tangazo hili linakuwa selective?

Wapo wengi mbona. Huja sikia kitu kinaitwa serengeti boys mkuu?
 
Tangazo hilo linaonesha aina ya jamii yetu: jamii yenye mfumo dume ambayo kila kitu mtendaji mkuu ni mwanaume, na ndiye mkandamizaji wa mwanamke kwa kila jambo. Ni tangazo la kibaguzi katika enzi hizi tunapozungumza juu ya usawa wa binadamu na usawa wa kijinsia. Kweli kuna kina mma waliokubuhu, wanaowalaghai wavulana wadogo. Kumbe tangazo hilo liongezewe kipengele hicho cha kina mama. Wasije wakafikiri kwamba wao haliwahusu, hata kama wenye tabia hiyo pengine ni wachache.
 
Mkuu heshima mbele. mambo ya haki sawa kwa wote uta gundua lina pigiwa bango tu kama huyo anaye nyimwa huyo haki ni mwanamke. Hiyo ndiyo hali halisi. Aki pendelewa mwanamke huto sikia mtu akisema chochote. Nadhani jamii ina bidi ijifunze kuwa haki sawa kwa wote ina maanisha haki sawa kwa wote.

Utasikia Wizara ya Jinsia, Wanawake na Watoto, Je kwanini hakuna Wizara ya akinababa? Mbona wapo akinamama wengi wanaowapiga waume zao? Mbona wapo akina mama wengi wanaowanyima waume zao haki ya ndoa? Kwani hayo siyo manyanyaso?
 
Kuna kina mama sikuhizi wanawapangishia vijana wadogo nyumba na kumhudumia kila kitu ili siku moja moja amliwaze na wana wivu hao asimkute anaongea na mwanamke au akute namba/sms za ajabu.
 
Kiini cha upendeleo katika tangazo ambalo dhamira lake nzuri ni niwafadhili. Kutangaza katika vyombo vya habari kunataka hela na mara nyingi wafadhili wetu wanaimpose ajenda zao wanapotupatia misaada yao kwa sababu hiyo utaona mifano mingi 'mizuri' ya usawa wa kijinsia inatoka kwao wakati papahapa nchini kuna mifano mizuri ya kimila kuliko hata ile ya kwao.

Urithi katika kabila la waluguru kwa mfano: Mtoto wa kike ni mrithi wa mali za famili ya baba yake wakati mtoto wa kiume ni mrith wa mali za famili ya baba mkwe wake. Kwa nini mifano kama hii haitumiki kubeza mfumo dume na matatizo ya mirathi nchini hadi iletwe mifano toka kwa wafadhili wa kampeni?

Wanawake kwao hao wafadhili siku hizi hawaoleki kwa sababu nao wanataka kuvaa viatu vya kiume bila kujali kuwa kila jinsia ina nafasi yake katika ndoa. Utashangaa kumsikia msichana wa kitanzania siku hizi ati naye anadai hataki kuolewa bali anataka kuoa kwa vile ana kila kitu na ana uwezo wa kummiliki mwanaume. Sijui kama lengo la kampeni nzima ya usawa wa kijinsia ni kuua mfumo dume ili kuendeleza mfumo jike badala yake!

Kampeni ya usawa wa kijinsia imesababisha talaka kuwa nyingi mno huko kwa wafadhili kwa kuwa wanawake wamependelewa kila idara na kuwa na kiburi dhidi ya wanaume kiasi cha vijana wa kiume kuzira kabisa ndoa. Kwa sababu hiyo ndoa ikidumu sana ni miaka 5 sasa hivi huko kwao.

Tunapopokea misaada, tusipokee na kila kilichomo bali tuchuje ili tujenge chetu kwa tamaduni zetu weneywe. Life would, otherwise, be so boring if the whole world was not made of a mosaic of cultures, norms and values. Let's use globalisation to cherish our cultural differences/varieties coz killing them is tantamount to attempting to discourage biodiversity, which is not healthy at all to the sustainability of life on earth...
 
Mkuu heshima mbele. mambo ya haki sawa kwa wote uta gundua lina pigiwa bango tu kama huyo anaye nyimwa huyo haki ni mwanamke. Hiyo ndiyo hali halisi. Aki pendelewa mwanamke huto sikia mtu akisema chochote. Nadhani jamii ina bidi ijifunze kuwa haki sawa kwa wote ina maanisha haki sawa kwa wote.

Unachosema MwanaF kwa kiasi fulani kina ukweli.Hii inatokana na mawazo-mgando au stereotypes katika jamii.Hata hivyo ni makosa kuendelea kushikilia imani hizi kwani mambo yamebadilika sana.
Baadhi ya stereotypes ambazo kwa sasa hazina maana ni pamoja na imani kuwa :
- Wahalifu ni wanaume - sasa hivi hakuna cha mwanaume au mwanamke kwenye uhalifu tena wa aina zote - wizi, ujambazi, utapeli,n.k
- Wanyanyasaji ni wanaume - wako wanawake wenye kunyanyasa pia
Tukiangalia hata Sheria ya Makosa ya kujamiiana ya 1998 ( SOSPA 1998) inaonyesha wazi kuwa makosa ya kujamiiana - ubakaji na udhalilishaji wa watoto kijinsia unawalenga zaidi wanaume - tunajua fika kuwa wapo wanawake wenye kuwanyanyasa watoto wa kiume kijinsia hivyo basi sheria haikulizingatia hili.

Inapokuja suala la Fataki pia tunaona hali ikijirudia.Inabidi tujitahidi zaidi kuelimisha watu kuhusu kuondokana na mawazo mgando kwani mgando huo unayeyuka siku hadi siku na tunahitaji mtizamo mpya kwa kuzingatia mabadiliko ya kijamii pia.
 
Tuwekeeni basi tangazo lenyewe hapa ndugu zetu mlioko nyumbani tulisikilize....
Mimi sidhani kwa Bongo- ubazazi wa kinamama kwa vijana wadogo ni mkubwa kiasi cha kufanyiwa campaign radioni, haya mambo yapo kwa wingi Dar lakini huko mikoani ni taboo kabisa. Lakini tukija kwa upande wa kina baba, its a massive problem tena ni kila mahali- mijini hadi vijijini, someone somehow was needed to do something about it. Na naamini kabisa kwamba tangazo litakuwa limetolewa na chombo kinachotetea maslahi ya wanawake, wanaume nasi kama hii inatukera tuunde vyombo vya kutetea maslahi yetu, tusitegemee wanawake watutetee kwenye campaigns zao.
 
Tena hao kina mama ni moto wa pumba. Muulizeni gates wa muhadhara. Bora wasichana hukataa kwanza wakitokewa na mafataki, ila hayo mabaruti yakitokea vivulana vinaona zali
 
Back
Top Bottom