Fanya malengo yako yawe ya kwanza sio mwanamke

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Ratiba zako, pesa zako na mawazo yako mengi yaelekee kwenye malengo.
Alafu utengeneze muda kwa ajili ya mwanamke na familia pia. Na sio kinyume. Yaani ukaanza na mwanamke alafu ndo ufate malengo yako, hapana.

Achana na wazo mwanamke ndo kila kitu kwako.
Achana na wazo mwanamke ndo anakukamilisha.
Achana na wazo ukimpata huyo mwanamke mambo yatakua sawa.
Au wazo la kuashiria mwanamke ndo kipaumbele chako.
Tambua kuwa mwanamke sio kila kitu kwako. Japo akili zetu zinawaza ngono sana lakini usiifanye iwe kipaumbele.

Usitongoze mwanamke ukiamini ndo atakukamilisha.
Usiwe na mwanamke na kumfanya ndo kila kitu kwako.
Ukifanya hivyo unampa presha kubwa kuliko anavyoweza kustahimili.
Ukimpa mwanamke nafasi kubwa kuliko anavyostahili hatokua na amani.
Japo atakulazimisha uwe naye muda wote au umfanye ndo kila kitu lakini sio anachohitaji.

Atajisikia furaha zaidi akiwa kama msaidizi wako.
Pia ndo sehemu anayopata changamoto ya kike.
Anataka awe chini ya mwanaume bora ili ampe motisha kuendelea na malengo yake zaidi.
Wanawake wana motisha nzuri, wape nafasi hiyo kwa kumfanya sehemu ya maisha yako.
Kama sehemu yako ya maisha na sio ndo maisha yako.

Kipindi cha nyuma mwanamke mmoja aliniambia “mi nataka nipate changamoto na niwe sehemu ya maisha yako tu” sikumuelewa sababu nilikua naamini inabidi mwanamke nimfanye ndo maisha yangu, nilikua nataka kumridhisha kila muda na nilikua nabadili ratiba zangu kwa ajili yake. Niliishia kumpoteza sababu nilimpa nafasi kubwa. Hapo nikajifunza kuwa mwanamke anapenda awe sehemu ya maisha yangu. Yaani awe chini yangu alafu mimi ndo niwe kama changamoto yake, na sio kipaumbele zaidi ya malengo yangu.
 
Vipi kama malengo yako ni wanawake (good time)

After all to each his / her own na ukiangalia kwa jicho la tatu unaweza kukuta kila umachohangaikia / kitafuta ni illusion...

Ushauri wangu kwako ishi maisha yako na fanya kile unachopenda bila kusahau kuishi within your means, ukifanya hayo maisha yatakuwa rahisi sana; hakuna haja ya complications. Sababu hayana destination kwamba nimefika ni safari mpaka siku unadondoka.....
 
Ratiba zako, pesa zako na mawazo yako mengi yaelekee kwenye malengo.
Alafu utengeneze muda kwa ajili ya mwanamke na familia pia. Na sio kinyume. Yaani ukaanza na mwanamke alafu ndo ufate malengo yako, hapana.

Achana na wazo mwanamke ndo kila kitu kwako.
Achana na wazo mwanamke ndo anakukamilisha.
Achana na wazo ukimpata huyo mwanamke mambo yatakua sawa.
Au wazo la kuashiria mwanamke ndo kipaumbele chako.
Tambua kuwa mwanamke sio kila kitu kwako. Japo akili zetu zinawaza ngono sana lakini usiifanye iwe kipaumbele.

Usitongoze mwanamke ukiamini ndo atakukamilisha.
Usiwe na mwanamke na kumfanya ndo kila kitu kwako.
Ukifanya hivyo unampa presha kubwa kuliko anavyoweza kustahimili.
Ukimpa mwanamke nafasi kubwa kuliko anavyostahili hatokua na amani.
Japo atakulazimisha uwe naye muda wote au umfanye ndo kila kitu lakini sio anachohitaji.

Atajisikia furaha zaidi akiwa kama msaidizi wako.
Pia ndo sehemu anayopata changamoto ya kike.
Anataka awe chini ya mwanaume bora ili ampe motisha kuendelea na malengo yake zaidi.
Wanawake wana motisha nzuri, wape nafasi hiyo kwa kumfanya sehemu ya maisha yako.
Kama sehemu yako ya maisha na sio ndo maisha yako.

Kipindi cha nyuma mwanamke mmoja aliniambia “mi nataka nipate changamoto na niwe sehemu ya maisha yako tu” sikumuelewa sababu nilikua naamini inabidi mwanamke nimfanye ndo maisha yangu, nilikua nataka kumridhisha kila muda na nilikua nabadili ratiba zangu kwa ajili yake. Niliishia kumpoteza sababu nilimpa nafasi kubwa. Hapo nikajifunza kuwa mwanamke anapenda awe sehemu ya maisha yangu. Yaani awe chini yangu alafu mimi ndo niwe kama changamoto yake, na sio kipaumbele zaidi ya malengo yangu.
Well
 
kipindi nipo Chuo, Kuna couple moja Tena yakisabato,
aisee walikua wanapenda hao watu sanaaaa.
Cha ajabu wakaachana.

Kikubwa ninachoelewa Dunia hii hakuna lisilo na Mwisho. 🤣😂😂😂😭😭 ndoa nyingi ni ndoano. bye 😟
Furahi leo kesho huijui.
 
Back
Top Bottom