Faida za lozi Almond

Hata Soko la Kisutu au mtaa wa Zanaki kwa wale wanaouza matunda kwenye corridor za maduka wanazo
Unajuwa kilo moja ya Lozi ni shilingi ngapi ya Tanzania? Huku nje nilipo mimi Kilo 1 ya Lozi aka (Almond) sawa na huko nyumbani Tanzania ni shilingi Elfu 25 sijuwi nyumbani kilo moja ya Lozi ni kiasi gani Mkuu?

FAIDA YA ALMOND.jpg
 
almonds.jpg

Lozi (Almond)

Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini


Wengi tumekuwana tukizifahamu aina mbalimbali za njugu kama vile karanga,korosho na nazi.


Lozi ni moja wapo ya njugu ambazo jina lake maarufu duniani ni Almonds. Yenyewe hukaangwa kidogo na huliwa kwa kutafunwa kama ilivyo karanga.

Kitafunwa hiki kinachofanana na karanga kinatajwa kuwa ni tiba kwa watu wenye matatizo ya moyo na husaidia kwa kiasi kikubwa katika kuratibu mapigo ya moyo.

Pamoja na hilo utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Purdue unaonyesha lozi kuwa na manufaa mengi kiafya ukilinganisha na aina nyingine za njugu.

Hiyo inatokana na kiwango kikubwa cha protini na virutubisho vingine kama vile madini na kusaidia kuratibu mfumo mzima wa mwili, moja wapo maradhi ya moyo.

Mtafiti katika Bodi ya Sayansi Jimbo la California nchini Marekani, Dk Karen Lapsley ambaye ni mmoja wa wataalam walioshiriki katika utafiti huo anasema lozi pia inasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari.

Anasema kuwa mtu mwenye kisukari anapotafuna lozi zinamsaidia kuratibu mfumo wake damu na kuhakikisha siku zote mishipa ya damu inakuwa inafanya kazi inavyostahili.

Dk Penny Kris Etherton wa chuo kikuu cha Pennsylvania anasema lozi zina uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha lehemu ndani ya mwili.

Madini yaliyomo kwenye lozi yanasaidia kuimarisha mifupa, misuli, viungo na kukabiliana na shinikizo la damu. Matatizo haya mara nyingi hujitokeza kwa wenye umri mkubwa.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward kwa msaada wa mtandao chanzo. Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini - mwanzo - mwananchi.co.tz
Utumiaji wake upoje unatafuna hivo hivo au zinapikwa km Karanga
 
Tandika mskiti wa chihota yupo chinga anauza.

korosho na hizo almond.

kuna pakti za 2000 na 5000.

Nikiipata mamba yake nitaiweka hapa.

unapotaka kwenda ni vzr ukampigia kwanza.

ili kujiepushia usumbufu
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Lozi Almond kiswahili inaitwaje? au kwa utafiti wako waweza kuipata katika mchanganyiko wa kitu gani kama food suppliment ambayo ni rahisi kupatikana madukani?
Zipo solo la kisutu kilo 30000 kipimo kingine 9000 na 4500
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom