Faida za lozi Almond

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Lozi (Almond):

Lozi inajulikana kama ni King katika jamii ya njugu, ina elements karibia ya zote zinazohitajika katika mwili wa mwanadam. Ni chakula chenye kutia nishati mwili na akili.

Kuna aina mbili za Lozi, kuna lozi zile tamu na kuna lozi chungu kuna zenye ngozi nyembamba (thin-skinned) na kuna zenye ngozi nene(thick-skinned) hii ni katika aina ya lozi tamu ambazo ndio tunazozitumia na tunahitajika kutumia ama zile lozi chungu zina prussic acid ambayo ni sumu hata hivo hizo lozi chungu zinatumika katika mambo ya kutengenezea cosmetics, mafuta ya lozi (almond oil) pia na perfumes.

Nchi mashuhuri yenye Lozi ni Morocco, pia lozi zilionekana katika miaka mingi nyuma katika nchi ya Syria na Palastine inasemekana katika zama za Nabii Issa A.S. Hata hivo sasa hivi lozi zinazalishwa sehemu nyingi duniani kama Italy,California,Australia,South Africa,Kashmir na sehemu nyingi za Asia.

Food Value: Minerals and Vitamins
Moisture 5.2% Calcium 230 mg
Protein 20.8% Phosphorus 490 mg
Fat 58.9% Iron 4.5 mg
Minerals 2.9% Niacin 4.4 mg
Fibre 1.7%
Carbohydrates 10.5%

Ndani ya lozi pia kuna upatikanaji wa copper, iron phosphorus na Vitamin B, vitu hivi vinasaidia katika upatikanaji wa new blood cells, haemoglobin pia inasaidia ubongo, mishipa, mifupa, moyo na ini kufanya kazi kwa wepesi kabisa. Lozi insaidia kupanua na kutia nguvu muscles za ubongo katika kuongeza fahamu.

Old ages:Utu uzima wa kiumri.
Chukua lozi kiasi na uziroweka katika maji na baadae utoe ngozi yake ikisha uzisage na kufanya paste kwa kutumia kama siagi, hii huongeza proteins ndani ya mwili na hasa kwa watu wazima, pia unaweza kutia katika maziwa na ukanywa hii nzuri kwa watoto.

Anaemia: upungufu wa damu
Kuna upatikanaji wa copper katika lozi katika rate 1.15mg per 100 grams, copper pamoja na iron na vitamins hizi zinatumika kama ni catalyst katika mfumo wa blood haemoglobin. Kwa hiyo wenye maradhi ya upungufu wa damu ni vizuri mtu kutumia lozi kwa sana.

Constipation: kupata choo
Kwa wale wenye matatizo ya kupata choo, ni uzuri kula lozi wakati wa usiku kabla ya kwenda kulala.

Impotency: upunguvu wa nguvu za kiume
Kwa wale wenye upunguvu wa nguvu za kiume na za kike, wale lozi kwa wingi.

Skin Disorder:maradhi ya ukoma
Kwa wale wenye maradhi ya ukoma, wasage lozi iwe laini ikisha wajipake pale palipoathirika, na pia kwa wale wenye pimples.

FAIDA YA LOZI.jpg

===
almonds.jpg

Lozi (Almond)

Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini

Wengi tumekuwana tukizifahamu aina mbalimbali za njugu kama vile karanga,korosho na nazi.

Lozi ni moja wapo ya njugu ambazo jina lake maarufu duniani ni Almonds. Yenyewe hukaangwa kidogo na huliwa kwa kutafunwa kama ilivyo karanga.

Kitafunwa hiki kinachofanana na karanga kinatajwa kuwa ni tiba kwa watu wenye matatizo ya moyo na husaidia kwa kiasi kikubwa katika kuratibu mapigo ya moyo.

Pamoja na hilo utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Purdue unaonyesha lozi kuwa na manufaa mengi kiafya ukilinganisha na aina nyingine za njugu.

Hiyo inatokana na kiwango kikubwa cha protini na virutubisho vingine kama vile madini na kusaidia kuratibu mfumo mzima wa mwili, moja wapo maradhi ya moyo.

Mtafiti katika Bodi ya Sayansi Jimbo la California nchini Marekani, Dk Karen Lapsley ambaye ni mmoja wa wataalam walioshiriki katika utafiti huo anasema lozi pia inasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari.

Anasema kuwa mtu mwenye kisukari anapotafuna lozi zinamsaidia kuratibu mfumo wake damu na kuhakikisha siku zote mishipa ya damu inakuwa inafanya kazi inavyostahili.

Dk Penny Kris Etherton wa chuo kikuu cha Pennsylvania anasema lozi zina uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha lehemu ndani ya mwili.

Madini yaliyomo kwenye lozi yanasaidia kuimarisha mifupa, misuli, viungo na kukabiliana na shinikizo la damu. Matatizo haya mara nyingi hujitokeza kwa wenye umri mkubwa.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward kwa msaada wa mtandao chanzo. Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini - mwanzo - mwananchi.co.tz

Lozi (Almond)

Chanzo:Mzizimkavu
 
Lozi Almond kiswahili inaitwaje? au kwa utafiti wako waweza kuipata katika mchanganyiko wa kitu gani kama food suppliment ambayo ni rahisi kupatikana madukani?
 
Uswahilini pia huwa zipo, ukizikosa tembelea supa maket yoyote nchini, siku hizi kimekuwa chakula muhimi sana nchini
sijui huko kariakoo zinauzwaje maana niliwahi kuona kwenye supermarket moja eti kilo moja Frw kati ya 30,000 mpaka 40,000 nikajisikia nimechoka. mana vitu kama hivi unatakiwa utumie mara kwa mara na kwa muda mrefu ndio uweze kuona matokeo mazuri na sio kutumia kwa siku moja. sasa kwa bei hiyo na mtu mwenye familia ataweza? labda matajiri.
 
almonds.jpg

Lozi (Almond)

Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini

Wengi tumekuwana tukizifahamu aina mbalimbali za njugu kama vile karanga,korosho na nazi.

Lozi ni moja wapo ya njugu ambazo jina lake maarufu duniani ni Almonds. Yenyewe hukaangwa kidogo na huliwa kwa kutafunwa kama ilivyo karanga.

Kitafunwa hiki kinachofanana na karanga kinatajwa kuwa ni tiba kwa watu wenye matatizo ya moyo na husaidia kwa kiasi kikubwa katika kuratibu mapigo ya moyo.

Pamoja na hilo utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Purdue unaonyesha lozi kuwa na manufaa mengi kiafya ukilinganisha na aina nyingine za njugu.

Hiyo inatokana na kiwango kikubwa cha protini na virutubisho vingine kama vile madini na kusaidia kuratibu mfumo mzima wa mwili, moja wapo maradhi ya moyo.

Mtafiti katika Bodi ya Sayansi Jimbo la California nchini Marekani, Dk Karen Lapsley ambaye ni mmoja wa wataalam walioshiriki katika utafiti huo anasema lozi pia inasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari.

Anasema kuwa mtu mwenye kisukari anapotafuna lozi zinamsaidia kuratibu mfumo wake damu na kuhakikisha siku zote mishipa ya damu inakuwa inafanya kazi inavyostahili.

Dk Penny Kris Etherton wa chuo kikuu cha Pennsylvania anasema lozi zina uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha lehemu ndani ya mwili.

Madini yaliyomo kwenye lozi yanasaidia kuimarisha mifupa, misuli, viungo na kukabiliana na shinikizo la damu. Matatizo haya mara nyingi hujitokeza kwa wenye umri mkubwa.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward kwa msaada wa mtandao chanzo. Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini - mwanzo - mwananchi.co.tz
 
nimeelewa sitashukuru kwa sababu ni moja ya majukumu ya media kuelemisha jamii na hata mimi nikiwa na changu kitu chenye faida nitakileta hapa
 
almonds.jpg

Lozi (Almond)

[h=1]Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini.[/h]
Wengi tumekuwana tukizifahamu aina mbalimbali za njugu kama vile karanga,korosho na nazi.

Lozi ni moja wapo ya njugu ambazo jina lake maarufu duniani ni Almonds. Yenyewe hukaangwa kidogo na huliwa kwa kutafunwa kama ilivyo karanga.

Kitafunwa hiki kinachofanana na karanga kinatajwa kuwa ni tiba kwa watu wenye matatizo ya moyo na husaidia kwa kiasi kikubwa katika kuratibu mapigo ya moyo.

Pamoja na hilo utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Purdue unaonyesha lozi kuwa na manufaa mengi kiafya ukilinganisha na aina nyingine za njugu.

Hiyo inatokana na kiwango kikubwa cha protini na virutubisho vingine kama vile madini na kusaidia kuratibu mfumo mzima wa mwili, moja wapo maradhi ya moyo.

Mtafiti katika Bodi ya Sayansi Jimbo la California nchini Marekani, Dk Karen Lapsley ambaye ni mmoja wa wataalam walioshiriki katika utafiti huo anasema lozi pia inasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya ugonjwa wa kisukari.

Anasema kuwa mtu mwenye kisukari anapotafuna lozi zinamsaidia kuratibu mfumo wake damu na kuhakikisha siku zote mishipa ya damu inakuwa inafanya kazi inavyostahili.

Dk Penny Kris Etherton wa chuo kikuu cha Pennsylvania anasema lozi zina uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha lehemu ndani ya mwili.

Madini yaliyomo kwenye lozi yanasaidia kuimarisha mifupa, misuli, viungo na kukabiliana na shinikizo la damu. Matatizo haya mara nyingi hujitokeza kjwa wenye umri mkubwa.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward kwa msaada wa mtandao chanzo. Lozi: aina ya njugu yenye manufaa mengi mwilini - mwanzo - mwananchi.co.tz
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom