Faida za kusameheana..

mi_mdau

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,104
1,476
wadau mi si mzoefu sana wa mapenzi lakini nimegundua kitu ambacho labda na wengine ambao pengine ni wazoefu linaweza kuwasaidia, hata walio kwenye ndoa.
Tulipoanza mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu wa kike, kwa hakika tulihisi kupendana na muda mwingi tulikuwa na furaha. Shida moja kubwa ilikuwa ni kugombana na kubishana kila baada ya muda mfupi sana. Kitu kidogo kinaweza kuwakosesha raha mliyokuwa nayo kutwa nzima na mkalala na maumivu. Baada ya muda na siku kadhaa nikaja kugundua kuwa hata ikiwa ni ugomvi mdogo, bila kujali nani ana makosa wote tulikuwa tukipanda juu na kila mmoja anajifanya ndo mwenye sauti, hakuna aliyetaka kujishusha.
Baada ya siku kadhaa tulikaa chini na kujiuliza kuwa labda kuna 'mdudu' na anatokea wapi. Kwa sababu mimi nilijua nampenda kwa dhati sasa kwa nn nagombana naye, na yeye kwa wakati wake akawa ananiambia kitu kama hicho. Niliwaza na kumwambia kuwa tuendelee kuishi maisha yetu ya kawaida bila kuigiza ila tu, mmoja anapokasirishwa, hata kitu kikubwa, since hataki kunipoteza kirahisi, aulize kwa upole tu. mfano "mpenzi, mbona nimekupigia simu, nimekutumia message, hujajibu?" badala ya "wewe mi napiga, nakutumia sms, hujibu? unaniringia kwa kuwa nakupenda au? ulikuwa unaongea na NANI?".
Tukagundua kuwa si mara zote mtu anafanya makosa kwa kukusudia, kwa hiyo ukimuuliza kwa ukali unasababisha aone unamwonea na yeye anapandisha hasira, na hakuna kuelewana. Lakini hata kama amekosa kwa kukusudia, ukimuuliza kwa upole, atajutia kosa lake (kama anakupenda) na atajirudi kwa upesi. Tangu hapo suala la ugomvi kati yetu limekuwa la nadra sana (halikwepeki kwa asilimia 100) na mapenzi ni raha zaidi.
TUJARIBU KUJISHUSHA, KUHESHIMIANA NA UAMINIFU
 
Ahsante sana kwa ujumbe na ushuhuda murua kiasi hicho.
Nakubaliana na wewe kabisa bila kusameheana familia haziwezi kuendelea kabisa.
Jawabu la Upole hushusha hasira kwa aliye kasirika.
Kuheshimiana na kusikilizana kunatia amani na furaha ndani ya nyumba.
Kwangu huu ujumbe wako ni wa mhimu sana na unaifanya siku yangu nzima ya jtatu kuwa safi na murua kabisa.
 
hasa wanaume wengi ndio zenu hizo!!! ila ni story nzuri inafundisha sana!!
 
Ushauri mzuri uliotokana na uzoefu....ubarikiwe sana Mdau......!!!!
 
Safi sana, nimekubaliana na uzoefu huu.

Pia mapenzi ni kitu cha pekee kabisa.

Hivyo mara unapokuwa na mpenzi wako epuka tamaa za vitu, anasa au vitu ambavyo sio muhimu hasa kwa wanawake.

na kwa wanaume, inabidi kuepuka vishawishi au tamaa za wanawake wengine. Ridhika na mkeo/mpenzi wako daima na uwe mwaminifu. hakika utaishi kwa furaha na mungu atakulinda
 
Back
Top Bottom