Faida za kiuchumi za Uwanja wa Ndege Chato

Hata mim nimekaa kuzubgumza na malecture hapa wa department of tourism.wanasema ile ni target kubwa ya kuutangaza utalii hasa wa Rubondo ambako kule kuna utalii anuwai,wa maji,wa wanyama kuogelea kuvua sato.yan kama hujafika Rubondo huwez kujua uzuri wake.

sasa ile ni mikakkat endelevu kuja kuitangaza.kwa Nchi zingine Rubondo peke yake ingekua a great tourist attraction haijwah kutokea.
serikal haipang mambo kuangalia leo serikal inapnga mambo miaka 50 inayokuja.

uwanja uke ni sahih kabisa. Wito wa kuiomba serikal yetu sikivu kuikarabat viwanja vyote vya mikoa ziweze kutua ndege zetu

Duh hicho chuo ni cha kufunga haraka sana,kitazalisha wasomi uchwara
 
Faida sita za uwanja wa gabolite ya chato kwa wana chato baada ya jamaa kuondoka.

1. kujifunzia kuendesha bodaboda na baiskeli.
2. Kufanyia mazoezi mnatano usiku
3. Kuvutia sigara kubwa
4. Kuanikia mihogo,mazao
5. kuchezea mdako,marede,
6. kuchungia mifugo
 
Tatizo watu mnachukulia utalii mwepesiii taguteni sababu nyingine kujustify ujenzi wa uwanja wa Chato ila si utalii.
 
Faida sita za uwanja wa gabolite ya chato kwa wana chato baada ya jamaa kuondoka.
1.kujifunzia kuendesha bodaboda na baiskeli.
2.Kufanyia mazoezi mnatano usiku
3.Kuvutia sigara kubwa
4.Kuanikia mihogo,mazao
5.kuchezea mdako,marede,
6.kuchungia mifugo
Gbadolite mpya inafuata
 
Hata mim nimekaa kuzubgumza na malecture hapa wa department of tourism.wanasema ile ni target kubwa ya kuutangaza utalii hasa wa Rubondo ambako kule kuna utalii anuwai,wa maji,wa wanyama kuogelea kuvua sato.yan kama hujafika Rubondo huwez kujua uzuri wake.

sasa ile ni mikakkat endelevu kuja kuitangaza.kwa Nchi zingine Rubondo peke yake ingekua a great tourist attraction haijwah kutokea.
serikal haipang mambo kuangalia leo serikal inapnga mambo miaka 50 inayokuja.

uwanja uke ni sahih kabisa. Wito wa kuiomba serikal yetu sikivu kuikarabat viwanja vyote vya mikoa ziweze kutua ndege zetu
Huyo lecture ni wale moja kwa moja shule mpaka kufundisha hajaingia field. Anaongea notes tu
 
Ngamanya Kitangalala

"Japokuwa kwenye ripoti nyingine ya 2019 kutoka World Economic forum ambayo utolewa kila baada ya miaka 5, imeonyesha Tanzania inashika nafasi ya 12 duniani na ya 1 kwa Afrika kwa kuwa na vivutio vingi vya asili vya utalii(Tumeshuka kwa nafasi 10)"

Hapo naona huna point zaidi unamdisi kiongozi wako kwamba kafeli kwa kiwango kikubwa. 2015 mpaka 2020 yuko yeye madarani na umetushusha ivyo. Hapo hamna haja ya kumpa mitano tena.

Ila kama umepewa Ela ulete bandiko humu Basi tatizo ni njaa zako. Au unasaka teuzi Kama Yule mwenzio wa kawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iliyojenga ni serikali siyo yeye binafsi. Fedha ya serikali inautaratibu wake wa kisheria na kibajeti tusimlaumu Rais kwa upotoshaji wenu.
 
Iliyojenga ni serikali siyo yeye binafsi. Fedha ya serikali inautaratibu wake wa kisheria na kibajeti tusimlaumu Rais kwa upotoshaji wenu.
Hiyo budget haikupitishwa bungeni ndio tatizo
 
Hata mim nimekaa kuzubgumza na malecture hapa wa department of tourism.wanasema ile ni target kubwa ya kuutangaza utalii hasa wa Rubondo ambako kule kuna utalii anuwai,wa maji,wa wanyama kuogelea kuvua sato.yan kama hujafika Rubondo huwez kujua uzuri wake.

sasa ile ni mikakkat endelevu kuja kuitangaza.kwa Nchi zingine Rubondo peke yake ingekua a great tourist attraction haijwah kutokea.
serikal haipang mambo kuangalia leo serikal inapnga mambo miaka 50 inayokuja.

uwanja uke ni sahih kabisa. Wito wa kuiomba serikal yetu sikivu kuikarabat viwanja vyote vya mikoa ziweze kutua ndege zetu
Mnavyojitoa ufaham mpk Basi jibuni izo hoja za makandokando na mauchafu yaliofanyika ktk kujenga iko kiwanja
 
DRCCC.jpg


MAGUFULI HAKUISAIDIA CHATO

Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania.

Lakini maendeleo ni nini?

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alijitanabaisha kama mtu anayependa maendeleo, lakini kuna uwezekano mkubwa hakujua tafsiri ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine, Magufuli alitamani maendeleo ya nyumbani kwao Chato, na hivyo alifanya mengi huko nyumbani kwao, lakini pengine hakupasaidia inavyotakikana.

Magufuli alijenga uwanja wa ndege wa kutua ndege kubwa wilayani Chato, wakati kuna majiji (mfano Tanga), manispaa na miji mikubwa kuliko Chato ambako hakuna viwanja vya ndege vya maana au vilivyopo havina hadhi ya maeneo hayo. Kwanini Chato?

Hoteli ya Nyota Tano ilikwisha anza kujengwa Chato. Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa ulikuwa kwenye mpango wa kujengwa Chato. Alilazimisha CRDB wapeleke huduma wilayani Chato ingawa hakuna tija ya kibiashara. Na Jengo walilopangisha CRDB huko Chato ni jengo lake huyo Magufuli.

Je! Magufuli aliipenda Chato? Jibu ni Ndiyo. Na sio kosa kupenda kwenu, sio kosa kupenda maendeleo ya kwenu. Shida inakuja kwenye tafsiri ya maendeleo.

Magufuli angetambua maana ya maendeleo; Angeanza kuboresha elimu wilayani Chato kabla ya kujenga Hotel ya Nyota Tano. Moja kati ya wilaya zenye mazingira magumu kwa wanafunzi na walimu ni Wilaya ya Chato. Hoteli ya Nyota tano ya nini wakati wanafunzi wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika? Nani ataijenga Chato wakati idadi kubwa ya vijana hawapati elimu yenye tija katika dunia ya leo (Na hili ni kwa maeneo mengi ya Tanzania).

Kanda ya Ziwa kuna Ng'ombe wengi sana, lakini hawana afya. Pesa ya kujenga uwanja wa ndege ingetosha kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna ya kufuga kwa faida pamoja na kujenga viwanda vidogodogo vya kusindika Nyama na Maziwa ambavyo vingetoa ajira ya kudumu kwa vijana wa Chato. Wafanyabiashara wangemiminika Chato kutoka maeneo ya jirani kwa ajili ya biashara ya Nyama, na mazao ya maziwa. Kwanini mwenyeji wa Geita anunue maziwa ya Tanga Fresh, au Asas kutoka Iringa wakati kuna Ng'ombe wengi ndani ya kanda ya ziwa kuliko Iringa na Tanga kwa pamoja?

Kuna ardhi kubwa wilayani Chato. Magufuli angeweza kupeleka wataalamu wa kilimo kutoa mafunzo kwa vijana juu ya kilimo chenye tija ya kiuchumi na kibiashara. Wakulima wangelima kibiashara zaidi na kuvutia masoko kutoka mikoa jirani na nchi jirani. Watu wangemiminika Chato na kuchangamsha shughuli za maendeleo.

Kuna Ziwa Viktoria. Angeweza kuwekeza kwenye kilimo cha samaki (kuzalisha samaki ndani ya vitalu vya Ziwani) ambacho kingewanufaisha watanzania wanaoishi Chato. Ajira zingepatikana, wafanyabiashara kutoka mikoa jirani na hata nchi jirani za Rwanda, Burundi na DRC wangefika Chato kufungasha mizigo. Angeweza kujenga Chuo Kikuu au hata matawi mawili matatu ya vyuo vikuu. Mji wa Iringa ni miongoni mwa miji iliyochangamshwa na uwepo vyuo vikuu. Chato ingechangamka pia.

Hayo yote yangewezekana kirahisi kutokana na nguvu aliyokuwa nayo kama Rais. Lakini nguvu ili iwe na tija sharti iambatane na akili.Halafu yangefuata hayo ya kujenga uwanja wa ndege na mahoteli kwa kuwa sasa watu wenye uwezo wa kuvitumia (labda) wangekuwapo.Lakini hawapo. Na sasa shirika la Ndege limesitisha safari za ndege Chato kwa sababu aliyekuwa anautumia uwanja wa ndege wa Chato hayupo. Nyasi zina tabia ya kuota hata juu ya zege. Baada ya muda kidogo ile hoteli ya nyota tano ambayo haijamalizika itabaki gofu. Uwanja wa mpira wa kisasa hautajengwa. Benki ya CRDB itaondoka kwa sababu wakazi wa Chato wanaoweka pesa benki ni walimu na watumishi wengine wa serikali - ambao wanatumia NMB.

Majengo mazuri ya mahakama na vituo vya polisi hayawezi kuchochea maendeleo.

Kuna suala la Hospitali kubwa ya kanda iliyojengwa Chato. Huduma za afya ni suala zuri lakini jengo pekee halitoshi. Huduma zitakapoanza zitapaswa kufanana na jengo lenyewe. Hata hivyo haikuwa lazima kujenga hospitali kubwa Chato kabla ya kuboresha huduma za zahanati (Primary Health Care) vijijini.

Hakuna maana ya kujenga hospitali kubwa eneo moja wakati zahanati katika vijiji mia au zaidi hazina ubora. Huduma za zahanati nyingi zikiwa bora, faida yake ni kubwa zaidi kuliko huduma ya hospitali kubwa moja. Kwahiyo, pamoja na hatua nzuri ya kujenga hospitali ile, naamini haikupaswa kuwa jambo la kwanza.

Magufuli hakuisaidia Chato kwasababu aliamini zaidi katika vitu (hardware) badala ya watu (Software). Angeanza kuwajenga watu kwa elimu na maarifa halafu akawajengea nyenzo za kuboresha elimu na maarifa yao; shule, vyuo, viwanda kwa ajili ya ajira, na mbinu zingine za kuvutia uwekezaji. Lakini wapi! Aliwaza matokeo badala ya mchakato. Alichojenga Chato kitabaki kuwa makazi ya popo na mijusi kwa sababu hakuna wa kukitumia.

Nawasilisha!

Dr Cyrilo Christopher
 
Tangu kuanza kwa mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu wa October mwaka huu, nimepata bahati ya kufuatilia kampeni za baadhi ya wagombea wetu wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa bahati mbaya kwenye baadhi ya mikutano ya kampeni ya baadhi ya wagombea, Kumekuwepo upotoshwaji mkubwa kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa katika mkoa wa Geita, unaoendelea kujengwa katika wilaya ya Chato.

Binafsi naamini sisi kama watanzania tunawajibu mkubwa wa kupima na kutafakari kwa umakini mkubwa tuhuma mbalimbali zitolewazo na baadhi ya wagombea dhidi ya wagombea wengine katika mikutano mbalimbali ya kampeni inayoendelea kwenye maeneo kadhaa hapa nchini.

Nadhani ipo haja ya sisi Watanzania, kuelewa umuhimu na faida za kiuchumi ( Economics Benefits) kwa uwanja wa ndege wa kimataifa Chato.

Kwanini uwanja wa ndege Chato?
Ukisoma ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2015- 2020 , ilieleza umuhimu wa serikali kuchukua hatua za makusudi katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii nchini,ili ifikapo mwaka 2020, Tanzania iwe na uwezo wa kupokea watalii wasiopungua 2,000,000 kwa mwaka toka watalii 1,200,000 ilivyokuwa mwaka 2014,hasa ukizingatia kuwa kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum ( WEF) iliyotolewa mwala 2014,ilionyesha Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi vya asili vya utalii baada ya Brazil.

Japokuwa kwenye ripoti nyingine ya 2019 kutoka World Economic forum ambayo utolewa kila baada ya miaka 5, imeonyesha Tanzania inashika nafasi ya 12 duniani na ya 1 kwa Afrika kwa kuwa na vivutio vingi vya asili vya utalii(Tumeshuka kwa nafasi 10)

Lakini pia ukisoma ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya 2020-2025, latika ukurasa wa 111, imeeleza lengo la serikali la kutaka kukuza sekta ya utalii, na kufikia kupokea watalii 5,000,000 kwa mwaka, ifikapo mwaka 2025, na kuongeza mapato ya utalii kutoka dola za kimarelani 2.6 billion mwaka 2020 hadi kufikia dola za kimarekani 6.0 bilionimwaka 2025

Na ni kwa nini utalii?
Sekta ya utalii Tanzania,ni moja ya sekta muhimu kabisa katika uchumi wa nchi yetu, kwani sekta hiyo ndio inayoongoza katika kuingiza fedha nyingi za kigeni kuliko sekta nyingine yeyote ile hapa Tanzania,Asilimia 25 ya fedha zote za kigeni( foreign currency) zinatokana na sekta ya utalii, Kwa mfano katika mwaka wa fedha wa 2018/ 2019 sekta ya utalii, iliingizia taifa takribani dola za kimarekani 2.4 bilioni( Tsh trilioni 5.2) pia katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 sekta ya utalii pekee, iliingiza takribani dola za kimarekani 2.6 billion ( Tsh trilioni 5.4 )

Lakini ukiangalia jumla ya thamani ya shughuli zote za kiuchumi hapa nchini, kwa maana ya pato ghafi la taifa( Gross Domestic product ), sekta ya utalii inachangia 17.6%, ya GDP

Lakini pia sekta ya utalii imetoa ajira za moja kwa moja takribani watu 6000 na ajira zisizo za moja kwa moja takribani watu 2,000,000

Sasa kwa Tanzania, ukanda pekee unaofanya vizuri katika utalii ni ukanda wa Kaskazini, ambapo unaopokea watalii wengi kuliko kanda zingine za utalii,kama, kanda za Kusini na Kanda ya Kaskazini magharibi, takribani 90% ya watalii wote wanaoingia hapa nchini wanaelekea ukanda wa Kaskazin

Sasa ili kufikia malengo ya kuongeza idadi ya watalii, serikali waliamua kufungua baadhi ya kanda zingine za utalii, kanda hizo ni Kanda ya Kusini( mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe,Songwe) ambapo Kitulo ilipandishwa hadhi na kuwa hifadhi ya Kitulo, na kanda ya Kaskazini magharibi yenye mikoa ya ( Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma)

Serikali walifanya nini kwa kanda ya Kaskazini magharibi?
Hatua ya kwanza waliofanya, ilikuwa ni kuyapandisha hadhi mapori tengefu ya Burigi, Biharamulo, Kimisi ,Ibanda, Rumanyika & Kyerwa na kuwa hifadhi za taifa( National parks)

1. Burigi- Chato National Park

2. Ibanda-Kyerwa National Park

3. Rumanyika-Karagwe National Park

Sasa ili kuweza kuvutia watalii waweze kufika Kwa urahisi zaidi katika hifadhi hizo, serikali waliona ipo haja ya kujenga uwanja mkubwa wa kinataifa wa ndege ulio karibu na maeneo hayo, ambapo watalii wataweza kufika kwa urahisi zaidi kuliko ilivyo sasa, ambapo kimsingi kunapatikana hifadhi ya tatu kwa ukubwa hapa Tanzania, hifadhi ya Burigi- Chato yenye ukubwa wa kilometa za mraba 4,702, ikitanguliwa na hifadhi za Serengeti na Sellou

Kwa hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa kukuza sekta ya utalii nchini, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato una manufaa makubwa sana katika kukuza uchumi wetu

Ngamanya Kitangalala Mwaswala
kngamanya@yahoo.com
This is a clear example of white elephant projects, crystal clear.
 
Tuzungumzie Umuhimu wa Chato International Airport Kwa Uchumi wa nchi yetu ya Tanzania
 
Hakuna kitu pale brother, ule ni U-Mabuntu Seseseko Kude Wazebanga. Currently return in investiment is approximate to zero. labda kwa baadae brother...Ile ni white elephant kama zilivyo projects nyingine alizoziacha akaenda zake yule Jamaa Katirii...
 
Back
Top Bottom