KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Kwako Mkuu wa Mkoa Arusha mteuliwa Ndg. Paul Makonda, ninakupongeza Kwa uteuzi wako ambao kimsingi umenipa furaha hususani Kwa kupelekwa mkoa ambao ni kitovu Kwa shughuli za utalii ndani ya nchi yetu.
Utalii ni Moja ya sekta tegemeo katika upatikanaji wa fedha za kigeni na upatikanaji wa ajira hivyo kama mazingira ya sekta hii yakiwa bora na ya kuhamasisha uchumi utakua sana.
Ndg. Makonda, ninafahamu uthubutu wako na uwezo wako kiuongozi unaweza kuwa ni motisha tosha ya kukuza utalii ndani ya Arusha. Kupitia mada yenye kichwa kinachosema Tumshauri Rais ateue vijana wasio na uzoefu lakini wana vipaji vya uongozi kwenye taasisi za Umma, hawa ni watu ' potential' sana niliwaelezea Kwa ufupi vijana wenye sifa kama zako ambao kwao matokeo ni jambo la msingi. Tunataka kuona matokeo kwenye sekta ya utalii hususani ndani ya Arusha kupitia wewe.
Kwa kuanza katika kukuza utalii na kuboresha mazingira ya utalii ndani Fanya yafuatayo:
Kwanza, anza Kwa kuonesha mfano. Wewe ni Moja ya watu ambao unafuatiliwa sana Kila siku kwenye vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii na sehemu mbalimbali. Ukianza Kwa kuonesha mfano wa kutembelea vivutio vya utalii na kuposti wengi wanaokufatilia watahasika zaidi na zaidi na kutamani kujionea wenyewe.
Pili, una ushawishi mkubwa mpaka Kwa wasanii na waigizaji wakubwa tumia ushawishi ulionao kuwashawishi kufanya matamasha ya utalii ndani ya Arusha hususani Ngorongoro.
Tatu, vijana wa Arusha wametumbukia kwenye ulevi wa kupindukia, matumizi ya bhangi na uendeshaji wa hovyo wa vyombo vya moto hususani pikipiki, haya yote yanatengeneza hofu Kwa wageni kuzuru jiji la Arusha. Utalii unahitaji mazingira ya utulivu na amani ,tunaomba hili ukalitizame.
Nne, tumia Kila njia, mbinu na mkakati kusaidia kutangaza utalii ndani ya Arusha sio tu hapa nchini bali hata nje ya nchi. Ukifanikiwa kuutangaza utalii ndani ya Arusha ka kuboresha mazingira bora ya utalii ,watanzania watajivunia uwepo wako zaidi.
Tano, simama kama wakala wa utalii ndani ya Arusha.
NB: Usikubali kushiriki siasa za Lema maana ni za kitoto sana ,atataka kukutoa kwenye mstari.