FAHAMU: Teknolojia ya IRON DOME inayotumiwa na taifa la ISRAEL kutungua makombora angani

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Iron Dome ni mfumo wa ulinzi wa kisasa wa anga ambao ni bora na mathubuti kwa dunia ya leo uliotengenezwa na Israel kwa msaada kiasi kutoka Marekani kwa lengo la kulinda dhidi ya makombora yaliyofyatuliwa kutoka kwenye maeneo ya adui.

1696874947357.jpg


Mfumo huu ulianza kutumika rasmi mwaka 2011 na umekuwa sehemu muhimu ya ulinzi wa Israel dhidi ya vitisho vya makombora.


1696874966159.jpg

Iron Dome inafanya kazi kwa njia ifuatayo:

Kuchunguza: Mfumo huu una vituo vya radar vilivyosambazwa kote nchini Israel. Vituo hivi vinachunguza anga kwa kutambua makombora yanayotoka upande gani wa adui. Mara tu kombora linapogundulika, taarifa zote kuhusu harakati za mwelekeo hupitishwa katika kituo cha udhibiti wa mfumo.

Uchambuzi: Kituo cha udhibiti wa mfumo hufanya uchambuzi wa mwelekeo na harakati za kombora, ikiwa ni pamoja na kujua ni tishio la moja kwa moja kwenda maeneo ya raia au lah, hivyo mfumo huu unaweza kutambua kama kombola limaelekea maeneo yenye watu au yasiyo na watu. Kwa kuzingatia taarifa hizi, uamuzi wa ikiwa kuangusha kombora hilo au lah hufanywa. Kama haliendi kwenye makazi ya watu basi mfumo huo uachana na kombora hilo.

Kutungua: Ikiwa uamuzi wa kuangusha kombora unafanywa, mfumo wa Iron Dome unatumia makombora ya kudungua angani ambayo yanasafirishwa kwa kasi na kurushwa kuelekea uelekeo wa kombora la adui. Makombora haya yana teknolojia ya kipekee inayowezesha kuyagundua na kuyashambulia makombora ya adui hewani. Mfumo huu ukigundua kombora lenye tishio kwa raia au maeneo ya watu, mara moja utuma makombora ambayo yataenda kugongana na kombora la Adui angani na kisha kulipuka huko huko angani.

Kugundua mabaki: Baada ya makombora ya Iron Dome kudungua kombora la adui, mfumo huu unafuatilia vipande vilivyosalia vya kombora hilo na kuhakikisha kuwa hayana uwezo wa kuleta madhara.

Screenshot_20231009-205113_1.jpg


Mfumo wa Iron Dome umethibitisha ufanisi wake katika kulinda maisha na mali za raia wa Israel dhidi ya vitisho vya makombora kutoka kwa makundi kama Hamas na Hezbollah. Hata hivyo, ni mfumo unaogharimu sana na hutumia rasilimali nyingi kwa kila kombora lililolengwa.

IRON DOME utumika kupambana na kutungua makombora ya umbali mfupi yani short range missiles. Huku kwa makombora ya masafa ya kati na masafa marefu (medium range and long range missiles) mfumo mwingine wa kujilinda ujulikanao kama ARROW SYSTEM hutumika kutungua na kuyaharibu makombora ya adui yakiwa angani. Hivyo mifumo hii miwili usaidia kulinda makazi ya watu dhidi ya mashambulizi ya makombora.
 
Sawa, lakini kinga kubwa ya kuzuia hayo makombora ni kukaa meza moja na kufanyika mazungumzo ya kidoplomasia.

Imagine nchi ina mfumo wa iron dome, lakini tunapata taarifa za mamia ya vifo kutika huko israel, si hilo tu, imeripotiwa kuwa maelfu ya waizrael wamejazana airport tayari kuikimbia nchi.

Sasa mpaka hayo yote yanatokea ujue hiyo irone dome, imezidiwa / ina fail sometimes nakupelekea mashambulizi kufanikiwa.

Kinga pekee ni maridhiano kidiplomasia tu.
 
Suluhisho la yote ni kukaa mezani na kla upande utambue haki za mwenzake
 
Kati ya makombora 100 inangusha 20 tu, hizo ni prolaganda za marekani isreael is over rated kijeshi
Umeniwahi,hiyo ni takataka isiyo na maana na inaweza fanya kazi Kwa wanamgambo dizaini ya Hamas ambao hutumia makombora ya kienyeji kushambulia na hawana location nyingi za kurusha.

Wakati wanauliwa watu zaidi ya 700 hiyo Iron dome Kwa nini haikugundua?

Nchi kama Iran yenye multiple launchers kutokea kwenye ndege,majini,ardhini hicho kitakataka kitadungua yapi? Tena ya masafa marefu na yenye Nguvu zaidi.

Russia yenyewe na kujigamba kote ila drones zinaingia Hadi Moscow na Yale mavyuma Yao ya s6 and such takataka yapo yanashangaa tuu.
 
Kati ya makombora 100 inangusha 20 tu, hizo ni prolaganda za marekani isreael is over rated kijeshi
Kuna sababu zinazofanya hayo mengine 80 yaachwe kwanza ni kama hayaendi kupiga makazi ya watu au walipo watu, lakini kama hayaendi kwa watu basi yaanachwa tu... Huenda hayo 80 hayakulenga maeneo ya watu au walipo watu.
 
Suluhisho la yote ni kukaa mezani na kla upande utambue haki za mwenzake
Ni kweli lazima ifikie makubaliano, hapo isreal imasha jua iko safe kabisa, lisha ya kua wamezingira Gaza kws miaka 10 sasa ( open prison) ila wameweza kupingwa je wangeweza kupata mahusiano ya nje hali ingekua je?
 
Umeniwahi,hiyo ni takataka isiyo na maana na inaweza fanya kazi Kwa wanamgambo dizaini ya Hamas ambao hutumia makombora ya kienyeji kushambulia na hawana location nyingi za kurusha...
Shida yenu mnasoma habari juu juu... Nimekwambia Iron Dome inashughulikia makombora yanakwenda kwenye makazi ya watu tu tena makombora ya umbali mfupi.

Hivyo kama kombora halina madhara ya moja kwa moja kwa watu linaachwa, kazi ya Iron Dome ni kulinda watu wasipigwe na makombora, lakini kama kombora linaenda kwenye makazi yasio na watu linaachwa. Hapa tunaongelea makombora ya angani na si ya chini kama yale ya mkono ya kubeba begani.

Pili hamasi wao vifo vyao vingi ni vya kushambulia kwa ambushi, yani wanaenda na risasi na makombora ya chini au ya mkono ya begani.

Yaani walienda kwenye maeneo ya watu kama kwenye lile tamasha la watu wakaanza kumimina risasi na kuua watu na wengine kuwateka. Mauaji yao mengi ni yale ya ambush na sio ya makombora ya angani
 
Sawa, lakini kinga kubwa ya kuzuia hayo makombora ni kukaa meza moja na kufanyika mazungumzo ya kidoplomasia.

Imagine nchi ina mfumo wa iron dome, lakini tunapata taarifa za mamia ya vifo kutika huko israel, si hilo tu, imeripotiwa kuwa maelfu ya waizrael wamejazana airport tayari kuikimbia nchi...
Sio kwamba IRON DOME imezidiwa bali ni kuwa Hamas wamaefanya shambulio kwa kuingia moja kwa moja kwenye makazi ya watu na kupiga makombora ya chini kwa chini yale ya kubeba kwenye mabega, pia wamevamia mikusanyiko ya watu na kwemye Tamasha la mziki, sasa wewe unataka IRON DOME nayo iende kwenye Tamasha? Kazi ya Iron Dome ni kulinda mashambulio ya anga tu ya makombora na sio risasi au makombora ya mabegani

Pili watu wanaondoka ili kutoipa serikali mzigo wa kuwalinda... Wananchi wakibaki eneo la tukio serikali na jeshi yanakuwa na wakati mgumu wa kupambana na maadui wakati huo huo kuwalinda... Kwa hiyo jambo la kwanza vitani uwa ni kuwaondoa raia (Evacuation) kisha mnabaki vidume mnafuana vilivyo
 
Umeniwahi,hiyo ni takataka isiyo na maana na inaweza fanya kazi Kwa wanamgambo dizaini ya Hamas ambao hutumia makombora ya kienyeji kushambulia na hawana location nyingi za kurusha.

Wakati wanauliwa watu zaidi ya 700 hiyo Iron dome Kwa nini haikugundua?

Nchi kama Iran yenye multiple launchers kutokea kwenye ndege,majini,ardhini hicho kitakataka kitadungua yapi? Tena ya masafa marefu na yenye Nguvu zaidi.

Russia yenyewe na kujigamba kote ila drones zinaingia Hadi Moscow na Yale mavyuma Yao ya s6 and such takataka yapo yanashangaa tuu.
Nakusahihisha tu katika hao 700 zaidi ya 250 waliuwawa kwa risasi walipokuwa kwenye sherehe.
Asante
 
Nakusahihisha tu katika hao 700 zaidi ya 250 waliuwawa kwa risasi walipokuwa kwenye sherehe.
Asante
Safi kabisa, hao ni wa kwenye sherehe, bado hujahesabu wa mitaani... Maana Hamasa walivuka border na kuingia mitaani kwenye makazi ya watu na kumimina risasi kwenye magari na kwa watu waliokutana nao na kuwateka wengine... Ndio maana nasema Hamas mashambulio yao mengi ni ya kupiga watu risasi na sio ya makombora ya angani na wao wanajua kabisa wakitumia makombora ya angani hayatafanya kazi kwa sababu kuna Iron Dome
 
Back
Top Bottom