Fahamu kuhusu Uchawi wa Mapenzi (Limbwata)

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Nasikia kuwa dawa hii huwa baadhi ya wake huwalisha waume zao, na baada ya hapo mume huwa kama zuzu analoambiwa hana upinzani yaani chochote kile kutoka kwa mkewe huwa anakifuata.

Je dawa hii mtu anaweza kumpa mkewe au kumlisha mkewe ? Na ni kweli ipo na inafanya kazi kama nilivyojaribu kusema au nilivyosikia!
=========================
Wadau kwa heshima na taadhima naomba mawazo yenu kuuhusu ili swala la limbwata! ni juzi tu hapa ninapo ishi kunajamaa wanasema amepewa limbwata! kwa vitendo vyake anavyo vifanya katika jamii.

Kikubwa ni kwamba anampenda mpenzi wake sana kwa kumfanyia mambo adimu kama kumfulia nguo za ndani, kuwachukia ndugu zake wanapo muomba msaada na wanaendelea kusema eti huyo mpenzi wake ana weza enda kwa ma boyfriend zake aka kaa hata wiki moja na pindi anaporudi mumewe huyo upokea bila kumuuliza chochote!

Kuna siku mkewe alimkuta akiongea na wapangaji hapo wanapo ishi aka mfokea mbele ya wapangaji kwamba ameanza lini tabia za kuongea na majirani na kudiriki kutoka nje? jamaa akaomba msamaha na kurudi ndani haraka.

Jamaa ni msomi mzuri na anakazi nzuri...jamani huu sio uwongo ni kitu ambacho nimesimuliwa. Na nimeambiwa eti mpaka huyo mwanamke achomoe izo naniii ndo jamaa anaweza pata ufahamu wake. Sasa wadau hivi kweli limbwata lipo? naomba kuwakilisha.

Fill free kusema chochote unachacho kijua au kukifahamu.
==============================
Mara nyingine mtu akiishi maisha ya kujali familia unaambiwa amelishwa Limbwata aidha na Ndugu au Marafiki.

Consider the following, LIMBWATA facts

A) If LIMBWATA is to allow your wife to be a partner and participant informulating the family budget, then I support it, becoz women are wiser spenders than men.

B) If LIMBWATA means that the family money is used by Mama Watoto to purchase stuff at Kariakoo rather than being drunk by the husband at RIVERSIDE or GAZA ONE then I support that men are affected by LIMBWATAz

C) If a LIMBWATAz husband is the one who won't spend ALL the monthly salary with NYUMBA NDOGO or at KITIMOTO Bar (while his KIDS starve) then HONGERA to all LIMBWATAz husbands.

E) If LIMBWATA means that a MUME spends quality time with his MKE and WATOTO, instead of engaging in dubious investments where he is CONNED then; "Watu Walishwe LIMBWATA forever".

f) If LIMBWATA means that when MKEO is SICK you help her with work, that when she is over burdened you extend a helping hand then LONG LIVE LIMBWATAz.

G) If LIMBWATA means that you DON'T BEAT UP your wife, that you seek assistance from your wife for they are called helpers when you have tried all the altanertives in vain, then LIMBWATAz LIDUMU MAISHA .

H) If LIMBWATA means that you treat your wife as a human being, that you are polite, don't bark at her like a dog, DONT growl at her like a hyena,consider that after work she is as stressed as you are then VIVA LIMBWATAz.

I) If LIMBWATA means that you are at home after work, and that your wife and kids are your next of KIN then HONGERA WALE WOTE WALILISHWA LIMBWATA.

Na ukae hivyo hivyo kaka! KAMA UMELISHWA LIMBWATA, WEWE NI BINGWA!!

Tell your WIFE to add More LIMBWATA
=============================
Imeandaliwa na John Haule wa Rumours Africa

Kama ilivyo kawaida ya Rumours Africa, kila siku ipo kazini kukuletea minong'ono ya mambo yaliyo jificha katika jamii yetu bila kujali aina ya minong'ono hiyo kwa kuwa lengo la Rumours Africa ni kutafuta tu suluhisho la masuala mbalimbali ya kijamii kwa ujumla wake.

Wiki hii nilitembelea kituo cha tiba asili maeneo ya Temeke. Kituo hiki kimejikita zaidi katika masuala ya LisheTiba na kinaitwa "MiracleFoods" kama shughuli za kituo hicho kilivyo. Watanzania siku hizi ni wastaarabu na kama kawaida nilimpigia simu mmiliki wa kituo hicho cha tiba aitwaye Dr. Febronia Kalongoti ambaye wengi wenu mnamjua huyu mama maarufu kwa vipindi katika runinga na magazeti mbalimbali nchini.

Yeye alifurahi sana kusikia azma yangu ya kumtembelea kwa kuwa kwanza mimi ni mwandishi mwenza wake katika gazeti maarufu sana la waganga na madakitari nchini liitwalo TABIBU, lakini pia mimi ni mtaalamu mwenza katika suala zima la tiba asili na uchawi baridi.

Jana ndio tulikutana. Maongezi yetu ya awali yalizama sana katika matatizo ya kiafya yanayowakabili watanzania na namna anavyo kabiliana nayo. Alionyesha umahiri mkubwa sana katika kuonyesha kuwa anazo LisheTiba bora zenye uhakika wa kumaliza matatizo ya kiafya kwa watanzania.

"Watanzania hawajui kula!" alianza kwa kusema. "Wakiwa na pesa basi wanashindana kurosti bila kujua kuwa nyama hupandisha hasira na uhayawani, baada ya siku chache unasikia mke aliyekuwa bingwa wa kurosti mtaani kaachika kwa mume wake… Hii ni hatari, lakini wenye akili huja hapa kuchukua Limbwata na kwa kweli linawasaidia" alimalizia Dr. Kalongoti.

Swali langu la kwanza lilikuwa nataka kujua limbwata hasa ni nini? Akajibu, "Swali zuri sana Haule. Limbwata ni jina tu ambalo kwa sasa lina tafsiri ya kutishia waume wajeuri lakini kwa undani wake limbwata ni chakula cha kila mtu, na Tanzania ingependeza sana iwapo kila mtu angekula chakula hiki kiitwacho limbwata."

Akaendelea. "Labda tu nikuambie ukweli kuwa jikoni ni maabara ya kutengeneza kemikali zenye uwezo wa kumjenga binadamu, kumbomoa, kumuua, kumbadili tabia na kadha wa kadha. Watu wote wenye akili timamu huajiri mpishi mwenye akili na taaluma ya upishi kwa sababu hii. Mpishi asiyejua kabichi ina magnesium kwa wingi basi atamfanya anayempikia akala awe mpole sana na kama hajui kuwa nyama inaua kuliko kumjenga mtu basi atakuwa hajui anampunguzia maisha mlaji wake kwa kuwa takwimu zinaonyesha wala nyama wote walikufa kwenye miaka ya 60 na waliobaki wapo hoi kwa maradhi ya moyo, figo, ini, na saratani za aina tofauti."

Msomaji wangu, Dr. Kalongoti alikuwa ameniacha hoi. Amenifunulia mengi, lakini bado sijajua limbwata ni kitu gani hasa. Nilirudia tena swali langu. "Ina maana sasa limbwata lina sura gani katika haya uliyonieleza?" Akameza mate, na kunigeukia tena. "Limbwata Dr. Haule ni mapishi. Ni mapishi ambayo humfanya mlaji apate utulivu wa ubongo kutokana na vitamin, madini, virutubisho pamoja na Amino acids zinazopatikana katika mlo unaomwandalia tu basi…

Utamwona tu mlaji wako kama alikuwa na tabia ya ukali inapotea taratibu na kama alikuwa na wasiwasi utaona unamtoka, kama alikuwa mwoga basi utaona anapata ujasiri lakini utafaidi sana kumwona mtu aliyekuwa hajui kuongea taratibu akiwa mkimya sana!" hili ndo jibu la Dr. Kalongoti kuhusu limbwata jamani.

Maswali lukuki sasa yalianza kujijenga akilini mwangu. Haraka haraka tu nilitaka kujua usalama wa walaji limbwata ukoje? Akajibu "Limbwata sio sumu wala uchawi, narudia tena Dr. Haule. Limbwata ni chakula tu ambacho kipo sokoni kinauzwa na kila mtu ananunua na anakula lakini bila kujua kama ni limbwata.

Hivyo limbwata kwa kuwa ni chakula na lishetiba kwa ajili ya wasiwasi, ukali, hofu nk basi kila mtu anapaswa kujua na kwa kweli mama ntilie wote wanapaswa kupata elimu hii maana kwa kutojua wanaandaa kemikali gani pale katika maabara iitwayo jiko, na inawabadilisha walaji vipi na kwa kiasi gani wanakuwa hawajui kuwa wanaandaa vifo baridi vya walaji bila kukusudia."

Dr. Kalongoti akamalizia kwa kusema hivi "Limbwata ni Domestic Science" tu na kila mpishi anatakiwa aijue tena hasa wanawake wa Tanzania ambao wamebeba jukumu la upishi kwa kiasi kikubwa sana. Hapa sigawi dawa, ila huwa natoa mafunzo ya kumpikia mtu mkorofi asiyetulia na hata familia nzima isiwe na mapepe ukala hasara. "Wanakuja hapa tunaongelea shida zao, tunakubaliana, wanalipa kuja kujifunza na kupata mafunzo haya adimu nchini."

Rumours Africa dukani kwetu tunazo limbwata za kizungu. Miaka mingi tu watu wanakuja na tuna wasaidia sana kuwatuliza akili wenza wao. Wengine walifuata hata kwa ajili yao wenyewe kwa kuwa hakuna kinachofanyika ukimeza dawa hizi zaidi ya kukutuliza ubongo na kukurejeshea uwezo wako wa asili kukumbuka na kutunza kumbukumbu zako kwa usahihi zaidi. Dawa zetu ni kutoka kampuni ya kutengeneza dawa lishe ya Nativa South Africa ambao nao wameleta hizi "stress killer" zikahakikiwa na TFDA na sasa ninazo hapa dukani muda wowote ukihitaji njoo.

Hii ni njia ya kupata limbwata haraka kwa waliozidiwa sana. Lakini kama utapenda kujua namna ya kutengeneza jiko lako liwe kiwanda cha kupika Limbwata basi usikonde. Njoo tuongee, tukubaliane, ulipie na uanze kujifunza namna ya kutengeneza limbwata.

Limbwata si SUMU. Nilichogundua ni kuwa Limbwata ni "STRESS KILLER" ambayo kila mtu anaihitaji kwa ajili ya uhakika na umakini wa masuala ya maisha iwe kazi, elimu n.k.

Asanteni kwa kunisoma.

Chanzo; JukwaaHuru

=============================
Wanawake / Mabinti baadhi wamekuwa watumiaji wazuri wa limbwata kama sehemu ya kuongeza chachu ktk mahusiano yao ya mapenzi. Zifuatazo ni baadhi ya teknolojia maarufu ama niseme pendwa za limbwata. Waweza kuongeza yoyote ile uijuayo:

Kinyama

Hii kitu kuna siku Mkuu MziziMkavu aliielezea vizuri tu. Katika hili, kipande kidogo cha nyama mfano wa mnofu mmoja wa "mshikaki" huwekwa katika maku ya mtaka tiba, kwa muda wa siku kadhaa kulingana na masharti ama maelekezo ya mganga husika "fundi", baadae kinyama hiki hupikwa na sehemu nyingine ya kitoweo kama mboga na kuliwa. Mlengwa wa limbwata ataathirika mara tu baada ya kula mlo uliohusiha mboga yenye kinyama hiki! Wanaoipenda njia hii wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alielishwa kinyama

Maji ya mchele:

Hii ni aina nyingine ya teknolojia ya limbwata. Ni kwamba kwa kutumia njia hii, maji ya kawaida hupelekwa kwa mganga kwa ajili ya kazi husika, na kisha maji hayo hurudishwa nyumbani, mwanamke mhusika huyatumia maji ya dawa haya kuoshea maku na baadae huyatumia kuoshea mchele ama hata kupikia kabisa! Limbwata hili hufanya kazi kwa mlengwa baada ya mlengwa kula chakula kilichopikwa kwa maji tajwa! Wanaoipenda njia hii wanasema ni ngumu sana kumuagua mwanaume alienyeshwa maji hayo, na kwamba ili kumuagua lazima apatikane fundi Yule Yule aliefanya yake!

Kisomo:

Nyingine. Hii haisemwi sana, ni kama siri kubwa, huwa haijulikani hasa ni aina gani ya "kisomo" hufanyika lakini wateja na wafuasi wa limbwata la aina hii wanakiri kuwa, mwanaume aliesomewa (msomaji ni fundi "mganga") huwa ni zaidi ya kondoo, kwa maana ya kuwa maisha yake yote yaliyobaki yanakuwa ni yale ya "ndio mzee" kwa mwanamke alietengeneza! Wanaoipenda njia hii wanasema sio nzuri sana kwa vile fundi mwingine yoyote anaweza akafanya kisomo kinyume.

Kifaranga:

Hapa mwanamke mhitaji huagizwa na fundi kupeleka kifaranga, na mara nyingi ni cha kuku. Fundi humfanyia kazi Kifaranga huyu katika karakana yake, namna fundi anavodili na kifaranga hiki ndio ndio kazi halisi ya kumuinamisha mme ama mpenzi wa mtu, kifaranga huyu hubaki ktk himaya ya fundi kwa maisha yake yote, na namna kifaranga huyu anavolelewa na huyu fundi, na kufuata anavotaka mfugaji, ndio hivo hivo mlengwa atakavopelekwapelekwa! Njia hii inachangamoto moja kubwa, usalama na uhai wa kifaranga huwa ni tatizo, na iko subjected to frequent updates!

Jina kuning'nizwa juu ya mti:

Hii inafanana na kisomo. Tofauti ni kwamba, baada ya fundi kufanya kazi yake, huku jina la mlengwa likiwa limenuiwa, karatasi lililoandikwa jina hili (jina la mwanaume mlengwa) huenda kuning'inizwa katika moja ya mti mrefu ambao ni sharti uwe mbali na wanapoishi wapenzi ama wanandoa hao, wakati mwingine inahusisha mkoa mmoja hadi mwingine! Wanasema kusipokuwepo na upepo, mwanaume huwa mjanja mjanja, lkn upepo ukivuma kidogo tu, mwanaume huyu akili huruka na kumuwaza aliemtengeneza! Ili upone kutoka katika limbwata hili, lazima huu mti utafutwe na kikaratasi kikatwe, ndio utapona!

Kaburi la mtoto

Hapa kuna vitu hufukiwa. Kama ilivo limbwata la hapo juu, limbwata hili linahusisha madawa na majina ya mlengwa. Kaburi husika hutafutwa maeneo ya mbali sana. Madawa na majina ya mlengwa hufukiwa katika kaburi la mtoto. Hapa huponi mpaka kaburi lipatikane na kazi ifanyike hap!

Unyayo kucha ama kinywele:
Hapa kuna mchanganyiko wa ufundi unaotumika. Wapo wanaotumia mchanga wa unyayo, wapo wanaotumia kipande cha v.u.z.i, wengine hutumia hata c.h.u.p.i ya mlengwa, lakini yote kwa yote ni kwamba fundi atadili na mlengwa kutumia aina mojawapo ya nyenzo hizi! Mafundi wengi inasemekana ni wataalamu wa kuagua wahanga wa njia hii!
 
hmm! kama unataka kujua kama unaweza kumpa mkeo ,kanunue then ujaribu kwake uone kama itafanya kazi,usiogope kujaribu,kujaribu ndio kujifunza kwenyewe huko.

naona ndugu yangu mkeo amekushinda hadi unataka kumuekea madawa? mlete kwangu nimpatie limbwata origino.
progress.gif
 
Limbwata ni fikra potofu kama zilivyo fikra zingine potofu. Wapo wanaotumia fikra hii kujinufaisha na hawa utawakuta huko kwenye mitaa ya watu waliochoka wakiwa na mbango makubwa kuelezea tiba wanazo toa. Nenda kawaulize, limbwata ni mojawapo ya huduma wanayoitoa na inawapa kuendelea kuwepo.
 
B: If the husband is the one who look for money then there is logic if some is spent on his own interrests. Men who spend money this way has motivation to look for more and are hardworkers and they usually are not only satisfied by single source of income. In fact the type of men you are discouraging are the ones who are entrepreneurs and hardworkers.

Money earned only for wife and family is useless. MEN OR WHOEVER WINS THE BREAD HAS TO SPEND ALSO ON THEIR OTHER INTERRESTS TO KEEP GOING!!!
 
watu wanajidai lakini limbwata lipo

watu wa kanda ya ziwa ndio mchezo wao sana wanaume/wanawake
na kila mara mtu inabidi aka renew kwa mganga, kwa hiyo hela pia zinakua zinaenda kwa mganga. wa mama wa mjini maarufu ndio mchezo wao siku hizi hata masista duu.

na limbwata ndio linawapa waganga hela ya kuishi mjini limbwata ni kama sigara kwenye duka kwa ajili wanasiasa ni wachache kama vijisenti, wateja wengi ni wanawake
 
Mimi pia naamini hakuna dawa kama hiyo. Nadhani ni concept tu ila wajanja wanaitumia njia hii kuvuna pesa za wajinga.
Karibu uswazi,then you will know kama limbwata lipo or not.

HII KITU IPO inaexist ,siyo hadithi na zidi kumwomba MUNGU isijepiga hodi nyumbani kwako.IBAKIE KUWA HADITHI YA KUSIMULIWA.

KATIKA NDOA ,WASHAURI NI WENGI ATI...
 
Jamani akina mama na akina dada wengi siku hizi wanaamini sana kwa mambo ya kumbana mke/mchumba/boyfriend/sugar daddy, you name all!! Zamani tujisikia kwa makabila machache kama yale ya Unyamwezi na usukumani lakini sasa ni kwa almost Tz nzima, yaani hata wachaga ambao walitegemewa kutojishughulisha na mambo haya, wamo siku hizi.

Ninachotaka kusema ni kuwa kwa nini upeleke pesa yako kwa maganga ili kutafuta kupendwa au kutumbua hela za mwanaume!!! Tafuta za kwako, kula jasho lako. Ukienda uswahilini ndiyo utajua mambo mengo ya haya nisemayo. Yaani hizi ni hadithi za wamama wa nyumbani wengi, hata wa ofisi wamo, cha kushangaza hata wasomi, aibu.

Limbwata unalo mwenyewe tu. Kama mume ni mkali sana, wewe uwe mpole na mnyenyekevu na mume huyo ni lazima atabadilika tu. Zidisha mapenzi kwa vitendo (maneno yako hasa), yale ya kule nani hii ni ya mwisho kabisa (hapa mnanipata???). Kwa akina mama hebu jaribu siku moja (kama hufanyi kwa sasa) upike chakula kizuri sana, mpokee mume wako kwa upendo na maneno ya kufariji, kaeni kidogo sitting room mpige story za utani, tena mkumbushe alivyokuwa anakulilia wakati wa uchumba, mkiondoka kulala mikono kiunoni hapo ndo koridoni mnaelekea chumbani. Mkifika hapo chumbani haki ya nani......Fanya hivyo kila wakati utaona mume wako atabadilika. Kama alikuwa anarudi saa za Chenge basi atakuwa anawahi Dinner, Kama alikuwa arudi anakaa sitting room anasoma gazeti na ku watch Tv, basi atakuwa anakuita darling maliza basi haraka huko jikoni uje upumzike hapa. Kama alikuwa ana......... yaani utabadilisha yote. Na wanaume tusichoke kuwabembeleza na kuwasifiwa wake zetu, hii ni fimbo kuu ya limbwata, kila huduma itakuwa exceled.!!!! Mwe msiinite baba/mama wa kitchen party!!!!
 
Ngojeni niwaambie Libwata lipo,
ni hivi mimi nimewahi kushuhudia haya mambo tena hata siku hizi wanaume wanawapa wanawake wao limbwata siyo wanawake tu wanawapa.
1. Ni hivi kuna limbwata ( dawa za kienyeji) ambalo mwanaume anapewa ili awe mjinga kila analoaambiwa na mwanamke wake anakubalia yani anakuwa mjinga kabisa hiyo ni mbaya
2. Kuna wanaume au wanawake ambao hawajatulia kwa hiyo wanawapa wapenzi wao ili watulie waachane na wanawake au wanaume wa nje. huyu hana nia mbaya hampelekeshi wala hamsumbui (huyu kinachomsumbua ni wivu uliopitiliza) na kwa upande mwingine anamsaidi mwenzake.
TATIZO
Tatizo ni kwamba haya mambo ni ya muda tu yanaisha na yakiisha hali inakuwa mbaya zaidi kuliko mwanzo.
Na inakufanya uwe na wasiwasi muda wote maana mtu akija na mawazo yake sijui kakorofishwa kazini unaanza kuwaza sijui dawa imeishakwa hiyo hutakuwa na amani.
 
Jamani niwaambie limbwata lipo, tena muwe makini kabisa na haya mambo!

Kuna ishu moja ilitokea huko mkoani Iringa mama mmoja aliamua kumpa mume wake limbwata kwa vile alikuwa anapata hela nyingi ila hatulii nyumbani kabisa.

baada ya kumuwekea hayo madawa aliyopewa kwa mganga mwanaume alitulia ndani kupitiliza,akawa haendi kufanya biashara zake,akawa hataki hata kutoka ndani ya nyumba,kunya humo humo,kukojoa humo humo,hata kuoga,baada ya miezi 3 kupita hela zikaisha mwanamke akaanza kuhangaika,alivyorudi kwa mganga ,mganga akamwambia yeye mwenyewe hawezi kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida kwa sababu alizidisha dawa tofauti na kipimo alichoambiwa na mganga.

ilikuwa shughuli pevu ndugu wa mwanaume walivyokuja kugundua ndugu yao yupo ndani miezi 3, wao walifikiri kasafiri, walipoenda kumtembelea ilikuwa shughuli kumtoa ndani,alikuwa anaonekana ana akili timamu ila hataki kutoka nje ya nyumba, walisaidiana wanaume kama 10 hivi ndio wakafanikiwa kumtoa nje.

yule mwanamke akachapwa viboko akamtaja mganga aliyempa dawa, nae akakamatwa na wanakijiji ila tatizo alikuwa hawezi kumrudisha kwenye hali ya kawaida. mpaka mzee mmoja alivyojitokeza akampa jamaa midawa ya miti shamba akawa kawaida kabisa.

ilibidi amfukuze mke wake na mganga akalipa faini ofisi ya kijiji.

Kwa hiyo wana jamii hii ishu acheni masihara ipo.Ni kuomba Mungu uliye nae asije kukuwekea hilo Limbwata la ukweli.Ila mimi mwenyewe naona hii kitu sio nzuri hata kidogo.
 
Nadhani kuna watu wameingiwa na uzungu sana hata wanasahau mila za kwao, unadhani kwa nini ndoa za zamani zilikuwa zinadumu sana?mje mtutafute wataalam tuwafanyie limbwata. Kama kuna msichana narudia msichana haamini kama kuna limbwata ani PM anipe details zake halafu atakuja kuwahadithia wenzake wanao bisha.
 
Back
Top Bottom