Fahamu kuhusu gari aina ya Land Rover Freelander

consigliori

JF-Expert Member
Mar 29, 2010
392
89
2002_land_rover_freelander_4_dr_se_awd_suv-pic-2803.jpeg
Heshima mbele wakuu,

Nataka kununua used Freelander, lakini watu wengi niliowauliza wanasema eti ni gari mbovu. sina utaalamu wa magari hivyo naomba ushauri kwa mtu yoyote anayeijua vizuri freelander.
Natanguliza shukrani.
==
SAME CASES:
Poleni wanaJF na shuruba zote za mwaka 2012.
Nawashakuru wanaJF mmekuwa mhimili mkubwa wa kazi zangu na maisha yangu kwa ujumla.

Kuna hizi gari aina ya Land Rover Freelender, kuna mwanajf mwenzangu anataka aniuzie, sinauzoefu nazo katika upatikanaji wa spea, utumiaji wa mafuta, uimara wake nk. Naombeni wana jf mnisaidie kuzifahamu vizuri.

Ahsanteni
---
Habari wanajamvi.

Hakuna gari nazipenda kama za kampuni ya landrover, na kwenye jamii hiyo, Freelander ndio chaguo langu la kwanza likifuatiwa na discovery hasa td5.

Nimeshaendesha sana 110 ya diesel zile za mwanzo, defender tdi, na range rover 4.0 ya mwaka 1998, (ila si freelander na discovery). Hizo zote nilizoendesha hazijawahi kusumbua engine kiasi cha kuitwa pasua kichwa, au niseme hazijasumbua kabisa.

Labda range rover inatesa kidogo system yake ya air suspension (au busta). Wengine hufunga suspension za kawaida ili kuondokana na hilo tatizo. Pia bei ya spare hasa za range rover pengine ni juu kidogo kuliko magari tuliyozoea kama ya Toyota

KUHUSU FREELANDER

Kama nilivyotangulia kusema ni gari ambazo nazipenda sana, kwa sasa nina toyota mark II ila ndoto yangu ni kumiliki freelander au discovery.

ILA SASA, habari nazosikia kuhusu freelander hazinitii moyo kabisa, sijui kama ishu ni mafundi hawazijui au ni kweli hizi gari ni pasua kichwa na zikianza kukutesa tiba ni kubadili engine tu kuweka ya rav 4 (3s).

Kikubwa naomba kwa wajuzi na wazoefu wa magari haya, mnipe mawazo yenu na ushauri. Natanguliza shukrani
---
Wakuu habari!

Naombeni msaada wa kujua machache kuhusu hii gari LandRover Freelander.

1. Kwa kulinganisha na Suzuki Escudo na Rav 4. Ni ipi inafaa kwa kuhimili mikiki ya barabara zetu?

2. Vipi upatikanaji wa spare zake kwa hapa bongo? Na je spare zake ni gharama au bei ni za kawaida?

3. Ipi ni bora? Inayotumia Diesel au Petrol?

Naomba ushauri na mengine ambayo sijauliza kuhusu hii gari.

Natanguliza shukrani zangu.

==
MAONI YA WADAU:
Freelander kimeo,niliwahi kuwa nalo kikavunjika kioo cha nyuma. Ilikuwa shughuli kukipata,Nairobi kilikuwa kinauzwa Kshs 99999/-. Nikabahatisha Kampala kwa bei ya chini kidogo. Labda kama una uwezo mkubwa
---
Kiongozi Freelander ni gari isiyopenda shida! Kwa sababu hii basi ikiwa wewe ni mwenzangu na mimi unayefukia ramps kwa mwendo wa kumbeep Israel tegemea kulipaki juu ya mawe likiwa jipya! Spea zake ziko juu
---
Mie pia sikushauri ununue Freelander. Mbali na spea na mafundi kushindwa kuzimudu.
Pia ujue ukinunua huna wa kumuuzia tena,labda ukubali kuuza kwa bei ya bodaboda.

Na ndio maana hata kwenye Yard nyingi Gari hizi huzikuti.

Ila kama unataka Kujaribu,huku ipo inauzwa 7m old model,zile zilizotolewa serikalini.
Ina miaka 8 haijapata wa kununua
---
Mie pia nina miliki freelander ya mwaka 1998, gari ni kichefuchefu hicho spare muhimu hazipatikani hata kama ukieenda autorover au morogoro stores ngumu sana wanazo chache na sio zote muhimu, option yako kubwa ni kwenye used Tabata dampo na Sinza darajani kwa mbele. Tena bei zipo juu iwe mpya ama used.

Ukipata Manual Diesel atleast machine inakaa lakini itakusumbua within three years.
---
Achana na hio gari mkuu,unless ununue Freelander td 4 2000 ambazo ni za kuanzia 2003 kwenda juu ambapo waliachana na engine kimeo za Rover K-series ambazo kuunguza head gasket ikiwa ndio ugonjwa wake mkuu na wakaanza kutumia engine za BMW's 2.0 common rail TD4 engine.

Inshort hilo gari hua ni kimeo tu,kuna watu wametoa engine zilizokuja na hizo freelander na kuweka engine za rav 4 ambazo ni 3S gari zinafanya kazi lkn performance yake ni ya kuunga unga tu.
 
kwa nini usifikirie kununua gari under Toyota logo unakuwa na uhakika wa spare na mahali popote pale.
 
Nunua kitu toyota kulger, nzuri kuliko freelander. freelander itakutesa bure, zina matatizo ya engine pamoja na mfumo wa umeme.
 
consgrioli, ushauri wa ujumla ni kununua magari ya TOYOTA, maana vipuri vyake vinapatikana kiurahisi (new na used spares), halafu mafundi hata wa uchochoroni wanaziwezea kufanya matengenezo/service, lakini kama LADHA yako ipo kwa Freelander basi nunua hiyo ambayo kitu roho inapenda mkuu,then utapata uzoefu ukishaimiliki.
 
Freelander kimeo,niliwahi kuwa nalo kikavunjika kioo cha nyuma. Ilikuwa shughuli kukipata,Nairobi kilikuwa kinauzwa Kshs 99999/-. Nikabahatisha Kampala kwa bei ya chini kidogo. Labda kama una uwezo mkubwa
 
poleni wanajf na shuruba zooote za mwaka 2012.
Nawashakuru wanajf mmekuwa mhimili mkubwa wa kazi zangu na maisha yangu kwa ujumla.

Kuna hizi gari aina ya landrover freelender, kuna mwanajf mwenzangu anataka aniuzie, sinauzoefu nazo katika upatikanaji wa spea, utumiaji wa mafuta, uimara wake nk. Naombeni wana jf mnisaidie kuzifahamu vizuri.

Ahsanteni
 
spea za landrover siyo issue zimejaa tele na bei yake ni poa nenda libya street kuna maduka ya spea za magari ya ulaya very cheap you cant imagine
 
spea za landrover siyo issue zimejaa tele na bei yake ni poa nenda libya street kuna maduka ya spea za magari ya ulaya very cheap you cant imagine


nimekupata mkuu, vipi ubora wa gari aina hiii ukoje?
 
Tatizo lipo kwenye rejeta unaweza endesha gari rejeta likastop kufanya kazi nini kinachofata injini kuchemsha
 
Zile za mwanzo zilikuwa na matatizo sana (Fleelander 1) ....utabalisha head gasket sana na wakati mwingine cylinder head-hii ni 1.8L na 2.5 V6 petrol engines (Rover Engine). Lakini za baadae zenye BMW engine hazina shida.
 
rejeta kweli ina tatizo? tatizo linaeza kuvuja na sio kugoma kugoma rejeta ni water pump igome sio rejeta mkuu, wengi wetu tunatia maji kwenye rejeta halafu sio safi inapelekea kuziba hiyo rejeta
Tatizo lipo kwenye rejeta unaweza endesha gari rejeta likastop kufanya kazi nini kinachofata injini kuchemsha
 
Ninaamini hapa nitapata majibu mazuri. Mimi pia nilikuwa nahitaji sana kujuzwa juu ya uimara na upatikanaji vipuri kwa Freelander
 
Wataalam, naomba kujua kama Land Rover Freelander ni gari nzuri kwa matumizi ya kawaida hapa kwetu Tanzania.
 
Kama una uwezo wa kwenda kwenye garage za maana nunua, otherwise uswahilini kwa wagonganyundo watakwambia, "hizi gari mbovu saaaana badilisha injini"!!
 
Pointi yako nimeichukua mkuu, ngoja tusubiri wengine pia wanasemaje maana hizi Garage za maana kwa sasa hazihepukiki. Magari mengi hata Toyota za 2007 lazima utaenda kwenye garage ya maana tu kwani hata RAV4 ya 2007 haitengenezeki mtaani kwa wagonga nyundo.

Kama una uwezo wa kwenda kwenye garage za maana nunua, otherwise uswahilini kwa wagonganyundo watakwambia, "hizi gari mbovu saaaana badilisha injini"!!
 
Kiongozi Freelander ni gari isiyopenda shida! Kwa sababu hii basi ikiwa wewe ni mwenzangu na mimi unayefukia ramps kwa mwendo wa kumbeep Israel tegemea kulipaki juu ya mawe likiwa jipya! Spea zake ziko juu
 
Back
Top Bottom