Fahamu Jinsi ya Kumpatia Mtu Mtaji na Kumasaidia kukuza Biashara yake

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,532
Habari za wakati huu wadau
Ufuatao ni muendelezo wa mada niliyoandika siku kadhaa zilizopita yenye kichwa
- Jinsi ya kushiriki katika Uwekezaji Huria (Venture and Angel Investment)

Mada hii ni mtiririko wa mada kadhaa ambazo huwa naziandika mara kwa mara kwa lengo la kuchangia katika kushirikishana maarifa na taarifa.Lengo la mada hizi pia ni kuibua mijadala kuhusu fursa na changamoto katika biashara na ujasiriamali.Wakati naandaa mada ile nilikuwa nimepanga kuiendeleza kama mjadala na huu ni mundelezo wake.Mada ile haikuchangmka/kuchangamsha jukwaa hata hivyo ilinipa picha ya aina ya taifa na uchumi tulio nao.Katika muendezo huu ambao ninalenga kuelezea jinsi ya kumpatia mtu mtaji huku ukiendelea kutengeneza faida na kumuinua kibiashara.

Wajasiriamli wengi huwa wanalalamika kwamba biashara zao zinakwama kwa sababu ya kukosa mtaji.Hata hivyo ukitazama kwa karibu unaona kabisa kwamba wengi hawana ufahamu na uelewa kuhusu huduma za kifedha na kibiashara ambazo zinaweza kuwasaidia katika kuanzisha na kukuza biashara.Sasa kabla sijazama katika hiyo namna napenda nieleze kwa ufupi dhana ya mtaji na uwekezaji.

Mtaji ni fedha au gharama zinazotumika katika uanzishaji na uendeshaji wa biashara.Nasisitiza sana hapa kuhusu Mtaji wa uanzishaji na Mtaji wa uendeshaji kwa sababu ni aina ya mitaji ambayo inatofautiana.Mtaji wa uanzisha huwa unahusiana na zile gharama zinazotumika katiak hatua za mwanzo za uanzishaji wa kampuni na gharama za uendeshaji ni zile gharama ambazo zinatumika katika kugharamikia shughuli za kila siku za uendeshaji wa biashara.Shughuli za uendeshaji ni kama vile kulipa suppliers,wafanyakazi na gharama za moja kwa moja za uendeshaji na uzalishaji.Gharama za uanzishaji ni zile gharama za kuanzisha mfano usajili,vibali,na gharama za mwanzoni kabisa za kuendesha ofisi kabla ya kuanza uzalishaji.

Sasa mara nyingi sana watu wanapotaka mitaji wanakuwa na wazo tu ambalo sio jambo baya lakini swala la msingi la kufahamu ni kwamba ni mwendawazimu tu ambaye atatoa pesa zake kuwekeza katika Wazo ambalo liko kwenye kichwa chako.Ni lazima wazo lako ulipo muundoa katika namna ya andiko na zaidi ni lazima wazo lako liwe tayari umeshaanza kulifanyia kazi hata katika kiwango cha chini.Katika maandiko yangu ya nyuma nimewahi kuzungumza kuhusu Briefcase Companies Fahamu Kuhusu Kampuni za Mfukoni-Briefcase Corporations na pia nimewahi kuandika kuhusu jinsi ya kuanzisha biashara kwa kutumia mtaji mdogo Fahamu jinsi ya kuanza biashara kwa mtaji mdogo (Mfano: Milioni 1) ambapo katika maandiko hayo substance kubwa ilikuwa ni kutaka kuchokoza fikra za wajasiriamali na kuwaonesha kwamba unapotaka kuanzisha biashara kuna hatua ndogondogo ambazo unawez akuanza kuzifuatilia kwa lengo la kuanzisha biashara amaboz zitaonesha kwamba umeshaanza kulifanyia wazo lako kazi.

Baada ya utangulizi huu sasa nirudi kwenye mada ya msingi kuhusu namna ambavyo unaweza kumpatia mtu mtaji wa kufanya biashara na kuhakikisha kwamba biashara yake inakuwa.Katika kujadili mada hii nitagusia kuhusu bidhaa na huduma kadhaa zinazotolewa na mabenki kama vile Fixed Deposit,Term Loan,Overdraft,Standby letter of Credit,Bankers Guarantee an huduma nyingine ambazo hutolewa na Mabenki ya kibaishara kwa lengo la kuwezesha ufanyaji wa biashara.Pia nitagusia kuhusu kitu kinaitwa LIEN ambacho ndio kiini cha msingi cha mjadala huu.

Biashara yoyote ile ambayo inabidhaa au huduma ambayo inauzika pamoja na soko la uhakika inakopesheka.Hata hivyo ili biashara iweze kukopesheka inahitajika kuwa na Mzunguko wa fedha unaoeleweka na wa uhakika lakini pia inapaswa kuwa na Dhamana.Haya ni maeneo ambayo mjasiriamali yeyote anayeanza ni lazima ayatazame na kuyazingatia hasa pale ambapo anahitaji baishara yake ikue.Benki kabla ya kukupa Mkopo itatazama mzunguko wa Fedha zako Benki yani Unaweka kiasi gani na unatoa kiasi gani kwa siku,mwezi,mwaka n.k.Pili watatazama Collateral Ulizo nazi kama ni Fixed Asset,au ni Cash etc.Sasa leo nataka kuzungumzia zaidi kuhusu Kuhusu Matumizi ya Casha kama Dhamana ya Mkopo.

Unapohitaji kumpa Mtu Mtaji wa kibiashara namna bora kabisha ambayo unaweza kufanya ni kumdhamini benki kwa kutumia Fixed Deposit Guarantee,Yaani unafungua Fixed Deposit Account ya Mwaka mmoja Kisha Benki inamkopesha hadi 80% ya hiyo amount kama fedha.Sasa hapa nitoe angalizo.Unapoamua kufanya hii arangement fahamu kwamba Mabenki yetu mengi hayana huduma kama hizo na hivyo itakupasa kuzungumza nao kwa kina kwani usishangae Banker akakwambi kwa nini unakopa wakati tayari una pesa?

Wewe kama Mwekezaji utakuwa ni mmiliki wa ile Fixed Deposit Accoun na ile pesa yako itamdhamini yule mlengwa wako kupata mkopo kutoka benki.Ushauri wangu Mara zote ni kumpa huyu mjasiriamali Overdraft.Kwa Mfano Mjasiriamali nahitaji Mtaji wa Milioni 80 kwa ajili ya uendeshaji wa biashara kwa kipindi cha mwaka mmoja.Wewe unafungua Fixed Account ya Milion 100 ambayo itakupa Riba ya 8% kwa mwaka na Unampa yeye Overdraft ya Milioni 15 kwa Mwezi.Maana yake ni kwamba huyu mtu ana uwezeo wa kupata Milioni 15 kila mwezi ya kugharamikia shughuli za uendeshaji wa biashara yake.Benki watamtoza riba akitumia hiyo huduma so atatakiwa kuclear overdraft ndani ya mwezi husika ili asipte penalt.Kisha huyu anaweza Pewa Banker Guarantee kutoka bank kwa ajili ya kulipa Suppliers wake yenye thamani ya Milioni 15 hadi 50 kwa kutegemea aina ya biashara na wakati huo huo akapewa milioni 15 kama Term Loan.

Huyu Mtu anakuwa na Access ya Financing ya uhakika kwa mwaka mzima lakini zaidi unakuwa umemsaidia kujenga uhusiano wake na Mabenki.Lakini Pia katika kufanya uendeshaji wa biashara anaweza kuanza kutengeneza Asset Base yake ili kujiongezea uwezo wa kukopa zaidi Baada ya kipindi cha mkataba wenu kupita.

Hii mada ni ndefu na ina mambo mengi lakini naweza kusema kwamba ni moja kati ya kanuni zinazotumika katika hedging au kama umewahi kusikia Hedgef Funds.Kwa sababu mimi sio msomi wa Taaluma ya fedha ila nayaeleza haya kutoka na uzoefu na kiu yangu ya kutaka watu wajue basi sitaendelea zaidi ili nawakaribisha wote ili kwa pamoja tujadili na wale wataaluma wenye walete madini zaidi ili kwa pamoja tuweza kuangalia namna bora kabisa ya kujikwamu na kulikwamua taifa letu kiuchumi.

Karibuni tujadili zaidi
 
Wenye elimu ya fedha tusaidieni mawazo yenu
 
Back
Top Bottom