Ezekieli Maige ampiku Magufuli, moto chini

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Amepiga marufuku matumizi ya kifisadi ya watendaji wa wizara yake kulipana posho za hovyo hovyo, kununua mashangingi TANAPA badala ya magari ya porini, kusafiri nje ya nchi hovyo hovyo. Awasuta wajumbe wa bodi ambao ni mchwa.

Chanzo: Star tv taarifa ya saa mbili usiku
 
inatakiwa afanye utalii uwe chanzo kinachoongoza kuingizia serikali kipato!kwa sasa sekta ya usafirishaji inaongoza!hapo ndipo nitajua anafanya kazi
 
Amepiga marufuku matumizi ya kifisadi ya watendaji wa wizara yake kulipana posho za hovyo hovyo, kununua mashangingi TANAPA badala ya magari ya porini, kusafiri nje ya nchi hovyo hovyo. Awasuta wajumbe wa bodi ambao ni mchwa.

Chanzo: Star tv taarifa ya saa mbili usiku
Gurudumu mwanetu huyu maige Hana jipya kwani ameshndwa hata kuwawajibisha waliokuwa walinzi wa faru wakati bosi wake jk aliahidi kuliko faru afee wafe askari kumi sasa tumeshapoteza mmoja na askari wapo nini kinaendelea? Pili kwanini Emanuel cheusi marehemu alimtimua ngorongoro? Hana jipya huyo
Naomba kuwakilisha
 
Tunashukuru KAMA KWELI NA YEYE ROHO INAMUMA NA MENGI HAYA yanayotukera. Lakini kwa kumlinganisha na KAMANDA MAGHUFULI ni makosa makubwa sana na kutafuta kushushiana hadhi bure.

Tunatamani kuona wapiganaji hasa VIJANA wakiongezeka ulingoni nje ya mipaka ya itikadi za kichama bali UTAIFA ZAIDI. Kijana mwingine ninayesubiri kwa hamu kubwa kumuona kiutendaji jukwani ni Dogo Ngungai kule bungeni Dodoma mwakani.

Mheshiiwa Maghufuli hakufikia hapo kwa kigezo cha utendaji mzuri juu ya jambo moja tu hivyo, au ndani ya wizara moja au hata ndani ya mwaka mmoja tu ya utendaji kazi. Tafakari kidogo. Mpaka walau tukamfananishe MAIGE au mtu mwingine yeyote na Mhe John Pombe Maghufuli na uwezomwake wa kazi MIAKA MINGI SANA YA KIUTENDAJI itahitajika.

Hata hivyo mwambieni huyo dogo mwenzetu AKAKAZE ZAIDI BUTI kwani Uchaguzi Mkuu wa 2015 ni kwamba tutawachagua tu MTU NA UTENDAJI WAKE KAZINI, UUNGAJI MKONO MABADILIKO YA KWELI BILA KIGUGUMIZI na wala si kwa kuangalia sana chama wala dini yake.

Wachapa kazi wazuri popote pale walipo; hata katika mashirika mengine tu ambayo si bungeni, uchaguzi kwao utakua ni MWEPESI SANA NA BILA KUHITAJI KUTOA RUSHWA YOYOTE KWETU SISI VIJANA alimradi tu atazingatia hayo maneno kwenye wino mwekundu hapo juu.
 
Hizi subject nyingine bana..... huyu alikuwa naibu waziri na tunamjua hana lolote wakati yy ndiyo bingwa wa kulilia kugawiwa tuposho posho. Hata kupata uwaziri kamili ilijulikana wazi maana lazima upate ntu wa kulinda miradi ya mafisadi, ambayo wamewekeza kule. Huwezi kabisa kumfananisha na Makufuli !!
 
Amepiga marufuku matumizi ya kifisadi ya watendaji wa wizara yake kulipana posho za hovyo hovyo, kununua mashangingi TANAPA badala ya magari ya porini, kusafiri nje ya nchi hovyo hovyo. Awasuta wajumbe wa bodi ambao ni mchwa.

Chanzo: Star tv taarifa ya saa mbili usiku

Nyoooo ! unafananishaje sasa hapa? shule ndogo wewe
 
Nyoooo ! unafananishaje sasa hapa? shule ndogo wewe

Kwani tangu magufuli ameshika uwaziri huu mpya amefanya nini tunachoweza kutafsiri kimeokoa matumizi mabaya ya pesa za serikali? Au ni imani tu?
 
Amepiga marufuku matumizi ya kifisadi ya watendaji wa wizara yake kulipana posho za hovyo hovyo, kununua mashangingi TANAPA badala ya magari ya porini, kusafiri nje ya nchi hovyo hovyo. Awasuta wajumbe wa bodi ambao ni mchwa.

Chanzo: Star tv taarifa ya saa mbili usiku

Ni mpaka pale viongozi wetu wataacha kuongoza kwa matamko na badala yake kuchukua hatua ndiyo Tanzania itasonga mbele otherwise we will just be the same!
 
Ni mpaka pale viongozi wetu wataacha kuongoza kwa matamko na badala yake kuchukua hatua ndiyo Tanzania itasonga mbele otherwise we will just be the same!

Tumsubiri mwezi wa Saba 2011 kuona wakati bajeti mpya itakapotoka kuona kama alitekeleza kauli zake.
 
Sifa za kijinga. Halafu media inapotosha sana watu. Hawajui kwamba hawa wanaitumia media kama turufu yao kisiasa. Hiki ndicho wao walipaswa kufanya ni wajibu wao. Media ya nini. Unajua napata hisia kwamba kuna baadhi ya waandishi wamewekwa mifukoni na hawa watu ili watupotoshe. Watu wakitimiza wajibu wao tuwaache. Kwani huyo Magufuli ama Maige ana impact gani kwa Mtanzania wa kawaida? Tuache propaganda za siasa.
 
Kwa hiyo STAR TV ndio wamesema kuwa Ezekiel Maige yuko kwenye mashindano na MAGUFULI?
Amepiga marufuku matumizi ya kifisadi ya watendaji wa wizara yake kulipana posho za hovyo hovyo, kununua mashangingi TANAPA badala ya magari ya porini, kusafiri nje ya nchi hovyo hovyo. Awasuta wajumbe wa bodi ambao ni mchwa.

Chanzo: Star tv taarifa ya saa mbili usiku
 
Aaaaaaaaaaaaah wapi!!!!!!!!Kiongozi jasiri hawezi patikana toka chama cha mafisadi. Huo ni moto wa mabua tu, au ngoma ya kitoto ambayo haikeshi.
 
Aaaaaaaaaaaaah wapi!!!!!!!!Kiongozi jasiri hawezi patikana toka chama cha mafisadi. Huo ni moto wa mabua tu, au ngoma ya kitoto ambayo haikeshi.

Mwanzoni nilidhani watu tu hawataki kuamini viongozi wao, lakini baada ya ngeleja kutangaza hakuta kuwa na mgao wa umeme wakati ndio kwanza umeongezeka na bei pia kupanda, nimechoka. Nashindwa kukataa mawazo yanayodai kwamba JK na serikali yake yote ni wasanii
 
Amepiga marufuku matumizi ya kifisadi ya watendaji wa wizara yake kulipana posho za hovyo hovyo, kununua mashangingi TANAPA badala ya magari ya porini, kusafiri nje ya nchi hovyo hovyo. Awasuta wajumbe wa bodi ambao ni mchwa.

Chanzo: Star tv taarifa ya saa mbili usiku
Comparing incomparables
 
pale tanapa watu wanatafuna fedha kuliko mchwa matangazo hewa kibao bado media agency wanalazimika kugawana fedha na watendaji 10.00 pcnt agnc 5 wanaume ukija prm shelutete na catherine wanakata posho za waandishi kama ukikataa kazi za tanapa sahau
Waziri akiangalia mashangingi na exbtion tu bado majamaa yanakula
 
Hizi kelele tu hata JK na Pinda waliahidi kuzipiga vita Shangingi na kushughulikia mafisadi lakini wameishia kupiga kimya na baadae kwenye uchaguzi kuwasifi kama alivyofanya kule Rombo kwa mramba, Monduli kwa Lowasa, Bariadi kwa Chenge etc.

Hawa jamaa hawana lolote, maana ndo wako madarakani kwa pesa za mafisadi, halafu watawafanya nini.

Dawa yao ni kuwaondoa kabisa 2015.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom