Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.
Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi! - Nyerere
Watanzania bado wana maswali juu ya Chama Cha Jamii (CCJ) hasa kama kweli hiki chama kimekuja kuziba pengo la uongozi nchini au ni geresha tu kama ya vyama vingine. Kabla hata ya kwenda kuomba usajili wa muda tetesi zilishasambaa juu ya ujio wa chama hicho na ndani ya wiki chache tu CCJ kimepata kutangazwa sehemu mbalimbali kwa bure kabisa huku kikivuta mioyo ya wananchi wa kawaida kabisa waliochosha na vyama vya kisiasa vilivyopo ambao kwa muda mrefu wamesubiria kuona matamanio ya Baba wa Taifa kuhusu chama mbadala cha upinzani yakitimia.
Tetesi kubwa ni uwepo wa vigogo nyuma ya CCJ na wapo ambao hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe au kufikiri wenyewe kuhusu CCJ hadi waone kwanza nani ameondoka CCM. Kwa wale ambao wanasubiri wasikie majina makubwa yakitoka CCM ndio waamini basi kutoka kwa Bw. Fred Mpendazoe hakuwatoshi. Ni wazi vile vile hata likitoka kundi jingine ndani ya CCM bado wapo watu ambao hawataamini na wataendelea kutafutua ufafanuzi kwanini hao siyo vigogo au kwanini kuondoka kwao ni nafuu kwa CCM.
Vyovyote vile ilivyo, Watanzania wana haki na sababu ya kuipima CCJ kwa katiba yake, malengo yake, mapendekezo yake ya kushughulikia masuala ya taifa na itikadi yake. Itakuwa ni upungufu wa hekima, na uwezo wa kufikiri kama tutajaribu kukipima CCJ kwa kuangalia nani anatoka CCM! Mtu mwenye hekima atachukua muda kusikiliza kile ambacho uongozi wa CCJ, mashabiki wake, Katiba na watunga sera wake wanasema juu yake na siyo kile ambacho waathirika wa uwepo wa CCJ wanasema juu yake.
Hivyo, mahojiano haya ya kwanza na Mhe. Fred Mpendazoe aliyekuwa Mbunge wa CCM wa kuchaguliwa kwa asilimia 81 (kura 64,000) na ambaye ameamua kuondoka CCM mapema yatatupa mwanga wa ni watu gani wako nyuma ya CCJ na kama tunaweza kukubali na kukumbatia uwepo wake katika kuendeleza demokrasia nchini na hasa katika kupatia uongozi bora ambao taifa limekuwa likiutamani na kuungojea kwa muda mrefu hasa baada ya kukatishwa tamaa na uongozi ulioingia 2005.
Sikiliza na uamue mwenyewe.
http://www.zumodrive.com/share/4GHHMjg2Nm