Ewura wanawajibika kuangalia upya viwango vya umeme

Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,486
3,468
Miezi karibu 10 iliyopita TANESCO ilipendekeza kuongeza bei ya umeme kutokana na gharama za uendeshaji kuongezeka.

Walidai kuwa gharama hizo zinawafanya kushindwa kusimamia sekta hiyo kikamilifu na inabidi waombe msaada serikalini ili kuziba pengo hilo.
Mimi nilihudhuria kikao cha wadau ambacho kilipinga hoja hiyo kwa nguvu sana wakidai kuwa uzembe, ukiritimba, ubadhirifu ndiyo chanzo kikuu cha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji.

Kutokana arguments hizi EWURA ilichukuwa njia ya katikati kwa kuamini kuwa walichodai TANESCO ni kweli lakini vilevile kutokana na unyeti wa umeme katika uchumi wa nchi kuzidisha kama walivyoomba TANESCO itaathiri sana uchumi na ustawi wa jamm.

Ssa leo hii imegundulika kuwa ni kweli ubadhirifu ndani ya shirika hilo ni mkubwa sana kiasi cha kutishia uhai wa shirika hilo.

kwa sababu kuna vijishirika vingi ndani ya tanesco ambavyo vinatafuna shirika hili kama mchwa na wahusika wakuu ni wafanyakazi wa shirika hilo [siyo vishoka]

Kutokana na hali hiyo kwa nini EWURA wasishushe bei ya umeme?? kwa nini isifanyike tathmini [independently] ya gharama halisi [waondoe vishiria vyote vya inefficiency] punguza privilege nyingine za wafanya kazi [kiwango units za bure kwa wafanyakazi- ambapo inasemekana wengine wanauza hizo units] .

Shirika hili la umma lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuna fair play kati ya shirika na wateja wake.
 
Back
Top Bottom