Eti polisi arusha wanasema hawajakosea kuvuruga maandamano ya chadema

Shapecha

Member
Oct 21, 2010
45
1
Mchana huu RPC wa Arusha, Naibu DCI na Kamishna wa operation wameongea na waandishi wa habari na kusema hawakukosea kuvuruga maandamano ya CHADEMA eti kwa sababu kama yangeachwa yangeleta maafa makubwa sana zaidi ya yaliyotokea hiyo juzi. Wamesema waliosababisha yote hayo ni CHADEMA wala siyo Polisi.

My Take!
Hivi polisi wameshindwa Kama kulinda maandamano hadi yatakakoishia na wakaona njia rahisi ni kuyavuruga kwa kuvunja magari vioo na kuua watu jamani. Kweli polisi wetu wengi STD 7 na Form 4 thats why hawajui warespond vipi kwa tukio lililo mbele yao.
 
Kwahiyo wao ni waganga wa kienyeji wanajua kuagua future siyo?
Kwanini wasingetumia hiyo intelijensia ku-intercept hao organizers wa fujo kama kweli walipewa tip?
Pumbaaaaf zenyu...!
 
lazima waeme hivyo kwani walikuwa wanatekeleza maelekeze ya wakubwa wao. si mmemsikia waziri wa mambo ya ndani, IGP wakisema hayphayo? kwanza nadhani kuongelea suala ambalo mabosi wao walikwishazungumzia ni utovu wa nidham ya kikazi, wawe waangalifu, wakilikoroga wao ndio watageuziwa kibao!
 
hawa mm sina hata imani nao

raha yangu kusikia nao wanuwawa tu, ili wahisi machungu, tunayoyafeel
 
Polisi ni wanyama. Utu wao ni kuwatumikia mafisadi na kulinda mali za mafisadi pia kunyang`anya haki za watanganyika wasio na hatia. Ndiyo maana mwakyembe aliwaambia wazi kuwa wanatumia uganga wa kienyeji ili kugundua kosa: Watakwepa leo lakini hukumu ya mungu haijali wanafahamika namna gani na mafisadi kaburi linawangoja na laana iwe juuyao.
 
Hatutasahau hili wala kuwasahau waliopeteza maisha yao. Kama wanadhani wanatetewa na serikali hii dhalimu wajue kuwa ina mwisho wake. Iko siku watafunguliwa mashtaka kwa mauaji ya raia wa Tanzania kwa sababu hizo finyu walizozitoa hapo juu. Hata kama itachukua miaka 50, tutakumbuka hii. Rejea Chile na Argentina, walifanyia raia unyama wakadhani kuwa watapona, hatimaye mkondo wa haki ukawafikia.
 
Mchana huu RPC wa Arusha, Naibu DCI na Kamishna wa operation wameongea na waandishi wa habari na kusema hawakukosea kuvuruga maandamano ya CHADEMA eti kwa sababu kama yangeachwa yangeleta maafa makubwa sana zaidi ya yaliyotokea hiyo juzi. Wamesema waliosababisha yote hayo ni CHADEMA wala siyo Polisi.

My Take!
Hivi polisi wameshindwa Kama kulinda maandamano hadi yatakakoishia na wakaona njia rahisi ni kuyavuruga kwa kuvunja magari vioo na kuua watu jamani. Kweli polisi wetu wengi STD 7 na Form 4 thats why hawajui warespond vipi kwa tukio lililo mbele yao.

Nadhani sasa imefika mahali ambapo kukiwa na maandamano, tuwaambie polisi wasionekane, halafu tuone hali itakuwaje. Pale Mwanza kuna wakati polisi waligomea kuongoza msafara wa Dr Slaa lakini wananchi wenyewe walijiongoza, magari ya watu wengine yakakaa pembeni kwa hiari, na kulikuwa na utulivu usio wa kawaida. Kwenye maandamano na mikutano, polisi ndiyo chanzo cha vurugu, na ushahidi ni huo ambapo unaonesha wapenzi wa CHADEMA kabla ya kukutana na polisi walikuwa wametembea kilometa 2, na huko kote hakuna hata mtu mmoja aliyelalamika kuwa hata chungwa lake limeporwa. Tuwakatae polisi kuendesha maandamano, wataendelea kutuletea maafa.
 
Hawa watu wanaropoka tuu, Wakati Basilio alipoagizwa aue hata mmoja ili Chadema waogope na kuwapa CCM nafasi ya kuchakachua alikataa sasa anasoma magazeti makao makuu, Andengenye kijana mtiifu yeye kakubali, lakini lazima CCM watambue njia yetu ni moja, na Damu hulipwa kwa damu.
 
Back
Top Bottom