WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Huyo mama ameongea vibaya kwa kweli. maneno ya namna hii ndiyo yanawafanya baadhi ya wanaume kujinyonga au kunywa sumu. Kamdhalilisha sana, hasa kudharau uwanaume wake. Ni kitendo kibaya. Hata kama jamaa akujaliwa sana ilibidi amheshimu kwani Bwana wa upendo ndiye aliyempatia.
Kweli kama ulivyosema ni Bwana wa Upendo ndiye aliyempatia.
Hakuna kitendo kiovu kama mwanamke au hata mwanaume kumkashifu mzazi mwenzie mbele ya watoto licha ya watu baki.Ni nani asiyeona mzazi wake kama ndiyo zaidi ya mtu mwingine hapa duniani?
Mama unapomdhalilisha baba wa watoto wako namna ile... ni sawasawa na kuwatusi wanao! Tena watoto kama ni wakubwa watakushangaa iweje hukuchagua mwanaume bora kwa ajili ya ubaba wa watoto wako?Tujisahihishe jamani.
Tukirudi upande wa pili kwa akina baba, ni mara ngapi tunasikia au hata kushuhudia wababa wakipiga wake zao tena wakati mwingine kuwaacha uchi wa mnyama bila kujali kuwa huyo mama ndiye aliyekufanya ukaonekana mwanaume mbele za watu kwa kukuheshimu na kukuzalia watoto?
Acheni hizo wakina baba.