ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Juzi nilikuwa maeneo ya dodoma, sarafina bar, napata soda huku pembeni meza ya pili wakiwa wamekaa wadada wanne nao wakipata moja moto moja baridi. Kwa chati nikawa nawaibia maongezi yao baada ya kuvutiwa nayo.
Walikuwa wanajadili mahusiano ya shosti mwenzao ambayo yamekufa baada ya kufumaniwa na mumewe/mpenzi wake. Kwamba mwanaume amekosa roho ya kusamehe kwani naye alishawahi kufumaniwa na Jane (sio jina halisi la diva aliyeachwa). Kilichonishangaza-pengine kutokana na ushamba wangu-ni pale dada mmoja miongoni mwao aliposema ingawa Jane anaonekana kuchanganyikiwa kutokana na ugumu wa maisha (ukizingatia alikuwa ni mke 'beki tatu') ni heri ataheshimiwa na jamii inayomzunguka eti coz alishawahi kuolewa tofauti na wanawake wengine wanaoishi maisha ya ki spinster tangu kuzaliwa kwao hadi sasa ingawa umri wao umekwenda.
Swali langu kwenu ni: Je ni kweli dada zangu eti kama umewahi kuolewa halafu ukaachika mnajisikia kuheshimika tofauti na unapokuwa umeenda umri lakini hujawahi kuolewa?
Hebu fungukeni tujue feelings zenu wadada mnapokuwa kwenye 'situations' hizi mbili tofauti.
Karibuni.