Eti kina dada kuna ukweli ktk hili?

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Juzi nilikuwa maeneo ya dodoma, sarafina bar, napata soda huku pembeni meza ya pili wakiwa wamekaa wadada wanne nao wakipata moja moto moja baridi. Kwa chati nikawa nawaibia maongezi yao baada ya kuvutiwa nayo.

Walikuwa wanajadili mahusiano ya shosti mwenzao ambayo yamekufa baada ya kufumaniwa na mumewe/mpenzi wake. Kwamba mwanaume amekosa roho ya kusamehe kwani naye alishawahi kufumaniwa na Jane (sio jina halisi la diva aliyeachwa). Kilichonishangaza-pengine kutokana na ushamba wangu-ni pale dada mmoja miongoni mwao aliposema ingawa Jane anaonekana kuchanganyikiwa kutokana na ugumu wa maisha (ukizingatia alikuwa ni mke 'beki tatu') ni heri ataheshimiwa na jamii inayomzunguka eti coz alishawahi kuolewa tofauti na wanawake wengine wanaoishi maisha ya ki spinster tangu kuzaliwa kwao hadi sasa ingawa umri wao umekwenda.

Swali langu kwenu ni: Je ni kweli dada zangu eti kama umewahi kuolewa halafu ukaachika mnajisikia kuheshimika tofauti na unapokuwa umeenda umri lakini hujawahi kuolewa?

Hebu fungukeni tujue feelings zenu wadada mnapokuwa kwenye 'situations' hizi mbili tofauti.

Karibuni.
 
kuolewa kunawakata vidomodomo/ngebe wachongaji mtaani.Kuolewa kuna heshima yake..
kuachana ni majaliwa/sababu iwe inakubalika
 
nani aliwaambia heshima ya mtu inatafutwa kupitia migongo ya watu wengine ,hivi ni lazima kila mwanamke anayezaliwa kwenye hii dunia awe na ndoa ndio maisha yake yakamilike kuna wadada wachache ambao nawafahamu ndoa haikuwa sehemu ya maisha yao lakini wanajiheshimu wanaheshimika na naheshimu michango yao kwenye jamii na maisha yao kwa ujumla.

EMBU TUWE TUNAACHA DHANA POTOFU ZISIZOKUWA NA MSINGI.
 
jameni! kuliko kuolewa nikaachika ni bora nisiolewa,thats why ni bora ukafanya chaguo sahii mwanzoni kuliko kuingia then ukatoka!!
 
Kumbe shida ni kuwakata vidomodomo watu, sooooooooooooo unaishi kwa ajili ya watu wengine kazi kweli kweli..........

kuolewa kunawakata vidomodomo/ngebe wachongaji mtaani.Kuolewa kuna heshima yake..
kuachana ni majaliwa/sababu iwe inakubalika
 
jameni! kuliko kuolewa nikaachika ni bora nisiolewa,thats why ni bora ukafanya chaguo sahii mwanzoni kuliko kuingia then ukatoka!!

Nakuunga mkono kabisa. Bora kutokuolewa kuliko kuolewa na kuachika. Maana ukiachika heshima inatoka wapi km ndoa imekushinda?
Kwanza ndoa za siku hizi unaolewa, alafu unakuwa nawenzako nje km kumi walioolewa kinyemela. Km mumeo hakuheshimu anakutafutia nyumba ndogo, unataka nani akuheshimu na ndoa yako?
 
Nakuunga mkono kabisa. Bora kutokuolewa kuliko kuolewa na kuachika. Maana ukiachika heshima inatoka wapi km ndoa imekushinda?Kwanza ndoa za siku hizi unaolewa, alafu unakuwa nawenzako nje km kumi walioolewa kinyemela. Km mumeo hakuheshimu anakutafutia nyumba ndogo, unataka nani akuheshimu na ndoa yako?
wanasema eti kuolewa ni kusafihsa nyota! ata ukikaa kwenye ndoa kwa masaa 2!!! mmh!! namkumba shekh yahya jameni!!
 
ndoa ni nzuri wasemavyo waolewaji,lakini ni vema kukurupuka!!! jioni njema nalof off kikwelikweli!
 
Lakini inakuwaje mwanamke 'unapopigwa' chini hali huwa ni kama kiama, huku wengi wao wakidai kupotezea muda? Huwa sielewi kwanini hasa hali hii huwa inatokea. Mi nadhani kuna kitu kilichijificha mioyoni mwa wanawake/wasichana ambacho wanawake wanapoolewa huwafanya wajihisi tofauti na wale ambao bado hawajaolewa. Suala la heshima inaonekana halikubaliki, lakini sasa issue sio heshima hebu fungukeni ni kitu gani?
 
Back
Top Bottom