Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,738
- 114,093
Preta asante kwa taarifa hii, Mkuu PK, kwa taarifa hii, you were right dege limetua Arusha under mistaken identity akifikiri ni KIA, I'm very sorry to doubt you. Samahani sana!.BOEING- ET 815 YA ETHIOPIA YATUA KWA DHARURA ARUSHA Dec 19, 2013
Dar es Salaam 19 December 2013
TUKIO LA NDEGE AINA YA BOEING 767-300 MALI YA ETHIOPIAN AIRLINES ILIYOTUA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ARUSHA BADALA YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA KILIMANJARO (KIA) TAREHE 18/12/2013.Jana majira ya 12;47 mchana , Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia aina ya ya Boeing 767-300 yenye injini mbili na uwezo wa kubeba abiria 260 ilitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Arusha badala ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro- KIA ilipotarajiwa kutua
Ndege hiyo ilikua ikitokea ADDIS ABABA ETHIOPIA ikielekea Kilimanjaro na Mombasa, ilitegemea kutua Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) saa 06:55 mchana katika safari yake ya kawaida ilikuwa na jumla ya watu 213 (Abiria, rubani na wahudumu wa ndege).
Mawasiliano ya kwanza ya ndege na uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro yalikuwa saa 06:29 mchana ambapo rubani alisema ametoka Addis Ababa, Ethiopia kwenda Kilimanjaro akiruka futi 36,000 kutoka usawa wa bahari na alitegemea kutua KIA saa 06:50 mchana.
Muongoza ndege alimwelekeza rubani njia ya kufuata kuelekea KIA hadi atakapouona uwanja na kisha kutua barabara namba 27 (Runway 27). Rubani pia alipewa tahadhari kuwa kuna ndege ndogo imekwama mwanzoni mwa barabara 09 (Runway 09) kutokana na tatizo la kupata pancha na barabara iliyopo ni namba 27 yenye urefu wa mita 3,200 ambazo zinaweza kutumika.
Baada ya kupewa taarifa hiyo, rubani alijibu na kusema atamwita tena baada ya kuachiwa na Nairobi. Baada ya muda mfupi, rubani aliita tena KIA na kuripoti ameachiwa na Nairobi na anaomba kuendelea kuteremka. Muongoza ndege wa KIA alimruhusu kuendelea kushuka hadi hatimaye kufikia futi 7,000.
Baada ya muda rubani akaripoti kwamba amekiona kiwanja na anaomba aendelee kutua kwa macho (visual approach) barabara namba 27. Rubani aliruhusiwa kuendelea kutua kwa kuona, na aripoti akiwa upande wa kushoto wa barabara namba 27.
Baadae rubani aliita tena na kuripoti kwamba yuko upande wa kushoto wa barabara namba 27 na anaiona barabara ya ndege namba 27. Wakati wote alikua kwenye masafa ya KIA (120.1 MHz) na hali ya hewa kwa wakati wote ilikuwa ni nzuri. Baada ya hapo muongoza ndege wa KIA alimruhusu kutua barabara namba 27. Baada ya kutokumuona akitua muongoza ndege wa KIA alianza kuita ndege hiyo bila mafanikio. Wakati muongoza ndege wa KIA akiendelea kuita ndege hiyo, alipigiwa simu na muongoza ndege wa Arusha kumtaarifu kwamba anaiona ndege aina ya BOEING inatua barabara namba 27 Arusha.
Hakuna taarifa ya tahadhari iliyotolewa na marubani wa ndege hiyo ya Ethiopia ET 815, kabla ya kutoa uwanja wa Arusha. Aidha uwanja wa ndege wa KIA ulikuwa unaruhusu ndege hiyo kutua licha ya ndege ndogo ya abiria kukwama mwanzoni mwa bara bara ya 09(Runway 09). Kwa vile bado ilikuwa na bara bara yenye urefu wa mita 3200 ambazo zingeweza kutumika.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania inashirikiana na Kitengo cha Uchunguzi wa Ajali, Wizara ya Uchukuzi, kubaini chanzo cha tukio hilo. Tayari timu ya wataalamu iko eneo la tukio, hivyo taarifa zaidi zitatolewa uchunguzi utakapokamilika.
Fadhili J. Manongi
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Usafiri wa Anga
19 Desemba 2013
Pasco