Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,415
- 106,023
Mw3anakijiji, hawa jamaa wanataka kutukoroga tu kwa kuweka vitu visivyokuwemo ebu soma ibatra ya 55 na 56 uone zinasemaje. Tena basi bora niiweke hii ya 55 hapa..
Ibara ya 55 kifungu cha:-
4) Mawaziri na Manaibu Mawaziri watateuliwa kutoka miongozi mwa wabunge.
5) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea kwamba rais anahitajiwa kumteua waziri au Naibu waziri baada ya bunge kuvunjwa. Basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye alikuwa mbunge kabla ya bunge kuvunjwa.
Buuuyaaa!....Ni msisitizo gani zaidi tunauhitaji hapa jamani?
.
Kwa nini ibara ya bunge kuvunjwa inapewa msisitizo wakati huu? Unajua tofauti ya bunge kuvunjwa na bunge kumaliza kikao mkuu? Unajua tofauti ya kusitishwa kwa mikutano ya bunge na bunge kuvunjwa?
Ibara ya bunge kuvunjwa haihusiki kabisa sasa hivi. Hebu kaangalie ibara ya 90 ujue maana na maainisho ya bunge kuvunjwa. Bunge likivunjwa kinachofuata ni uchaguzi.