Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
TANROADS katika mgogoro mpya
MRADI wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Makofia-Msata, ambao umepewa jina la 'ng'ombe wa maziwa' umeingia katika mgogoro mpya baada ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kumfuta mkandarasi aliyeshinda na mwenye gharama nafuu na kuchukua kampuni iliyoshindwa kwa tofauti ya zaidi ya Sh bilioni 20.
Habari za ndani ya TANROADS zimethibitisha kwamba kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) imeenguliwa Julai mwaka huu na kuchukuliwa kampuni ya Estim Construction Co. Ltd yenye mahusiano na mfanyabiashara maarufu familia ya Subash Patel.
Pamoja na kushinda katika vigezo vingine, kampuni ya CHICO ilikuwa ndiyo iliyokuwa na gharama nafuu kwa kupanga kutumia Sh 84, 176, 440, 756.96 wakati Estim wamepewa kwa Sh 105, 604, 611,700.00 pamoja na kuwa walishindwa katika zabuni ya awali.
Huu ni mgogro wa pili kuhusiana na barabara hiyo baada ya TANROADS kuingia katika mgogoro na kampuni ya Korea ya TAKOPA Construction Ltd ambayo Serikali iliilipa Sh bilioni 15 za awali (advance payment) lakini ikaitimua kutokana na kudaiwa kushindwa kazi bila kurejeshwa kwa fedha zilizotolewa kwa kampuni hiyo.
Zabuni hiyo ya 2009/2010 ilitolewa kwa kampuni hiyo ya CHICO ya China baada ya kuondolewa kwa TAKOPA kabla ya uongozi wa TANROADS chini ya Mtendaji wake Mkuu, Ephraem Mrema kuingilia kati na kuvuruga taratibu za zabuni zilizoipa ushindi CHICO.
Raia Mwema imefahamishwa kwamba hata Sheria ya Manunuzi ya Umma haikufuatwa katika kuingoa kampuni ya CHICO na kuiparua Estim inayodaiwa kuwa karibu zaidi na watu walio karibu na uongozi wa juu wa serikali.
Tayari TANROADS imeisababisha Serikali hasara ya mabilioni ya shilingi ikiwa ni pamoja na fedha zilizolipwa kutokana na kesi mbalimbali zilizofunguliwa na wawekezaji baada uongozi wa wakala kukiuka mikataba na sheria ya manunuzi.
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema imezipata pamoja na habari za ndani ya TANROADS, baadhi ya mikataba imekatishwa kutokana na sababu zinazoweza kutajwa kuwa ni mizengwe ama maslahi binafsi.
Tayari wakandarasi hao, baadhi wakiwa wa kimataifa, wamewasilisha mashitaka yao katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (Arbitration Court) Paris, Ufaransa na London, Uingereza. Mashitaka mengine yamo kwenye mahakama za usuluhishi Tanzania.
Miongoni mwa migogogro inayotajwa ni pamoja na unaohusu barabara ya Marangu-Rombo-Mkuu na Mwika-Kilalacha ambako TANROADS iliingia mkataba wa Sh bilioni 23.4, lakini baadaye mkandarasi akafukuzwa kwenye eneo la ujenzi akidaiwa kushindwa kutimiza wajibu wake.
Mgogoro mwingine ni kati ya TANROADS na kampuni ya PRISMO-BADR, ulioko katika Mahakama Kuu ya Tanzania, ukihusisha madai ya malipo ya awali na udhamini.
Mgogoro mwingine unahusisha Shirika la China Estate Construction Eng. (CSCEC), ukihusu kuboresha kiwango cha barabara ya Kigoma-Lusahunga, deni likiwa Sh bilioni 46.8.
Eneo jingine ni la mkataba wa Sh bilioni 1.39 kati ya kampuni ya Norconsult AS dhidi ya TANROADS, ukihusu utoaji huduma ya usimamizi kwa ajili ya kuinua kiwango cha barabara ya Geita-Sengerema na Sengerema-Usagara.
Kampuni nyingine katika mgogoro na TANROADS ni pamoja na Roughton International, Kundasingh, Shabbirdin & Associate na Grineker-LTA Ltd.
Kampuni nyingine ni Konoike iliyoingia mkataba wa Sh bilioni 103.47 na TANROADS. Mkataba huo ulihusu kubuni na kujenga barabara ya Dodoma-Manyoni.
Shauri la kampuni ya Konoike na TANROADS kwa sasa liko katika Mahakama ya Usuluhishi jijini London, Uingereza, na kampuni hiyo inatajwa kufukuzwa kwenye eneo la ujenzi kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya mkataba.
Mrema, ambaye hata uteuzi wake kuongoza TANROADS ulihojiwa ndani ya Bunge, amekuwa katika dimbwi la tuhuma kadhaa; huku mwenyewe akihaha kujaribu kuzima tuhuma hizo kwa njia mbalimbali.
Baadhi ya tuhuma zinazomuelekea ni pamoja na kuingia mikataba na kampuni za ujenzi; hata kabla ya Serikali kuu kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara husika na hivyo kuisababishia Serikali hasara ya kulipa fidia kwa kampuni husika ambazo zimejikusanya bila kazi.
Imeelezwa kwamba kutokana na hali hiyo, Mtendaji huyo mkuu wa TANROADS amejikuta akishindwa kuelewana hata na wasaidizi wake wakuu ambao amewaona kama tishio kwa ajira yake; huku akijiweka karibu na viongozi wa juu wa serikali na vyombo vya dola.
Mrema ambaye uteuzi wake umekuwa na utata mkubwa ameelezwa kuwa baada ya muda wake wa ajira uliotajwa kuwa miaka mitatu kutofautiana na mkataba aliongia na Wizara ya Miundombinu wakati Andrew Chenge akiwa Waziri ambao unampa miaka mitano.
Ndani ya Bunge tayari Serikali imekiri kuingia hasara ya Sh bilioni 300 kutokana na Mrema kuingia mikataba tata ambayo imeilazimu Serikali kulipa fedha hizo kama fidia. Tuhuma hizo kwa sasa zinachunguzwa na vyombo vya dola kwa mujibu wa taarifa ya serikali bungeni.
Hata hivyo, Wizara ya Miundombinu imepata kigugumizi kuchukua hatua pamoja na kushauriwa kufanya hivyo na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi (PPRA) baada