EPA na mambo yake

Date::11/4/2008
Majina ya vigogo wa BoT walioshiriki kashfa ya EPA yadaiwa kupelekwa kwa DPP
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi


BAADHI ya maafisa wa Benki Kuu Tanzania (BoT) waliofukuzwa kazi kutokana na tuhuma za ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), wanadaiwa kuwa miongoni mwa watu wanaoweza kuburuzwa mahakamani.

Uwezekano huo umetokana na majalada ya watuhumiwa wa ufisadi wa EPA kuwa mkononi mwa Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), ambaye atafanya uchambuzi wa kisheria kuangalia kama kuna kesi kwa kila mtuhumiwa.

Wakati DPP, Eliazer Feleshi akiweka bayana kwamba sasa hivi anaandaa hati za mashitaka baada ya kuchambua jalada moja baada ya jingine, gazeti hili limethibitisha hadi jana kuwepo majina ya maafisa wawili (majina tunayo).

Duru huru za habari za kuaminika kutoka serikalini, zilifafanua kwamba maafisa hao ni miongoni mwa sita ambao rufaa zao zilitupwa na Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi wa jinai, ilibaini maafisa hao kunufaika na fedha za EPA kwa namna moja ama nyingine.

"Kilichofanyika baada ya BoT kuwachukulia hatua za kinidhamu, ilikuwa ni Takukuru kuwachunguza kwa jinai kama wanefuaika, na wawili kati yao wanaopaswa kufikishwa mahakamani," kilisema chanzo chetu kutoka ofisi ya DPP.

Taariga nyingine zilifafanua zaidi kwamba, mmoja kati ya majina yanayotajwa kufikishwa kwa DPP hakuwahi kukata rufaa kupinga uamuzi wa Jopo Maalumu la Kamati ya Nidhamu BoT, la kuwaadhibu kinidhamu.

Maafisa wanne wa BoT hadi jana majina yao hayakuwepo kwa DPP, huku taarifa zaidi zikisema kuwa uchunguzi wa Takukuru huenda haukubaini kwamba walitenda jinai.

Awali, maafisa sita ambao mmoja wao alipaswa kustaafu tangu mwezi Machi, walifukuzwa na Jopo Maalumu la Kamati ya Nidhamu inayoongozwa na Naibu Gavana, ndipo baadaye wakakata rufaa kwa Gavana kama Mwenyekiti wa Rufaa, lakini nazo zikatupwa.

Wakati BoT ilipochukua hatua za kinidhamu, Takukuru ilichunguza jinai kuona kama maafisa hao walinufaika na fedha za EPA kwa namna moja au nyingine.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, uamuzi huo unatokana na kuwepo ushahidi unaothibitisha namna vigogo hao walivyoshiriki kwa kushindwa kuwajibika hadi kukatokea ufisadi huo wa zaidi ya sh133 bilioni za EPA.

Tuhuma za ufisadi katika EPA ziliibuka katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi wa Kampuni ya Ersnt&Young, ambao awali ulifanywa na Kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini, kabla ya kusitishwa ghafla kufanyakazi hiyo.
 
Jamani hivi ni kweli wanvyo eleza majirani zetu kenya uganda kuwa WATANZNIA akili zao ni zakawaida hata akiwa profesa au msafishaji ?hivi nyinyi mnaamini kuwa serekali ikawapele wezi wa epa katika mahakama inakuwaje leomwanadamu mwenye akili akakubali hilo akijuwa ya kuwa mbinu ujanja unaonekana dhahiri na mbinu zinavyopangwa nakupeni pole wa Tz na sasa namini hii nchi watu wake ni wapole na unalowambia wao waponawe ukiwa unawaongoza
 
Watuhumiwa wa wa wizi wa fedha za EPA watafikishwa mahakamani Kisutu muda si mrefu leo.
 
Last edited by a moderator:
Kuna habari mahakama ya Kisutu muda si mrefu, tusubiri tuone muda si mrefu tutasikia
 
Lets stop contribute ili tusiongeze kurasa katika hii thread hadi hapo atakapoiweka hapa.
 
Breaking use has been broken!!!

Kama hauna news wait until u are sure then make it a breaking news!! Umenipotezea dakika kadhaa.....
 
of course posted by HALISI

what did we expect?

FIRST FAMILY?

xpskcz.jpg
 
Back
Top Bottom