EPA na mambo yake

Ochu, bluhende, Boniface G. Mduma, Dark City, Domo Kaya, Freetown, Halisi, Kinyamana, Lione, Madaha, mahesabu, Maskini Mimi, Mfuatiliaji, Mtu Kwao, MyTanzania, Nungunungu, pingiring'ombe, Shy, ThinkPad, wendos, WomenofSubstanc

all these people are in suspense!!!
 
Tayari Jeetu Patel na wenzake wako mahabusu ya wote pale Kisutu wanaminyana wanasubiri mabasi luxury kwenda lupango. KUndi lingine linafikishwa kati ya leo kama watawahi kabla ya saa tisa ama kesho mapema. Tusubiri.
 
Kwa wale waliuliza Jeetu Patel ni nani; hii itawapa mwanga kidogo....


Vigogo wa Kagoda, Jeetu Patel waogopwa

Mwandishi Wetu Oktoba 29, 2008

Yadaiwa ushahidi dhidi yao 'dhaifu'


'Kondoo wa kafara' ndiyo watakaoshitakiwa

ZIKIWA zimebakia siku mbili kwisha kwa muda uliotolewa kwa timu ya Rais iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, watuhumiwa wakuu watatu wa wizi huo wanaelekea kuumiza vichwa vya viongozi na watendaji wakuu serikalini na ndani ya chama tawala cha CCM kutokana na nguvu kubwa waliyonayo.

Wanaoteswa na jinsi ya kuwashughulikia watuhumiwa hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, aliyeunda timu na baadaye kuiongezea muda huku akitoa kauli zinazopishana kuhusu hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwashitaki waliohusika na jinai hiyo na ile kauli ya kuwa wasiolipa fedha ndio watakaofikishwa mahakamani.

Habari za uhakika kutoka serikalini zinaeleza kwamba, suala la kuwachukulia ama kutowachukulia hatua watuhumiwa hao wakuu limekuwa likiisumbua timu ya Rais inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kutokana na kile kinachoelezwa kwamba watuhumiwa hao wakuu walikuwa "makini" katika kuchukua fedha za EPA na hata wakati wa urejeshaji wake.

Ofisa Mwandamizi wa serikali ameliambia RAIA MWEMA kwamba watuhumiwa wakuu watatu ambao wananchi wengi wanataka wafikishwe mahakamani hawataguswa; angalau kwa sasa kutokana na watuhumiwa hao kuwa makini wakati wa mchakato wa kuchukua fedha za EPA na ndio pekee waliorejesha fedha zote walizochukua kwa wakati, ikiwa ni "kutimiza masharti yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete".

"Wakati wa mchakato wa kuchukua fedha za EPA watuhumiwa hao ambao watu wengi, vikiwamo vyombo vya habari, wanataka wachukuliwe hatua walikuwa makini mno kiasi cha kuwafanya wachunguzi wakose makosa ya kijinai ya kuweza kuwafikisha mahakamani na walipopewa muda wa kulipa walilipa kwa wakati na kwa uangalifu mkubwa kiasi cha kuwa vigumu kuwabana," alisema ofisa huyo.

"Hata hivyo, bado kuna mambo yanayoangaliwa ikiwa yatakamilika lolote linaweza kutokea; hasa ikiwa uongozi wa juu wa serikali utafanya maamuzi magumu kwa kuwa uamuzi wa kisiasa pia ni muhimu katika kufikia maamuzi katika suala la fedha za EPA kwa kuwa linaweza kusababisha mtikisiko mkubwa katika siasa za Tanzania," alisema Ofisa huyo ambaye hata hivyo anakiri udhaifu katika kuwashughulikia wahusika hao.

Uchunguzi wa RAIA MWEMA kwa muda mrefu sasa umebaini kuwapo kwa watuhumiwa ambao wanaweza kufanywa 'kondoo wa kafara' kutokana na msimamo wao katika kutoa maelezo kwenye timu iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza tuhuma hizo, na pia kwa kile kilichoelezwa "kiburi cha ajabu" walichoonyesha watuhumiwa hao.

Watuhumiwa wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani ni wale ambao wanaelezwa wamegoma kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kushindwa kulipa fedha na baadhi kukataa kutoa maelezo waliyotakiwa kuyatoa, na badala yake wamekuwa wakitoa maelezo kuonyesha kwamba wao walishiriki katika uchukuaji wa fedha za EPA kwa kufuata taratibu na sheria na baadhi walidai kupata fedha hizo kwa kazi walizofanya.

Utata mkubwa zaidi unaelezwa kutarajiwa kuibuka kuhusiana na fedha hizo kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2005 hususan katika kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM; huku baadhi wakitajwa kuwa na ushahidi wa jinsi fedha hizo zilivyotumika, jambo ambalo tayari limekwisha kukanushwa na viongozi wa chama hicho tawala.

Imeelezwa kwamba mmoja wa watuhumiwa, ambaye ni mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya kiasia, ameelezwa kujitokeza kulipa fedha za kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, kampuni iliyochota zaidi ya Shilingi bilioni 40, lakini pamoja na kujitokeza kwake, kumekuwa na kigugumizi cha kumuunganisha na makosa ya jinai yaliyofanywa wakati wa kuchukua fedha hizo.

"Unajua ni kichekesho, tunaambiwa wahusika wa Kagoda hawajulikani, lakini anakuja mtu analipa fedha za Kagoda na anajulikana kuwa analipa kwa niaba ya nani, halafu tunaendelea kusema hatuwafahamu wahusika wa kampuni hiyo ambayo imethibitika kufanya jinai. Kwa kweli inatuaibisha sana sisi tuliosomea kazi ya upelelezi wa mambo ya jinai na ni aibu pia kwa serikali nzima kuwaogopa watu," anasema ofisa mwingine mwandamizi wa serikali mwenye uzoefu na mambo ya upelelezi wa jinai.

Kampuni ya Kagoda imekuwa ikitajwa kutofahamika ofisi zake wala wahusika wake wakuu kutopatikana, lakini kitendo cha kujitokeza kwa mtu kulipa fedha za kampuni hiyo kwenye timu ya Rais, kimeelezwa kutokuwa na tofauti yoyote na watuhumiwa wengine wa wizi wanaokutwa na mali, hata wale walionunua mali hiyo kwa wezi.

"Kuna wafungwa wengi ambao wamefungwa kwa kukutwa na mali za wizi, baadhi hawakuhusika hata na wizi; bali walinunua mali hizo kwa watu wengine tena baadhi bila hata ya kujua kama ni mali za wizi, sasa mtu anakuja analipa fedha zilizoibwa unamwachia, si tungewaambia kina Kasusura (Justine) na wenzake walipe tu fedha walizoiba wakati ule badala ya kuwashitaki?" anasema ofisa huyo ndani ya serikali.

Habari zaidi zinaeleza kwamba miongoni mwa watuhumiwa ambao Serikali inapata kigugumizi kuwashitaki ni pamoja na mfanyabiashara Jeetu Patel na wenzake wanaofahamika ambao makampuni yao manane ni miongoni mwa makampuni yaliyochukua zaidi ya Shilingi bilioni 90 ambazo zimethibitika kupatikana kwa njia ya udanganyifu na kwa kutumia nyaraka za kughushi.

Imeelezwa kwamba, pamoja na kuwa katika orodha ya makampuni yaliyopata fedha za EPA kwa kughushi nyaraka, Jeetu Patel, anaelezwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa timu ya Rais, huku akiwa na kumbukumbu kubwa ya kuchangia kwa kiwango kikubwa kampeni za CCM za mwaka 2005, ikiwa ni pamoja na kuchangia ununuzi wa magari na misaada mingine, mambo ambayo yameelezwa kumpa kinga mfanyabiashara huyo.


Wanaotajwa kuwa wanaweza kufikishwa mahakamani, ni wale ambao kampuni zao zimo katika kampuni zilizochukua jumla ya Shilingi bilioni 44, fedha ambazo wakaguzi walisema wameshindwa kuthibitisha kuwapo kwa jinai na kupendekeza kufanyika kwa ukaguzi mpana zaidi wa kutumia kampuni za kimataifa zenye uzoefu katika uhakiki.

Imeelezwa kwamba kesi zitakazofunguliwa sasa zinalenga kushusha joto la kisiasa lililopanda kutokana na kuonekana kwamba watawala hawachukui hatua thabiti juu ya tuhuma za ufisadi zinazowakabili wanasiasa na matajiri kadhaa walio karibu na chama tawala wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kwa mujibu wa habari hizo, kesi hizo zinatakiwa ziendelee hadi hata baada ya 2010 ili kutoa picha kwamba utawala umedhamiria kupambana na ufisadi hata kama kesi hizo zitakuwa zikitajwa tu na watuhumiwa, hasa wale wa EPA wakiwa ndani chini ya tuhuma kama za hujuma ya uchumi, kughushi na kula njama kuiba.

Wanaotajwa kufikishwa mahakamani ni wamiliki wa kampuni za Changanyikeni Residential Complex Limited, Malegesi Law Chambers, G&T International Limited na Karnel Meals Holdings Ltd zinazomilikiwa na Jose Van de Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina, Beredy Maregesi, Octavio Timoth, Johnson Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukazas.

Raia Mwema limefahamishwa kwamba watakaofikishwa mahakamani kwanza ni Maregesi, Mapunda na Lukaza katika hatua inayozua minong'ono ya kuwa watuhumiwa wakubwa wa fedha za EPA wanakingiwa kifua kwa kuwa wana uhusiano wa karibu na chama tawala ama kuwapo kwa 'mikono michafu'.

"Ni kama sasa wanataka kutolewa kafara. Hata muda uliotolewa wa Oktoba 31 ni kama uliwalenga wao. Wamekuwa wakikataa kurudisha fedha wakidai kwamba wao walifanya kazi, walioiba ni hao ambao sasa wanaelezwa kwamba wamerudisha. Kwamba wao sasa wanataka kushitakiwa huku wakubwa wakiachwa maana yake kubwa ni kwamba watawala wanafunika kombe," alisema mmoja wa watu walio karibu na watuhumiwa hao.

Kampuni zilizokwiba fedha nyingi zaidi kutoka akaunti ya EPA na ambazo sasa kwa utaratibu huu wamiliki wake hawataguswa ni pamoja na ya Kagoda Agricultural Limited kampuni nane za Jeetu Patel.
Kwa mujibu wa wakaguzi, Kagoda ilighushi nyaraka zilizotumika kuchota zaidi ya Shilingi bilioni 40 wakati Jeetu Patel naye amechota zaidi ya nusu ya fedha zilizoibwa akitumia kampuni nane.


Maofisa wa Serikali hususan wale wa vyombo vya dola, wakiwamo wajumbe wa kikosi kazi (task force) kilichokabidhiwa kazi ya kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wahusika waliochota fedha hizo, walipoulizwa kuhusu kushitakiwa kwa wachache tu katika wizi wa EPA wote walidai kwamba muda aliotoa Rais Jakaya Kikwete kukamilika kwa suala hilo haujakwisha na ni yeye mwenye kauli ya mwisho.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), Robert Manumba, ambaye alitajwa na vyanzo vya habari kwamba ofisi yake ndiyo inakamilisha taratibu za kuwashitaki wahusika aliiambia Raia Mwema wiki iliyopita kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa msemaji wa kikosi kazi (task force) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye naye amenukuliwa akisema suala hilo linapaswa kuzungumziwa na Rais ambaye ndiye aliyetoa muda wa ziada.

Kauli kama hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea ambaye naye hakuwa tayari kuzungumzia hatua ambayo wamefikia katika kuwashitaki wahusika, huku Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, akisema kwamba kila kitu kitajulikana siku chache zijazo.

Hata hivyo, Raia Mwema limethibitishiwa kwamba Maregesi, Mapunda na Lukaza, wanatajwa kuwa watu watakaotolewa kafara kutokana na kile kilichoelezwa kwamba wamekuwa na "jeuri ya Kiafrika" kwa kukataa kulipa fedha wanazotuhumiwa kuzichota.

Imeelezwa kwamba tokea awali watuhumiwa hao wamekuwa wakigoma 'kutoa ushirikiano' jambo ambalo limeelezwa kuwakera baadhi ya wanasiasa na watendaji wa Serikali walioamua sasa kuwaburuza mahakamani.

Raia Mwema imethibitisha kwamba bado akaunti na hati za kusafiria za watuhumiwa hao zinaendelea kushikiliwa hata baada ya muda wa miezi sita kisheria kupita kwa maelekezo ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Habari zinaeleza kwamba awali watuhumiwa hao walikuwa wafikishwe mahakamani sambamba na maofisa wa BoT waliohusika katika mchakato wa EPA, lakini uamuzi huo ulibadilishwa baada ya tishio kutoka kwa watumishi hao kwamba 'wataanika' kila kitu hadharani wakitolewa kafara.

"Baada ya watumishi hao wa BoT kutishia kumwaga kila kitu hadharani, mwelekeo umebadilika na sasa wataitwa kama mashahidi wa upande wa serikali kesi hizo zitakapofikishwa mahakamani, lakini bado wanaweza kuiharibia serikali watakapoamua kutaja watu ambao wamefichwa," anasema mtoa habari wetu aliye karibu na vyombo vya dola.

Raia Mwema imefahamishwa kwamba kesi hizo zinatarajiwa kutumika kama mwavuli wa kuivusha serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kukwepa wimbi la manung'uniko ya wazi kwamba serikali ya CCM imekuwa ikiwalea watuhumiwa wa ufisadi, wengi wakiwa ni wafadhili wa chama hicho.

Wakaguzi wa ndani na wale wa nje, walibaini kuwapo kwa wizi mkubwa wa fedha katika akaunti ya EPA katika kipindi cha mwaka mmoja pekee wa 2005/2006 ambako zilipotea zaidi ya Shilingi bilioni 133.

Wakaguzi hao walibaini kwamba kati ya fedha hizo shilingi bilioni 90 ni zile ambazo zimethibitika kuchotwa kwa kutumia nyaraka za kughushi, sehemu kubwa zikiwa zimekwenda kwa wafanyabiashara wawili, wamiliki halisi wa Kagoda Agricultural Limited na Jeetu Patel kupitia kampuni zake nane.

Ripoti ya Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young waliofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilionyesha kwamba kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa kampuni 13 ambazo zilitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi na kwamba kampuni hizo hazikustahili kulipwa chochote.

Wakaguzi hao na Ikulu, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wake, Philemon Luhanjo, Januari 9, 2008, walipendekeza moja kwa moja bila kuuma maneno kwamba wahusika wa kampuni hizo 13 wachukuliwe hatua za kisheria mara moja, kauli ambayo Rais Kikwete aliirejea katika hotuba yake bungeni, lakini bila ukali tena.

Makampuni ambayo Jeetu Patel anahusika nayo na ambayo yamethibitika kughushi nyaraka na kuchota fedha BoT ni Navycut Tobacco (T) Limited, Ndovu Soaps Limited, Bina Resorts Limited, Bencon International Limited, Maltan Mining Company Limited, Bora Hotels & Apartments Limited, Venus Hotels Limited, and B.V. Holdings Limited.

Pamoja na kampuni hizo za Jeetu Patel, kampuni nyingine zilizohusika na jinai ya kughushi nyaraka ni pamoja na Kagoda Agriculture Limited ambayo wanaoonekana katika nyaraka ni John Kyomuhendo mwenye hisa 40 na Francis William anayemiliki hisa 60 katika kampuni hiyo.

Kampuni nyingine ni V.B & Associeties Company zinazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel na Changanyikeni Residential Complex Limited inayomilikiwa na Jose Van de Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina ikiwa na makao yake, Sinza, Kumekucha, Dar es Salaam.

Pia katika orodha hiyo ya kampuni 13 zilizoghushi nyaraka ambazo wahusika wake wamependekezwa kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja ni Money Planners & Consultants inayomilikiwa na Paul Nyingo na Fundi Kitungi na kampuni ya Njake Hotel & Tours Limited inayomilikiwa Japhet Lema, Anna Lema, Abel Lema, Derick Lema na Benard Lema wa Arusha.

Jeetu Patel katika baadhi ya kampuni anashirikiana na wafanyabiashara wengine wa Dar es Salaam ambao wanatajwa kushiriana naye katika kuhamisha fedha hizo kwenda nje kwa kuzibadili kutoka shilingi za Kitanzania kwenda Dola za Merakani ama Euro bila kufuata mkondo halali wa fedha kinyume cha Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu.

Miongoni mwa wanaotajwa kushirikiana na Jeetu Patel ni Sidik Yacoubu kupitia kampuni yao ya Ndovu Soap Limited ambayo kwa mujibu wa nyaraka za Wakala wa Leseni na Usajili wa Kampuni (BRELA), kampuni hiyo yenye namba ya usajili 20536 ya Februari 3, 1992, wamiliki wake ni Jayantulal Chandubhai Patel na Sidik Yacoubu.

Katika kampuni ya Bora Hotels and Apartments iliyosajiliwa Septemba 8, 2005 inaonyeshwa katika orodha ya BRELA kwamba wamiliki wake wamo Jayantkumar Chandubhai Patel na Devandra Patel wakati Bina Resort Limited iliyosajiliwa Machi 31, 2005, wamo Jayantikumar Chandubhai Patel na Devendra Patel.

Kampuni ya Maltan Mining Company iliyosajiliwa Machi 8, 1993 inamilikiwa na Jantkumar Chandubhai Patel na Hariharier Radhakrishna wakati Navy Cut Tobacco iliyosajiliwa Oktoba 12, mwaka 1995 inamilikiwa na Jantkumar Chandubhai Patel na Radakrishna.

Kampuni nyingine ni Bencon Limited, B.V Holdings, Venus Hotels na V.B & Associeties Company zinazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel, ambazo zote zilisajiliwa Aprili 4, 2005.

Katika orodha ya BRELA imo pia kampuni ya Excellent Service Limited inayomilikiwa na Emil Samanya, Peter Sabas na Elisifa Ngowi ambaye anatajwa kuwa ni Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye yumo katika task force inayochunguza wizi huo. Kampuni hiyo ilisajiliwa Mei 13, 1992 na kupewa namba 26959.

Ngowi anahusishwa pia katika kampuni nyingine ya Clyton Marketing iliyosajiliwa Juni 6, 2005 akiwa na mwenzake Edwin Mtoi, ambaye haikuweza kufahamika mara moja anafanya shughuli gani zaidi ya kuwa katika kampuni hiyo.

Wamiliki wengine waliofahamika ni Rajabu Maranda na Thabit Katunda ambao wanatajwa kumiliki kampuni ya Liqiud Service Limited ambayo usajili wake ulifanyika Desemba 12, 2004 na kupewa namba 15007.

Wamiliki wengine waliofahamika ni Johnson Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukaza ambao wao wanamiliki kampuni ya Karnel Meals Holdings Ltd ambayo usajili wake ulipatikana Agosti 4, 1998, Mibale Farm iliyosajiliwa Septemba 2, 2005 na kupewa namba 154039 ambayo inamilikiwa na Kizza Selemani na Farijala Hussein, Malegesi Law Chambers inayomilikiwa na Beredy Malegesi ambayo ilisajiliwa Septemba 24, 2001.

Wamiliki wengine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki Kampuni ya Money Planners & Consultants iliyosajiliwa Machi 22, 2005 na Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa, ambayo ilisajiliwa Aprili 8, 2005.

Katika ukusanyaji wa fedha hizo, task force ya serikali inaelezwa kukusanya shilingi 53,738,835,392/= fedha ambazo Rais Kikwete ameagiza ziingizwe katika mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo zikichanganywa na nyingine zinazotarajiwa kufikia shilingi 64,844,770,688/= .
 
Halisi, hapo umenichangaya (samahani lakini nipo slow kidogo nadhani)... Una maana wamekataliwa dhamana?? Kingine ni kama una nyeti za makosa waliyosomewa manake hapo napo kuna mtego!!

Asante kwa dataz kaka manake hii kitu imefanywa - KIMYA KIMYA..........

Finaly...............Imani imenaza kurudi lakini mkuu hayo maswali mawili yatasaidia zaidi Mkuu.... Asante
 
Last edited:
Halisi, hapo umenichangaya (samahani lakini nipo slow kidogo nadhani)... Una maana wamekataliwa rufaa?? Kingine ni kama una nyeti za makosa waliyosomewa manake hapo napo kuna mtego!!

Asante kwa dataz kaka manake hii kitu imefanywa - KIMYA KIMYA..........

Finaly...............Imani imenaza kurudi lakini mkuu hayo maswali mawili yatasaidia zaidi Mkuu.... Asante

Habari ni kwamba kwa sasa wamefika kumi na tisa ni Wahindi mmoja Mwafrika. Angalieni Chanell ten muda si mrefu
 
Jamani kwani Jeet Patel bado yupo bongo?
Si nasikia alisha anza long time.
 
Halisi, hapo umenichangaya (samahani lakini nipo slow kidogo nadhani)... Una maana wamekataliwa rufaa?? Kingine ni kama una nyeti za makosa waliyosomewa manake hapo napo kuna mtego!!

Asante kwa dataz kaka manake hii kitu imefanywa - KIMYA KIMYA..........

Finaly...............Imani imenaza kurudi lakini mkuu hayo maswali mawili yatasaidia zaidi Mkuu.... Asante

Nadhani alikuwa anamaanisha wamenyimwa dhamana
 
Habari ni kwamba kwa sasa wamefika kumi na tisa ni Wahindi mmoja Mwafrika. Angalieni Chanell ten muda si mrefu

Una maana jumla wako 10. kati yao ni wahindi 9 na mwafrika 1 ama nimechanganya mambo?
 
Inavyoonekana wanapeleka mahakamani jalada moja moja na hilo ni lile la Jeetu na washirika wake
 
Ochu, bluhende, Boniface G. Mduma, Dark City, Domo Kaya, Freetown, Halisi, Kinyamana, Lione, Madaha, mahesabu, Maskini Mimi, Mfuatiliaji, Mtu Kwao, MyTanzania, Nungunungu, pingiring'ombe, Shy, ThinkPad, wendos, WomenofSubstanc

all these people are in suspense!!!

Umejuaje? Au na wewe ni shekh Yahya Hussein!! I look like Thomas
 
Halisi hapa naangalia Channel ten sioni ama wameshatangaza. Ama ulihisi tu kuwa wataonyesha?
 
@ # 53,

Using the Sheikh Yahya called 'Currently Active Users Viewing This Thread' at bottom of this very thread..

Karibu
 
Wametoa tangazo la maandishi chini ya TV lisemalo " WATUHUMIWA WA FEDHA ZA EPA WAMEFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM LEO"
 
Jeetu Patel na wengine jumla wako saba wa EPA akiwamo wakili anayetajwa kwa jina la kamala na mwanamke mmoja

Halisi vipi tena ndugu yangu? Mbona unatuacha solemba? Ni kweli JF tunapenda kupata habari moto moto tena nyeti ambazo ndiyo kwanza zimeipuliwa toka jikoni, lakini ni vizuri kuwa na habari kamili inayoeleweka kwa wasomaji wa JF na pia kuifanyia uchunguzi (kama inawezekana) ili kujua ukweli wa habari hiyo. Vinginevyo tutaanza kuweka madudu hapa baadaye ikaja julikana kwamba ilikuwa ni udaku tu. Tusishushe hadhi ya JF.
Haya siku na kazi njema :)
 
Back
Top Bottom