Emotional Intelligence ni nini? Unawezaje kuifikia au kuipata?

Wenyewe wanasema emotional intelligence ni uwezo wa kuzitambua hisia zako pamoja na kuzicontrol katika mazingira tofauti tofauti
Sio hivyo tu emotional intelligence inajumuisha pia uwezo wa kutambua hisia za wanaokuzunguna na kureact kwazo in a friendly way .
Emotional intelligence ni miongoni 21st century skills muhimu sana katika maisha ya sasa ya mwandamu because when you are good at emotional intelligence una uwezo wa ku control mambo mengi sana in today's world.
Emotional intelligence inaenda mbali zaidi na kugusa mambo ya personal branding, team work, na vingine vingi kama hivyoo
Hicho ndo kitu kidogo nnachoweza kushare na wew about emotional intelligence kutokana na nilivo fundishwa na ninavyoielewa.
Maelezo mazuri. Kwa namna nyingine: mfano ukizidiwa na hasira ukatukana mtu wewe sio emotionally intelligent. Kukasirika hovyo au kirahisi sio emotional intelligence. Kufurahi mno hadi unalia sio emotional intelligence. Kuchukia kitu au mtu hadi unachanganyikiwa sio emotional intelligence. Kuonesha furaha penye huzuni au huzuni penye furaha sio EI. Kushindwa kuonesha furaha penye furaha sio emotional intelligence.

Emotional intelligence ni uwezo wa kumudu hisia zako na kuonesha hisia sahihi kwa jambo husika.
 
Kulingana na Wanasaikolojia,kuna aina nne za Akili:

1)Kiasi cha akili ya Uelewa (IQ)- Intelligence Quotient.

2) Kiwango cha akili ya Kihisia (EQ)- Emotional Quotient.

3) Kiwango cha akili ya kushiriki mambo ya Kijamii (SQ)- Social Quotient.

4) Kiwango cha akili ya kuhimili Shida (AQ)-Adversity Quotient.

1.Intelligence Quotient (IQ):

hiki ndicho kipimo cha kiwango chako cha ufahamu. Unahitaji IQ kutatua hesabu, kukariri vitu, na kukumbuka masomo.(Genius)


2.Emotional Quotient (EQ):

Hiki ni kipimo cha uwezo wako wa kudumisha amani na wengine, kuweka muda, kuwajibika, kuwa mwaminifu, kuheshimu mipaka, kuwa mnyenyekevu, mkweli na mwenye kujali.


3.Social Quotient (SQ):

Hiki ni kipimo cha uwezo wako wa kujenga mtandao wa marafiki na kuudumisha kwa muda mrefu.

Watu ambao wana EmotimalQ ya juu na SocualQ huwa wanaenda mbali zaidi maishani kuliko wale walio na IntelligenQ ya juu lakini EmotionalQ ya chini na SocialQ.

Shule nyingi hujali zaidi katika kuboresha viwango vya IQ huku EmotionalQ na SocialQ zikiachwa chini.

Mtu mwenye IQ ya juu anaweza kuishia kuajiriwa na mtu mwenye EmotionalQ ya juu na SocialQ ingawa ana IQ ya wastani.

EmotionalQ yako inawakilisha Tabia yako,wakati SocialQ yako inawakilisha karisma yako.

Zingatia tabia ambazo zitaboresha mambo haya matatu lakini haswa EmotionalQ yako na SocialQ.

Sasa kuna aina ya 4 ya akili ambayo ni dhana mpya:


4.Kiwango cha akili ya ustahimilivu wa mambo Magumu (AQ): Adversity Quotient.

Kipimo cha uwezo wako wa kupitia sehemu mbaya ya maisha,na kutoka humo bila kupoteza akili yako(ku-loose focus) inapokabiliwa na matatizo,

AdversityQ huamua ni nani atakayekubali kuacha jambo,ni nani atakayeiacha familia yake, na nani atafikiria hata kujiua.

Wazazi tafadhali fundisheni watoto wenu maeneo mengine ya maisha kuliko Masomo tu pekee.

Watoto wanapaswa kupenda kazi za mikono (kamwe wasione kazi kama aina ya adhabu),wajifunze na kufundishwa pia Michezo na Sanaa.

Kuendeleza IQ yao, pamoja na EmotionalQ yao,SocialQ na AdversityQ.

Wanapaswa kuwa wanadamu wenye sura nyingi za uelewa na wenye uwezo wa kufanya mambo bila ya nyinyi wazazi wao.

Mwisho, usiwatayarishie watoto wako barabara.
Tayarisheni watoto wenu namna kwa ajili ya kupita barabarani

View attachment 2548267
Yaani Bora EQ kuliko IQ.
Mana ukiwa na high IQ unakuwa Kama robot Ila the highest EQ ndio unakuwa binadamu zaidi.
Big up mno mkuu nimependa hii nawaza hata tuwe tunachati hizi mambo always na wewe
 
Kwa kifupi sana...

Uwezo wa kuwa na ufahamu wa hisia zako, uwezo wa kudhibiti hisia zako, uwezo wa kuelewa hisia za wengine, uwezo wa kujenga uhusiano wa karibu na wengine, na uwezo wa kutatua migogoro kwa njia ya kuheshimu hisia za wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom