Emotional Intelligence ni nini? Unawezaje kuifikia au kuipata?

Habari za leo ndugu na dada zangu wa hapa jukwaani? Natumai kuwa nyote hamjambo, wenye changamoto poleni, YATAPITA.

Tafadhali husika na kichwa cha habari.

Naomba kujuzwa au kuelimishwa juu ya EMOTIONAL INTELLIGENCE.

Kwanza ni nini?
Pili ninawezaje kuifikia au kuipata? Maana naona huenda likawa ni jambo muhimu sana maishani.

Nimetafuta google lakini maelezo yake hayajanitosha..

Natanguliza shukrani..
Kwanza umeleta swala muhimu sana hongera kwa hilo

Nielewavyo ni kuwa Emotional Intelligence (EI) ni hali ya kuweza kuzielewa, kuzidhibiti na kuzisimamia hisia zako binafsi na kuzielewa hisia za wengine.

Hisia ni mihemko ambayo inachochewa na kemikali ndani ya miili yetu, ambazo huwa ni majibu (response) za mazingira au matukio fulani, mfano Furaha, Chuki, Huzuni, Upendo, Hamu n.k

JINSI YA KUIPATA EI
Nitakwambia kwa uzoefu wangu.
Ni mchakato mgumu ambao unajumuisha kuzielewa, kuzisimamia na kuzidhibiti hisia zako.

Kwanza ni lazima ujijue kwanini Unahisi huzuni au furaha au hasira au chuki… kujua huku si kuishia kuwa unahisi chuki kwakuwa fulani kakukera, hapana. Hiyo ni Konklusheni nyepesi sana

Lazima uelewe ukikasirika ni nini exactly kinatokea kwenye mwili wako hapa nazungumzia kemikali gani ina react vipi

(Ukifanikiwa hili wallah utajiona sio wa kawaida, unaweza jua haya kwa kusoma na kuwa mdadisi sana hapa sana sana ni biology)

Ukifanikiwa ukiudhiwa unakuwa unajua; fulani kakuudhi lakini mwili wako umereact kwa kutoa kemikali fulani inayokufanya kuhisi hivyo unavyohisi

Lakini pia ni kwa ku reason; ukiwa mtu wa reasoning hisia unakuwa unazielewa sana

Mfano mtu kakutukana… ukiwa mtu wa reasoning utaanA kutafuta sababu ya kwanini kakutukana, alivyokutukana anajisikiaje,
(Reasoning hutumia hisia ila unatafuta sababu ya kila kitu)
Kiukweli ukimaster hii kitu unakuwa mtu huru sana, unakuwa na uwezo wa kuelewa matendo ya wengine juu yako na utaweza kujielewa vyema wewe mwenyewe.

NB: Nimeeleza kwa uzoefu wangu binafsu tu
 
Lazima uelewe ukikasirika ni nini exactly kinatokea kwenye mwili wako hapa nazungumzia kemikali gani ina react
Ahsante mkuu, kuzama kwenye kujijua biologically na kuboresha reasoning ni key take aways..
 
EI is very important than IQ.
Sema hili somo Ni Pana mno yaani mno.

Nikuulize swali nikikutukana unakasirika na kuumia tusi fulani kwa kiswahili. Ila tusi Ilo Ilo nikikutukana kwa lugha usiyoielewa hukasiriki so Yale maumivu huwa yanatokea wapi.

Pia why unafurahi ukila chakula kizuri na kitamu ama ukasifiwa yaani Ni Nini kinafanya mpaka unafurahia mfano unafanyiwa masaje,ukavuta bangi etc
 
Kuhus tusi ni kwa vile sielewi lugha uliyotumia, chakula na bangi reward system kwenye ubongo inakuwa activated DOPAMINE INAKUWA RELEASED..

Though sijaelewa haya yanahusiana vipi na EQ??
 
U
Kwanza umeleta swala muhimu sana hongera kwa hilo

Nielewavyo ni kuwa Emotional Intelligence (EI) ni hali ya kuweza kuzielewa, kuzidhibiti na kuzisimamia hisia zako binafsi na kuzielewa hisia za wengine.

Hisia ni mihemko ambayo inachochewa na kemikali ndani ya miili yetu, ambazo huwa ni majibu (response) za mazingira au matukio fulani, mfano Furaha, Chuki, Huzuni, Upendo, Hamu n.k

JINSI YA KUIPATA EI
Nitakwambia kwa uzoefu wangu.
Ni mchakato mgumu ambao unajumuisha kuzielewa, kuzisimamia na kuzidhibiti hisia zako.

Kwanza ni lazima ujijue kwanini Unahisi huzuni au furaha au hasira au chuki… kujua huku si kuishia kuwa unahisi chuki kwakuwa fulani kakukera, hapana. Hiyo ni Konklusheni nyepesi sana

Lazima uelewe ukikasirika ni nini exactly kinatokea kwenye mwili wako hapa nazungumzia kemikali gani ina react vipi

(Ukifanikiwa hili wallah utajiona sio wa kawaida, unaweza jua haya kwa kusoma na kuwa mdadisi sana hapa sana sana ni biology)

Ukifanikiwa ukiudhiwa unakuwa unajua; fulani kakuudhi lakini mwili wako umereact kwa kutoa kemikali fulani inayokufanya kuhisi hivyo unavyohisi

Lakini pia ni kwa ku reason; ukiwa mtu wa reasoning hisia unakuwa unazielewa sana

Mfano mtu kakutukana… ukiwa mtu wa reasoning utaanA kutafuta sababu ya kwanini kakutukana, alivyokutukana anajisikiaje,
(Reasoning hutumia hisia ila unatafuta sababu ya kila kitu)
Kiukweli ukimaster hii kitu unakuwa mtu huru sana, unakuwa na uwezo wa kuelewa matendo ya wengine juu yako na utaweza kujielewa vyema wewe mwenyewe.

NB: Nimeeleza kwa uzoefu wangu binafsu tu
Perfecto
 
Yaani binadamu tumeumbwa na hisia mbalimbali kv ; fear,hope, greedy, envy,ego, happiness,angry,etc so maamuzi huwa tunafanya kulingana kuwa unajisikiaje mfano ukiwa umeshiba ama una Hali nzuri maongezi yako yata base kwenye Hali yako ya kushiba tumbo ama mfukoni kinyume chake pia ukiwa na njaa story zinabadilika.
Yaani ndio Mana unaona mtu akishalewa akafurahi anatoa ahadi nzuri nzuri na akiwa amekasirika anatoa ahadi kulingana na hisia zake
 
Tunafanya maamuzi kulingana na hisia na sio hii logic or reasoning brain ,na ndio Mana ukitegwa kingono unaingia mkenge baadaye unarudiwa na fahamu unajiuliza why ulifanya vile.
So Kuna eneo la ubongo dogo mno ambalo linitwa amygdala ama brain linalodili na hisia.
Kuna cortex brain inayodili na logic.
Limbic brain Ina dili na belongings mfano ukiwa unaendesha BMW unajiona kuwa u wa thamani kuliko mie mwenye baiskeli
 
Hii topic kubwa yaani mno kuliko unavyoweza kudhania naweza ijaza server.

Yaani Ni logic ama reasoning braining huwa inakuja ku rationalize emotions Ni kwa Nini umefanya tukio fulani Ila muda unalifanya huu ubongo wa kibinadamu unazidiwaga na emotional brain ndugu zangu. Why jiulize ikitokea Hali ya hatari like kuvamiwa,ama Simba ama Moto imetokea amygdala Ina hijack,or Ina bypass central neuropathway from cortex to amygdala brain kufanya maamuzi ya fasta mno yaani in lightning speed ambayo hata mie na wewe hatujui.
Haya maamuzi huwa Ni matatu; freeze,flight or fight back.
Na ndio Mana ukiwa kwa Hali iyo unaua baadaye ndio unakuja kuwaza kwa akili ya cortex brain.

Yaani hii amygdala huwa inaitwa caveman brain. It's the brain that we inherited from our cavemen ancestors.
During that time they needed very fast lightning speed decision to survive Mana wanyama wa kuwala walikuwepo nje nje.

So pia hii ndio region inayo defend one self, survive,self image, na ndio Mana ukitukanwa unapigana kuilinda self image Kama uhai wako ama kutaka kukubalika Ina your tribal
 
Hii wanaitumia mno hata wafanyabiashara wakubwa wenye makampuni ku trigger your emotions Mana zikishakuwa juu huwezi fanya normal decision unanunua kitu kisa ulivutiwaa na mwanamke mzuri aliyekuletea huduma.
Ama unanua kitu kisa ronado anakutumia so it's feel Inadequacy mpaka ukitumie na wewe utajiona unalingana na huyo mtumiaje hadhi.
Mana kutokana na ego yaani tumeumbwa wote tuna ego sema Ile intensity or magnitude ama asilimia Zina differ.

Mfano wote Ni wavivu Ila tunazidiana viwango.
Wote tunapenda Raha Ila tunazidiana.

Yaani emotions are biological huwezi kuzitoa kwa binadamu sio psychological.
 
Hili ni somo pana sana....
 
Kulingana na Wanasaikolojia,kuna aina nne za Akili:

1)Kiasi cha akili ya Uelewa (IQ)- Intelligence Quotient.

2) Kiwango cha akili ya Kihisia (EQ)- Emotional Quotient.

3) Kiwango cha akili ya kushiriki mambo ya Kijamii (SQ)- Social Quotient.

4) Kiwango cha akili ya kuhimili Shida (AQ)-Adversity Quotient.

1.Intelligence Quotient (IQ):

hiki ndicho kipimo cha kiwango chako cha ufahamu. Unahitaji IQ kutatua hesabu, kukariri vitu, na kukumbuka masomo.(Genius)

2.Emotional Quotient (EQ):

Hiki ni kipimo cha uwezo wako wa kudumisha amani na wengine, kuweka muda, kuwajibika, kuwa mwaminifu, kuheshimu mipaka, kuwa mnyenyekevu, mkweli na mwenye kujali.

3.Social Quotient (SQ):

Hiki ni kipimo cha uwezo wako wa kujenga mtandao wa marafiki na kuudumisha kwa muda mrefu.

Watu ambao wana EmotimalQ ya juu na SocualQ huwa wanaenda mbali zaidi maishani kuliko wale walio na IntelligenQ ya juu lakini EmotionalQ ya chini na SocialQ.

Shule nyingi hujali zaidi katika kuboresha viwango vya IQ huku EmotionalQ na SocialQ zikiachwa chini.

Mtu mwenye IQ ya juu anaweza kuishia kuajiriwa na mtu mwenye EmotionalQ ya juu na SocialQ ingawa ana IQ ya wastani.

EmotionalQ yako inawakilisha Tabia yako,wakati SocialQ yako inawakilisha karisma yako.

Zingatia tabia ambazo zitaboresha mambo haya matatu lakini haswa EmotionalQ yako na SocialQ.

Sasa kuna aina ya 4 ya akili ambayo ni dhana mpya:

4.Kiwango cha akili ya ustahimilivu wa mambo Magumu (AQ): Adversity Quotient.

Kipimo cha uwezo wako wa kupitia sehemu mbaya ya maisha,na kutoka humo bila kupoteza akili yako(ku-loose focus) inapokabiliwa na matatizo,

AdversityQ huamua ni nani atakayekubali kuacha jambo,ni nani atakayeiacha familia yake, na nani atafikiria hata kujiua.

Wazazi tafadhali fundisheni watoto wenu maeneo mengine ya maisha kuliko Masomo tu pekee.

Watoto wanapaswa kupenda kazi za mikono (kamwe wasione kazi kama aina ya adhabu),wajifunze na kufundishwa pia Michezo na Sanaa.

Kuendeleza IQ yao, pamoja na EmotionalQ yao,SocialQ na AdversityQ.

Wanapaswa kuwa wanadamu wenye sura nyingi za uelewa na wenye uwezo wa kufanya mambo bila ya nyinyi wazazi wao.

Mwisho, usiwatayarishie watoto wako barabara.
Tayarisheni watoto wenu namna kwa ajili ya kupita barabarani

IMG_20230313_064504.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom