Elimu ya kova inanipa utata

Swala la bwana Muro Polisi wanalichululia kishabiki kwamba wamempata mtu alie waumbua, Kova alikua anaonekana anavutia upande wa jeshi la polisi na jinsi hata Muro alivyo kamatwa inaonekana kabisa iwe isiwe askari walikua wanamtaka siku hiyo lakini inaonyesha wazi kabisa jinsi askari polisi wa Tanzania wanavyo fanya kazi (UN PROFESSIONAL) pia huwa hawana changamoto kabisa issue ya Muro inaonekana ni issue kubwa wakati kuna mambo mengi sana yanatokea, wanashindwa kuwadhibiti Wasomali wanao ingia nchini, kuna Wanyarwanda wanaosumbua Biharamuro wanahangaikia swala la rushwa, Naomba niulize swali JE PCCB WAKO WAPI?.
 
Naona hakuna mtu anayejua CV yake,mpaka niko page 5 sasa!
Ukichukua majiji makubwa ya dunia ,Kamanda wa polisi amesoma sana,maana hapa sio polisi tu,kuna administration,politics skills etc.Ukichukua kama jiji la London,the last kamanda ,alikuwa na digrii ya Oxford,ine of the top university in the worlsd.

Bongo sasa hivi tuna mediocre wengi sana,sababu ya elitism na udini
 
.... mwambie ashuke ung'eng'e kama ataweza

Binafshi nadhani Ung'eng'e hauhusiani kabisa na utendaji wake wa kazi! Kama utendaji wake wa kazi ni m bovu basi hapo ni tatizo, ila kama utendaji wake wa kazi ni mzuri lakini hajui ung'eng'e mimi binafsi sioni tatizo kabisa.

Sidhani kama ana tofauti na wakuu wengine wa jeshi la polisi au viongozi wetu wengi tu nchini. Yeye hapo labda tumtumie tu kama kielelezo (spaceman) ya viongozi wetu nchini na wengi wao wanavyopenda kuongea kabla hawajafikiri.

Je huko ni kutafuta sifa? Labda, kutoelewa mambo? Labda, shule ndogo? labda!, papara? pia inawezakana....Ama labda utawanzi na 24/7 media inawazuzua. Kwani hatu ndugu yetu Jerry naye anafanya vivyo hivyo!


"...Bongo sasa hivi tuna mediocre wengi sana,sababu ya elitism na udini"

Nadhania huo ndo ugonjwa sugu unaotukabili, kwani hata hapa Jamii Forums wengi wanachekeana kinafiki tu, udini umewajaa!

Na kwa sababu hiyo ndo maana mara nyingi nakimbilia kule kwenye lugha kwani mijadala yote lazima udini udini uingizwe kwa njia moja au nyingine!

Huyu Kova na Tibaigana binafsi naona wanafanana kwa mengi na wote media 24/7 inawazuzua bado!

Hebu fikiria kama Kova anakuwa IGP na Makamba anakuwa Rais, Agness Nyoni aliyeko Afya awe Katibu Mkuu Kiongozi, Waziri wa fedha awe Gavana wetu wa sasa na Waziri mkuu awe Pesambili. Mwanasheria wa serikali awe nani nani yuleeeee mwanasheria aliyehama kutoka CHADEMA kwenda kuwa mawanasheria wa CCM. Kiongozi wa upinzani awe Mtikila. Patakalika mkao gani Tanzania? ....Leka
Kwani hao wote uliowataja si ndiyo wanaosababisha watanzania tunapelekwe puta hivyo? wote ni vilaza kwa aina moja au nyingine, matokeo yake sisi ndiyo tunalipia umbumbumbu wao na mara nyingi kwa roho zetu! wengine tuliobaki ni longolongo tu, hakuna anayefanya kufanya kweli hata mmoja!
 
Communication ni tatizo la kitaifa bongo.

I miss Kuhani at times like these.

By the way hata Jerry naye ana mengi ya kujifunza. Wote walikuwa wanaongea kama wako kijiweni fulani hivi tu.

Jerry anafoka Kova ni mtu mdogo tu, Kova ni RPC wa Dar at that, Jerry yeye ana ukubwa gani wa kusema Kova mdogo?

Nami nilimuona Jerry akijitutumua kuhusu udogo wa Kova, kwa kweli alinilinisikitisha sana, sikutegemea aseme maneno yale
 
issue ya jerry, ni kova amehamanika tuu, elimu yake fresh tuu. Nakumbuka nilimuona kamanda zombe siku alipokaimu nafasi ya tibaigana, wakati akitangaza zile habari za polisi kufanikiwa kuwauwa wale majambaz wanne msitu wa pande, baada ya kujibizana risasi na polisi, alitangaza kwa masifa sana, na kuita waandishi kushuhudia polisi wakipongezwa, kilichofuatia sote tunakijua.

Ukimuona kamanda kova anavyoongea, ni wazi, anaongea kwa masifa na mapozi ya kusmile mbele ya camera. Kamanda tibaigana pia alikuwa akiongea na waandishi daily ila was serious.

Pamoja na elimu zao zote, pia ni kweli na kuna uthibitisho, debe tupu hupiga kelele!. Si unaonaga mwenyewe hata baadhi ya magreat thinkers miongoni mwetu humu jf yunavyopigaga kelele za kidebe tupu?.

mimi hata sijakuelewa nini unaeleza hapa............
 
Back
Top Bottom