Elimu ya CCM kuhusu uwekezaji wa bandari yahamia kaskazini

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,829
21,460
Babati. Katibu Mku wa CCM, Daniel Chongolo kesho atawahutubia wanachama na viongozi wa chama hicho wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Lengo la mkutano huo ni kuwajengea uelewa kuhusu mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai, yanayohusisha uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Mkutano huo ni mwendelezo wa kiongozi huyo, baada ya kuifanya katika mikoa ya nyanda za juu kusini (Mbeya, Njombe na Iringa), uliofanyika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya. Pia Chongolo aliyeambata na mawaziri wa sekta ya uchukuzi alifanya hivyo kwa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara, Peter Toima amewaambia wanahabari leo Ijumaa Julai 21, 2023 mjini Babati mkoani Manyara kuwa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika huku akiwataka wanachama wa mikoa hiyo kuhudhuria kwa wingi.

Toima amesema kupitia mkutano huo wanachama na viongozi wa CCM Arusha, Kilimanjaro na Manyara, watapata uelewa sahihi kuhusu suala la uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam lililoibua mjadala hadi sasa.

“Lengo ni kuondoa mijadala potofu iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa bandari ya Dar es Salaam imeuzwa ilihali siyo jambo la kweli.Suala la uwekezaji lipo kwenye ilani ya uchaguzi wa CCM wa mwaka 2020/2025, " amesema Toima.

Toima amesema wanachama na viongozi wa CCM wa kanda ya kaskazini, wanapaswa kushiriki kwenye mkutano ili kumsikiliza Chongolo na kwenda kuyaeneza kwenye matawi na mashina.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Simanjiro, Mosses Makeseni amesema wameshatoa taarifa kwa viongozi wa kata zote ili kuhakikisha wanajitokeza kwenye mkutano huo.
 
Kazi kweli kweli.
Baba ana ndevu.
Mtoto ana ndevu.
Dada ana ndevu.
Mama ana ndevu.
Kaka ana ndevu.
Nchi ya kambale.
Haijulikani nani ni nani na anatakiwa afanye nini na wakati gani!
 
Mkataba usingevuja kwa bahati mbaya hiyo Elimu wangeitoa lini?
 
Babati. Katibu Mku wa CCM, Daniel Chongolo kesho atawahutubia wanachama na viongozi wa chama hicho wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Hawa ccm kwenye chama Chao hakuna wanasheria wa kuchambua mafungu ya mkataba wa dpworld yanayolalamikiwa badala ya kuedelea kusikiliza hawa ambao siyo wanasheria?
 
Katibu Mwenezi CCM anasema..Bandari haijauzwa Kwani kinachouzwa huwa kinawekwa kwenye mfuko au begi !?Sasa badandari haiingii kwenye Begi inauzwaje!
 
ccm wajue huku kaskazini ujinga tulishaukataa zamani hatuhitaji udanganyifu wao wakabaki kule kule dodoma na Tabora
 
Babati. Katibu Mku wa CCM, Daniel Chongolo kesho atawahutubia wanachama na viongozi wa chama hicho wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

Lengo la mkutano huo ni kuwajengea uelewa kuhusu mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai, yanayohusisha uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Mkutano huo ni mwendelezo wa kiongozi huyo, baada ya kuifanya katika mikoa ya nyanda za juu kusini (Mbeya, Njombe na Iringa), uliofanyika uwanja wa Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya. Pia Chongolo aliyeambata na mawaziri wa sekta ya uchukuzi alifanya hivyo kwa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara, Peter Toima amewaambia wanahabari leo Ijumaa Julai 21, 2023 mjini Babati mkoani Manyara kuwa maandalizi ya mkutano huo yamekamilika huku akiwataka wanachama wa mikoa hiyo kuhudhuria kwa wingi.

Toima amesema kupitia mkutano huo wanachama na viongozi wa CCM Arusha, Kilimanjaro na Manyara, watapata uelewa sahihi kuhusu suala la uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam lililoibua mjadala hadi sasa.

“Lengo ni kuondoa mijadala potofu iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa bandari ya Dar es Salaam imeuzwa ilihali siyo jambo la kweli.Suala la uwekezaji lipo kwenye ilani ya uchaguzi wa CCM wa mwaka 2020/2025, " amesema Toima.

Toima amesema wanachama na viongozi wa CCM wa kanda ya kaskazini, wanapaswa kushiriki kwenye mkutano ili kumsikiliza Chongolo na kwenda kuyaeneza kwenye matawi na mashina.

Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Simanjiro, Mosses Makeseni amesema wameshatoa taarifa kwa viongozi wa kata zote ili kuhakikisha wanajitokeza kwenye mkutano huo.
Chongololo aulizwe ikiwa anaweza kuwauzia wageni makaburi ya ukoo wao!!!

Bandari zetu ni URITHI wetu, hazitauzwa, kubinafsishwa Wala kugawiwa Bure Kwa wageni.

Pia wajue kuwa RUSHWA Huwa haidaiwi irudishwe mahakamani!!!

Epuka matapeli 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom