Elimu Tanzania uwafikie TIE

A Father

JF-Expert Member
Nov 11, 2012
1,206
373
Hakuna taasisi ya elimu ya ajabu kama yetu. Kweli kabisa inakera mara hakuna idadi. Kuna wakati natamani sijui ukutane nao wapi uwarushie hata mawe au kuwamwagia kinyesi. Just think.

Hii taasisi ina jukumu, yaani ni wajibu wao kuhakikisha vitabu hasa vya kiada vinakuwepo kwa wanafunzi wote wa Tanzania. Haijaleta shuleni hata kitabu kimoja, mwaka wa Tano sasa, yaani kuna wanafunzi wapo kidato cha tano hawajawahi kuipata huduma yao; walimu na wanafunzi tuna hangaika kutafuta materials, wao wanatuwekea tusome mtandaoni, kweli? Kila kitu ni biashara kweli! Yaani wanafunzi hawaruhusiwi kumiliki simu, afu unawawekea kusomea mtandaoni, sasa kama kuwapiga mawe au kuwamwagia mavi hakuwafai ni nini kuna wafaa? Je, wanafunzi watoe wapi hela ya kununua bundles daily? Mbona vitabu vya Kenya, Uganda na Rwanda East Africa hii hii tunadownload freeee? Na angalia wanavyotoboa. Tizama ubora wa elimu katika nchi zao. Leo hii, nchi yenye wakazi kama DSM kubwa kama Itigi, inatoa makocha, wafanyabiashara wakubwa na wataalamu wa IT, wachezaji wengi wa kimataifa, mainjinia na walimu bora hadi wa kiswahili, sisi milioni 60, hatuna hata kocha mmoja maarufu katika tasnia ya soka. Kila kitu ni dili tu.

Kwani wakiweka katika PDF, watu wakadownload, hata wasipo let's shuleni, si inatosha? Vitabu vyenyewe huwa vimeandikwa haviuzwi, isipokuwa vile feki vilivyouzwa 8,000/@ kitabu. Kweli, mwanafunzi anasomeshwa bure, na taasisi ya serikali inamuuzia kitabu kweli? Huu ujumbe naomba uwafikie. Binafsi siwaelewi hata kidogo. Wanafanya kazi yetu walimu kuwa ngumu sana. Lakini hawaonekani kama wanachangia kudororesha elimu ya nchi hii. Wanavaa suti na nguo za vitenge, wanaendeshwa kwenye magari ya serikali na kuishi kwenye ofisi za kupendeza, lakini sijui wanafanya nini? Kuna taasisi hata zikifutwa, nchi haitojua. Wanashindwaje kuwaiga NECTA? Kama taasisi zote nchi hii zingefanya kazi kama NECTA walau kwa asilimia 50% tu, tungekuwa mbali sana. Nashauri, taasisi ifumuliwe kwa viongozi wake kuwajibishwa. Huu ndio ujumbe naenda kumtumia waziri wa Elimu na waziri wa wizara yetu ambaye ni Rais.

 
Serikali nayo kama haioni, hivi Hawa wezi kuIbana hizi taasisi kweli kujua namna gani elimu inadorora na wao wapo? Yaani kila mtu amekua mtu wa mchongo tu.. Apigw ale pesa apotee.. Hawa jua watoto na wajukuu wao ni waathirika wa matendo yao😢😢😢
 
Back
Top Bottom