Edward Lowassa: Mwanasiasa, mchapakazi, mfanyabiashara anayetabasamu!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Lowassa.jpg

Edward Ngoyayi Lowassa ni mwanasiasa na mjasiliasiasa nchini Tanzania, mfanyabiashara wa anga za ukanda huu wa kusini mwa Jangwa la Sahara, Mume wa Bibi Regina na Baba wa Familia huru. Safari ya maisha ya Lowassa ni safari ndefu yenye milima na vilima vingi vyenye kusukuma hadi utosi wa unywele zake mweupe. Maisha ya Edward Lowassa yanaanzia katika vilindi vya upwa wa Monduli kunako Mkoa wa Arusha chini ya vipaji na mapaji ya Mzee Ngoyayi siku ya Alhamisi ya saa nne za asubuhi kwa majira Afrika Mashariki katika Boma la mzee Ngoyayi katika tarehe 26 ya mwezi 8, mwaka 1953

Edward Ngoyayi Lowassa alianza masomo ya shule ya msingi katika vilima na vilindi vya upwa wa Monduli tarehe sita ya mwezi kwanza kwa mwaka 1961 na kuhitimu masomo hayo ya msingi mwaka 1967. Tarifa za maendeleo yake shuleni zinamuweka kwenye sehemu ya wanafunzi waliotoka kundi la wafugaji wenye uwezo mzuri darasani hali iliyomfanya afaulu kujiunga na Shule ya sekondari ya Arusha mwaka 1968, Bado Lowassa aliendele kudhihirisha uwezo wake darasani ambapo mwaka 1971 alihitimu vizuri na kufanikiwa kujiunga na masomo ya kidato cha sita mwaka 1972 katika shule ya vipaji maalumu ya Tabora na kuhitimu mwaka 1973.

Uwezo wa Edward Lowassa ulikuwa mzuri zaidi darasani ambapo mwaka 1974 alijiunga na Chuo kikuu Dar es Salaam akichukua shahada ya kwanza katika taaluma ya MAZINGAOMBWE, ambapo mwaka 1977 alihitimu akiwa ni muigizaji mzuri wa mazingaombwe na tamthiria aliyepikwa kitaalamu kabisa, Edward Lowassa alijaribu kwa miaka sita akisota kusaka ajira ama kujiajiri kupitia taaluma yake lakini kwa bahati mbaya soko la filamu na mazingaombwe lilikuwa duni nchini, hivyo mwaka 1983 aliamua kurudi masomoni kusaka fani nyingine ambapo mwaka 1984 alipata shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini Uingereza.

Baada ya kuhitimu shahada ya pili, Lowassa alifanikiwa kupata kazi serikali akihudumu nafasi ya Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993) na Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989 - 1990) na mwisho akahudumu Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umasini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000).

Mwaka 1990 uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja Lowasa alichaguliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano akichukua nafasi ya Luteni Lepilal Ole Molomeit Baada Ya Jimbo La Uchaguzi La Longido Kuanzishwa Na kumshinda Dr Toure Katika Kinyanyang'anyiro Cha Ubunge

KISIASA.

Siasa za Lowassa ni siasa za mrengo wa kulia zinazoishi na kuamini katika uwezo wa fedha na shibe, Lowassa ni muumini mzuri wa Ubepari ijapokuwa anahudumu katika chama kinachojinasibisha katika mrengo wa kushoto. Ndani ya CCM Lowasa anasifika kwakuwa mwanamitanda (makundi) na hili ameliishi tangu alipoingia kwenye siasa rasmi mwaka 1990. Kisiasa Lowasa anakabiliwa na tatizo la kubuni, kuibua, kujenga hoja na kuisimami hiyo mpaka mwisho. Kwamjibu kwa kumbukumbu za Bunge hakuna mahali panapoonyesha Lowasa aliwahi kupeleka hoja Bungeni na kuisimamia tangu alipoingia Bungeni 1990. Lowasa anakabiliwa na tatizo lingine la uwezo wake mdogo/kutojua kabisa kutoa hotuba thabiti za kisiasa ama za kijamini. Kwaujumla Lowassa sio mwanasiasa bali ni mjasiliasiasa mahiri nchini kwakuwa ameitumia vema siasa na fursa zake na kuwa mkwasi mkubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

UADILIFU WA LOWASSA.

Katika nyanja hizi tunamuona katika sura mbili, kwenye masuala yake ya ndani Lowassa ni Baba wa familia mwaminifu kwa mkewe kipenzi Regina, Lakini sura nyingi ni mbaya kwake na inamuondolea sifa za kiongozi bora kwasababu ya mapito na makandokando yake.

Kashifa ya kwanza ambayo haijawahi kukanushwa na Lowasa mwenyewe ama yeyote yule sababu iliyoitwa na inayoaminika mpaka sasa kuwa “Lowassa ana utajiri mkubwa usio na ufafanuzi alikoupata kwa mda mfupi tu na ulianza alipokuwa yu mkurugenzi wa AICC"

Ikumbukwe mwaka 1995 ikiwa ni miaka mitano tu tangu aingie katika siasa na kuwa Mbunge alichukua fomu ya kuwania Urais sambamba na rafiki yake wa karibu Jakaya Kikwete, huu ulikuwa uamuzi mkubwa na uliolazimu idara kumchunguza japo tayari walikuwa na taarifa zake, hoja hii ilisimamiwa Mwalimu Nyerere na ilikuja baada ya Lowassa na wapambe wake kukodi ndege binafsi kutoka Arusha kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya uteuzi wa urais mwaka 1995, kitendo hiki kilimfedhehesha sana Mwalimu na wazalendo wengine na hata kufikia kushinikiza kuliondoa jina la mwanasiasa huyu nguli wa Tanzania.

Uadilifu wa Lowassa unatiliwa shaka kwakuwa mpaka leo Mamlaka ya mapato Tanzania haijaweza kututhibitishia uhalali wa utajiri aliona Edward Lowassa kupiti kodi anayotakiwa kulipa mtu huyu. Tangu astaafu kama wafuasi wake wanavyopenda kusikia na kuona ama afukuzwe uwaziri mkuu mwaka 2007 taarifa za kuaminika kutoka vyanzo muhimu ndani ya ofisi zake za Political Entrepreneurshipp iliyopo Msasani mkabala na Ubalozi wa USA, Team Lowasa iliyopo Upanga na Umoja wa Wabunge wa CCM iliyopo Dodoma nikuwa Lowassa alitenga Tsh 35 bilioni kwa ajili ya kujitakasa, ambapo mpaka leo hii ameshatumia Tsh18 bilioni.

Kuna maswali mengi sana yanazaliwa kutokana na mwenendo wake kisiasa, Je pesa hii ameipata wapi? Imelipiwa kodi kiasi gani? Atairudishaje?

Labda niwaelekeze watafiti na wadadisi wenzangu wa siasa hebu watafute jalada la Edward Lowassa la enzi za TANU pale Lumumba. Mzee Paul Sozigwa suala hili analifahamu fika.

Ndiyo, Mwl. Nyerere alichukizwa na tabia ya Lowasa ya kujitajirisha kwa kuiba mali ya umma. Lowasa, licha ya tuhuma za wizi enzi akiwa AICC, kujimilikiaha majumba ya Masajili wa Majumba wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, Mwl. Nyerere alikuwa akifahamu wizi wa Lowasa tangu enzi za TANU. Kati ya mwaka 1974 na 1977 Lowasa aliiba pesa za TANU alizopewa kusimamia ujenzi wa ofisi ya TANU vijana Arusha akiwa Katibu na msomi toka UDSM.

Badala ya kujenga ofisi ya TANU Lowasa alinunua kiwanja na kujenga nyumba yake binafsi. Jambo hilo lilipogundulika mwaka 1982, lilimkasirisha sana Mwl hivyo kuamuru afukuzwe kwenye chama. Wazee walipiga magoti kumuombea msamaha kuwa kijana atajirekebisha, Ni marehemu Edward Moringe Sokoine ndiye alimwombea msamaha zaidi kwa Mwl. mpaka abadilishiwa adhabu.

Edward Lowasa alipewa adhabu mbadala; kuhudhuria Ofisi Ndogo ya Chama Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam kila siku bila kukosa, kuwa kazini masaa 8 bila kutoka lakini bila kupangiwa kazi yoyote hadi Chama kingeona ametubu na kujutia na hatimaye apangiwe kazi nuingine. Lowasa alitumikia adhabu yake hadi Sokoine alipofariki.

Hiyo ndio sababu kuu ya Mwl. Nyerere kumkatalia Lowasa kugombea urais. Kikwete, Mkuchika, Twaha Khalifan, Kinana, Bagenda na Msekwa wanajua ukweli wote kuhusiana na jambo hili. Ila maadamu kwa sasa hakuna tena maadili ya uongozi wa kisiasa nchini Tanzania, Lowassa anaweza kuachiwa awatawale wezi, wala rushwa na mediocre wa nchi hii.

Jambo kubwa zaidi kwa Lowassa na ambalo litamtesa zaidi ni tuhuma hizi October | 2011 | WikiLeaks zinazosema kuwa alihusika katika mauaji ya Mwalimu Julius Kamparage Nyerere, taarifa hizo ziliibuliwa na mtandao wa Wikileaks 2011 na mpaka leo Lowassa hajakanusha.

UTENDAJI WA LOWASSA.

Lowa ni mchapakazi mzuri anayefanya kazi kwakutarajia makofi ya shukrani, katika eneo hili Lowasa ni mmoja ya Watanzania wengi wachapakazi vizuri hii ni kwakuangalia matokeo ya utumishi wake huko nyuma hasa kisiasa zaidi. Tatizo kuu la Lowasa nikuwa hana fikra mpya ama wazo jipya katika utendaji, huamini uasili wa jambo/kitu bila kubuni na kukipa sura mpya kizae matoke chanya, hilo ni tatizo kuu na la hatari kwa nchi yenye ndoto za kusonga mbele. Pia hathamini utalamu ama taaluma bali huamini pesa inaweza yote.

Lowassa amehudumu katika serika na chama kwenye nafasi za Waziri wa ardhi na makazi mwaka 1993 - 1995, Waziri wa Maji na Mifugo mwaka 2000 - 2005 na Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 - 2008.

Sehemu hii amehudumu kwa ufanisi japo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa hakuwahi kukuibua hoja iwe binafsi au ya kiwizara na ikazaa matunda, kuna hoja inayoimbwa mitaani kuwa Lowasa ndie aliyebuni na kuanzisha ujenzi wa shule za kata nchini, lakini ukweli suala hili ni zao la aliyewahi kuwa waziri mwandamizi Makweta, yeye ndie alilibuni na kulifikisha serikalini na Lowasa alipoingia akiwa Waziri Mkuu ilikuwa ni Utekelezaji tu.

Mtazamo wangu kwa aina ya mwanasiasa kama huyu hata vizazi vyetu vitakuja kuyatandika mboko makaburi yetu ikiwa tutahongwa hela Watanzania wote nakisha tukampeleka Ikulu. Kazi yake ya kwanza itakuwa ni kurudisha pesa yake.

Ikulu sio pango la WALANGUZI

 
Ivi anagawa pesa kweli? Ni zake? Na kama Anagawa pesa ni kwa sababu gani? Atazirudishaje?
 
Ulivyoanza nikashtuka nikajisemea tumeishampoteza kamanda Yericko maana pesa mwanaharamu...maana unasema mtu aliwika sana matokeo ya form six alafu akaishia kwenda Mlimani kusomea DEGREE YA MAZINGAOMBWE NA SINDIMBA??

Hapa bila shaka form six hakupata marks za kusoma kozi zingine ndio maana akaishia kusomea MAZINGAOMBE NA KUCHEZA SINDIMBA.
 
Mimi sipendi kuona mtu yoyote anatungiwa habari ya uwongo ili wananchi waaminishwe uwongo kwa faida ya ubinafsi.

Hoja yangu inajikita kwenye paragraph yako hii hapa chini, tuhuma zingine ziwezi kuziongelea kwa sababu hazihusishi watu wengine au pande nyingine nje ya Edward Lowassa mwenyewe.
Jambo kubwa zaidi kwa Lowassa na ambalo litamtesa zaidi ni tuhuma hizi https://wikileaks01.wordpress.com/2011/10/ zinazosema kuwa alihusika katika mauaji ya Mwalimu Julius Kamparage Nyerere, taarifa hizo ziliibuliwa na mtandao wa Wikileaks 2011 na mpaka leo Lowassa hajakanusha.

Hoja ya kusema kuwa Edward Lowassa alihusika na kifo cha Mwl. Nyerere huku ukituelekeza eti kwenda kusoma kwenye mtandao unatumia jina la weakleaks01.wordpress ni uwongo na uzandiki.

Kama Edward Lowassa hajakanusha tuhuma haina maana kwamba tuhuma niza kweli. Tuhuma zenye msingi wa kipuuzi huwa hazikanushwi bali zinapuuzwa.

1) Kwa mtu mwenye fikra pevu atagundua kilicho nyuma ya kutumia jina la weakleaks ni kutaka kuaminisha baadhi ya watu kama hii ni weakleaks iliyotumika kwenye kufichua mawasiliano ya Serikali ya Marekani na taasisi zake au ni mtandao unaofanana na kazi hiyo wakati siyo kweli.

2)Mwandishi wa habari na Picha iliyotumika kama ndiyo mwandishi wa habari yenye kichwa cha habari kinachosema ''Mwalimu Julius Kambarage Nyerere was killed'' kwenye huo mtandao wa wikileaks01.wordpress.com ni magumashi(fake). Hakuna binadamu anayeitwa Lane Ludov lakini vile vile picha iliyotumika ni picha ya mwanamziki anayeitwa Andy Stack wa bendi inayoitwa Wye Oak ambayo imekuwa copied kutoka kwenye habari nyingine ili kujenga mazingira ya kuifahanya story ya kutunga ionekane kama ni ukweli kwa kuonyesha mwandishi ni mzungu.

Hii hapa chini ndiyo picha ya mtu anayedai ni mwandishi wa hiyo article kwenye wikileaks01.wordpress.com ambaye anajiita Lane Ludov.

wiki21.jpg

By. Lane Ludov
Habari ndiyo hii,
"I'd like to explain a complicated notion about the death of Mwalimu Julius Nyerere whom many have been led by Dr. Mwakyusa, Nyerere's personal physician, to believe that he died of leukemia. Nyerere was healthy and walking normally when he left Dar for general check up, only for him to be brought back in a coffin draped with the national flag. He had not even gone to seek for medication or treatment. He was healthy and sound. That really devastated me, particularly when I was called from the Tanzania's Ambassador in Moscow and requested to head back home urgently."...
Kwa kukusaidia, hiyo picha imetolewa/imenyofolewa na kuwa cropped kwenye blog hii https://sundaybarrel.wordpress.com/2014/03/31/why-oak/

Picha yenyewe ni hii hapa,
Wye%20Oak1%20by%20Dan%20Stack_jpg_640x503_q85.jpg


Watanzania tuacheni siasa nyepesi zenye ulaghai na uzandiki kwa faida ya muda mfupi.

Tufanye siasa safi kwa faida ya taifa letu endelevu
 
MwanaDiwani

Vema sana mkuu umetusaidia wengi kuanza kupata mwangaza wa tukio hili, lakini bado hiyo sio utetezi wa mwisho kwa jambo hili. Tunahitaji ufafanuzi wa kina zaidi juu ya madai haya ya kuuwa kwa Mwalimu Nyerere, Karibu msemaji utujuze zaidi.
 
Last edited by a moderator:
ngoja niendelee kuona hii muvi ya kuingia ikulu itaishaje, ila majeruhi nawaomba msituharibie nchi.
 
Vema sana mkuu umetusaidia wengi kuanza kupata mwangaza wa tukio hili, lakini bado hiyo sio utetezi wa mwisho kwa jambo hili. Tunahitaji ufafanuzi wa kina zaidi msemaji.
Ndugu,
Mimi kama nilivyosema nimesimama tu kwenye hoja ya kilaghai kuhusu kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.

Tuhuma zingine ulizozileta zinamuhusu Edward Lowassa pekee kwa manufaa yake pakee na kwa maana hiyo, siwezi kuzijengea hoja wakati muhusika pekee yupo. Kama Edward Lowassa ataona zina umuhimu wa kujibiwa nadhani atajibu lakini kutokujibu haina maana kuwa tuhuma hizo niza kweli.

Hata hivyo, wewe unatabia ya kuleta mara kwa mara hoja za kutunga na kilaghai kiasi kwamba hata hoja zako zingine zenye ukweli zinakosa msingi unaojengeka kutokana tabia ya mleta mada.

Mimi ninasimama kwenye siasa safi kwa faida ya taifa letu endelelevu katika msingi wa kukubaliana au kukubali kutokubaliana.
 
Lowassa,Lowassa hadi kero,

Kila kukichaLowassa, Lowassa,oooo mtu mawazo yake binafsi tu anakujanakusema ametumwa na wanainchi katikaeneo lake mfano mkoa au kanda amshauri lowassa agombee Urais.

Lowassa jamani hafai, mtu anayejitajirishakwa kutumia wadhifa wake katika utumishi wa umma hafai kuwa kiongozi kwa sababusiyo mfano wa kuigwa, yaani kuiba mali za umma siyo sifa ambayo inafaa mtumwingine aige.

Lowassa kuwa kiongozi wa ofisi ya juukutavutia wezi wenzie kuinajisi ofisi hiyo, yaani kama ukifuga fisi tegemeafisi wenzie kumtembelea fisi mwenzao hawezi kutembelewa na swala.

Jamani Lowassa hafai.

Kikwete, Mangula hebu mwambieni huyo mtu kwamba hanasifa za kiti cha urais, anaweza mambo mengine na siyo urais, ni nyie mnamlealeamnamchelewesha mpeni sure za moja kwa moja na wala siyo mafumbo mafumbo
CC.

  1. Jajaya Mrisho Kikwete
  2. Jack Zoka
  3. Philip Mangula
  4. Abdrahiman Kinana
  5. Benjamin Mkapa- Uliwakemea maaskofuukasema na majoho yao haiwezekani serikali tatu kwa sababu baba wa taifaalikataza mbona Lowassa humkemei? Mnafiki wee.
  6. Ali Hassan Mwinyi
  7. Nape Nnawiye
  8. Delvis Adolf Mwamunyange
  9. Ernest Hamis Mangu
  10. JohnKomba-na unafiki wako, kama Lulu Michael kakukomba mali zote usitegemee uibukiekatika kumpigia dabe fisadi Lowassa, kufa na lywako
  11. RostamAzizi –ikulu siyo pango la walanguzi unatumia mapesa yako ya wizi ili umwekeLowasaa ikulu ili uwe ndio uchochoro wako.
 
Mkuu kweli nimekubari Mmejipanga ipasavyo ndo maana amjibu tuhuma za kipuuzi du.
Ndugu,
Siasa za Tanzania kwa sasa zimechafuka na zinaendelea kuchafuliwa na watu/wanasiasa wanaotafuta uongozi kwa njia ya kilaghai na kizandiki.

Ina shangaza na kusikitisha sana pale mtu anaamua kutunga story kuhusu kifo cha binadamu ili amuhusishe mtu ambaye wana mitazamo tofauti kisiasa.

Hii story ya kutunga kuhusu kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere inasikitisha sana.
 
Yote sawa lakini Lowasa hafai kuwa raisi kwa sababu hana maadili .maaskofu,mashehe na vijana wote mnaotaka pesa za bure nendeni kwa Lowasa monduli.
 
Ila hapo kwenye shule aliyosomea A level sio Tabora boys ni Milambo wakati huo ikiitwa st mary's
 
Back
Top Bottom