Edward lowassa anapovaa viatu vya kikwete na wote wakapendeza

kichenchele

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
539
176
Kupitia TBC1 nikiwa naangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku, niliweza kuona Jk akimnadi kwa wapiga kura waliopauka na kuonekana wamechoka na naweza diriki kusema wanamatumaini kidogo sana juu ya kesho yao, Lowassa na kikwete wakiwa wameng'aa na kunawili. Hoja yangu hapa mimi naomba kuuliza usafi wa lowassa ambao kikwete alikuwa anaupigia mistari kila mara ni upi? nukuu: Huyu ni mgombea safi, mchapakazi,na mtu wa watu mpeni kura, yaliyopita si ndwele-tugange yajayo. ni baadhi ya maneno ya JK, sasa mimi nashangaa, kikwete ndiye aliye mwambia Lowassa apime uzito wa kashifa za Richmond na mwisho wake akaachia ngazi, ripoti ile ilikuwa ikimtaja Lowassa ushiriki wake ktk mikataba ile mibovu kwa kutoa maagizo au kwa kushinikiza kusainiwa kwa mikataba hii,sasa hii ripoti chini ya mwenyekiti wake Dr.Mwakyembe inatakiwa ifanyiwe editing kwa kufuta vipengele vinavyomtaja Lowassa maana mkuu wa nchi ameshamsafisha kuwa yeye ni mtu safi.
 
Mkuu kwa kweli huu ni unafiki mkubwa na uongo wa hali ya juu. Lowasa ni mchafu ni mchafu tena mchafu wa kupindukia. Tatizo waTz sijuwi ni nani katuloga maana haiingii akilini mtu unakwenda kupiga kura halafu unampigia kura Lowasa.
 
Jamani waTZ naona tunakuwa wasahulifu sana na ndo maana tunalalamikia mambo ambayo hatupaswi kuyalalamikia kama tuna kumbukumbu nzuri. Mkuu wa kaya (JK) bado anasumbuliwa na ule ugonjwa uliomwangusha jangwani kwa hiyo kauli zake nyingi zinatolewa na mgonjwa na hivyo si za kuzichukulia maanani. Mtu mwenye akili timamu hawezi kushawishi wananchi wampigie kura EL na Mramba na kuwasifia kuwa ni watu safi. Lazima uwe mgonjwa wa akili kufanya mambo hayo.

Ushauri wangu: Puuzieni kauli za JK mpaka tutakapothibitishiwa kuwa amepona na sisi tukapima (kwa kauli zake anazotoa) kuwa kweli amepona,
 
JK nae kumbukumbu hana kama ni msafi mbona alipotender resignation ya UPM alikubali si ingebidi amkatalie
 
Anajua kazi alofanya mpaka wenzie 2005 wakaonekana wazee,si chaguo la mungu,wengine waarabu.
so anajua nguvu zake za kifisadi zikoje otherwise anaweze akamgeuka thus anataka amalize tumiaka twake 5
 
Back
Top Bottom