Ebu Tuone na Kusikiliza hii Single ya Mrisho Mpoto Chocheeni Kuni

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
Chocheeni kuni moto uwake ugali uive mnachotaka kitokee
Halikeni mamruki, wakija wangojee, mikeka wawekee
Wanachotaka kitokee
Chochea X 8

Watanzania mwenda kwao siku zote haogopi giza
Acheni nirudi nyumbani safari imenishinda
Nauri zenu ntarudisha

Mtu anatapika nyongo yake anairamba tena anaangaliwa
Ni sawa na tawi kavu linapoanguka watu wakapiga kelele ‘’Hayaaaa”
Katika misimu minne kwa mwaka tuongeze msimu mwingine wa tano wa kujistusha

Raha ya janvi siku zote ni viraka viraka na dungu linamficha mlinzi wa ndege wakati wa mvua tu.
Eti ooh imenyesha juzi tu maji sio mengi nisubirini kule!
Ilishindikana vipi kuyapima maji kwa mti ndo muwaambie watu wavuke?

Mjomba! Binadamu ni kama ganda la kitabu mpaka umfungue maandishi ndiyo uweze kumuelewa.
Eti lililotokea mbali tufanye limepita na haliwezi kumdhuru mwingine ‘kweli’

Inayotaka kunyesha huwa haisubiri mawingu,
Mi sidhani kama kujiponya katika mambo mazito tunahitaji cheti kilichogongwa muhuri wa moto au mtaalamu wa magonjwa ya akili, zaidi ya kutumia neno sahau tu,
Unawaulizaje watu magongo ya nini wakati unasema kuna nyoka?

Mjomba! We si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake piripiri harafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga.

Mngekuwa mnajua anachokuala nyuki msingethubutu kusema asali ni tamu,
Niwashukuru kwa kufikiri, kwani mmeonyesha ukomavu wa kutoka chini kwenye shingo na sio juu.

Mbona hamkumfikiria aliyekuwa ndani kafungiwa kwa nje usingizi hapati anawaza jinsi ya kutoka?
Nikisema uwezo wa watu kufikiri na mahitaji vinatofautiana mtaanza kusema ninadharau, nina matusi lakini kumbukeni ulimi unauma kuliko meno,
Mnawezaje kumfikiria aliyekuwepo ndani kajifungia mwenyewe, funguo anazo mwenyewe, kalala fofofofo asijue hata idadi ya misumari iliyoshikiria mlango wake?

Kulipamba jeneza kumfanya aliyekufa kufufuka nini
Kama kusema nimekwisha sema sana mwisho wake ntakuwa kama mwanasiasa
Hawajitokezi mpaka kuwe na maafa”NTATOA KATON 20 ZA SABUNI YA UNGA’ aliyekuambia wale ni wachafu nani, kasafisheni kwanza nyoyo zenu ndiyo mrudi kwa wananchi.
Ndugu zangu tawi kavu kuanguka wala sio ajabu
Wakati wao wanatenganisha mavi ya panya kwenye unga nyinyi chocheeni kuni zilizolowa, maji yapate moto ugali usongwe,
Wakiwauliza waambieni huu ni utani, hapa kwetu tuna makabila 120 tunataniana

Waliopo hatuwataki, wanaotaka tuwape hatuwaamini
Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukielewa maana yake.
Kwa mfano neno la kitoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza
Neno la kitoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakua
Mtoto akisema baba ile ndege yangu, baba hata kama hana biskeli umwambia ikitua ntakuletea. Lakini maneno ya kitoto mtu mzima kumwambia mtu mzima kunawalakini

Mimi safari imenishinda na sitaki kuulizwa tena kwa nini.

Chocheeni kuni moto uwake ugali uive mnachotaka kitokee
Halikeni mamruki, wakija wangojee, mikeka wawekee
Wanachotaka kitokee
Chochea X 8
 

Attachments

  • Mrisho Mpoto - Chocheeni Kuni .mp3
    5.8 MB · Views: 1,280
maajabu mengine ya dunia, watalii waje watembelee kuona waziri wa elimu elimu imempita na wanafunzi wake 5ooo hawajui kusoma na kuandika lakini wapo sekondari. wapi tena duniani hili liliwahi kutokea??
 
hahahahaha,inawezekana mjomba ameshapigwa pilipili ndy maana haoni watu wanabutua tu!..

Mjomba We si uliwapaka wanja ngoja wao wakupake piripiri harafu kwenye kombolela iwe zamu yako kuzinga.
 
waliopo hatuwataki na wanaokuja hatuna imani nao.

mpoto anahitaji kujengewa uwezo ili aielewe chadema.
 
...hahaha usiombe kucheza kombolela, afu kichaka cha kujifichia kiwe karibu. Kila wakati watakuwa wanabutua...

Watoto wa siku hizi hawajui hata maana ya kombolela...

ndo mana walisema...ngoma ya kitoto haikeshi

Mwenye masikio na asikie
 
Rudi tu mjomba tulijua safari ni nzito.
NAULI YANGU NUNUA MAJI UNYWE,
Karibu Karibu Si kila asafirie hupata alichofuata
 
Mjomba pole sana,tulikwambia safari huiwezi ukasema tuna gubu,mara hatuna malezi ya baba na mama,leo umekiri mwenyewe safari imekushinda! Naomba tu nauli yangu nilokupa ninunue hata yebo yebo mjomba.
 
Jamani audio yake please

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom