Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

TUNARUDI NYUMA 'KIDEMOKRASIA'

KILA ENEO NA MATATIZO, NINI KINAENDELEA?

Mwanzoni mwa miaka ya 1990 wakati wa mageuzi, ilikuwa ni marufuku kufanya mikutano ya kisiasa nje ya CCM. Baada ya mfumo wa vyama vingi, hali haikubadilika.

Ilikuwa Polisi kufukuzana na vyama mitaani kamata kamata na kila aina ya vurugu

Hali iiendelea hadi Mwl alipohoji, wanaofanya mikutano wanavunja sharia gani?

Tangu wakati huo mikutano ikaruhusiwa na kuwa jambo la kawaida.
Ilikuwa ni sehemu ya maisha ya Watanzania . Hakukutokeaa tatizo la aina yoyote.

Kazi ya Polisi ilikuwa kutoa ulinzi pale inapohitajika na kufuatilia panapokuwa na uvunjifu wa Amani kwa namna moja au nyingine, na ilitokea nadra sana.

Tangu awamu ya tano iingie madarakani hali imezorota sana, kwamba, mikutano ya siasa imekuwa kama 'uhalifu'. Kumekuwa na marufuku zisizo na sababu za aina yoyote.

Ni awamu ya tano, waziri mkuu yupo ktk rekodi akiwataka Polisi wazuie mikutano

Mikutano ya kisiasa ni haki ya kikatiba ya mwananchi, waandalizi na wasikilizaji.

Si jukumu la serikali kuratibu mikutano hakuna 'msimu' wa siasa kama inavyoelezwa

Ipo mamlaka ya vyama vya siasa inayoangalia utaratibu mzima wa utendaji wa vyama.

Si jukumu la Polisi kubashiri matatizo yanayoweza kutokana na mikutano hiyo.

Polisi hawa wabashiri ndio wanaoshindwa kuzuia uhalifu unaolisumbua taifa sasa

Hili limepelekea wananchi kuliangalia jeshi la Polisi kwa jicho la kutumikia matakwa ya wanasiasa nje ya kanuni za utumishi.

Kwa mantiki, ipo sehemu ya jamii isiyo na Imani na jeshi la polisi

Huko Bungeni kuna mapambano kati ya naibu Spika na wabunge wa Upinzani.
Kwa ufupi kuna kila sababu za kuamini naibu Spika ameshindwa kuunganisha Bunge.

Bunge linayumba, limepoteza heshima na nguvu kama mhimili unaojitegemea

Serikalini hali nayo inasikitisha, Rais akitueleza vilaza, waziri akisema ni wahadhiri
Hakuna kuheshimu taratibu za ngazi za serikali.

Hatuoni mantiki za Rais kuelekeza ujenzi wa barabara ndani ya Jiji, ili hali kuna serikali ya mkoa, Jiji n.k. Na tangazo la ujenzi huo likitolewa sehemu ya kiroho

Baada ya uchaguzi, tuliandika katika safu hii Taifa limegawanyika, na kazi ya awali ya Rais Magufuli ni kuliunganisha. Hakuna taifa linalofanikiwa likiwa katika vipande.

Kwasasa Taifa limegawanyika Zaidi kuliko hapo awali

Yapo mambo yanayosumbua wananchi wajiulize, nini hasa kinafichwa na serikali hii kwa kutumia nguvu za dola?

Kuna kitu gani serikali ya awamo ya tano inaogopa kisiwekwe wazi?

Wananchi wanajiuliza, nguvu za kuzuia mikutano ya kisiasa zimelenga kuficha nini?

Kwavile serikali imekuwa inatenda 'mambo' kwa uwazi utumbuaji na uwajibikaji, nini inahofia hadi kuzuia mikutano ya wapinzani, ya kawaida kabisa?

Kwa hali ya ilivyo, kila kitu kipo kipo, hakuna anayejua nini kinafanyika Zaidi ya shamra shamra za majipu, ukurupukaji na maamuzi yanayoumiza wananchi kama la sukari

Tunabomoa misingi ya demokrasia tuliyojenga kwa gharama kubwa na kutupa heshima

Tunarudi enzi za Polisi kukimbizana na wapinzani bila sababu za maana.

Tunaishi kwa hofu ya kuzuia wananchi wasijadili hatma zao eti watachonganishwa.

Serikali inayojiamini haigopi tuhuma au uzushi, hii ya 5 inaogopa hata kivuli chake

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, leo nimechukua time nimesoma kila kitu ulichoandika toka mwanzo hadi mwisho na nina neno moja tu nalo ni wow! Natamani ungeandika kabisa kitabu kwani ni mara chache nimekutana na hekima kama ulivyoimwaga hapa ndani na sisemi hivyo kwa unafiki, la hasha, I am honestly impressed. Laiti mkulu mwenyewe angepitia maandishi yako haya na kuyasoma! Nina hakika ushauri unaoutoa angeufanyia kazi badala ya huu usanii anaouonesha kila leo.
 
Wakuu Ngongo na Mag3 tuwashukuru kwa dhati kwa kuendelea kututia moyo

Taifa hili ni letu sote na hatuwezi kufanikiwa tukiwa katika makundi au vipande vipande
Hatuwezi kufanikiwa ikiwa hatukubaliani kutokualiana, hatuheshimu mawazo mbadala

Bahati mbaya, wapo wenzetu wanaoona hoja mbadala ni uhalifu. Tatizo la hili ni kuwa na Taifa lililogawanyika

Sote tunakubaliana tulipo si pazuri. Tunabadiliakaje ikiwa hatuna mawazo mbadala?

Mawazo mbadala yanapatikana kupitia njia anuai, vyombo vya habari rasmi, vyombo vya habari vya kijamii na uwakilishi wa wananchi katika vyombo rasmi kama bunge

Baadhi ya hatua zinazochukuliwa na serikali ni matokeo ya nguvu ya habari
Wazungu husema information is power.

Suala ni kuongeza wigo wa kujadiliana , na kupitia hiyo tunapata majibu ya matatizo

Katika hali isiyo ya kawaida, uhuru wa kujieleza sasa ni jambo tete sana.
Hata uhuru wa kupata habari imekuwa tatizo.

Kwa njia hiyo, wahusika wataelewaje yanayotokea katika jamii?

Tatizo la serikali ni kuamini kuwa kazi yake ni ku-impose sharia na kudhibiti habari.

Ni kutumia nguvu nyingi za vyombo vya dola bila kutafuta au kusikiliza wananchi

Bunge limepoteza makali na kuwa 'sehemu ya serikali' hata kufikia mahali pa kuchangisha pesa za madawati badala ya kuisimamia serikali itimize wajibu wake

Wabunge hawatakiwi kufikisha mawazo yao hadi wabadilishe ili kupendeza watu

Mikutano ya vyama imezuiliwa bila sababu kwa sababu za kuogopwa uchonganishi

Sheria ya mitandao imedhibiti wananchi kuonyesha matatizo na kuibua maovu

Ndio, watafanikiwa kwa kutumia nguvu za dola lakini hawatafanikiwa kutambua, au kutafuta suluhu za matatizo yanayotukubili.

Wanajiwekea uzio na mzingo.Mwisho wa siku tutafeli sote tukibaki kulaumiana

Swali tutakalojadili bandiko lijalo ni, je wamefanikiwa katika kudhibiti habari?

Tusemezane
 
KUDHIBITI HABARI
Jitihada za kuzuia matangazo ya bunge, kubana vyombo binafsi hazitoi matokeo tarajiwa.

Kama itakumbuka, tulieleza waziri Nape ni mtu wa chama na kama angependa kufanikiwa inambidi atofuatishe shughuli za chama alizozoea na za serikali

Tangazo la kuzuia matangazo ya bunge liliwekewa sababu za gharama kubwa.

Hoja ilikufa pale walipojitokeza mfuko wa wakfu kuhudumia matangazo hayo ambayo kwa mujibu wa Nape yaligharimu serikali bilioni 4

Bilioni 4 ni pesa nyingi, hata hivyo kwa kuangalia haja na umuhimu wake ni pesa kidogo.

Bunge limerudisha takribani bilioni 6, na ofisi ya uchaguzi NEC imerudisha bilioni 12
Vipi basi tuseme bilioni 4 kwa walipa kodi kushiriki katika kufuatilia mijadala ni kubwa?

Kuzuia vyombo binafsi kutafuta habari za bunge kunaeleza mengi

Ni vema kusema hoja ya gharama haina mashiko na imetia doa kwa walioshadidia

Ikaletwa hoja ya wananchi kuwa makazini. Nayo ikapata majibu,iweje basi TV ziendelee na vipindi wakati wananchi wakiwa makazini?

Je, kuna tofauti ya kufuatilia bunge au kuangalia vipindi vingine kwa wakati huo huo?

Majuzi waziri amesoma bajeti ya nchi 'live' Haijulikani kwanini suala la gharama na muda wa kazi havikuzingatiwa. Hii inaonyesha nia ya kuzuia matangazo haikuwa njema

Tofauti na mAtarajio, njia hiyo imezua hamasa na habari za bunge zinapatikana kuliko ilivyokuwa. Tumeona , tumesoma na kusikia yote yanayoendelea bila shaka

Kwa bahati nzuri au mbaya, wanaoathirika na zuio ni CCM.

Habari zinazotoka kupitia 'njia' za mkato zimeonyesha 'madudu' tu ya CCM hata kama wapo waliotoa michango ya maana sana.

Kwa maneno mengine kuna 'vita' baridi kati ya vyombo vya habari/wananchi na serikali

Waathirika wa hili ni CCM ambayo imeonyeshwa katika ubovu tu.
Wanaoangalia habari zilizochujwa na zile zinazotoka kwa njia nyingine ni tofuti sana.

Habari njema zitakuwa za makundi mengine, habari mbovu ni za CCM

Majuzi tumeona streaming ya mkutano uliofanyika Washington.
Habari hiyo imewafikia wengi kutokana na hamasa ya kutafuta habari.

Vyombo vya habari vya kijamii vimeziba ombwe lililokusudiwa.

Tumalizie kwa kusema, zuio la matangazo ya bunge limeondoa credibility ya serikali.
Limewafanya CCM wawe wahanga wa mbinu zao wenyewe.

Zoezi hilo limeshindwa na mbadala wake ni kuiumiza CCM kwa kukosa coverage au kupewa coverage inayowaonyesha katika ubovu kila siku

Tusemezane
 
SHERIA YA MTANDAO
TUNATUMIAJE RASILIMALI KWA BUSARA?

Ni kawaida vyombo vya sheria,shauri kuamuliwa nje ya mfumo rasmi.
Mahakama inaweza ridhia shauri ima jepesi linahitaji busara, au halina madhara

Upo msemo 'ukubwa ni jalala' wakimaanisha unaambatana na mengi
Kwamba, ukiwa mkubwa una dhamana ya kila jambo,kusotwa vidole ni sehemu yake

Popote duniani viongozi huchorwa, hukashifiwa, kejeliwa n.k.
Siyo jambo geni na wala halimpunguzii kiongozi uwezo, hadhi au heshima yake

Silaha kubwa ya kiongozi ni namna gani anakabiliana na changamoto.

Miongoni mwa viongozi waliopachikwa majina, kejeliwa, kashifiwa ni Mwalimu Nyerere,tena si nchini bali kimataifa, na anabaki kuheshimika sana duniani

Matumizi ya sheria ya mtandao yanazua maswali.
Sheria ilitengenezwa pamoja na kuzuia cyber bullying na character assasssination

Inafikirisha sheria ya mtandao inatumika kwa walioandika maneno ya kashfa kwa Rais!
Kashfa na kejeli si jambo jema, hata hivyo ni sehemu ya maisha yetu ya kawaida tukitambua tunatofautiana kwa weledi na mitazamo

Wanaoandika impact yao katika jamii ni kama haipo, na pengine ni frustrated au tu ni upungufu wa malezi, matumizi ya vileo n.k.

Inashangaza jinsi serikali ilivyokamia kuwafikisha mahakamani.
Hivi tuna rasilimali nyingi kiasi cha mambo kama haya kukuzwa kiasi hicho?

Lipo tatizo la usalama katika miji kama ongezeko la uhalifu n.k.
Tuna matatizo ya ufisadi, ubadhirifu na ufujaji wa kiwango kikubwa nchini
Kwanini tusielekeze nguvu zetu huko?

Labda tujiulize, matukio mangapi ya kutisha ambayo hatuna majibu hadi leo?

Vipi nguvu nyingii zitumike kushughulikia watu ambao huenda wakati wanaandika walikuwa wamelewa au hatuna ufahamu na afya zao za akili?

Hivi kweli kutafuta nani kasema nini kuhusu Rais katika Instagram, facebook, whatsapp n.k. ni kipaumbele katika usalama wa taifa letu?

Ni matumizi mazuri ya rasilimali chache tulizo nazo?

Tusemezane
 
SHERIA YA MITANDAO

Kama tulivyoona hapo juu, kwa uchache sharia ya mitandao ililenga kukabiliana na uhalifu wa mitandao kwa ujumla wake na ndiyo hasa maana ya 'cyber crime'

Sheria ilipitishwa na bunge katika mazingira tatanisha. Ilipingwa na wadau na wananchi.
Haikupingwa kwasababu ni sharia mbaya, bali vipengele vyake havikuwa sawa

Na kwa sehemu kubwa sheria hiyo ililenga kubana mitandao ya jamii kutoa habari au kusambaza habari zinazohusu serikali zikiwemo kashfa kuelekea uchaguzi mkuu

Katika kufanilikisha hilo, kiliwekwa kifungu kisemacho kuwa 'mto habari ana hatia sawia na mpokeaji au msambazaji' kwa maana kuwa anayetoa habari ana makosa, na mitandao itakayosambaza habari hizo ina hatia na wasomaji wa habari hiyo wana hatia

Tunachokishudia sasa hivi ni watoa habari kukamatwa na kushtakiwa.
Lakini habari zao zinapita katika maeneo mengi na kupokelewa na wasomaji.
Iweje badi sharia hiyo isifanye kazi kama ilivyokusudiwa?

Hili linaonyesha kuwa sheria hiyo haikufanyiwa tathmini, ililetwa kama mswada wa dharura kwa makusudi mengine yakiwa chini ya mwamvuli wa makosa ya mtandao.

Ni kwa msingi huo, tunaona sheria ina utata na matatizo

Ni muhimu kuelekeza rasilimali zetu chache kuchagua vipaumbele katika mambo yanayotukabili. Ni kweli kosa ni kosa na hatutetei utovu wa nidhamu wa aina yoyote. Hata hivyo, nchi yenye watu milioni 45 itakuwa na mchanganyiko wa tabia

Rais Nyerere alikejeliwa,kashfiwa kwa majina sera n.k. Jambo moja tunalikumbuka ni uwezo wake wa kusimama na kile anachokiona ni sahihi.
Hakuyumbishwa na matusi au kashfa, alibaki katika mstari,anabaki mashuhuri daima

Viongozi waliofuata kila mmoja ana shea yake.
Wote walipachikwa majina, wakasema , wakakejeliwa bado wamebaki na heshima zao.
Rais Magufuli hatakuwa tofauti na watangulizi wake,jamii anayolea ni ile ya miaka 50

Tuelekeze nguvu na rasilimali zetu kupambana na matatizo ya ujambazi, wizi, vibaka, ufujaji, mafisadi n.k. kuliko maneno ya mtu mmoja yasiyo na athari yoyote yakipuuzwa.

Huenda wanaofanya hivyo ni wana matatizo ya kimaisha, kiafya au ni walevi tu

Kwanini tutumie nguvu nyingi kuhangaika na madogo tukifumbia macho makubwa?

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3

Hakuna kitu kibaya kama kutawala nchi ukiwa hujiamini... unakuwa kiongozi uliejawa na woga na kurect vibaya kwa kila kitu kinachoonekana kuwa ni pinzani kwako. Unakuwa sensitive kupita kiasi kwa kila aina ya criticism inayokuja upande wako!

Na hicho ndicho kinachoendelea kwa utawala huu. Ndio maana zinafanyika kila jitihada kuzima sauti zozote zenye mwelekeo wa kuwapinga au kuwakosoa. Walianza kuzuia bunge kuoneshwa live, wamezuia mikutano ya vyama vya siasa, wabunge wa upinzani wanadhibitiwa vilivyo bungeni (sakata la naibu spika), sheria ya mtandao n.k.

Yote yanayoendelea sasa sio bahati mbaya hata kidogo.....
 
Mkuu Nguruvi3

Hakuna kitu kibaya kama kutawala nchi ukiwa hujiamini... unakuwa kiongozi uliejawa na woga na kurect vibaya kwa kila kitu kinachoonekana kuwa ni pinzani kwako. Unakuwa sensitive kupita kiasi kwa kila aina ya criticism inayokuja upande wako!

Na hicho ndicho kinachoendelea kwa utawala huu. Ndio maana zinafanyika kila jitihada kuzima sauti zozote zenye mwelekeo wa kuwapinga au kuwakosoa. Walianza kuzuia bunge kuoneshwa live, wamezuia mikutano ya vyama vya siasa, wabunge wa upinzani wanadhibitiwa vilivyo bungeni (sakata la naibu spika), sheria ya mtandao n.k.

Yote yanayoendelea sasa sio bahati mbaya hata kidogo.....
Ukitazama kwa undani hayo yanatokana na kukosa kujiamini.

Na inatokana na maamuzi mengi yaliyofanywa bila kuangalia athari zake

Kwa mfano, suala la sukari halina maelezo kwanini limekuwa mwiba
Sukari haikuwa tatizo wakiingia madarakani.

Tatizo ni transition ya kulinda viwanda iliyofanyika bila kuzingatia utaalamu.

Serikali haina maelezo yakujitosheleza, njia nyepesi ni kuzuia mijadala bungeni au katika mikutano ya hadhra, ni self defense

Suala la ujenzi mabondeni, halikuwa na utaratibu, na hakuna maelezo yanayojitosheleza. Njia nyepesi ni kuzuia mijadala bungeni na mikutano ya siasa

Ukitazama jambo kama la Lugumi, kusita sita ni kuogopa, na kuondoa kujiamini

Lakini yote ni makosa makubwa kisiasa. Dunia na Tanzania ya leo imebadilika.
Uwezo wa watu kupima umeongezeka.

Watu wanaifahamu serikali yao na mbinu zao. Kinachofanyika ni kukimbia kivuli tu

Miwsho, serikali ya awamu ya tano haitakuwa tofauti na awamu nne zilizotangulia.

Dalili zinaonekana, kuficha maovu , kukwepa ukweli, na kutotaka ukweli usemwe.

Laiti wangejifunza hii ni serikali ambayo ingefanikiwa sana.
Kuingia na kasi kulitokana na kuwa na template ya matatizo

Kilichotakiwa ni kuwaacha wananchi/wapinzani waisaidie serikali kufanya kazi si kukimbizana nao kuwazuaia mikutano, kuwafukuza katika bunge n.k.

Hayo yanawafanya wananchi wajiulize sana, hii serikali inaficha nini kisichotakiwa kujulikana? yaani curiosity, na hapo ndipo serikali itakuwa exposed vizuri sana

Kwa miezi michache, kama Taifa tuna tatizo kubwa sana
 
Sehemu I

KAULI YA RAIS KUHUSU 'ZUIO' LA SIASA

YA BUNGE NA NAIBU SPIKA


Rais amepokea taarifa ya uchaguzi Ikulu Dar es Salaam.
Amezungumzia umuhimu wa umoja wa Taifa kwa masikilizano

Katika bandiko hili mwanzoni kabisa tulieleza wajibu wake baada ya uchaguzi. Kwamba, kipaumbele ni kuwaunganisha Watanzania siyo majipu au ziara

Kazi yake ni rahisi nchi ikiwa moja, na ngumu ikiwa 'mapande' kama ilivyo sasa.
Hakuna shaka ugumu huo ameuona na kukumbana nao na kuona haja ya umoja

Pili, tuliwahi pia kumuasa kuhusu waandishi wa habari, kwamba, wanaweza kumjenga au kumbomoa. Rais alitegemea vyombo vya chama/serikali vinatosha

Hilo nalo kaliona ni tatizo na kawafikia kwa lugha laini tofauti na lugha aliyotumia alipoongea nao kwa mara ya kwanza. Ameona nguvu ya vyombo vya habari.

Lipo jambo lililotisha katika maongezi. Na hili limejirudia bila kujua athari zake.
Kwamba ni muda wa kufanya kazi na si siasa.

Wakati serikali inazuia matangazo ya bunge hoja ilikuwa hiyo hiyo

Rais anakwenda mbali na kusema siasa ni baada ya miaka 5.

Huku ni kuvunja katiba , kunayng'anya haki za wananchi na dalili za maguvu

Haki ya kukusanyika, iwe mikutano ya kisiasa ni ya kikatiba.

Na wala hakuna kifungu kinachozuia wananchi kufanya shughuli zao za kisiasa au muda wa shughuli za kisiasa. Mh Rais anapata wapi haya?

Inaendelea
 
Sehemu ya II

Mkutano alioufanya Ikulu ulihusu mambo ya siasa, mbona haukuzingatia muda?

Ni wapi imeandikwa muda wa siasa nchini kwa tarehe, mwezi au mwaka.

Picha inayojitokeza haraka kutokana na kauli za Rais ni kuwa

1. Zuio linalofanywa na Polisi ni maagizo ya serikali, hakuna sababu nyingine

2. Matatizo bungeni 'yana mkono' wa serikali kudhibiti kisiasa !

3. Huenda nguvu ya naibu spika inachagizwa kutoka nje ya bunge

Kuna maswali mengi ya kujiuliza. Ili kauli ya Rais ilete maana iliyokusudiwa kuna mabadiliko yanayopaswa kufanywa katika Taifa na nchi kwa ujumla

1. Litoke tangazo la kusimamisha shughuli za kisiasa.
Na lionyesha shughuli hizo zianze lini kwa tarehe, mwezi , mwaka na saa

2. Serikali ipige marufuku shughuli za kisiasa zikiwemo za Bunge

3. Serikali isimamishe idara zifuatazo kwa mujibu wa kauli Rais kuhusu siasa
a) Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa (b) Tume ya uchaguzi ya Taifa

4. Serikali izuie mkutano mkuu wa CCM mwezi ujao ambao ni wa kisiasa hadi pale muda wa siasa utakapowadia kwa mujibu wa kauli yake kwa vyama vyote

Tutakafakari, Taifa likiongozwa kwa matakwa na si katiba,tumefika pabaya.

Hakuna sehemu ya katiba inayonyang'anya haki za watu kushiriki shughuli halali.
Hakuna mahali muda wa siasa umeelezwa au sheria inayokataza mikutano halali

Pengine tunayayaona bungeni yana baraka kutoka kwingine.
Kauli za Polisi kuzuia mikutano na mikusanyiko ni maagizo kutoka kwingine

Tunachosubiri sasa ni marufuku ya watu kufanya harusi au birthday

Sehemu ya II tutaangaali kwanini serikali ina hofu, ina wasi wasi! kiasi cha kuona demokrasia ni adui, na kwamba njia ya makato ni kuiua kifo cha haraka!

Tusemezane
 
KWANINI WANA HOFU!

Habari za 'kuzuia' shughuli za kisisasa si ngeni. Waziri mkuu Mh. Majaliwa alifungua pazia akiwaagiza Polisi wasaidie katika kazi hiyo ili kuhakikisha watu wanafanya kazi

Zuio hilo likaenda sambamba na lingine la matangazo ya bunge yasionyeshwe hadi yatakapohaririwa kuhakikisha wananchi wanapewa habari serikali inazotaka wazisikie

Viongozi wa wa awamu ya tano walitumikia awamu ya nne.
Waliona serikali ilivyokumbana na hoja mbadala mbele ya macho ya umma

Serikali inatambua weledi umeongezeka, mambo yatapitia mchujo wa akili za wananchi

Awamu ya tano inafahamu ugumu wa matatizo ya nyuma, isingependa kunasibishwa au kuwa sehemu ya suluhu yake kwani kuna ugumu ikichelea ugumu wa 'kulindana'.

Kwa mfano, kashfa ya kampuniiliyohudumia vifaa vya jeshi la Polisi inahusiswa na wakubwa. Maazimio yoyote yatagusa 'wazito' wa siku za nyuma!! Watalindanaje?

Awamu hii imekuwa na maamuzi yanayotiliwa mashaka na kulazimu kubadili misimamo kila mara ikiitwa kukurupuka.

Wizara ya afya imebadili msimamo kuhusu chakula Muhimbili siku chache baada ya uamuzi huo kusimamiwa na serikali kwa nguvu

Lipo la suala la Sukari lilivyoumiza wananchi, tatizo lililotengenezwa kwasababu ya kukosa maono na mipango sahihi. Serikali haina maelezo kwa wananchi nini kimetokea

Kuna tatizo la wanafunzi wa UDOM ambalo kimsingi si tatizo la wanafunzi.

Ni tatizo la serikali ya awamu ya nne ambayo viongozi waliopo waliitumikia na sasa wanaligeuza kuwa la wanafunzi. Udahili, mikopo n.k. ilifanywa na serikali si wanafunzi.

Masuala ya nyumba za mabondeni hayana majibu ya kutosha.Zoezi lilifanyika bila tathmini na kugeuka adha . Hii haina maana zoezi lilikuwa baya, la hasha.
Tatizo ni kuwa zoezi zima lilifanywa katika majukwaa badala ya karatasi na kalamu

Kuna jambo jingine linalozidi kuleta tatizo awamu hii. Viongozi wake wanatoa kauli bila kupima uzito wake kwa jamii. Wamelewa sifa na kujisikia pengine ni karibia ya miungu.

Kauli zao zimekuwa za kudharau, maudhi au kudhalilisha sehemu za jamii bila ulazima
Katika hali hii serikali isingependa kuingia katika malumbano na wapinzani au wananchi.

Mathalani, serikali inafahamu uwezo wa wapinzani kujenga au kubomoa hoja kwa mantiki.Ni kwasababu wapinzani hufanya 'tafiti' ya hoja badala ya kushangilia

Na serikali inatambua CCM haina umaarufu' inanuka' katika uso wa umma kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi. Serikali haina uwezo wa kujitenga na mzazi wake CCM!

Njia nyepesi ni kuhakikisha mijadala inayohusu mambo ya taifa inazuiliwa.

Wananchi wanafungwa midomo kujadili , vitisho vinatamalaki na kuwageuza wananchi 'mazezeta' ili wasione , wasiseme au kuhoji, bali kushangilia kila jambo

Vyombo vya maguvu vinatumika kufanikisha azma hiyo.
Tena si kuzuiliwa, bali inajengewa hoja na viongozi,wengine wakipaswa kuwa 'neutral' .

Utetezi huo tutaona bandiko lijalo ambalo katika hali ya kushangaza Msajili wa vyama vya siasa amejitokeza kutetea serikali!

Tusemezane
 
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

AFAFANUA KAULI ZA MAGUFULI KWA UNDANI

HAJAFAFANUA MIGOGORO YA VYAMA VYA SIASA!!!

Kauli aliyotoa Rais Magufuli kuhusu 'siasa' imeacha maswali mengi.
Wapinzani wakiiangalia kama hatua za kuminya demokrasia nchini.

Vyama vya siasa vime 'react' kwa taharuki vikijiuliza siasa za miaka 5 zimeaninishwa katika sharia gani za nchi na serikali ingependekeza lini shughuli za kisiasa zifanyike

Siasa , maendeleo na demokrasia haviwezi kutengwa.
Uwepo wa mihimili ya nchi unaeleza shughuli za mihimili hiyo ni endelevu.

Tunawaambiaje wananchi ni muda wa kazi tu,wanasiasa wakiratibu shughuli zao?

Mathalani, mkulima anategemea kazi zake katika mazingira ambayo wanasiasa huyaanda. Mijadala ya bei za mazao, pembejeo n.k. ni mifano michache

Tunawaambiaje wafanyakazi waendelee na kazi na siasa ikiwa mishahara na kodi zao zinapangwa na wanasiasa Dodoma.

Demokrasia yetu inaeleza tunapanga mipango tukishirikisha maeneo ya kisiasa,uchumi na kijamii. Vipi tunaondoa siasa tukitegemea mengine yanaweza kufanya kazi yenyewe?

Kauli ya Rais imedhukuliwa na wengine kama 'tangazo' la marufuku shughuli za siasa.
Wapo wanaoona ni sahihi kwamba siasa zitoe nafasi za shughuli nyingine.

Ukweli utabaki kuwa sheria zinaturuhusu kuendelea na Uhuru wa kutoa mawazo
Na kwamba hakuna sheria inayozuia wanasiasa kufanya siasa za 'msimu'

Katika watu waliotolea maoni kauli ya Rais ni msajili wa vyama.
Inaelekea msajili alikuwa anawajibu wapinzani kuhusu tamko lao dhidi ya kauli ya Rais

Msajili wa vyama ni mlezi wa vyama vya siasa nchini.

Wajibu wake ni kusimamia shughuli za siasa kila siku. Hiyo inaeleza siasa ni jambo endelevu na msingi wa uwepo wa kitengo hicho kila siku na si miaka 5 inayosemwa.

Endapo msajili anakubaliana na siasa za msimu ofisi yake ifungwe kwanza hadi vyama vya siasa vitakaporuhusiwa kufanya shughuli zao. Vivyo hivyo tume ya uchaguzi n.k.

Pengine msajili wa vyama vya siasa angetutendea haki kwa kufafanua, iweje Hamadi Rashid amefukuzwa na chama na bado amebaki kuwa mbunge?

Katika mgogoro wa Hamadi na chama chake msajili alikaa kimya bila ufafanuzi, haya yanayohusu kauli ya Rais yanamhusu vipi kuyatolea ufafanunuzi na si ofisi ya Rais?

Ni msajili wa vyama aliyevitaka vyama vishiriki uchaguzi wa 'marudio' Zanzibar bila kufafanua ni kwa msingi gani na sheria gani za nchi zinazoambatana na kauli yake

Ni kwa mtazamo huo, msajili wa vyama ambaye huteuliwa na Rais anatia shaka kama kweli ni kiungo cha vyama vya siasa. Kama kweli ni mlezi wa vyama vya siasa nchini.

Na kama kweli hakuna 'kuegemea' upande katika shughuli zake

Tunahitaji kukaa chini na kuandika utaratibu mpya 'katiba' utakaohakikisha serikali inabaki kuwa serikali, mahakama na bunge vinabaki kuwa hivyo.

Idara au vitengo kama msajili wa vyama, tume ya uchaguzi na Polisi zinabaki vitengo huru visivyofungamana na mihimili mingine

Tusemezane
 
MSAJILI NA KAULI YA 'SIASA KANDAMIZI'

Katika mwenelezo wa bandiko linalohusu kauli ya msajili, lipo eneo alilotolea ufafanuzi
Msajili anasema Rais alikuwa anawaambia wanasiasa 'waache siasa kandaimizi'

Kauli hii inatia shaka sana. Hivi wanasiasa wanapofanya siasa, kuna siasa gani kandimizi wanazofanya? Msajili alipaswa kufafanua hilo la siasa kandamizi

Hakuna siasa kandamizi zikiwa zinafanywa kwa mujibu wa sharia za nchi.

Katika kutoa maoni yake, msajili angejiepusha na kauli zenye utata.
Tayari kauli ya Rais ina utata, halafu inakuja nyingine yenye utata Zaidi inatia shaka

Msajili kama mdau wa siasa anayo haki ya kutoa maoni yake.
Hata hivyo, maoni yake yanapaswa kuzingatia uzani wa habari na nafasi yake

Anapotoa maoni kama msajili, maoni hayo si yake ni ya ofisi ya masjili.
Na kwavile yataweza kutafasiriwa kama ni maoni ya ofisi ya msajili wa vyama;Maswali mengi yasiyo ya lazima yanaweza kujitokeza.

Moja, kauli aliyotoa Rais ni kauli ya kiongozi wa serikali.
Pengine ofisi ya mawasiliano Ikulu ina nafasi nzuri ya kutoa ufafanuzi wa suala hili

Pili, kauli yenye kuhitaji ufafanuzi inaweza kutolewa na msemaji wa serikali.

Kwa hili, msajili alipaswa kuangalia kauli yake binafsi na kauli ya ofisi yake

Leo vyama vya siasa vitakimbilia wapi ikiwa msajili wanayetegemea kama mlezi na msuluhishi anaonekana kama 'msemaji' wa masuala ya serikali?

Hili la kauli tata halikutolewa na kiongozi wa chama bali serikali.

Msajili alipaswa kuliangalia hivyo, kwamba hakuna msuguano wa vyama.

Ingalisaidia sana kama angewaita walalamikaji na kuwapa ufafanuzi akiwa msajili na si kuzungumza katika vyombo vya habari na kukuza suala hili isivyotarajiwa

Nani anasimama na vyama vingine vya siasa katika hali hii?

Tusemezane
 
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

AFAFANUE 'POSITION YAKE''

Kufuatia kauli ya msajili wa vyama ya kuwataka wapinzani waache siasa 'kandamizi' ambazo hazijulikani,maswali yanazidi kugonga akili za wananchi

Kwanza, msajili afafanue siasa kandamizi ni za aina gani?

Pili, msajili afafanue wakati anatoa kauli kumtetea Rais wa JMT

a)Alifanya hivyo kwa maoni tu kama Jaji Mutungi ambaye ni Msajili
au
b) Alitoa kauli hiyo kama Msajili wa vyama vya Siasa nchini

Kauli ya msajili inaonekana ni nyepesi, kimantiki inaweza kuzua mtafaruku usio na ulazima nchini.

Kwa mfano, zipo hisia tu kuwa Msajili alijivika jukumu la msemaji wa Rais.

Zipo hisia tu za mitaani alisimama kutetea Rais aliyemteua.

Na zipo hisia tu kuwa anafungamana na chama cha siasa, kukiwa na hisia za Jaji mwingine aliyechukua Fomu za Urais

Hizi zote ni hisia ambazo zaweza kuwa hazina hata chembe moja ya ukweli.

Hata hivyo,hisia hizo zinapozungukwa na maswali yasiyo na majibu zinaweza kuwa ukweli usio na chembe ya uongo hata sivyo.

Katika kuondoa utata huo na hasa kujenga imani kuwa ni msajili wa vyama vyote vya siasa, na kwamba yeye ndiye msuluhishi na kimbilio la vyama kunapokuwa na matatizo, msajili ajitokeza afafanue kauli zake

Msajili anaweza kupuuza haya ya mitaani, hata hivyo aelewe ofisi yake itapoteza credibility.

Yeye kama Jaji na Msajili atapoteza imani kwa wananchi

Yote hayo yanaweza kutufikisha mahali ambapo vyama vitaona havitendewi haki na serikali na taasisi zake, na jina la msajili halitaepukika

Tusemezane
 
BUNGE NA LUGUMI

Tarehe 22 May 2016 tuliandika haya


HATUA HIZI NI SAWA LAKINI ZINA DOA

LUGUMI NI TATIZO KWA AWAMU YA TANO

Wiki hii yamatokea mambo kadhaa yenye kuleta fikra.

Huko Bungeni wizara kivuli ya mambo ya ndani ilisusia kutoa hotuba, kisa ni kugusia mambo ya uuzwaji wa nyumba, na mikataba tata ukiwemo wa Lugumi

Picha nzima ilionyesha kuwepo na 'kinga' dhidi ya tuhuma kutoka kwenye kiti

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, waziri wa mambo ya ndani alitoa majibu akiwa amelewa jambo lililopelekea utenguzi wake mara moja.

Wizara ya mambo ya ndani ni wizara nyeti za nchi. Ndiyo yenye mamlaka zinazosimamia sheria kama Polisi inayoshughulikia usalama wa Raia na mali zao

Kitendo cha waziri kuingia bungeni akiwa amelewa si tu kilikuwa utovu wa nidhamu bali ukiukwaji mkubwa wa kanuni za utumishi kwa kiongozi aliyepaswa kuonyesha mfano

Hatua ya 'kumtumbua' ni sahihi kwasababu hakukuwa na namna ya kuficha uozo ule.
Hata hivyo, hatua hiyo inafunikwa na makando kando mengine

Gazeti la Mwananchi siku chache zilizopita liliandika kuhusu ufungwaji wa vifaa vinavyolalamikiwa kuwa na ufisadi vikihusisha kampuni ya Lugumi.

Katika tuhuma, ipo kampuni inayosemekana kuwa na masilahi na ''waziri mtumbuliwa''

Gazeti limeeleza kwa undani maeneo vifaa hivyo vinapofungwa.

Likaeleza jinsi ambavyo kamati ya bunge PAC inayochunguza suala hilo ilivyocheleweshewa pesa kuanza kazi ya uchunguzi

Hapa kuna hoja,ucheleweshajwi umefanyika kutoa nafasi ya wahusika kufunga vifaa.

Hizi ni hisia zinazozunguka katika maongezi ya kawaida ya wananchi.

Ikizingatiwa kuwa bunge nalo lilikataa suala hilo kujadiliwa, huku kamati yake ikicheleweshwa kwa pesa za kutimiza wajibu, na ikizingatiwa pia ufungaji wa vifaa unaendelea kama ilivyoripotiwa na gazeti, wasi wasi wa nini kinaendelea unazidi ukubwa wa subira ya matokeo

Mchanganyiko huo pamoja na uwajibishwaji wa waziri, unaacha maswali kuliko majibu. Ni kweli tatizo la waziri lilikuwa ulevi tu au linahusishwa na Lugumi kwa njia nyingine?

Hakuna anayeweza kujibu kwa uhakika, kwani waziri anawajibika kwa Rais na ni haki msaidizi huyo kuondolewa wakati wowote na mteule wake

Jambo ambalo ni wazi ni kuwa, suala la Lugumi linafunika kila hatua inayochukuliwa

Utaratibu wa 'kufunika' tatizo kuanzia bungeni na hizi harakati za kufunga vifaa zikiambatana na 'kuikwaza' kamati husika inatoa picha mbaya kwa serikali

Suala la Lugumi litahusishwa na kila hatua, litakuwa kipimo cha kila hatua na litakuwa ndiyo 'bar' ya utendaji wa serikali kwa kuzingatia kauli zake na maadili kwa ujumla

Ni vema serikali ikaliona hili kama tatizo,jawabu si kulifunika bali kuacha mkondo wa shEria za asili 'natural justice' ufanye kazi zake. Kwamba, ukweli ujulikane bila kificho

Tumeshuhudia matatizo kama Richmond ,n.k. yakIfunikwa na kujirudia kila siku.

Hatuoni Lugumi kuwa tofauti, na linapofungamanishwa na utendaji wa serikali ni mbaya

Serikali ijiulize, kila inapofanya jambo likahusishwa na Lugumi , je hilo ni jambo jema?

Lugumi itaendelea 'kuitesa' serikali hadi lini? Kwanini kuna kila 'namna ya ' kulifunika?

Tusemezane
Kama kuna tatizo awamu hii imejitafutia na itaishi na tatizo ni Lugumi.

Huu ni mtihani mgumu katika uadilifu, kuaminika na kueleweka. Serikali imefaulu au imefeli?

Tutaendelea na Lugumi iliyoelezwa bungeni katika uzi huu Duru za siasa: Ndani ya Bunge
 
NINI KINAENDELEA NYUMA YA PAZIA?

LIPO LINALOHITAJI MAREKEBISHO YA HARAKA

NI HOFU INAYODUMAZA FIKRA NA WELEDI?

Yamekuwepo matukio ya kujiuliza tangu awamu iingie madarakani.
Siku za awali ilidhaniwa ni ugeni na muda utatoa nafasi

Kadri siku zinavyosonga mbele mkanganyiko unaendelea. Kuna nini?

Awamu ilianza kwa muda mrefu bila baraza la mawaziri.
Ikaelezwa kwasababu nyingi ambazo ni ngumu kuzielewa au kueleweka

Baraza likatangazwa likisemwa kuandaliwa kwa umakini wa juu.
Hiki ni chombo kinachomshauri Rais katika shughuli zake za kila siku

Ikafuata utekelezaji wa mambo, tumbua za watendaji, na kuhamisha watu wa mabondeni kwa kuvunja nyumba. Muda haukupita zoezi likasitishwa

Yakatokea malalamiko ya mawaziri kutokuwa na 'instruments' ambayo hayakukanushwa. Kukawepo malalamiko bunge 'kuporwa' haki ya kudihinisha mafungu na kuyaelekeza maeneo kwa mujibu wa sheria

Tangazo la kuzuia kuagiza sukari likatolewa na kufuatiwa na uagizaji wa sukari kutoka nje kwa muda mfupi tu wa tangazo la awali

Wakateuliwa mablozi bila vituo vikisubiri kupangiwa

Wakateuliwa wakurugenzi na teuzi zao kufutwa chini ya siku mbili

Bodi zikafutwa, uteuzi ukarudisha baadhi ya wajumbe wa zamani.

Ikafuata utumbuaji hadharani zikiacha waathirika kuonekana wahalifu kabla ya sheria za asili 'natural justice' hazijatumika

Iktangazwa kodi za miamala, mabenki yakaweka kodi kinyume cha tangazo la bunge. Serikali ikisema hili, benki kuu lile na mabenki jambo jingine

Inaendelea... sehemu ya II
 
Ukaja uteuzi wa wakuu wa wilaya hivi karibuni.

Tukio moja la Mkuu wa Wilaya kuondolewa dakika za mwisho tatiza fikra.

Tuliambiwa umakini ulitumika kuwapata, inakuwaje mtu anafika dakika ya mwisho bila kujulikana hakupaswa kuwemo?

Ukubwa wa tatizo ni pale kamishna wa tume ya maadili alipomuomba 'mteule' awapishe. Ni kama vile mteule alivamia shughuli 'gate crasher' ndani ya Ikulu.

Mosi, kwanini mkuu wa tume ya maadili achukue jukumu hilo?

Pili, huyo 'mteuliwa' aliingia vipi Ikulu ikiwa hakupaswa kuwemo ndani?

Tatu, kwanini asiitwe faragha na kuelezwa bali

Kulikuwa na sababu gani za 'kumdhalilisha' kana kwamba alitumia 'fojari'.

Mtu asiyehusika aliingiaje Ikulu na kupitia wapi na kwa utaratibu gani?

Mlolongo wa matukio yanayoonyesha kukosekana mpangilio (disorganization)

Inatosha tu kusema kuwa lipo tatizo nyuma ya pazia.

Kwamba, kazi ima zinafanywa kwa kasi kubwa na kusahau mambo muhimu.
Au hazifanywi kwa umakini na watumishi husika

Je, ni kutokana na hofu iliyotanda watumishi na kufunika weledi na umakini?

Je, hofu inatokana na utumbuaji au kasi wasioimudu inayosemwa?

Je, ni kutokana na wahusika kutoshaurika?

Watumishi waliopo, wengi ni walitumikia awamu iliyopita.

Pengine lipo tatizo nyuma ya pazia!

Tusemezane
 
UHARAKA WA SERIKALI NI WA NINI?
'TUNATENGENEZA MAGARI' SI MAJEMBE AU KANDILI

Sehemu ya I

Mabandiko mawili hapo juu tumehoji kuna kitu gani kinaendelea katika awamu ya tano!
Inaonekana tatizo la umakini ni kubwa kuliko tunavyoliona.

Soma habari hii ili tufuatane kwa ukaribu Kiwanda cha magari sasa kujengwa nchini

Waziri wa viwanda na biashara anasema upo mpango ndani ya miezi 6 wa kujenga kiwanda cha kutengeneza magari kupitia SIDO na VETA .
Kwamba ekari 2,500 zinatafutwa kwa kazi hiyo

Hizi zinaonekana ni habari njema kabisa kwa Watanzania. Hata hivyo, kwa kuziangalia kwa jicho mujarabu 'critique' tunaona zipo hoja za kujadili kutokana na habari iliyopo

Hoja ya kwanza
Kutengeneza gari kunaanza na injini kisha ujenzi wa bodi. Gari ni injini siyo bodi inayoweza kuundwa na kampuni yoyote.

Kwa mnaokumbuka, zamani ilikuwa kawaida kusoma magari yakiwa yameandikwa 'Body Built by... etc' hawa hawakutengeneza magari waliunda bodi

Hivyo, ingalipendeza mheshimiwa waziri kama angalisema SIDO na VETA wataunda magari(assembly) na si kutengeneza (manufacture)

Hoja ya Pili
Tulikuwa na kiwanda cha kuunda magari cha TAMKO -Kibaha.

Nini kiliua kiwanda hicho na kuna ushahidi wa sababu zimetoweka kiasi kwamba SIDO/VETA watafanikiwa?

Kuna kiwanda cha Nyumbu-Kibaha.
Kwanini serikali isikiendeleza kwa kushirikiana na SIDO/VETA?

Hoja ya tatu
Katika nchi za wenzetu zipo taasisi zinazofanya kazi za R&D (Research and Development).

Taasisi hizi ushirikiana na Vyuo vikuu katika miradi mikubwa kama huu wa magari.

Lengo ni kuangalia thamani (value), ubora (quality) gharama za mradi (cost and returns) na uendelevu wa mradi (sustainability) na faida za mradi, kwa uchache wa kuzitaja

Ili hoja hii ieleweke tungependa kutoa mifano kadhaa

Chuo kikuu cha Muhimbili kina uhusiano wa karibu na London school of tropical medicine
Muhimbili inahusiano mzuri na Marylanda University katika mambo ya medical research
Sokoine Univ ina uhusiano wa karibu na vyuo vya Scandinavia
Chuo cha Ufundi Arusha kina ukaribu na vyuo vya Ujerumani
UDSM ni mama wa vyuo nchini na kina uhusiano na vyuo vingi sana duniani

Ukaribu huu unawezesha vyuo/taasisi nyingine kufanya tafiti za suluhu zinazoikabili jamii

Mathalani, Sokoine University walitafiti Panya wanaoweza kugundua mabomu na sasa panya hao wana uwezo wa kugundua maradhi ya TB.

Thamani ya utafiti wa SUA imelenga mazingira yetu na kutoa suluhu ya matatizo

Tujiulize SIDO/VETA vina mahusiano na taasisi gani nyingine kiasi cha kufikiria 'kutengeneza' magari?

Je, hilo ndilo lengo la kuanzisha SIDO au VETA? na je, magari ndiyo tatizo linalotukabili?

Inaendelea sehemu ya II
 
Sehemu ya II
Lengo la kuwa na SIDO ilikuwa kuendeleza viwanda vidogo vinavyoweza kutoa suluhu ya matatizo yetu bila kutegemea bidhaa za nje.

Sido ilikusudiwa kujenga uwezo wa shughuli ndogo kama utengenezaji wa majembe, mashoka, mapanga, Plau n.k.

Hakuna ushahidi kuwa lengo la kuundwa kwa SIDO lilifikiwa na kuvukwa kiasi kwamba SIDO sasa inaingia katika ushindani na makampuni ya Toyota na Mercedes Benz.

Je, SIDO imeweza kutatua matatizo japo ya kutengeneza mashine za kufyeka mapori, kupanda, kulima, viwandani na kwenye taasisi kama mashuleni?

Kwanini SIDO wasifikirie kutengeneza kifaa kama 'computer' inayotumia nishati rahisi ili mtoto wa kijijini apate uelewa wa kompyuta inakuwaje kabla hajaiona University!

Kwanini SIDO wasifikirie kutengeneza mashine ndogo itakayomwezesha mkulima kuinunua kwa shamba lake la ekari 10 au 15 katika gharama nafuu!

Kwanini SIDO wasifikirie kutengeneza vitanda vya hospitali na mashuleni vyenye ubora kwa kutumia rasilimali zilizopo nchini?

Kwanini Sido wasifikirie kutengeneza solar panel zitakazokuwa rahisi ili wanakijiji wamudu na kuokoa muda wa kutafuta nishati na uharibifu wa mazingira

Kwanini SIDO wasifikirie kutengeneza baiskeli kwa kufufua kiwanda cha swala, au boda boda ambazo mtu wa kawaida atamudu.

Kwanini tununue bajaji za india na kuzifanya 'ambulance' badala ya SIDO kuunda Bajaji zenye ubora Zaidi wa kuwa ambulance katika mazingira yetu.

Na hali hiyo ipo katika VETA ambayo ni mamlaka ya ufundi mdogo unaowezeha vijana wasio na nafasi kupata ujuzi wa kuendesha shughuli ndogo ndogo

Dar kama utapata real auto electrician ni kwa bahati sana.

Waliopo ni uzoefu tu wa kukaa na babu fundi. Kwanin VETA isitumie fursa ya kufindisha vijana tasnia hiyo ili tuwe na mafundi wanaojua magari yaliyotengenezwa Japana na njia zake za umeme!

Inaendelea sehemu ya III
 
Sehemu ya III

Tumalizie kusema, ili tuweze kupiga hatua lazima tutumie taasisi na wataalamu wetu.

Tungeimrisha R&D katika taasisi na vyuo vikuu ingalikuwa bora kuliko miradi kama huu

Tunajichanganya na kuichanganya dunia pale tunapofanya mambo kutoka 'no where' badala ya kutumia taasisi zetu zenye mitandao na zinaoeleweka.

Pesa za kuimarisha SIDO/VETA kutenegeneza magari zingalikuwa na thamani kama zingelekezwa UD CoeT ua Arusha Tech

Hatuhitaji kutengeneza magari kwani hakuna ushahidi wowote wa kitaalamu kuwa yatauzwa kwa bei atakayomudu mtanzania asiyemudu gharama za pancha ya boda boda

Na matatizo yetu si magari, ni kujikwamua katika umasikini kwa kutumia rasilimali zetu.

Kuna sababu gani za kuunda magari ikiwa machungwa yetu yanakwenda Kenya na kurudi katika mabosi kwa bei ya juu?

Tunadhani hatchery unit zetu zitakazotuwezesha kukidhi mahitaji ya soko la ndani na majirani ni muhimu Zaidi ya kuunda magari.

Tunaundaje magari ikiwa hatuna solution ya mbu wanaotuua kwa malari, hatuna suluhu ya ajali za barabarani na hatuna suluhu ya vyoo hadi balozi wa Japan aje kutupa msaada.

Dhana ya Tanzania yenye viwanda ina mantiki, tatizo wengi hawajui mantiki yake

Na hilo ni kutokana na watu wetu kujengewa woga, nidhamu ya kutengeneza, kufikiria kutumbuliwa n.k. Haraka haraka za nini na kwa faida gani?

Tutengeneze kandili za kutumia gesi yetu ya Mtwara kwanza kabla ya kupambana na Lexus au Limboghin.

Tusemezane

Ronal Reagan
 
Back
Top Bottom