Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

HILI LA CCM DODOMA LIMETIA DOA
KUENDELEA KULITETEA NI KUHARIBU ZAIDI

Bandiko 121 tulizungumzia kauli ya 'walk the talk' kwa maana ya kuishi katika kauli.
Katika siku za karibuni kumekuwa na mvutano 'tension' kuhusu 'marufuku ya mikutano ya siasa

Mvutano huo umeletwa na uwepo wa mkutano wa CCM Dodoma tofauti na marufuku yaliyopo.
Wengi wamejiuliza, tangazo la kupiga mikutano marufuku lilihusu akina nani au kundi gani la jamii?

Tatizo kubwa ni pale utetezi wa uwepo wa mkutano huo unapopinga kila uchao.
Msajili wa vyama vya siasa alisema ' Wapinzani hawakumwelewa Rais, na wala hakupiga marufuku bali kuwakaribisha katika siasa za kuendeleza nchi na kuacha siasa za ukandamizaji'

Msajili hakueleza nani anafanya siasa za ukandamizaji au siasa za ukandamizaji ni kitu gani.

Tukasikia jeshi la Polisi likisema, taarifa yake ya June ilipotoshwa. Marufuku ya mikutano na maandamano hayahusu shughuli za kiutendaji za vyama vya siasa.

Na kwamba marufku hayo yalitokana na hali ya usalama kutokuwa nzuri.
Kauli ya hali ya usalama haikuwahi kusemwa na wasemaji wa awali kama Rais au msajili wa vyama

Rais alisema, alihitaji nafasi ya kutekeleza ahadi zake za uchaguzi na kwamba siasa zifanywe katika maeneo ya uwakilishi kna madiwani au wabunge.

Tumesikia viongozi wengine nao wakidai marufuku ya mikutano maeneo yao.
Sababu zinazotolewa ni kutoa nafasi ya shughuli za maendeleo.

Huko nyuma waziri mkuu alishawahi kutoa maagizo kama hayo kwa kuruhusu 'walioshinda' na siyo walioshindwa. Ilisemwa pia uchaguzi umekwisha sasa ni muda wa watu kufanya kazi.

Mtiririko mzima unazua maswali mengi kuliko majibu

1. Je, kuzuia mikutano ilikuwa kuwaalika wapinzani kama alivyosema msajili wa vyama?
2. Je, kuzuia mikutano ni kutokana na hali ya usalama isiyoridhisha kama alivyosema Polisi?
4. Je, zuio ni la mikutano ya nje pekee au linahusu ya ndani?
5. Je, kuzuia mikutano ni kutoa nafasi za watu kufanya kazi ?
6. Je, kuzuia mikutano ni katika kuisaidia serikali kukamilisha ahadi zake za ilani ya uchaguzi?

Inaendelea...
 
Majibu ya maswali hapo juu yanazua hoja nyingine

Ikiwa mikutano imepigwa marufuku, je, ule wa CCM unaangukia katika eneo gani?

Ikiwa mikutano ya ndani imeruhusiwa, je, ule wa ACT Wazalendo ulizuiwa kwa kigezo gani?

Kwa mtazamo huo, haielweki kwa uwazi nini hasa kimezuiliwa na kwa kutumia sharia gani.

Ikiwa katiba na sharia za vyama zinaruhusu, marufuku yalitakiwa kupatikana katika katiba au sharia za vyama. Waswahili wanasema mwiba hutoka ulipoingilia.

Kauli tatanishi kutoka kwa kila mtu zinaeleza jambo moja, hakuna uhakika ni kwanini haya yametokea

Yote yanaitia doa serikali iliyoungwa mkono sana na wananchi kwa kauli ya kusimamia sharia.

Ni ukweli, tulizembea sana katika kusimamia sharia na ndicho chanzo cha matatizo tunayoyasikia

Majipu ni zao la business as usual na kila mmoja alifarijika na hatua zinazochukuliwa.

Kwasasa kuna mshangao, je kilichosema ndicho kinachotendwa? walk the talk?

Hili linatufikisha katika eneo jingine.

Kwamba, kuna kitu kinachoitwa 'breach of trust', halafu kuna public trust na mwisho kuna mistrust.

Haya yanapoingia katika fikra za wananchi, lipo tatizo

Inaendelea....
 
Hivi unawezaje kupiga marufuku mikutano ya siasa wakati kila kitu ni siasa.
Kabla hatujaendelea, hili ni swali muhimu,wengi hawaelewi siasa inagusa vipi maisha yao.

Inawezekanaje kutenga siasa na maisha ya kila siku. Wenyewe wanasema 'politics is everywhere'
Nikunukuu kauli ya Mag3 , siasa ipo level kuanzia familia

Mipango ya familia,kuna matamanio,vipaumbele, majadiliano),maleng, utakelezaji na matokeo. Ndivyo ilivyo katika level zote za siasa

Hakuna mafanikio bila kushikirisha wahusika, na kama Taifa ni wananchi.
Ndio wanaotengeneza chombo kinachoratibu shughuli nzima, yaani serikali kupitia siasa

Serikali zinawekwa na watu na ni za watu '...of the people by the people'
Serikali ikijitenga na mfumo ulioiweka.. inabaki' watawala na watawaliwa'

Kama sehemu ya mfumo wa siasa, mipango ya serikali inagusa maisha ya watu

Kwa mfano, serikali inatekeleza malengo yalioidhinishwa na wanasiasa Bungeni
Inapozungumziwa ajira walengwa ni watu mmoja mmoja au kwa pamoja.

Mipango ya serikali kama tulivyoona marufuku uagizaji sukari iligusa maisha ya watu
Iwe lengo ni kutengeneza ajira au ongezeko la bei,hayo ni maamuzi ya kisiasa

Wanaopanga mishahara/kodi n.k. ni wanasiasa kwa ajili ya wafanyakazi.
Mipango kama ya Kodi ya miamala ya benki iligusa maisha ya walaji 'consumers'

Kwa upande mwingine lengo ni kupata kodi jambo linalogusa maisha ya watu pia
Bei za mazao/pembejeo zinapangwa na wanasiasa na zina anaathiri ya siasa.

Huduma za afya, elimu, jamii n.k zinapangwa na wanasiasa.
Wanaoatahirika na maamuzi ni wananchi mmoja mmoja na kwa wingi wao.

Bei ya mafuta na kodi inaathiri anayeendesha Vogue hadi mwasha kibatari

Mtu wa mwisho kupokea matokeo ya kazi za kisiasa ni mwananchi.(at the receiving end)

Inakuwaje aachwe nje ya mfumo wa kujadili mambo yanayogusa maisha yake?

Kwavile kila jambo/tukio/mipango n.k. inagusa maisha, siasa ni sehemu ya maisha kila siku. Kuzuia mikusanyiko ya watu ni kuitenga siasa na maisha yao.

Wananchi 'wataiutumikia siasa' na si kuitumia katika mambo yanayowagusa
Ilimradi maisha yapo,siasa ipo ndani ya maisha hayo,na mijadala ya siasa haina muda
 
WIKI HII KATIKA NCHI YETU

NINI KINAENDELEA?

Prof Ndalichako yupo Sahihi
Serikali yaleta tension isiyo na ulazima

Katika bandiko 53 la uzi huu tuliandika kuhusu wizara ye elimu. Tulisema , hataua anazochukua waziri Ndalichako kurudisha hadhi ya elimu zaina mwelekeo mzuri.

Katika uzi huu, tulieza kuingiliwa maamuzi ya kitaalamu na wanasiasa.
Tulisema, wanafunzi wasio na sifa hawafai kupata nafasi kwasababu za kisiasa

Jitihada za waziri kuhusu chuo kikuu cha Dodoma, ziliingiliwa na wanasiasa na siasa kiasi cha lengo muhimu la alichotaka kukifanya kupotea

Pengine angalipewa nafasi ya kutenda bila kuingiliwa, zoezi la UDOM lisingetia aibu.

Tunadhani zoezi lilidhindwa kuwa na ufanisi kwasababu ya amri za kisiasa zilisizozingatia mambo mengi kama usalama

Wiki hii, waziri Ndalichako amefungia baadhi ya vyuo vikuu kudahili wanafunzi
Hatua imekuja wakati muafaka . Tunajua awamu ya nne haikutilia maanani elimu

Elimu ilifanywa sehemu ya siasa za kila siku, hakukuwa na usimamizi, ni eneo lililoathirika

Jambo la kutisha ni kufumuka kwa vyuo vikuu. Nyerere alkiondoka hakuacha Zaidi ya vitatu, Mwinyi na mkapa nao wakawa na ongezeko lao

Awamu ya nne vyuo vikuu vilifumuka kama utiriri. Hakukuwepo uhakiki, ilimradi kuna jengo lenye kuta nne, basi ni chuo kikuu.

Idadi imefikia kiwango cha kutisha. Hakuna ubora, kilichoangaliwa ni kuzuka kwa vyuo

Hili limeleta tatizo kubwa, kwamba elimu ya chuo kikuu inapatika katika eneo hovyo, wanafunzi wakifundishwa na watu wasio na sifa, mazingira mabovu n.k.

Kwa ufupi, awamu ya nne ilileta tatizo kubwa elimu. Wao, walijuvunia wingi wa vyuo bila kujali ubora. Haya ni katika kutafuta sifa za kisiasa bila kujali athari kwa taifa.

Hatua anazochukua Prof Ndalichako ni muhimu sana na za kuungwa mkono.

Kusafisha vyuo ili vitoe wataalam waliova na wenye hadhi,vipate heshima na kupata fursa kwingine dunia, ni jambo la tija sana

Wasi wasi wetu ni kama Ndalichako atapewa nafasi ya kutumikia taaluma yake bila kuingiliwa na wanasiasa.

Na Endapo prof atasimama katika ukweli, sisi lazima tuungane naye na kuwakataa wanasiasa kuingilia mambo ya kitaaluma

Kwa hili tumpongeze waziri na jitihada zake.

Tension isiyo na ulazima inafuata

Tusemezane
 
'TENSION' YA NINI NCHINI?

Ipo tension ya kisiasa inayoendelea nchini.
Tangu awamu hii iingie madarakani utangamano kama taifa unazidi kupoteza nguvu.

Vyama vya upinzani vimetangaza kuanza mikutano mwezi sept.
Serikali na Rais zikiwemo za mikoa zimepiga marufuku shughuli za kisiasa

Huko nyuma jeshi la Polisi lilitoa sababu za kuzuia mikutano ya kisiasa.
Kadri muda ulivyosonga, sababu zimeonekana dhidi ya kundi mengine yakiendelea...

Kauli ya Rais akiwa Singida inaonyesha Polisi walifuata maagizo hawakuwa na sababu

Hilo linaoenakana katika sababu waziokuwa wanazitoa zikibadilika badilika kila siku

Hoja kubwa inyaojenga sasa ni kuzuia mikutano wananchi wafanye kazi.

Jukumu la serikali ni kupanga mipango ya nchi na kuitekeleza, si jukumu la serikali kujua nani anafanya nini kupata mlo wake.

Katiba ya nchi inatoa nafasi ya wananchi kukusanyika. Inatoa taratibu za kisiasa kwa kuziwekea vyombo kama msajili wa vyama na tume za uchaguzi.

Vyombo hivyo hufanya kazi kila siku kwasababu siasa ni tukio endelevu.

Mikutano inazuiwaje vyombo hivyo vikiendelea na kazi za kisiasa?
Nini kinazuiawa hasa, ni mikutano ya kisiasa au shughuli za kisiasa?
Wapi imeelezwa katika sharia za nchi?

Kuzuia mikutano hakujawahi kutokea katika historia ya nchi hii.

Mwalimu Nyerere akihutubia mkutano wa vyama vingi Jangwani, alisema;
'kama yupo anayetaka kubebwa mtu huyo kavunja sheria gani ya nchi'?

Kauli hiyo ilimaanisha, siasa zisizovunja sharia za nchi zifanyike bila masharti

Hakuna sheria inayozuia mikusanyiko ya watu wa kisiasa hadi leo hii.

Kitendo cha kuzuia watu kufanya siasa popote nchini ni kukiuka sheria za nchi, haki za binadamu na kuliweka Taifa katika tension isiyo na ulazima

Kauli za Serikali si kuwa zinawagawa wananchi tu, zinadhalilisha taasisi kama ya Polisi. Hivi leo Polisi watasema nini waaminiwe na umma?

Kila sababu iliyoteolewa na Polisi imebaki kuwa ni uongo
Kwa mujibu wa serikali zinazosema 'wananchi wafanye kazi' isipokuwa mtu mmoja tu

Jambo moja linalozunguka katika maongezi ya baadhi ya sehemu za jamii yetu ni kuhoji, marufuku ya mikutano yanalengo gani. Wapo wenye mitazamo tofauti kama ifuatavyo

Hofu ya serikali kuwa 'madudu' ya nyuma,mikataba feki, uuzaji wa rasilimali za taifa n.k. Kuna hisia CCM wanatumia serikali na vyombo vya dola kuficha maovu yao yasiwekwe hadharani ili kusafisha chama.

Hisia la suala la Zanzibar.Zipo pia za serikali kutokosewa na kutaka kuua upinzani

Zote hizo ni hisia tu kasababu ya kujichanganya kwa kauli na kutokuwa na mantiki ya kuzuia mambo halali kikatiba na kisheria

Pengine serikali ingalitoka na kufanya jambo hilo kisheria.
Moja, kupeleka mswada bungeni wa kuzuia shughuli za kisiasa na ukikubaliwa uwe sharia

Pili, Rais kutumia nguvu yake ya kikatiba 'presedentila decree' kutangaza marufuku kwasababu yoyote ile iwe ya kiusalama n.k

Kwa namna inavyofanyika sasa hivi, tunaiweka nchi katika tension isiyo na ulazima.

Tunavunja sheria zetu wenywewe tukichagua nani zinamgusa nani hazimgusi.
Wakati huo huo tunasisitiza utawala wa sheria

Hizi ni 'conflicting message' kwa wananchi. Umoja wa kitaifa unapoteza nguvu, serikali iliyoanza kwa kusifiwa sana duniani inapoteza umaarufu kwa kasi ya hali ya juu

Hii ni nchi yetu sote, lazima tuwe wamoja chini ya sheria

Tusemezane
 
WIKI INAOISHIA 30 JULY

SERIKALI KUHAMIA DODOMA I

Wiki hii kama mnavyoona mabandiko imekuwa na matukio mengi
Moja ya matukio yaliyochukua uzito ni la serikali kuhamia Dodoma kabla 2020

Kauli imetolewa na Rais akihutubia mkutano mkuu, kisha waziri mkuu aliyetamka kuhamia Dodoma Sept, ikiwa ni siku 33 kuanzia siku ya leo.

Mtafaraku na taharuki ya mawaziri imeanza kuonekana kila mmoja akitoa azimio la wizara yake kuhamia Dodoma

Suala la kuhamishia makao makuu ya nchi lipo tangu mwaka 1970 ndiyo msingi wa kuanzisha mamlaka ya CDA. Ukiacha awamu ya kwanza, zile za pili ,tatu na nne hazikuwa na msisimko wala mkazo wa kuhamia huko

Hivyo kisheria ni suala linalohitaji kupelekwa Bungeni kwani ni la kisera kwa wakati huu kuliko kisheria.

Kuhamia Dodoma ni wazo zuri kwavile kisera lilikubaliwa na wengi. Hata wanaokataa bado hawajatoa sababu za msingi ukiachilia mbali hoja ya gharama

Tatizo lilopo ni kufanya mambo bila mpangilio na mwisho wa siku tutajikuta katika wakati mgumu kuliko unavyodhaniwa. Kuhamisha mji ni suala la mipango si amri kama inavyosomeka sasa

Hapa ndipo tunapaswa kujadili Zaidi kuliko kujadili kuhamia au kotuhamia
Kuna matatizo mengine yanayoambatana na hatua zinazochukuliwa

Tutazijadili kwa kina katika mabandiko yanayofuata
 
KWANINI UHARAKA BILA KUZINGATIA MAMBO MENGINE? IV

Rais amesema, serikali yote itahamia Dodoma kabla ya 2020
Kilichotakiwa si kuamrisha shughuli kabla ya mapgilio

Ilipaswa shughuli ziandaliwe na CDA na wadau kama NHC na Mifuko ya jamii

NHC ingeombwa kusimamisha ujenzi wa nyumba kwingineko na kupewa muda wa miezi sita kujenga makazi ya watumishi kupunguza msongamano utakaopandisha bei za pango

Mifuko ya jamii ingeombwa kuangalia uwezekano wa kuwekeza Dodoma na kupewa na kupewa incentives kama misamaha ya kodi ili kuharakisha upatikanaji miundombinu

Mashirika mengi yaandae miundo mbinu, mashule, Hospitali , masoko , malls n.k. ili kupunguza 'strains' katika mji unaokumbwa na dharura ya influx ya wahamaiaji wa ndani

Reli ilitakiwa iimarishwe na kuanza kazi kwa dharura wakati ya std gauge ikiendelea.
Hii ni pamoja na kuongeza huduma kati ya Dodoma na Dar hata mara 3 kwa siku ili kusaidia 'smooth transition' ya watumishi

Wengi wataacha familia zao Dar waliko na makazi, ni muafaka wakapata huduma za uhakika za mawasiliano na familia hizo wakati wakiandaa kuhamia Dodoma

Kuhamia kulipaswa kutanguliwa na ofisi zinazoratibu mambo hayo kama wizara ya tawala, ofisi ya waziri mkuu na hata makamu wa Rais

Kisha wizara zipewe ratiba ya kuhamia huko kwa mpangilio ili kutoa nafasi ya mji kuji adjust kila ongezeko linapotokea.

Ikiwa Rais ameseama serikali itahamia huko yote ikifika 2020, kuna ulazima gani wa ku panic kwa wakuu wa wizara, idara n.k. kiasi cha kuhamia katika siku 30?

Endapo wizara na idara zote zitahamia huko katika kipind cha siku 30 au hadi mwisho wa mwaka, tamko la Rais kuhamia kamili 2020 halitakuwa na maana

Tunadhani Rais aliposema 2020 alimaanisha utaratibu mzima kwa mpangilio.
Hakuwa na maana ya siku 30 kama inavyochukuliwa sasa hivi

Tatizo linaloonekana ni la viongozi kuwa na nidhamu ya woga, kutoweza kufikiri kwa upana na kutojiamini.

Hilo ndilo linapelekea kuchukulia kauli ya Rais kama kuhama katika siku 30

Nidhamu ya woga itazua mtafaruku mkubwa mbele ya safari, na watakaolipa gharama za nidhamu hiyo ni watu wasiohusika na wasiopaswa kama watumishi wa umma

Yes, utaratibu wa kuhamia Dodoma ulikuwepo. Yes, ni vema ukatekelezwa badala ya kubaki vitabuni, au ufutwe. Yes, ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili kutorudi nyuma.

Lakini hatua za haraka haina maana siku 30, na hatua hizo lazima zifanyike kwa mantiki na weledi. Ni muhimu kupanga kwanza na si amri

Yes Dodoma! inavyofanywa kwa sasa ni NO, itaishia kwa Dissapointment kubwa sana.

Hili ni suala la kitaalamu kuliko siasa. Ni suala linalohitaji mipangilio

Tutaanguka sote tukitafuta mchawi asiyekuwepo, kufeli kwa hili hakuepukiki

Kufeli si kushindwa kuhamisha mizigo na mafaili, ni chaos, frustrations and disappointment inayokuja mbeleni kwa kasi kama dhoruba. Hiyo haiepukiki

Tusemezane
 
KUHAMIA DODOMA

TUSIFANYE MZAHA , SI JAMBO RAHISI

Katika uzi huu tuliandika, katika mambo yatakayomkwaza na kumuangusha Rais ni pamoja na vyombo vya habari hasa vya umma.

Vyombo hivi havimsaidii katika kuona mambo kwa mtazamo mpana.
Vimejikita katika kuandika habari za 'faraja' za kusifia na ushabiki

Mfano ni gazeti la Habari leo la J'pili, likionyesha urahisi wa kuhamia Dodoma

Kwamba, bei za nyumba ni chini , vyakula vinapatikana n.k.

Gazeti linasema, vyumba katika baadhi ya maeneo ni 15,000-30,000 zikiwa ni za udongo na vyoo vya nje vya kuchangia wapangaji, eneo la Mlimwa C.

Gazeti limeonyesha maeneo ya Uzunguni na Area C gharama ni 300,000+

Habari leo imenukuu takwimu kutoka NBS zikionyesha hali ya maish kwa sasa
Mwandishi ameipa habari hiyo kichwa 'Mambo rahisi 4 kuhamia Dodoma'

Hoja yetu
Mwandishi amenukuu takwimu bila kuzifanyia tathmini.

Na habari yake haikuzingatia idadi ya watu wa sasa na wanaotaraji kuhamia.
Haikuangalia furstations zinazotokana na makazi kama ya Mlimwa

Mtu mwenye nyumba yake Dar au chumba kimoja, akimabiwa ahamie nyumba ya udongo ya kuchangia choo, kisaikolojia ni jambo kubwa sana.

Mtu mwenye nyumba , umwambie aanze kulipa laki 400,000 kutoka mshahara tofauti na ilivyo sasa, inaathari sana kisaikolojia na kimaisha

Mwandishi ameeleza mambo 4 kwa urahisi sana bila kuzingatia ukweli kuwa kwa muda mfupi mji utakuwa na ongezeko lisilotarajiwa.

Hakueleza athari katika huduma za jamii zinazotokana na ongezeko la watu

Watumishi dadi ya 50,000 inatosha kuongeza population kwa mamilioni.

Kuongezeka kwa idadi ya watu kunakwenda sambamba na huduma nyingine, kuanzia biashara, huduma za jamii n.k.

Demand and supply itapandisha bei ya chumba anachosema,mara 5-10.

Gazeti linaweza kuwa faraja kwa watawala,haliwaelezi ukubwa wa tatizo.

Wananchi watakapokuwa frustrated watawala watajikuta katika hali tofauti.

Tuambizane ukweli, tusifiche matatizo kwa 'sugar coat' Haya ni maisha

Vyombo vya habari vimsaidie Mh Rais kwa kueleza ukweli ulivyo
 
HOJA YA WAZIRI WA ELIMU

Mabandiko 6 mfululizo tumeongelea sana suala la kuhamia Dodoma.
Hili ni si suala dogo kama linavyoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari
Si suala dogo kama linavyochukuliwa na baadhi ya viongozi

Ni suala linalohitaji mipango , kushauriana , kukosoana kisha kwenda pamoja
Nidhamu ya woga inachangia kulirahisha, nani atakayehoji kwa hofu ya kutumbuliwa?

Tutaendelea kulijadili, lakini kwa sasa tunaomba radhi turudi bandiko 166 tulilosema Waziri wa elimu anafanya kazi nzuri ya kusafisha uozo kama ule wa uyoga wa vyuo vikuu vingine vikiwa havina hadhi hata ya high school

Kinachotusukuma kulirudia ni hoja ya 'mdau' aliyewasiliana nasi akiuliza, je, anayofanya waziri Ndalichako ni sustainable? kwa maana ni endelevu?

Hoja hii ni ya msingi sana kuijadili. Tunakumbuka mwenyekiti wa Jiji Mzee Keenja aliwahi kulisafisha jiji kila aina, likitengeneza miradi, likishughulikia miundo mbinu na kubwa Zaidi kuwa mfano wa majiji safi katika Afrika

Tangu ameondoka, Jiji limerudi katika hali yake ya 'kawaida' ya uvundo
Keenja alifanikiwa kama yeye, hakufanikiwa kama system'muundo'
Kuondoka kwake kuliondoka na kila jema aliloacha

Ndivyo ilivyokuwa kwa watu kama Sokoine waliosifika kwa kupambana na rushwa, leo imerudi kuliko wakati wake. Ndivyo ilivyokuwa kwa akina Mrema na siku 7, leo mambo ni kama 'kawa' wakisema wenyewe

Waziri Ndalichako anatakiwa ajiulize, tumefikaje mahali hapa?
Akina nani wametufikisha hapa? Je, wapo au wameondoka?

Hakuna mantiki ya kumfukuza mwanafunzi au kusimamisha kozi ya chuo kama hakuna wahusika. Mh Waziri, waliotufikisha hapa pa vyuo hovyo chini ya viwango ni akina nani? Wamechukuliwa hatua gani?

Mwanafunzi mwenye FFF akiwa registered katika chuo kikuu kwa alama hizo anakosa gani mbele ya sharia ikiwa alama zake zilipitiwa na kuridhiwa?

Mwanafunzi mwenye AAA za kufoji, vyeti vyake viliwezaje kumpatia nafasi ikiwa wapo wenye kazi za kufuatilia na kuhakiki vyeti? Kosa la mwanafunzi ni kufoji na anastahili adhabu. Je, aliyemruhusu kuingia na kumpa mikopo amechukuliwa hatua gani?

Inaendelea..
 
WAZIRI WA ELIMU

Inaendelea

Ujenzi au uanzishaji wa vyuo vikuu unahakikiwa na tume ya vyuo vikuu(TCU)
Ilikuwaje vyuo hivyo vikapewa hati za kudahili wanafunzi na kuendesha kozi endapo havikuwa vimekidhi matakwa ya kuwa vyuo vikuu?

Ipo bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB). Bodi iliwezaje kudhamini wanafunzi ikiwa vyuo husika havikuwa vimepata uhalali wa TCU?

Katika vyuo kuna registrar (wasajili) , wapo Deans of faculties or school, yupo chief academic officer, mkuu au makamu mkuu wa chuo husika. Ilikuwaje wote hawa wasione tatizo la mapungufu ya vyuo?
Ilikuwaje wote hao wasione wanafunzi wasio na sifa ?

Ssytem inapofeli kuanzia serikalini hadi katika vyuo tena vya elimu ya juu, tatizo ni kubwa sana kuliko wanafunzi wanaoingia bila sifa.

Wanafunzi hao ni dalili tu ya uwepo wa tatizo na wala si tatizo
Lau kungalikuwa na system imara, yote yasingetokea

Wizara ya elimu kama taasisi inyohusiana na jamii, lazima ishirikiane na mamlaka zingine kama msajili wa vifo na uzazi, idara ya vitambulisho vya taifa, shule nchini n.k. katika kuetengeneza mfumo unaojiendsha wenyewe

Kwa nchi za wenzetu wamefikia mahali ambapo mzazi anaweza kuhojiwa kwanini mtoto wake hajaanza kindergarten ( siyo msingi, sekondari au chuo)

System zao ni kuwa mwanafunzi ana apply online, anachagua shule aliyosoma baasi. Habari zingine za matokeo yake zinapatikana bila yeye kujua

Bodi za mikopo zinatumia uhakiki wa usajili wa mwanafunzi, zinatumia namba za jamii (Social insurance number) kubaini uzazi wa mhusika, aliposomea, umri wake, wazazi wake n.k. Zikiridhika ndipo mkopo unatoka

Prof Ndalichako anajua system za wenzetu zilivyo 'tight' zinavyofanya kazi bila kutumia makaratasi kama uthibitisho wa mwanafunzi eti ni cheti

Kuna uwezekano kwa uzembe ulioonekana wapo wanafunzi wanaotoka nje, wanasoma bure na kuondoka bila mtu kujua. System mbovu

Prof wakati unafanya hayo mazuri, fikiria kuhusu mfumo wa kudumu

Tusemezane
 
'TENSION' INA ULAZIMA GANI?

SERIKALI INAPOTEZA FURSA

Sakata la marufuku ya mikutano limekuwa mjadala kila siku.
Viongozi wakiandaa dola, vyama vya siasa vikiendelea na mpango wao

Kama tulivyosema awali katika hili serikali inapoteza fursa nyingi sana.
Wakati inatatekeleza iliyoahidi na hatua mbali mbali inazochukua, jambo hili linaondoa focus

Badala ya wananchi kuzungumzia bomba la mafuta, kuhamia Dodoma, wafanyakazi hewa, mikataba feki na mambo mengi ya usalama na maendeleo, wanazungumzia marufuku ya mikutano

Badala ya viongozi kusimamia mambo muhimu kama usalama wa wananchi sasa wanahimiza kusimamia marufuku ya mikutano.

Mfano, mkuu wa mkoa wa Dar ametoa amri askari wafanye kazi ya kuzuia mikutano ya kisiasa

Mkoa wa Dar unachagamoto ya usalama. Mkuu wa mkoa angeelekeza jitihada kwa kusaidiana na Polisi ingalikuwa muhimu. Hofu ya wananchi si mikutano, ni sumbuko la vinaka na ujambazi

Kuna hoja za uchafu wa jiji na changamoto nyingi ambazo ni kubwa kuliko mikutano

Yapo mazuri yanayotokea, kwa bahati mbaya hayasikiki kutokana na kugubikwa na suala hili

Kwa mtazamo huo, serikali inapoteza fursa ya kufanya, kueleza na kusikilizwa na wananchi kwa sababu ambazo si kuwa hazieleweki kwa wananchi bali zinajenga hisia zenye mtazamo hasi

Katika awamu zote tangu vyama vingi, na hata Mwalimu alipokuwepo hakukuwa na mazuio ya mikutano ya vyama vya siasa. Na zipo sheria zinazoonyesha wazi kazi hiyo ya siasa ni endelevu

Uwepo wa msajili wa vyama ni ushahidi mmoja. Moja ya majukumu ya msajili ni ulezi na utatuzi wa migogoro. Hili la mikutano linahusisha CCM kama linavyohusu vyama vingine

Tulidhani msajili angetoka na kufafanua hali husika kwa kutazama sharia za uendeshaji wa siasa. Kinyume chake, kakemea uchochezi anaodai ulitolewa ingawa hakuna chombo kingine kilichoona

Tulitegemea kauli ya Msajili ingalipewa kipaumbele na kuwachukulia hatua wachochezi hao.
Hakuna aliyechukuliwa hatua, hivyo kumwacha msajili katika hali inayoleta hisia tofauti

Hapa ndipo tunaona tatizo kubwa. Vyombo husika havisimami kueleza marufuku ya mikutano yamelenga nini na kwa sharia zipi, vimeegemea katika kutekeleza.

Mara zote vyombo hivyo vimetoa sababu za kujichanganya na kuonekana hazina mantiki

Serikali yenye dola ina fursa ya kuwaonyesha wananchi kwa vitendo nini kinafanyika, ni yapi matarAjio na yAnafikiwa kwa njia zipi.

Vyama vingine vingekuwa na hiari ya kusaidiana na serikali au kwenda kinyume.

'Hukumu' ya vyama ipo mikononi mwa wananchi, kuchambua mchele na chuya.
Ni kwanini basi hali ya mivutano kama hii inatokea?

Serikali ijiulize, kwa marufuku haya , na kwa kuwa hakuna sababu zilizoanishwa zinazoeleweka kwa wananchi, ni maswali mangapi yanayozunguka vichwani mwao?

Majibu yatakapokuwa mengi, mengine yasiyo na maana, serikali itakuwa imefaidika vipi?

Kwa hili, serikali ijitathmini , kuna kukosa fursa adhimu pengine kwa hofu au hisia tu!



Tusemezane
 
''TENSION'' INA ULAZIMA GANI?

Bandiko hapo juu , aya ya pili kutoka mwisho tumeeleza wananchi kutoelewa marufuku ya mikutano

Tumesema hakuna sababu zilizoanishwa,mwananchi wa kawaida kuzifahamu
Hii ni kutokana na ukweli kuwa , sababu za marufuku zimekuwa zikibadilika badilika

1. walioshindwa uchaguzi kutofanya mikutano. Walioshinda waliruhusiwa
Haikugusa wengine ambao hawakushiriki chaguzi kama viongozi wa vyama n.k.

2. Marufuku ya mikusanyiko, kama ule wa 'Mazishi' ya chama kimoja kule Mwanza

3. Marufuku kutokana na magonjwa ya milipuko kama kipindu pindu na ule wa Dodoma

4. Marufuku kutokana na hali ya usalama kuwa tete

Sababu 2-4 zimetolewa na Jeshi la Polisi na 1 imetolewa na Mh Kiongozi wa serikali

Sababu zilipoteza mashiko baada ya nyingine kuibuka, 'Wananchi waachwe wafanye kazi'

Tumeona viongozi wakizunguka katika mikutano kila wanapokwenda.
Je, wananchi wanafanya kazi wakati gani wakiwa katika mikutano hiyo?

Kubwa ni la leo,wafanyakazi eneo moja wamelazimishwa kwenda mkesha wa Mwenge.
Huyu mwananchi aliyelala kwenye mkesha, ana nguvu gani za kazi siku inayofuata?

Je, shughuli za mwenge ni tukio linalowahusu watumishi wa umma?

Hao wanaokimbiza mwenge na wakiwa na makundi ya watu wanafanya kazi muda gani?

Sababu zinapojiondoa zenyewe mwisho hakuna sababu itakayobaki.

Kitakachofuata ni wananchi kujitungia maswali na kujipa majibu wao wenyewe
Hapo ndipo tatizo litakazozuka hasa kwa taswira ya serikali.

Mathalani, mtu akijiuliza kwanini ya mikutano?Nini kinahofiwa au kuogopwa?

Mtu huyo atafikia mahali anatoa majibu yake, ya ukweli , uongo au uzushi
Yatakuwa ni majibu sahihi kwake kwasababu ndiyo majibu yake!

Je, ndicho serikali inakitaka kwa wakati huu?

Serikali inakosa fursa kubwa.Hoja ya hii imepoteza mijadala muhimu ya maisha ya watu.

Hili waliangalie tena kama lina tija!

Walitazame kama linaongeza thamani 'add value' katika mikakati yao

Tusemezane
 
SIASA ZA MIAKA 1990

Tuna kumbuka sakata la migomo la vijana wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kuhusiana na masuala mbali mbali ya kijamii wakati wa Mzee Mwinyi (miaka ya 1990)

Mkasa ulihusisha kampeni ya 'OMO' na mmoja wa washiriki ni Mh Mbatia (MB)
Wengine kwa kuwakumbuka na kama tupo sahihi ni Matare na Dr Kimaro wa Muhimbili

Masuala waliyopigania yalihusu maisha ya wananchi ikiwemo dampo la Tabata

Katika hali ya kujinasua , serikali ilitoka na hoja, vijana wanatumiwa na mataifa ya magharibi ili kuvuruga umoja wa kitaifa, Amani na utulivu.

Hadi leo hakuna anayefahamu ni Taifa gani na liliwatumia vijana hao kwa njia zipi
Imebaki hadithi isiyo na ithbati. Baadhi ya vijana hao ni viongozi wa kitaifa leo.

Vijana wale wale waliotuhumiwa kutumiwa leo wana nyadhifa kubwa nchini

Mataifa ya Ulaya kama Spain, Greece na Italy yana kipindi kigumu cha uchumi.

Mengine unemployment(ukosefu wa ajira)ni asilimia 30.
Hayo ni mataifa ya magharibi,mataifa makubwa hayahitaji kusafiri ili kuyafikia

Kinachofanywa na wenzetu ni kuangalia mustakabali bila kutafuta sababu au mchawi.
Wao wanaamini matatizo yao yapo kwasababu yao

Kuna hisia miongoni mwa watu, ili nchi za magharibi zifanikiwe kuingia katika mataifa, ni lazima zilete mtafaruku wa kuziwezesha kupata upenyo huo.

Hoja hii ina mantiki kwa nyakati fulani lakini si nyakati zote.
Mataifa mengi hasa ya Afrika ni wahanga wa uongozi wao.

Pesa zinazofichwa Uswiss n.k. zinawekwa na Waafrika wenyewe kwa usalama.
Ndivyo ilivyo kwa mataifa mengine kama tulivyoona WikiLeaks na Panama.

Kwa nchi yetu, matatizo si rasilimali bali namna gani tunazitumia

Nyerere alisema 'madini hayaozi, Watanzania wakiwa tayari watayachimba'

Akiondoka, Mwl hakuacha ujangili kama uliotokea kipindi kifupi kilichopita.
Misitu haikuvunwa kama inavyovunwa, madini hayakuchimbwa kama ilivyo sasa.

Mchanga haukusafirishwa wala ndege hazikubeba dhahabu kutoka migodini

Hayakufanywa na serikali za chama kingine bali CCM iliyoko madarakani

Matokeo ya ujangili, misitu na madini hayaonekani kusaidia wananchi zaidi ya kwenda nje
Kuporwa rasilimali zetu kungeelezwa vema na CCM kuliko chama kingine

Haya yamefanyika nchi ikiwa na amani na utulivu, iweje tudhani ni lazima mataifa ya nje yawepo ili kuleta mtafaruku na kupora rasilimali zetu?

Kwanini tusikae kitako kutafuta suluhu ya matatizo yetu kama Taifa?
Tunatafuta mchawi wa kubumba ili hali tuna ukweli kuhusu rasilimali zetu?

Kitu kimoja tofauti na miaka ya 1990, weledi wa wananchi ni mkubwa.

Wananchi hawahitaji mazungumzo baada ya habari RTD, mbiu za mikoa n.k. kubaini masuala yanayowahusu kimaisha.

Siasa za 1990 kwasasa zimepitwa na wakati

Mzee wetu Mwinyi , nguli wa Kiswahili , alisema' Kila zama na kitabu chake''


Tusemezane
 
ZIPO NYAKATI, BAADHI YA VIONGOZI WA DINI WAPUUZWE

NI WAKOSEFU WA MAADILI NA WANAFIKI

Sehemu ya I

Katika uzi huu lipo bandiko linalohusu ' Wananchi wasichanganye dini na siasa'

Tumehoji, kama ni hivyo iweje viongozi wachanganye siasa na dini?

Viongozi wanapokwenda kwenye majumba ya ibada na kushiriki sughuli kwa nyadhifa zao na si uchamungu au uumini wao, huko ni kupeleka siasa katika dini.

Ni kuwakaribisha viongozi wa dini katika siasa, kwanza, kwa kuwaonea haya na pili kama msaada kwa nyakati watakazohitajika kwa kujua nguvu yao ya ushawishi katika jamii

Ukweli,siasa imejengwa katika misingi ya dini , hivyo kutengenisha vitu hivyo ni ngumu.

Na matumizi ya siasa yanahusisha uadilifu na hata sala na maombi ya wana dini.

Viongozi wa dini zama hizi wamekuwa 'mamluki' wa wanasiasa badala ya Utumishi wa mwenyezi mungu.

Kuna nyakati inaonekana ''wananunulika'' kuliko sehemu nyingine ya jamii

Sakata la mikutano linaloendelea sasa hivi limechukua sura mpya.

Viongozi wakizungumzia kuhusu mikutano bila kuzungumzia chanzo halisi.

Wanajua, kazi yao ni kusimamia haki na haki si ya vitabu vitukufu tu,makubaliano y jamii yana misingi ya haki.

Kwasasa hawazungumzi haki zingine bali matokeo ya kupotea kwa haki

Tuliwategemea kama ipo haja, wazungumzie tatizo na ukubwa wake kuanzia mapema

Inashangaza,leo wanazungumza kama wanasiasa na si watumishi wa mungu.

Mfano, gazeti moja la kiingereza la August 8 limemnukuu kiongozi mmoja akisema '' wapinzani wasitishe maandamano. Rais yupo madarakani kwa miezi michache na ingefaa akapewa miaka 4 kabla ya kuanza kuonyesha madhaifu yake''

Akaendelea kusema amewaita viongozi wa CDM, hakuna aliyemjibu kwasababu ya viburi.

Inaendelea.......
 
VUIONGOZI WA DINI

Sehemu ya II

Kiongozi huyo ameshindwa kutambua misingi ya uadilifu na utendaji wa haki.
Kitendo cha kuita viongozi wenzake 'viburi' kinaonyesha kukosa stara ya kichamungu

Ni halali amepuuzwa kwasababu nyingi. Moja, inajulikana alimkaribisha kiongozi mmoja katika eneo lake la ibada. Hilo linamsukuma kutetea bila msingi kama ifuatavyo

1. Serikali iliyopo ni ya tano. Katika zote hakuna mahali kiongozi huyo alitetea muda wa kiongozi wa kisiasa kutekeleza majukumu yake. Nini kinamsukuma leo hii kusema?

2. Kiongozi huyo atambue, hakuna mahali pameaanishwa katika katiba muda wa kuanza siasa baada ya uchaguzi mkuu. Kama mtumishi wa mungu wapi haki imekiukwa

3.Kazi ya vyama vya siasa si kuonyesha mapungufu ya Rais kama anavyodai.

Kazi za vyama ni kuendeleza siasa zao, kujipanua na kujipambanua , kutafuta wanachama na kuungwa mkono kila siku kama katiba na sharia za msajili wa vyama zinavyoonyesha

Kwa mtazamo huu,kiongozi wa kidini kudhani kuwa kazi ya vyama vya siasa ni kuongelea mapungufu ya Rais, ni ushahidi hakupaswa kuwa msuluhishi kwasababu

a)Hajui maana ya siasa ,wala kazi za siasa. Anaweza kusuluhisha nini?

b)Matamshi yake yanaonekana 'ameagizwa' kwasababu miaka 4 aliyosema ya kusubiri ameipata wapi? Na ni muda huo ambao serikali imeusema, hapa kuna nini?

4. Kwanini awapigie simu Chadema na si kutafuta pande zenye mzozo.

Yaani kiongozi huyu anataka kusuluhisha mgogoro kwa kuzungumza na pande moja

Huyu anatueleza huko anakofanya kazi za kiroho, anaweza kusuluhisha tatizo kwa kusikiliza upande mmoja. Mathalan, kusuluhisha ndoa kwa kusikiliza upande mmoja tu

Kwa mantiki hizo,kiongozi huyu ameonyesha ufinyu wa fikra, udhaifu kimaadili na kiroho.

Kwa CDM kudharau wito wake, hilo ni jambo sahihi kwani kumsikiliza ingalikuwa dhalili ya hali ya juu sana. Ni vema akaachwa na kuongoza kundi lake huko aliko

Huyo ni kada wa siasa aliyevaa joho akiaminisha uma anafanya kazi ya mungu.

Viongozi wa dini ni watu wenye heshima katika jamii yetu.
Ni watu wenye dhamana kiroho na kimaadili. Wanaotakiwa kuishi kwa mifano, wakisimamia mambo ya dunia kwa kutumia utashi wa kiroho.

Utashi wa roho unahimiza kufuata amri za mungu, ikiwa ni pamoja na kuwa mkweli, kuacha unafiki,uongoz uzushi na uzindaki na kusimamia haki na hata kutokubali kununulika kirahisi

Kwa hapa nchini, wimbi la viongozi wa kidini kupotoka katika matamshi na matendo yao linaongezeka kila uchao.

Ni vema wakajiangalia na kuziangalia nafasi zao kama zinaakisi maandiko matakatifu.

Kwa wananchi, wapo viongozi wa kusikiliza, wapo wa kupuuzwa tu na kuchwa walivyo.

Wananchi wasiste kuwaambia viongozi hao wasio na chembe za maadili ya kiroho kuzisafisha nafsi zao kwanza, kabla ya kusimama katika mimbari, vizinda, altare au madhabahuni kuhubiri usafi wa nafsi za wengine


Tusemezane
 
'TENSION' YA MIKUTANO

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

KATIBU MKUU CDM APWAYA!

Mbandiko mengi tumezungumzia hili jambo. Kama linavyochukua sehemu kubwa ya mijadala yetu ndivyo linavyochukua sehemu kubwa ya mijadala ya serikali

Tumesikia viongozi ngazi zote wakizungumzia marufuku ya mikutano na hili la wapinzani

Kwa namna na vipimo vyote, anayepoteza ni serikali
Badala ya kuzungumzia changamoto viongozi wapo na hadithi za kufikirika

Wamepoteza mwelekeo, hawazungumzii agenda walizoanza nazo.
Ni kama wameziacha. Tumeeleza, jambo hili lisilo na ulazima linaharibu focus

TUME YA HAKI NA UTAWALA BORA

Tume imeitisha kikao cha wadau kujadili mustakabali wa mikutano ya septemba

Huko nyuma, msajili wa vyama alitoka na msimamo bila kufafanua sharia za ofisi yake zinasemaje.

Kikao cha tume kimekwisha, kwa mujibu wa gazeti moja, mwenyekiti aliulizwa kwanini Polisi, Ofisi ya mwanasheria mkuu hawakuhudhuria, alisema wametoa sababu

Kwa upande wa CCM, mwenyekiti aliwataka waandishi waende kuwauliza wenyewe!!!
Yeye ndiye mwenye kikao,hajui kwanini CCM hawakufika!

Mwisho akatoa tamko la kuwataka CDM waahirishe mikutano.
Zaidi akasema yatakayotokea viongozi watawajibika.

Kwamba, anatupa mzigo kwa viongozi wa CDM bila kufafanua nini chanzo cha mgogoro

Anasema, ni vema Chadema wakatoa muda wa mashauri yaliyopo mahakamani.

Kama alijua hayo kwanini aliitisha kikao!!! Hili ni jambo la kufikirisha
kwamba kuna shauri, bado anataka kuongelea suala hilo!!!

KATIBU MKUU CHADEMA

Kiongozi huyu alizungumzia kuhudhuria kikao hicho kabla ya kufanyika

Katika mazingira ya kushangaza na kuonyesha kupwaya, pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu na Polisi kutohudhuria majadiliano, katibu mkuu wa Chadema aliendelea na kikao

Katibu mkuu wa CDM alipaswa kuelewa, mazungumzo si kati ya tume na Chadema bali tume na wadau.

Kwavile baadhi ya wadau hawakuhudhuria, kikao kimepoteza sehemu muhimu ya majadiliano.

Kwa maneno mengine kilikuwa kikao cha CDM na Tume
Katibu mkuu alipaswa kuelewa, kuendelea na kulikuwa na mashaka haikuwa sahihi
Mwenyekiti amaeonya chochote kile kitakachotokea viongozi watahusika.

Katibu mkuu alipaswa kutambua kikao hicho ambacho mwenyekiti wa tume amesema kuna mashauri mahakamani na baadhi ya wadau hawakuhudhuria hakikuwa katika muktadha stahiki

Tumesisitiza mara nyingi, nafasi ya katibu mkuu wa CDM imepwaya.

Hili linaonyesha wazi jinsi katibu mkuu anavyoweza kuwa 'framed' kirahisi sana

Upo umuhimu wa CDM kutathmini kama katibu mkuu anakidhi haja ya kazi za chama kikuu cha upinzani nchini.

Tusemezane
 
OMBWE LA WAZEE KATIKA JAMII

NIDHAMU NA HOFU NI VITU TOFAUTI

Jamii zetu zina utamaduni wa kuamini wazee ni watu wa kusikilizwa
Ni kutokana na uzoefu wao wa mambo mbali mbali waliyokutana nayo

Kauli za wazee hueleza busara hasa palipo na changamoto.
Si lazima busara zimpendeze awaye, ni muhimu zikielezwa

Mwl Nyerere baada ya kustaafu alichukua role ya uzee na ulezi wa Taifa
Alikemea chama chake kilipokwenda kombo. Alikemea serikali na Jamii

Tunakumbuka hotuba yake ya Jangwani wakati wa uchaguzi wa 1995
Mwalimu alisema' kama yupo anayetaka kubebwa'kavunja sheria gani ya nchi?

Wengi walidhani Mwl angetumia ushawishi kuwasema wapinzani
Tofauti kabisa, Mwl aliangalia tatizo lililopo katika jamii na kulitolea kauli

Mikutano ya kisiasa kitu cha kawaida.Mivutano ikaondoka, serikali ikitimiza wajibu na wananchi wakipewa haki za kujadili ya serikali kwa uwazi bila kificho

Kauli ya Spika wa Bunge hivi karibuni inatia shaka sana.
Spika anasema, '...Trump na Hillary wanaparurana' baada ya uchaguzi hutasikia mikutano tena ya kisiasa ni wakati wa kujenga nchi'

Kwanini Spika haeleweki!

1. Viongozi wanakaririwa wakisema 'Tuna demokrasia' yetu hatupaswi kuiga au kufundishwa kutoka Magharibi.

Inakuwaje Spika analinganisha demokrasia yetu na ya Wamarekani?

Inaendelea
 
Kwanini Spika haeleweki

2. Spika hakueleza sheria inayowazuia Wamarekani kufanya siasa baada ya uchaguzi. Ukweli,siasa za Marekani zimekomaa, hazina muda, kipingamiza wala ruhusa ya mtu.

3. Spika kama ilivyo viongozi wengine angeeleza lini utaratibu huo umeanza

Spika ametumikia mabunge matatu, anayo nafasi nzuri ya kueleza marufuku ya mikutano baada ya uchaguzi yalianza katika awamu gani na kwa sheria gani za nyuma au za sasa

4. Spika ange eleza, sheria za msajili wa vyama zinasemaje kuhusu shughuli za siasa

Ni kifungu gani kinakataza mikutano ya kisiasa baada ya uchaguzi.

Mh Spika kama walivyo viongozi wengine hawaendi huko! wala hawaelezi kingine !

HILI LINATUELEZA NINI

Kwamba, Taifa linaweza kuongozwa bila misingi. Tulikubaliana katiba na sheria ziwe mwongozo, inakuwaje viongozi wakiwemo wa dini hawaelezi kwa uyakinifu suala hili?

Kwa upande mwingine, Taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa wazee.

Hakuna anayesimama kati na kati kueleza busara hata kama haipendezi upande wowote.

Hakuna sauti za wazee, kilichopo ni hofu

Hofu imefikia mahali jamii imekuwa 'paralysed'. Hakuna anayezungumza si wataalamu, si wazee, si watunga sheria au wasimamizi.Watu wanadhani hofu na nidhamu ni vitu sawa

Hofu na nidhamu ni vitu viwili tofauti.

Hofu inajengwa katika misingi ya kujilinda (defense)
Nidhamu inajengwa katika misingi ya kujithamini na kuwajibika

Uhusiano wa hofu na nidhamu una mstari mwembamba sana(thin line)

Ndiyo maana ni rahisi kuvuka mipaka ya hofu na nidhamu bila kujijua

Ni rahisi kutoka katika nidhamu na kuparamia hofu
Ni ngumu sana kutoka katika hofu na kukumbatia nidhamu.

Tutapigia hatua tukiwa na nidhamu, si woga na hofu

Tusemezane
 
Kwanini Spika haeleweki

2. Spika hakueleza sheria inayowazuia Wamarekani kufanya siasa baada ya uchaguzi. Ukweli,siasa za Marekani zimekomaa, hazina muda, kipingamiza wala ruhusa ya mtu.

3. Spika kama ilivyo viongozi wengine angeeleza lini utaratibu huo umeanza

Spika ametumikia mabunge matatu, anayo nafasi nzuri ya kueleza marufuku ya mikutano baada ya uchaguzi yalianza katika awamu gani na kwa sheria gani za nyuma au za sasa

4. Spika ange eleza, sheria za msajili wa vyama zinasemaje kuhusu shughuli za siasa

Ni kifungu gani kinakataza mikutano ya kisiasa baada ya uchaguzi.

Mh Spika kama walivyo viongozi wengine hawaendi huko! wala hawaelezi kingine !

HILI LINATUELEZA NINI

Kwamba, Taifa linaweza kuongozwa bila misingi. Tulikubaliana katiba na sheria ziwe mwongozo, inakuwaje viongozi wakiwemo wa dini hawaelezi kwa uyakinifu suala hili?

Kwa upande mwingine, Taifa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa wazee.

Hakuna anayesimama kati na kati kueleza busara hata kama haipendezi upande wowote.

Hakuna sauti za wazee, kilichopo ni hofu

Hofu imefikia mahali jamii imekuwa 'paralysed'. Hakuna anayezungumza si wataalamu, si wazee, si watunga sheria au wasimamizi.Watu wanadhani hofu na nidhamu ni vitu sawa

Hofu na nidhamu ni vitu viwili tofauti.

Hofu inajengwa katika misingi ya kujilinda (defense)
Nidhamu inajengwa katika misingi ya kujithamini na kuwajibika

Uhusiano wa hofu na nidhamu una mstari mwembamba sana(thin line)

Ndiyo maana ni rahisi kuvuka mipaka ya hofu na nidhamu bila kujijua

Ni rahisi kutoka katika nidhamu na kuparamia hofu
Ni ngumu sana kutoka katika hofu na kukumbatia nidhamu.

Tutapigia hatua tukiwa na nidhamu, si woga na hofu

Tusemezane
Dr. Tulia Ackson Mwansasu, ingawa anaitwa daktari wa sheria, liko jambo moja tu la msingi kabisa ambalo hata bila kukanyaga milango ya shule alitakiwa alijue...

Shughuli zote za Mamlaka ya nchi zinatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo vitatu navyo ni;
  1. Serikali...yenye mamlaka ya utendaji ikiongozwa na Rais.
  2. Mahakama...yenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ikiongozwa na Jaji Mkuu.
  3. Bunge...lenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma likiongozwa na Spika.
Mamlaka yote hayo yaliyotajwa yanasimamiwa na Katiba ambayo kwenye utangulizi wake imeandikwa, "Kwa kuwa SISI, Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani..."
katiba-jpg.382896

Hakuna hata sehemu moja inasema, "kwa kuwa mimi Rais nimeamua...", hapana, badala yake Rais kabla ya kuchukua madaraka anatakiwa aape kwa jina la Muumba kuwa atailinda na kuitetea Katiba ya wananchi iliyomweka madarakani. Je Dr. Tulia Ackson iwapo Rais atashindwa kuilinda na kuitetea katiba, amejipangaje?

Swali hili linanisumbua sana si kwa Spika peke yake bali hata kwa wakuu wa mihimili mingine ya mamlaka ya nchi kama Mahakama. Ni wazi Rais Magufuli kashindwa kuheshimu Katiba na kila siku kwa vitendo na matamko anaonekana kama vile yuko juu ya Katiba lakini linalotia hofu zaidi ni swali kwamba imekuwaje wananchi tuko kimya?
 
Back
Top Bottom