Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,811
- 15,404
Jana usiku mwanangu Ngina kanistukiza na swali, akitaka kujua eti Senene wanaitwaje kwa kiingereza.
Nilijifaragua, kisha nikamwambia nitamjibu baadae, hata hivyo nikamtoroka nikaenda kulala, leo alfajiri nimewahi kuondoka bila hata kumuaga, maana nilijua atanikumbusha swali lake.
Najua nikirudi jioni nitapambana na hili swali, hebu wana JF niondoleeni hii fedheha!
Najuuta kusoma shule za Ngumbaru!