Duh! Kumbe Brazil imelipwa kuja kucheza Bongo!

Kila sehemu ni mzaha tu! hivi hatuna vipaumbele jamani? Mkuu wa kaya lazima akauze sura na kujichesha na kuiga picha na Dunga
 
Inasemekana Ni zaidi ya dolla million 2!!

Inasikitisha kuwa Watanzania hawana vipaumbale kwa maendeleo ya Watu wake.

Hizi fedha zinatosha kutengeneza madawati 60,000 na kuondoa tatizo la watoto kukaa chini.

Ukweli ni kuwa matatizo mengi walionayo wananchi yanatatulika lakini bahati mbaya hayako katika vipaumbele vya wanasiasa wetu
 
Hii nchi imejaa wapumbavu watupu. 3bn ingetosha hata kuinvest kwenye tz football kuinua vipaji vya new generation au kuchangia masuala ya elimu.
 
Ni bora hizo dollers wapewe brazil kuliko hizo hela ziende kwenye kampeni za CCM
 
unajua nini, hii inanikumbusha nikitembelea mashangazi zangu vijijini, huwa wananichinjia kuku kibao hadi nachoka kuzila....lakini wao pindi mimi sipo, hawali kuku wala nini, hivyo wananichinjia mimi niliyetoka town..hahaha, wakieta kwenye bakuli, huwa naokota kipapatio halafu zingine nasema wale wenyewe, kwasababu mimi nakula kuku karibia kila siku town huku, wao wanakula mboga za nyasi village....ndo kujifanya una pesaaaa, mtu wa hali ya juuu mgeni akija, unatoa hadi hazina ya chakula cha watoto, mgeni akiondoka mnaendelea kulala njaaa, kwanini tujifanye matajiri? nchi kama brazil kuexploit iyo hela kwa nchi masikini kama tz hawaoni huruma?.....uwanja watumie wetu bure, si ajabu na ndege tunawakodia, hotel, ulinzi kila kitu halafu na hela tuwalipe, jamani iyo nchi tunayoitangaza, hizo billion kadhaa zingejenga shule hata za msingi tu ngapi watoto wanasomea kwenye mibuyu? hospitali wamama wanashindwa hata pa kujifungulia only a million dollar ingefanya kitu kikubwa sana, lakini inakuja kupotezwa siku moja tu.unatangaza nini kwanza, kwani watu hawaijui tz.....mbona wanaijua sana kwamba ni nchi masikini ya kufa mtu, yenye vivutio vingi, mbuga za wanyama na mlima knjaro lakini barabara zetu mbovu wanaogopa kudongoka na magari, vibaka wengi, karaha tupu....au wanataka na sisi watz tutoke kwenye luninga...hahahaha.

matumizi mabaya ya pesa kwa waafrika ni tatizo kubwa sana, hasa pesa usoitolea jasho, ile ya msaada. Tff izo billions of dollars wamezitoa wapi uwanja wenyewe unaingiza pesa chache sana....
 
Duuh ndio maana wameenda kukopa STANBIC maana hii billioni tatu haikuwa kwenye budget- just think aloud
 
inaitwa investment,tusubiri tuone itakuwaje huenda tukapate faida maradufu ya hiyo,sema ni v2 vya kihistoria hivi,japo inaonekana indirect kuliko direct,tusilaumu sana tusubiri matokeo ya mapato wasilete ujanja ujanja huwezi jua kina lucio,kaka,gilberto silva wanaweza kuja kufungua investment zao eg makanisa na hao wengine labda mashule,kusaidia watoto yatima kuleta wadhamini kuwachukua wachezaji wetu kuenda kucheza sao paulo,rio nk.
 
"
the tanzanian football federation admits to paying several million dollars to persuade brazil to play the taifa stars"

safari bado ni ndefu kwa nchi hii kwa kweli! Ila tactic nzuri kwa uchaguzi!
sio uchaguzi tu na soka pia mzee yaani mimi hapo duuuu sina lakusema na sama hii nitakuwa bongo,...simba lazima itapata changamoto na kufanya kweli we suburi tu
 
lengo ni la kwenye mabo ya utalii sio siku hio ya mechi tu hapana wameangalia kwa mbeleni kwamba nchi itajitangaza kupitia mechi hii na kuweza kuwaleta watalii.

Non sense.,ni mambo magapi ambayo tumeshafanya lakini utalii hauendelei, tunashindwa hata kufanya cost-benefit analysis, wanadhani hizo billions wanazowapa Brazil zitarudi?.,watafute means nyingine ya kujitangaza na wala sio kutubebesha mzigo wa gharama zisizo na msingi.
 
Kila sehemu ni mzaha tu! hivi hatuna vipaumbele jamani? Mkuu wa kaya lazima akauze sura na kujichesha na kuiga picha na Dunga
soka ni ajira pia mzee kwenye ukweli lazima tukubali..MSANILO wewe ni great thinkerfikiria soka bongo likikua AJIRA zisizo na longongo za vijana wenye vipaji zitakuwaje,.si ni vema tu

KUMBUKA KINA JELA MTAGWA ,ALLY KATOLILA,ZAMOYONI MOGELA,MOHAMED BAKARI TALL,SEMBULI,KINA MASHA na wengineo wangeingia kwenye soka ya dunia tanzania ya leo ingekuwaje?aJIRA NGAPI ZINGETOKEA DIRECTLY AU INDIRECTLY,.Nenda Nijeria au GHANA uone aina hizo za ajira mzee.Maendeleo huja kwa kuiga mzee,.na tunatakiwa kumuiga aliye juu.,matatizo mengi tunayo na vipaumbele vingi vipo,.Lakini acha waje tu hawa MZEE...
Mimi ninaishi na jirani zangu ambao ni WANAIJERIA ,nikiwakumbushia jinsiSIMBA tulivyowatandika ENUGU huwa wanataka kunipiga.ACHA waje tu MASANILO
 
Ujio wa Brazil Tanzania: Hatimae siri ya Mtungini yafichuk

Brazil inakuja Tanzania na inatarajiwa kucheza na timu ya taifa Taifa Stars katika Uwanja wa Taifa hapo Juni 7 wakati wa usiku. Brazil inapanga kutua Dar es salaam usiku wa Juni 6.

Mipango ya kuja Brazil pengine ni ya muda mrefu, kwa vile Tanzania ilikuwa na kiu ya kujiweka katika jukwaa la kimataifa la soka kwa kutumia fainali za Kombe la Dunia za huko Afrika Kusini.

Inaeleweka Tanzania imeunda kikosi kikubwa cha watu maarufu na wenye fedha ili kutafuta fursa mbali mbali za kuitangaza Tanzania. Katika hilo Tanzania imetengeneza machapisho yenye taarifa za vivutio vya kitalii ambayo yatasambazwa Afrika Kusini kuanzia wakati huu.

Lakini ilikuwa ni kiu ya Tanzania kupata timu ya kuja kucheza Dar es salaam au kufanya mazoezi. Zilijaribiwa nyingi, nyengine zikiwa zimewahi kucheza Dar es salaam kama Cameroon na Ivory Coast kwa upande wa Afrika na nyengine za Ulaya.

Ila hakuna aliyeitupia jicho kwa mfano Korea Kaskazini, ambao hadi sasa wanashikilia kwa kasi msimamo wao wa Ujamaa, kwa sababu ingawa ingekuwa rahisi kuwapata, lakini wasingeleta sifa na ujiko ambao Tanzania inautafuta.

Brazil, Brazil, Brazil ndio ikawa lengo, ila ingepatikana vipi. Kocha wa Tanzania Marcio Maximo akaruka mpaka nchini kwao katika likizo yake na akajaribu kuifanya kazi hiyo. Mguu hapa na mguu kule.

Akasema ingekuwa vigumu na haiwezekani hasa. Alitoa sababu za kiufundi ambazo sote tulikubali. Maana timu kama Brazil kwenda pahala hata urefu wa majani ya kiwanja cha mazoezi hupimwa seuze mahitaji mengine mengi.

Alichosema Maximo ni kuwa Brazil wasingeweza kuja maana hali ya hewa ya Dar es salaam haitafanana na ile ya kituo chao katika kundi lao huko Afrika Kusini.

Nikakutana na Maximo uso kwa uso, na akaniambia hay ohayo, na kunihakikishia kabisa haitawezekana.

Ila aliniambia jengine pia. Kuwaleta Brazil ni gharama kubwa sana na hakuwa na hakika kama Tanzania ingeweza kuthubutu kufanya hivyo.

Na mimi nilikubali hilo kwa sababu huko nyuma nilijaribu kuileta Brazil. Nina maajenti walioko Austria ambao wana viungo muhimu katika ulimwengu wa soka na walinipa ofa hiyo na mie nikaitupa kwa Shirikisho la Soka la Tanzania TFF.

Brazil walidai kulipwa dola milioni moja kwa kucheza mechi moja. Hiyo ni mbali ya tiketi za wachezaji na maafisa lakini pia watu wengine kadhaa. Kwa ujumla kawaida msafara wa Brazil huwa watu 60 hivi.

Leodgar Tenga Rais wa TFF akaanza kuhesabu vidole. La haitawezekana aliniambia. Kabisa haiwezekani. Maana kwa maana hiyo ya gharama zitazohusika basi ni wazi kuwa kiingilia cha chini kitabidi kiwe kikubwa kiasi ambacho cha kutisha na kiingilio cha juu kitakuwa kikubwa kiasi cha kuwa kufuru.

Na Tenga ameshaanza kusema hivyo hivi sasa. Kuwa wadau wa soka wajue kuileta Brazil ni gharama ambayo mzigo wake watabidi waubebe wao.

Huko nyuma Tenga na TFF pia walikataa ofa zangu kadhaa kuleta timu za Amerika Kusini hasa na sababu siku zote ikiwa ni gharama- yaani vipi mchezo utalipa. Nitakupeni mifano ya timu kama hizo.

Kulikuwa na jaribio nilofanya ya kuileta timu ya Paraguay ikashindikana. Nikajaribu Bolivia ikawa hivyo hivyo. Pia nimejaribu timu za Ulaya Mashariki.

Niliwahi kuwaambia TFF kuwa hata siku moja hatutaweza kuipata timu ya Ulaya kuja kucheza bila ya mchango wa makampuni. Kwa kutarajia viingilio tu hatutaweza kupata fedha za kutosha kulileta kundi la nyota ambao huunda timu za taifa za Ulaya.

Wakati huo pengine walikuwa na sababu kwa pembeni kukataa ofa hizo kwa kuwa sikuwa wakala rasmi wa mambo ya soka. lakini sasa nina kibali rasmi cha fifa kufanya kazi kama hizo.

Sasa tunaambiwa Brazil inakuja. Inakuja kwa kupitia Afrika Kusini.Hapa inabidi tujiulize suala moja kubwa sana. Inakuaje timu ishafika Afrika Kusini ambako ndio lengo lake kisha tuitoe huko na kuileta huku.

Tunaambiwa Brazil inakusudia kucheza Tanzania na baadae Zimbabwe katika programu ambayo hatukuwa tumeisikia mapema. Timu zote takriban tumejua mapema zinacheza mechi gani, na hakuna hata timu moja iliyopanga kwenda Afrika Kusini kisha ndio itoke kwenda kucheza mechi za kirafiki.

Lakini hayo ni maaleshâŚtuseme naiwe hivyo. Hebu tutizame basi imekwendaje mpaka Brazil ikaja Tanzania? Hilo limetokezea baada ya Tanzania kwa njia moja au nyengine kukutana au kuijua kampuni inayoitwa kentaro na tembelea Kentaro - Home utapata mengi.

Kwa ufupi tu Kentaro ni kampuni ya mawasiliano au public relations na ni moja ya zile kubwa duniani na wateja wake ni wale wenye fedha za kupukutika.

Na mimi sikujajua hayo mpaka nilipoona Philippe Huber ndipo akili ilionigonga kwa sababu huyu bwana niliwahi kusoma habari zake kadhaa wa kadhaa katika medani ya soka na ni mmoja ya watu maarufu kama vile wakala wa Kiisrael Pini Zahavi.

Sifa za watu hawa katika mipango ni kubwa sana. Marafiki zao ni marais, mawaziri wakuu na wanasiasa wakubwa wakubwa. Hunywa chai Ikulu na kwenye majumba ya watu wenye ulwa na vyao.

Mwili wangu unatetemeka kama tumba la uvi nikifikiri kiasi gani Phillipe Huber na kampuni yake wamelipwa ili kuwezesha kuipata Brazil kuja kucheza Dar es salaam? Kiasi gani nasubiri watu wengine waniambie kama angalau wanaweza kukisia?

Inaaminika katika dunia ya soka haiwezekani kitu akitake Phillepe Huber Mswisi anayemiliki makampuni kadhaa au huyu Zahavi na kitu hicho kishindikane. Na Huber alipewa kazi na Tanzania na haingewezekana kabisa kushinda kuileta Brazil ukitizama kazi ambazo kampuni yake imezifanya.

Sawa Brazil itakuja itacheza. Mpira wa Tanzania hautapanda kwa kuwa imecheza na Brazil. Wala wachezaji wa Bongo hawatachukuliwa kwenye timu za Ulaya kwa kuwa usiku mmoja wamecheza na Brazil. Wala mimi siamini kuwa Tanzania itakuwa imejitangaza hivyo kwa mechi ya siku moja ambayo nayo imekuja mwishoni mwishoni.

Pengine mtu angejiuliza lipi lingekuwa bora. Kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye soka yetu au kuwaalika watu kuja kucheza usiku mmoja. Hapa ndipo ninapopiga jicho katika sababu halisi ya kuileta Brazil.

Jee si kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi?

makala na Ally Saleh "Alberto" wa BBC.



 
Upuuzi mtupu. Modes naomba miniruhusu nitukane hapa jamvini kwa mara ya kwanza nimekwazika.
 
Nafikiri serikali imekosa priorities, dada zetuwanakufa sehemu za kujifingulia, watoto wetu wanakufa kwa ukosefu wa chloroquine, watoto wanakaa chini kabisa sakafuni, and so on , mwenyezi mungu atuzindue tujue priorities zetu AMEN
 
Brazil are to play Tanzania on 7 June in a World Cup warm-up match ahead of this summer's finals in South Africa. The Brazilians have become the first non-African team to schedule a friendly in Africa in the build-up to the tournament, which kicks off on 11 June.
Tanzanian Football Federation (TFF) spokesman Florian Kaijage told BBC Sport that a contract would be signed within the next two to three days.
Brazil also plan to play Zimbabwe but no date as yet has been set.
Regarding Brazil's friendly against Tanzania in Dar es Salaam, Kaijage said: "Brazil have already put this game in their plan, so obviously they are sure of coming, unless something unusual happens.
o.gif
It's very exciting. Finally we've succeeded in attracting Brazil


TFF president Leodegar Tenga


"On our side, we were given some conditions to meet. The federation and the government have been meeting but chances are higher that the conditions will be met for the game to go ahead," he added.
The terms include an appearance fee requested by Brazil, which Kaijage described as being "several million dollars".
Tanzania have been eager to play a part in the World Cup build-up by hosting one of the finalists, and the TFF president Leodegar Tenga stated it would be an exciting prospect for the east African country.
"It's very exciting. Finally we've succeeded in attracting Brazil, who are obviously the biggest team in the world, to play our national team," Tenga commented.
The government earlier this year appointed a committee led by a minister and with a budget of about $6m (Ł4.17m) for the purpose, but most teams contacted by the TFF turned them down.
North Korea had planned to play two friendlies in Zimbabwe, but that was shelved after protests over Matabeleland, where rights groups say a North Korean-trained army unit killed thousands of people during the 1980s.
Brazil are currently training in the southern Brazilian city of Curitiba and are due to depart on 2 June.
Taifa Stars are currently in a training camp ready for an African Nations Championship (CHAN) final round, second leg qualifier against Rwanda, which will take place on 5 June in Kigali.

BBC Sport - Football - Brazil to play Tanzania in pre-World Cup friendly
 
sasa mkuu si tunataka kuwatumia brazil kutangaza nchi kwenye utalii? ndio tunawapa fungu lao kwa kutupa nafasi ya kurusha tangazo letu duniani? inamana ulitegemea wao wapoteze hela zao kuja kucheza na sisi kwa kiwango kipi mkuu?

Si mdo hapo mkuu! Tumetaka wenyewe kujitangaza kwa kupitia wao.....SASA tunalalamika nn?
Kwani tulikuwa tynataka tucheze na world soccer super stars bure?
 
Tanzania ina nchi mbili ndani yake.

Kuna the haves wanaoweza kukaa chini na kufikiri kulipa "several million dollars" kwa mechi moja na Brazil.

Halafu kuna the have not wanaoshindia less than a dollar a day na kukaa chini mashuleni.

Kuna watu wengine hawana aibu dunia hii jamani.Halafu walimu wakiomba nyongeza za mishahara hatuna. Huku kuna mamia ya matumizi mabaya ya fedha kama haya yanaendelea kila siku, na tunajua machache sana yanayofika magazetini, mengine tisa kati ya kumi hata hatuyajui.

And then tunashangaa kwa nini bado tu masikini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom