Duh! Kumbe Brazil imelipwa kuja kucheza Bongo!

Heeee, kumbe kuna watu humu walidhani kuwa Brazil ingekuja tu bila gharama zozote zile kutoka Tz, mbona hayo mawazo ni finyu sana. Unategemea ile timu iliyoundwa na mastaa namna ile ingekuja tu kuuza sura hapo bongo bila malipo, wenzetu kila wachezaji wao wanapogusa mpira wanalipwa na sio kujifurahisha tu, level waliofikia ni kubwa kiasi kwamba gharama za kuwalipa kila wanapocheza ni kubwa. Suala la hilo game kuwa expensive na zimeweza kupatikana hizo "several dollars" inaonyesha kuwa tunao pia uwezo wa kushughulikia matatizo mbalimbali coz pesa zipo ila zinatumika kiholela tu na wanacnhi hawajui. Nchi ina hali mbaya mfano hizi hospitali nyingi wakina mama wajawazito wanalala chini, hakuna mchakato wowote wa makusudi kama huu uliofanyika ili kutatua tatizo hilo.... kwa ujumla ni kwamba maisha magumu ni kwako wewe mlala hoi ila kwa fisadi maisha ni mstarehe tu, hawaumizwi kichwa na matatizo ya wananchi coz wao wanakula na kushiba.

You are totally missing the point. Kuileta Brazil kama ni lazima kuwe na gharama ya $ 6 m, tunaelewa hili.

Tusiloelewa ni hiki kimbelembele cha nchi masikini ambayo mtu wake kwa wastani anafanya uzalishaji wa chini ya $ 1000 kwa mwaka (some figures put this as low as $ 500) kutaka kujitutumua kwa anasa tusizozimudu.Hii mechi itagharimu gharama sawa na uzalishaji wa Watanzania 12,000 wanaozalisha katika level ya $ 500 kwa mwaka. Watu 12,000 wata-toil kwa mwaka mzima ili kuweza kuzalisha (sio kupata faida, kuzalisha) mazao yaliyo sawa na gharama za upuuzi huu.

Kwa hiyo usije hapa na kututaka tuamini kwamba mechi na Brazil ni maji ya kunywa, na kama tungekosa mechi tungekufa.Hasha.

Kuna nchi kibao hazijawahi kucheza na Brazil, na kiutalii zinafanya vizuri zaidi yetu na hata kwenye soka hatuzifikii.

Tatizo letu tuna mentality isiyojua "fiscal responsibility", hatujui nini tunahitaji kimsingi kabisa na nini ni anasa tunayoweza kuachana nayo.

Hapo hapo tunasema hatuwezi kuwaongezea walimu mishahara, huku mimilioni ya dola kila siku inatumiwa vibaya kama hivi, kila siku.
 
Wajinga ndo waliwao haya na mtajuana na fahari zenu...kesho mtaambiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM...ha ha ha ha ha!!
 
kati ya vitu vinavyoniuma hiki ni kimoja wapo..izo hela ni nyingi sana. Brazil nao hawana roho nzuri kabisa, hawawezi kumkamua mtu maskini kiasi hicho...hivi hawawezi kufanya hata contribution tu jamani kwa kuja kucheza bila mabilion hayo? kwakweli tumeliwa...
 
Anyway thank you kama Umeona DNA yangu kansa but i think tanzania inahitaji watu wenye kansa yenye akili kama mimi maana wenye DNA sahihi i wote ndo hivyo . hahahaha

Sasa kwa kuwa mtoto anakosa tiba utasema tusiwe na Wizara ya utamadanuni na michezo? Tusiwe na wizara ya habari??

Kuwa na Wizara ya utamaduni na michezo na kuileta Brazil ni mambo mawili tofauti.Si lazima kuileta Brazil ili uwe na Wizara ya utamaduni na michezo.Nchi kibao zina wizara hizi na hazijawahi kucheza na Brazil.Mimi sipingi kuwa na Wizara, ingawa kuna case inaweza kujengwa kwamba kwa nchi masikini michezo ni luxury, lakini hili la kuileta Brazil at the cost of $ 6 m kwa nchi kama yetu ni upuuzi.

In short badala ya kuhaingaka kuwapeleka watoto wa mbulu shule za kusoma physics na chemistry tulitakiwa tuwe na shule za kukimbia kule meru na mbulu. Wakati wenzake wa dar wanasoma Archmedes priciple yeye wa mbulu angekuwa anakula tizi la kukimbiz upepo.

Sawa, let's say unafanya michezo kuwa investment which is quite feasible.Huoni kwamba hiyo idea yako ya kuanzisha shule ya michezo Mbulu ingeweza kuzitumia hizo $ 6 m vizuri zaidi? Tungejenga kitu cha kudumu, tungeandaa wanamichezo wengi kila mwaka, na baada ya miaka michache tungeweza kuwa na wanamichezo wengi ambao wangeweza kuitangaza Tanzania kwa bure na kwa muda mrefu zaidi.Hiyo hiyo $ 6 m ingetumika vizuri ingefanya makubwa sana.

nimetoa mfano huu

Anyway mimi sioni Tatizo Kwa brazil kulipwa hela hizo kucheza sababu najua kuna hela nyingi zaidi ya hizo zimetumika vibaaya kuitanganza tanzania.

Hapa unachekesha sana.I bet ukichomwa mkuki ubavu mmoja halafu mtu aliyekuchoma akikuambia anataka kukuchoma upande wa pili utamwambia nichome tu maana ushanichoma upande wa kwanza?

Mtu akikuibia $ 1000 na akiwa anataka kukuibia $ 1000 nyingine utamwambia iba tu kwa sababu umeshaiba?

Two wrongs do not make a right, the fact that there is gross misuse of public funds in Tanzania does not justify further misuse of public funds.Kama mnapenda sana mpira changeni $ 6 m muipe FA kuileta Brazil Tanzania, tutawaona wajinga msiojua priorities but you know what? Hela zenu, hata mkitaka kuzifungia tumbaku na kuzichoma kama sigara (no this would be illegal) hata kama mnataka kuzigawa poa tu. Lakini hizi ni fedha za umma, za watu wote, tena wengi wao ni masikini. Mambo ya aibu haya.

Suala la wototo ,wazazi ,wazee na watu wote kupata tiba bora ni la muhimu but that is anter subject.Kwangu Binafsi naona it is FEASIBLE.

Hapa ni sawa na baba anayepata mshahara halafu anaenda straight bar kulewa a good portion of his earning huku akisema watoto kupata tiba ni muhimu, but that is another matter.Wewe utamuonaje huyu baba.Ana akili kweli?

Usichoelewa hapa, au unachotaka kujifanya huelewi, ni ukweli kwamba pesa ni kama maji.Huwezi kuwa na maji katika ndoo, halafu ukasema nimechukua maji ya juu kwa hiyo sijachukua ya chini.Ukichukua lita moja kutoka katika ndoo, ndoo imepungua maji kwa lita moja na huwezi kubadilisha hili.

tatizo sio Kuwaleta Brazil tatizo ni kutumia resources ndogo tulizonazo vizuri. Nina hakika Gharama ya brazil na faida ya kuja kwa brazil ni feasible zaidi kuliko njia nyingi zilizotumika kuitangaza tanzania au kuendeleza michezo.

Kama kuwaleta Brazil kumekuwa directly linked na gharama kubwa sana kwa nchi kama Tanzania huwezi kusema "Ttaizo si kuwaleta Brazil, tatizo ni kutumia resources ndogo tulizo nazo". Huwezi kutenganisha kuwaleta Brazil na gharama, hawafanyi kazi ya kanisa wale.Kuwaleta Brazil ni tatizo kwa sababu kuwaleta Brazil ni gharama tusiyoweza kui justify.

Wakulu wamebreak down mambo ya ma ad, prime time, nationwide,USA, kwa hela hiyo hiyo wangeweza kununua ads 60 za 30 seconds ambazo airtime yake ingekuja ku total 30 minutes.Mnaonyesha Tanzania over and over, hamna mpira wala nini, prime market, prime time, prime TV, Nationwide na tungeweza kuspan muda wa wiki mbili hizi watu wanakuja South Africa kwenye World Cup wangeweza kusema ngoja tukaone na hapo Tanzania.

Instead tunanunua mechi kwa gharama ya ajabu.
 
Wajinga ndo waliwao haya na mtajuana na fahari zenu...kesho mtaambiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM...ha ha ha ha ha!!

Mazee umeniwahi, nilitaka kusema Kikwete kaona uchaguzi unakaribia, hana la maana alilofanya, sasa ngoja awalete Brazil halafu akiulizwa umefanya nini atasema nimewaleta Brazil.

Yule mshairi wa kale wa Roma aliyeitwa Juvenal alisema ukitaka kuwatawala walalahoi wape sarakasi na mikate.Utawapata.

Naona sisi hata mikate hatupati.Sarakasi tupu!
 
Kwanza kabisa hiyo figure ni karibu zaidi na shilingi bilioni 9 kuliko 3, kwa sababu ni US $ 6 million.

kati ya vitu vinavyoniuma hiki ni kimoja wapo..izo hela ni nyingi sana. Brazil nao hawana roho nzuri kabisa, hawawezi kumkamua mtu maskini kiasi hicho...hivi hawawezi kufanya hata contribution tu jamani kwa kuja kucheza bila mabilion hayo? kwakweli tumeliwa...

Halafu biashara ya kimataifa haiendeshwi kwa "roho nzuri".Brazil hawajatulazimisha tutoe hizo hela, tumetaka wenyewe.Kisha na wao wanazihitaji vile vile.Kwa hiyo usitake kuwawekea lawama kwa kitu ambacho tumejitakia wenyewe.

Hawafanyi kazi ya kanisa hawa. Na kuna nchi kibao zinataka kucheza nao sasa kama wakitaka kucheza bure wacheze na nani wamuache nani?
 
Kwanza kabisa hiyo figure ni karibu zaidi na shilingi bilioni 9 kuliko 3, kwa sababu ni US $ 6 million.

Halafu biashara ya kimataifa haiendeshwi kwa "roho nzuri".Brazil hawajatulazimisha tutoe hizo hela, tumetaka wenyewe.Kisha na wao wanazihitaji vile vile.Kwa hiyo usitake kuwawekea lawama kwa kitu ambacho tumejitakia wenyewe.

Hawafanyi kazi ya kanisa hawa. Na kuna nchi kibao zinataka kucheza nao sasa kama wakitaka kucheza bure wacheze na nani wamuache nani?

kuna biashara gani ya kimataifa unayoifanya hapa mkuu, mbona unatoka nje ya mada, au sijakuelewa?
 
kuna biashara gani ya kimataifa unayoifanya hapa mkuu, mbona unatoka nje ya mada, au sijakuelewa?

Biashara ya kimataifa ni biashara inayofanywa kwa kuhusisha transactions zinazovuka mipaka ya mataifa.

Hapa Watanzania wanafanya biashara na Wabrazil. Watanzania wanawalipa WaBrazil ili WaBrazil waje kucheza mpira Tanzania.

Hela za Tanzania zinatoka Tanzania zinaenda Brazil.

Huoni biashara ya kimataifa hapo?
 
nyie watz mmeuza nini na wabrazil wamenunua nini? unafikiri kila transaction ya kimataifa huwa inakuwa biashara, zingine ni zawadi, si lazima uwe unauza kitu. nikiwa na mtu brazil nataka kumpa hela naweza kufanya international transaction kupeleka kwenye account yake brazil, ni biashara gani nimefanya hapo? unataka kulazimisha mambo wewe hueleweki. hapa hawajafanya biashara yoyote, wamewapa wabrazil zawadi tu kwa kuja kucheza nasisi..unatoa zawadi ya chakula wakati watoto wako wanalala njaaa....nipe defition ya biashara tafadhali....
 
WaTZ si wauzaji hapa, ni wanunuzi.Wametoa hela ili Brazil ije kucheza.Ukiangalia kwa undani wamenunua mvinyo wa mamilionea wakati wao ni hohehahe, halafu wanataka kutugelesha kwamba wanatangaza nchi.

Si kila transaction ya kimataifa ni biashara, na mimi wala sikusema hivyo. Ila kwa hii ni biashara kwa sababu imehusisha kubadilishana pesa na huduma.

Si lazima Brazil wauze huduma zao, wanaweza kutoa zawadi.Lakini wenye uamuzi wa ama watoe zawadi au wauze ni wenyewe Brazil, huwezi kuwalazimisha wakupe zawadi eti kwa sababu wewe ni masikini.Kama vile ambavyo huwezi kumlazimisha mtu mwingine yeyote akupe zawadi eti kwa sababu wewe ni masikini. Utaitiwa polisi kwa usumbufu.

Typical bongo mentality, gimme gimme and entitlement mentality.Hao Brazil wenyewe kwao kuna rhumba kaa nini, watu wanakaa kwenye mi favella hapo Rio utadhani viota vya ndege.Kwa hiyo usitake kuwafanya Brazil kama watu fulani ambao hawana shida ya pesa.Utakuwa huwatendei haki.

Ukitaka kumpa mtu wa Brazil fedha ya zawadi una weza, lakini hilo utakalofanya litakuwa tofauti kabisa na hili lililotokea kati ya Tanzania na Brazil, kwani hapa hamna zawadi iliyotolewa, watu wamefanya BIASHARA, kwa hiyo usilete kimfano chako ambacho hakipo applicable hapa.

Inaonekana kama unataka kuwa force waBrazil waje kucheza na sisi bure, eti kwa sababu sisi ni masikini.Guess what? Hawafanyi kazi ya kanisa (hata kanisa nalo linakusanya sadaka, watu weeeeeeeeeh)

Kama Brazil wangekuwa wametusainisha mkataba wa mechi kwa kutushikia mtutu wa bunduki tungewasema kwamba ni wabaya, hawana roho nzuri, ni majambazi wanaowaibia watu masikini.

Lakini hatukushikiwa bunduki, tumekubali wenyewe fair and square.Utawalaumu vipi Brazil?

Kama sisi tunasema masikini mbona hata wao wana masikini wao ambao watafurahi kupata nafasi ya kulamba makombo ya hizi dola milioni sita?

Typical wabongo rationale, tunaharibu wenyewe halafu tunatafuta mtu wa kumlaumu.
 
WaTZ si wauzaji hapa, ni wanunuzi.Wametoa hela ili Brazil ije kucheza.Ukiangalia kwa undani wamenunua mvinyo wa mamilionea wakati wao ni hohehahe, halafu wanataka kutugelesha kwamba wanatangaza nchi.

Si kila transaction ya kimataifa ni biashara, na mimi wala sikusema hivyo. Ila kwa hii ni biashara kwa sababu imehusisha kubadilishana pesa na huduma.

Si lazima Brazil wauze huduma zao, wanaweza kutoa zawadi.Lakini wenye uamuzi wa ama watoe zawadi au wauze ni wenyewe Brazil, huwezi kuwalazimisha wakupe zawadi eti kwa sababu wewe ni masikini.Kama vile ambavyo huwezi kumlazimisha mtu mwingine yeyote akupe zawadi eti kwa sababu wewe ni masikini. Utaitiwa polisi kwa usumbufu.

Ukitaka kumpa mtu wa Brazil fedha ya zawadi una weza, lakini hilo utakalofanya litakuwa tofauti kabisa na hili lililotokea kati ya Tanzania na Brazil, kwani hapa hamna zawadi iliyotolewa, watu wamefanya BIASHARA, kwa hiyo usilete kimfano chako ambacho hakipo applicable hapa.

Inaonekana kama unataka kuwa force waBrazil waje kucheza na sisi bure, eti kwa sababu sisi ni masikini.Guess what? Hawafanyi kazi ya kanisa (hata kanisa nalo linakusanya sadaka, watu weeeeeeeeeh)

Kama Brazil wangekuwa wametusainisha mkataba wa mechi kwa kutushikia mtutu wa bunduki tungewasema kwamba ni wabaya, hawana roho nzuri, ni majambazi wanaowaibia watu masikini.

Lakini hatukushikiwa bunduki, tumekubali wenyewe fair and square.Utawalaumu vipi Brazil?

Kama sisi tunasema masikini mbona hata wao wana masikini wao ambao watafurahi kupata nafasi ya kulamba makombo ya hizi dola milioni sita?

Typical wabongo rationale, tunaharibu wenyewe halafu tunatafuta mtu wa kumlaumu.

umekoti message ambayo sikukuuliza swali,na unasababisha kutoka kwenye mada halisi...nilipoangalia thread ulizochangia mara nyingi naona una matatizo ya kutoka nje ya mada na kwenda porini kabisa...wewe si mtu wa kubishana, naomba nikuache hivyohivyo...hakuna mtu anataka msaada hapa....wala hakuna mtu amesema wanafanya kazi ya kanisa...siku njema mkuu, tuachane na hili. bye.
 
Kati yangu mimi na wewe unayebisha kwamba hii si biashara ya kimataifa nani yuko nje ya mada?

Kati yangu mimi ninaye discuss maada iliyo katika thread hii, na wewe unayetaja thread zilizo nje ya maada hii kimkupuo kupuo tu, nani anatoka nje ya maada?

Usirushie watu mawe wakati wewe mwenyewe unaishi kwenye nyumba ya kioo.Usilete sheria ambayo wewe mwenyewe huwezi kuitunza.

Yaani pesa mtoe wenyewe kununua huduma za Brazil, kwa hiyari yenu wenyewe, bila kushurutishwa, halafu mnataka kuwalaumu Brazil?

Wewe unachekesha sana.
 
mkuuu, tujadili kama kuna justification yoyote to spend the billions, ndio mada halisi...tuachane na ubishi wa watu wawili binafsi, hata kama una bifu na mimi, elekea moja kwa moja kwenye mada usinijadili mimi. ...au niseme umeshinda uridhike ndo urudi kwenye mstari? haya basi, UMESHINDA, tuendelee na mada sasa. OK!
 
Of course najadili kama kuna justification.

Lakini akija nincompoop akisema hii siyo international trade nina wajibu wa ku set the record straight.

And this is not about mashindano ya ligi, this is about the examination of facts.

And the fact remains, mwisho wa financial year, Brazil watarekodi kwamba waliuza huduma kwa Tanzania katika mechi hii, na walichukua kitita cha dola milioni sita.

Na Tanzania (kama wanakeep records) watarekodi kwamba walinunua huduma za mechi ya mpira na timu ya Brazil kwa gharama ya dola za kimarekani milioni sita.

Sasa unataka nini zaidi ili ukubali kwamba hii ni international trade.Au lazima uone contena linaingia bandarini ili ujue kwamba ni trade?
 
Of course najadili kama kuna justification.

Lakini akija nincompoop akisema hii siyo international trade nina wajibu wa ku set the record straight.

And this is not about mashindano ya ligi, this is about the examination of facts.

punguza hasira bwana mdogo, kunani?
 
punguza hasira bwana mdogo, kunani?

Hasira umeiona wewe mimi siioni. Tatizo letu mojawapo ni hii complacency na uvuguvugu wa bora liende, akija mtu ana passion na anachokisema mshaona hasira.

Kuna tofauti kati ya passion na hasira, na mara nyingi wanaojitia kusema "punguza hasira" sehemu ambapo hamna hasira ndio wenye hasira.

Otherwise wangeionaje hasira sehemu ambapo haipo?
 
hahaha.
 
Tatizo la nchi yetu ndo hili, there is no way you can justify anything. No priorities, no planning what do you expect. ni kukurupuka tu kwa kwenda mbele, hawakufanya study yoyote kama safari hiyo ni viable, mara viingilio vimepangwa leo na leo unaambiwa tiketi zote zimekwisha. TFF Totally False and Faulty
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom