kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 236
Umakini unaonekana kwa vitendo, na kazi ya mtu au kikundi chochote inaonekana kwa mafanikio na matukio. Chama cha Demokrasia na maendeleo kimekuwa mstari wa Mbele kutetea wanyonge, kufichua maovu na kukemea uovu.
Wakati huo halamashauri zilizoongozwa na CDM zikiwa ni mfano wa kuigwa kwa mafanikio moja wapo ni ya karatu.
Uadilifu, kazi kwa bidii na kutimiza wajibu kwa waajiri ndio imekuwa nguzo pekee ya mafanikio ya CDM . Chama hiki kina haki na kinastahili kupewa nchi ili iweze kuifikisha kwenye ahadi ya kweli ya maisha bora kwa kila mtanzania.
Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe na katibu mkuu Dr. Slaa wamekuwa wakiwaambia Watanzania sababu kubwa ya matatizo yetu kuwa ni uongozi mbovu wa serikali ya CCM, wizi wa mali ya umma chini ya baraka za viongozi wa CCM na ufisadi usio na mifano unao asisiwa na Mwenyekiti na viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya taifa mpaka kijiji.
CCM walitoa lugha zote za kejeli, matusi, maudhi, na kupandikiza chuki za aina zote dhidi ya viongozi na chama cha demokrasia na maendeleo kwa ujumla. Nakumbuka kauli ya Dr. Slaa kwamba ukweli husimama imara hata kwenye mateso na matukano, tutashinda.
CCM chini ya kauli za mwenyekiti wao, huku akinadi kila anayeitwa fisadi kuwa ni msafi na hawawezi kutishwa na kelele za mlango, watanzania wameshuhudia idadi kubwa ya list of shame wakiwa mahakamani kwa wizi, ufisadi, madaraka mabovu.
List yenyewe ambayo CCM imekiri ni kweli wote waliotajwa na DR. Slaa ni mafisadi, wakiwa kina Yona, Mramba, Chenge, Lowasa, Rostam, Mgonja, Mkono, Kikwete nk na wao sasa wanaimba wimbo wa CDM kwamba mafisadi watoke ndani ya CCM.
Kwanza inabidi CCM wakiongozwa na mtuhumiwa mwenyekiti wao wamuombe radhi Dr. Slaa na CDM kwa ujumla kwa kitendo cha kukataa kuwa wao sio mafisadi kumbe kweli. Wawaombe watanzania msamaha na kukiri kuwa hawata rudia tena kukataa ukweli.
Wakati umefika wa wananchi kujua kuwa CCM ndio wanaomaliza uchumi wa Tanzania, na kuwashukuru Viongozi wa CDM kuwa mstari wa mbele kufanya kazi ya CAG na PCCB kubaini wizi, ufisadi, uonevu na siasa chafu za CCM na viongozi wake wezi.
Tuwape nguvu na matumaini wote wanaotutetea katika mazingira haya ya vitisho, na kukatishwa tamaa. Tanzania yenye neema ni pamoja na mimi na wewe kutimiza wajibu wetu kwa vitendo.
haya shime saidia harakati hizi kwa nguvu zako zote.