Dr. W. Slaa kwenye Channel 10; Pongezi zake!

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
235
Umakini unaonekana kwa vitendo, na kazi ya mtu au kikundi chochote inaonekana kwa mafanikio na matukio. Chama cha Demokrasia na maendeleo kimekuwa mstari wa Mbele kutetea wanyonge, kufichua maovu na kukemea uovu.

Wakati huo halamashauri zilizoongozwa na CDM zikiwa ni mfano wa kuigwa kwa mafanikio moja wapo ni ya karatu.

Uadilifu, kazi kwa bidii na kutimiza wajibu kwa waajiri ndio imekuwa nguzo pekee ya mafanikio ya CDM . Chama hiki kina haki na kinastahili kupewa nchi ili iweze kuifikisha kwenye ahadi ya kweli ya maisha bora kwa kila mtanzania.

Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe na katibu mkuu Dr. Slaa wamekuwa wakiwaambia Watanzania sababu kubwa ya matatizo yetu kuwa ni uongozi mbovu wa serikali ya CCM, wizi wa mali ya umma chini ya baraka za viongozi wa CCM na ufisadi usio na mifano unao asisiwa na Mwenyekiti na viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya taifa mpaka kijiji.

CCM walitoa lugha zote za kejeli, matusi, maudhi, na kupandikiza chuki za aina zote dhidi ya viongozi na chama cha demokrasia na maendeleo kwa ujumla. Nakumbuka kauli ya Dr. Slaa kwamba ukweli husimama imara hata kwenye mateso na matukano, tutashinda.

CCM chini ya kauli za mwenyekiti wao, huku akinadi kila anayeitwa fisadi kuwa ni msafi na hawawezi kutishwa na kelele za mlango, watanzania wameshuhudia idadi kubwa ya list of shame wakiwa mahakamani kwa wizi, ufisadi, madaraka mabovu.

List yenyewe ambayo CCM imekiri ni kweli wote waliotajwa na DR. Slaa ni mafisadi, wakiwa kina Yona, Mramba, Chenge, Lowasa, Rostam, Mgonja, Mkono, Kikwete nk na wao sasa wanaimba wimbo wa CDM kwamba mafisadi watoke ndani ya CCM.

Kwanza inabidi CCM wakiongozwa na mtuhumiwa mwenyekiti wao wamuombe radhi Dr. Slaa na CDM kwa ujumla kwa kitendo cha kukataa kuwa wao sio mafisadi kumbe kweli. Wawaombe watanzania msamaha na kukiri kuwa hawata rudia tena kukataa ukweli.

Wakati umefika wa wananchi kujua kuwa CCM ndio wanaomaliza uchumi wa Tanzania, na kuwashukuru Viongozi wa CDM kuwa mstari wa mbele kufanya kazi ya CAG na PCCB kubaini wizi, ufisadi, uonevu na siasa chafu za CCM na viongozi wake wezi.

Tuwape nguvu na matumaini wote wanaotutetea katika mazingira haya ya vitisho, na kukatishwa tamaa. Tanzania yenye neema ni pamoja na mimi na wewe kutimiza wajibu wetu kwa vitendo.

haya shime saidia harakati hizi kwa nguvu zako zote.
 
Heshima kwako na wana CDM pamoja na waTZ wanochukia mafisadi.
 
Mkuu Dr. Slaa anaeleza falsafa ya CDM kuwa inatokana na ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano. Jamaa anayeongoza kipindi anachanganya mambo lakini DR. anamrudisha mstarini. Slaa yuko na Arcado Ntagazwa.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Nipo mkuu fasta kwenye kiti..............nimeacha hata kula...JK nae mpeni taarifa...........
 
Mimacho yote mimi iko hapa jf maana sina tv mnitonye basi kinachoendelea si mnajua tv zetu za kibongo hakuna hata moja inayopatikana HD.
 
Jamani yaani jamaaa anaeleza sera ipasavyo. Aneleza jinsi kutokuwepo usawa kielimu unavyosababisha matabaka hapa nchini. Anasema ni wananchi wachache wenye uwezo wa kulipo tuition fees kwa ajili ya chuo kikuuu
 
Mkuu Dr. Slaa anaeleza falsafa ya CDM kuwa inatokana na ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano. Jamaa anayeongoza kipindi anachanganya mambo lakini DR. anamrudisha mstarini. Slaa yuko na Arcado Ntagazwa.

asante mkuu ngoja tumsikilize
 
tujuzeni wenye access na tv.......vp anaendelea kuwataja mafisadi still?:spy:
 
Anasema wachache wataimudu elimu, hasa wale ambao wazazi wao wana uwezo na ndio hao hao watakao shika nyadhifa za juuu.
 
Wakuu,
kwa wale wenye access fungulieni chanel ten Rais wetu yuko live anadadavuwa mambo mazito ya kisomi.
Msiulize source: kipindi ni je tutafika? cha makwaia wa kuhenga.
 
Ninamwona hapa. amefunika kipindi cha Mzee Makwaia. Slaa ni kiboko, anauelewa na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo.
 
Kuna mdau anauliza kuwa imekuwaje CH.10 ya RA imruhusu DR Slaa na Ntagazwa aeleze uzembe wa serikali hasa kusiamia wananchi pale wawekezaji wanapowanyanyasa wananchi waliowapa ardhi.
 
Naangalia hapa, he is so fine, to the point, soo visionary, anaiangalia na kuiongelea Tanzania yote namna hii yoote iko kichwani anaichambua kama daktari wa upasuaji anavyoufahamu mwili wa binaadamu, kweli huyu ni daktari wa falsafa, yaaani akiongea anatema thesis tu, something we Tanzanians are missing, this is the Caliber of leaders we long to have! He is sooo Charismatic!
Halafu hivi kumbe Arcado Ntagazwa yuko Chadema!?
 
Slaa kaeleza kuwa Chadema ni chama cha Mlengo wa Kati ( Sio wa kushoto wala Kulia). Ntagazwa anasema ccm wanamuogopa wasimchokoze akaja kusema yale ayajuayo maana alikula kiapo. Anasema wakimchokoza eti kwa vile aliihama ccm ataeleza yote. Anasema anashangaa aliokula nao viapo kuwa watailinda katiba wamekiuka viapo.
 
Kipindi kimiesha na wameahidi kuendelea kipindi kijacho na mada imedokezwa kuwa CDM itapambanaje na Wawekezaji wanyonyaji kama wale wa upande wa madini? Nitafuatilia next time na kuapa full info ila nisaidieni kujibu swali la mdau ambaye yeye kani PM eti " imekuwaje CH.10 ya RA imruhusu DR Slaa na Ntagazwa aeleze uzembe wa serikali hasa kusiamia wananchi pale wawekezaji wanapowanyanyasa wananchi waliowapa ardhi?"
 
Kipindi kimiesha na wameahidi kuendelea kipindi kijacho na mada imedokezwa kuwa CDM itapambanaje na Wawekezaji wanyonyaji kama wale wa upande wa madini? Nitafuatilia next time na kuapa full info ila nisaidieni kujibu swali la mdau ambaye yeye kani PM eti " imekuwaje CH.10 ya RA imruhusu DR Slaa na Ntagazwa aeleze uzembe wa serikali hasa kusiamia wananchi pale wawekezaji wanapowanyanyasa wananchi waliowapa ardhi?"

aliye ku pm ni RA
 
Back
Top Bottom