Mvuni
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 343
- 66
Mwambie kikwete aliye utangazia umma kuwa anamajina ya vigogo wote wanaofanya biashra hiyo haramu. Kushindwa kwake kuwataja yaelekea kunanamuna ya uhusika wake au jamaa zake katika biashra hiyo. Kama siyo kwanini hakuwataja au kuwadhibiti?Dr Slaa,
Ni wazi kuwa ulipotangaza list of shame pale Mwembeyanga mwaka 2007 kuliibuka kauli nyingi za kupinga kutoka serikalini na baadhi ya makundi ya jamii, lakini ukweli wa mambo ulibaki pale pale, na baadae tukaona mafisadi wa EPA wakiombwa warudishe pesa na kusamehewa (jambo la ajabu sana duniani kutokea).
Hili la vigogo wa biashara ya Madawa ya kulevya nalo linabidi liwekwe hadharani. Nina amini kabisa Dr Slaa una uwezo wa kupata majina ya hawa jamaa, hata Serikalini wanayo ila sijui kwanini hawataki kuwachukulia hatua hadi sasa. Kwa mawazo yangu naona ni busara yakawekwa hadharani ili walao kushtua mchakato wa kuanza kuwashughulikia, vinginevyo taifa litazidi kuangamia huku tukizidi kulindana. Kazi kubwa ya Chama cha upinzani ni kukosoa na swala la kutaja na kukemea maovu yanayofanyika nchini ni wajibu mmojawapo wa chama cha upinzani makini.
Nawakilisha