Dr Slaa, Tutangazie Majina ya Vigogo wa Madawa ya Kulevya!

beko

Senior Member
Apr 11, 2011
189
91
Dr Slaa,

Ni wazi kuwa ulipotangaza list of shame pale Mwembeyanga mwaka 2007 kuliibuka kauli nyingi za kupinga kutoka serikalini na baadhi ya makundi ya jamii, lakini ukweli wa mambo ulibaki pale pale, na baadae tukaona mafisadi wa EPA wakiombwa warudishe pesa na kusamehewa (jambo la ajabu sana duniani kutokea).

Hili la vigogo wa biashara ya Madawa ya kulevya nalo linabidi liwekwe hadharani. Nina amini kabisa Dr Slaa una uwezo wa kupata majina ya hawa jamaa, hata Serikalini wanayo ila sijui kwanini hawataki kuwachukulia hatua hadi sasa. Kwa mawazo yangu naona ni busara yakawekwa hadharani ili walao kushtua mchakato wa kuanza kuwashughulikia, vinginevyo taifa litazidi kuangamia huku tukizidi kulindana. Kazi kubwa ya Chama cha upinzani ni kukosoa na swala la kutaja na kukemea maovu yanayofanyika nchini ni wajibu mmojawapo wa chama cha upinzani makini.

Nawakilisha
 
we thubutu? Dr Slaa hana ubavu wa kumtaja hata mhusika mmoja wa biashara ya madawa ya kulevya. sanasana atafanikiwa kupata orodha ya mateja tu. watu wan madawa ya kulevya ni hatari sana na akitaka ajiharibie au apoteze maisha athubutu kucheza na watu hao. hawa jamaa ni kama dola nyingine ambayo kiongozi wake yupo Mexico na Msaidizi wake yupo Pakistan. serikali ya Mexico ilijaribu sana lakini ilishindwa
 
nadhani niwazo jema. naliunga mkono. ila kumbuka CDM nichama makini na hawakurupuki. yahtaji ushahdi na uhakika. nadhan tungeanza na JK aliyetangaza hadharani kuwa anawafahamu.

si aliwataja na miongoni mwao walikuwepo wachungaji wenu? unataka awataje mara ngapi?
 
we thubutu? Dr Slaa hana ubavu wa kumtaja hata mhusika mmoja wa biashara ya madawa ya kulevya. sanasana atafanikiwa kupata orodha ya mateja tu. watu wan madawa ya kulevya ni hatari sana na akitaka ajiharibie au apoteze maisha athubutu kucheza na watu hao. hawa jamaa ni kama dola nyingine ambayo kiongozi wake yupo Mexico na Msaidizi wake yupo Pakistan. serikali ya Mexico ilijaribu sana lakini ilishindwa

R.I.P Amina Chifupa.
 
nadhani niwazo jema. naliunga mkono. ila kumbuka CDM nichama makini na hawakurupuki. yahtaji ushahdi na uhakika. nadhan tungeanza na JK aliyetangaza hadharani kuwa anawafahamu.

Kumbe huwa mnaropoka wakati hamna ushahidi.
 
nilivyopiga na maisha hiyo biashara hata mimi ukinipa mchongo fresh niko tiayari kufanya tumbo langu conteiner.
maisha yangu magumu na umri unasonga kwa kasi
 
R.I.P Amina Chifupa.

Ameeen. Huyu ni miongoni mwa mfano wa watu waliojaribu kutamka tu kuwa wanayo orodha ya dealers wa madawa ya kulevya lakini kabla hajawataja, afa kifo ambacho inasadikika kuwa Mume wake Mpaka Njia alihusika kwa vile na yeye alikuwepo kwenye orodha hiyo
 
sasa wewe unatafuta kesi na uongozi tawala, angalia usijemwagwa lupango bure yakakakukuta yaliyowakuta wengine chezea madaraka wewe
 
ni wazo zuri mkuu! ila kama rais wetu tulie mwamini na tukampa dhamana ya kuongoza taifa letu list anayo na aja chukuwa hatuwa yoyote hapo kuna walakni ..sizan kama SLAA akiwataja kama watachukuliwa hatua....
 
Dk Slaa hana ulinzi wa kutosha kwa sasa hivi,ila akiwa rais wa Tanganyika mwaka 2015,hili liwe jukumu lake la kwanza
na kama atapewa wizara ya mambo ya ndani Mh Lema hili atalimudu bila tatizo,Kura kwa wingi kwa Chadema ndio italeta mabadiliko
 
we thubutu? Dr Slaa hana ubavu wa kumtaja hata mhusika mmoja wa biashara ya madawa ya kulevya. sanasana atafanikiwa kupata orodha ya mateja tu. watu wan madawa ya kulevya ni hatari sana na akitaka ajiharibie au apoteze maisha athubutu kucheza na watu hao. hawa jamaa ni kama dola nyingine ambayo kiongozi wake yupo Mexico na Msaidizi wake yupo Pakistan. serikali ya Mexico ilijaribu sana lakini ilishindwa

uoga ndiyo dhambi kubwa kuliko zote .
 
Nani awataje kila mtu anasema nina list nitawataja ....kimya:tape:......siku hizi wanang'oa kucha na meno wakati ule walikuwa wanakuchifupa
 
Mkuu , umesikika na bila shaka Dr Slaa atashughulikia ombi lako , usikatishwe tamaa na wachangiaji waoga au wenye maslahi kwenye hiyo biashara , Dr Slaa hajawahi kumuogopa mpuuzi yoyote .
 
Rais wako mwenyewe alisema kwa mbwembwe watu wapeleke list na ikapelekwa alipoisoma akagwaya!!! Anze yeye kama mkuu wa nchi kuitangaza!! Thubutu!!! Yaani mfupa uliomshinda Rais wako mnataka mumpatie our next presidaaa? Kama kweli huyu wenu ana ubavu atoke hadharani asome!!!!
 
Back
Top Bottom