utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,812
7000 per day
Soma hapa wee 200/= per post
Askofu ambomoa Dk.Slaa,amuonya na dhambi ya uzinzi!!!
Askofu wa kanisa la pentecost Church Of God Emmanuel Mwamakula.amelaani kitendo cha katibu mkuu wa CHADEMA bwana W.Slaa kwenda kufanya idaba ya hijja nchini israel na mwanamke hajafunga nae ndoa. Slaa aliondoka nchini feb 24 mwaka huu akiwa na mtu aliyemtambulisha kama mchumba wake na ambaye amekiri kuzaa nae mtoto,Josephene Mushumbusi kwa ndege no QR 545 kwa ajiri ya kwenda kutimiza ibada hiyo ambayo yeye anadai ni ya kuliombea taifa.
Akizungumza na gazeti hili Askofu Mwamakula alisema ameshangazwa na kitendo cha Slaa kuwa ujasiri wa kwenda kufanya idaba hiyo takatifu na mwanamke ambaye hajafunga nae ndoa(hawara). Hiki alichofanya Slaa kinapaswa kukemewa na kulaaniwa vikali,haiwezekani mtu akamchukua mwanamke ambaye hajafunga nae ndoa na kuambatana nae kwenda sehemu takatifu ambako ni mbele za mungu na kufanya ibada,huu ni 'uchafu' uliopitiliza,alisema askofu huyo.
Aliendelea kusema kwamba Slaa alipaswa kwanza kutubu kwa kitendo chake cha kupora mke wa mtu na kuzaa naye wakati anajua wazi kufanya ni kutenda zinaa,kwani kwenye maandiko matakatifu imewekwa wazi kwamba mwanamke au mwanaume anayemuacha mume au mke wake na kwenda kwa mwingine anazini.
Slaa amewahi kuwa padre wa kanisa katoliki anajua maandiko kwamba ndoa ya kikristo inapofungwa,kinachotenganisha ni kifo tuu!lakini kinachoshangaza yeye amepora mke wa mtu na kwenda nae sehemu takatifu bila aibu. Ninasema ni kwamba,Slaa alipaswa kwanza kutubu na kutumia nafasi hiyo kuomba mungu amuepushe na adhabu kali ikizingatia umri wake amesonga sana.
Lakini yeye anaona fahari kufanya matendo ambayo hayaendani na umri wake na kibaya zaidi ni matendo yanayokwenda kinyume na dini yetu.Alisema Askofu huyo kutoka Mbeya. Slaa amekwenda Mbeya kutembea tu,hana usafi wa kutosha kuliombea taifa wakati yeye ndiye alipaswa kuombewa kwanza kutokana na dhambi nzito ya uzinifu inayomkabili!
Hata hivyo,uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa,katika kuficha uhusiano wake huo na mchumba wake huyo(Josephine Mshumbusi) kwenye orodha ya wasafiri ambayo mwandishi wa habari hii ameiona,Slaa akiwa namba 70,mchumba wake huyo amejitambulisha kama mke wa Aminiel Mahimbo na sii mchumba wa Slaa.
Chanzo:Africa Leo toleo no 72.
Bubu Msemaovyo, Mahesabu, Timtim and 8 others like this.