Dr Slaa kutikisa Arusha Jumamosi

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbriad P. Slaa anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha siku ya Jumamosi tarehe 06.10.2012 kuanzia saa 8 mchana. Pamoja na mambo mengine Kiongozi huyo wa CDM pia atatumia mkutano huo kuzindua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya daraja mbili,uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vilivyopo mtaa wa NDARVOI.

Tayari kuna hekaheka kubwa katika jiji la Arusha kuhusiana na mkutano huo ambapo mazungumzo ya watu mbalimbali yanazungumzia mkutano huo unaotarajiwa kuwa gumzo.

Taarifa za awali zinasema mkutano huo pia utatumika kufuta nyayo za chama cha CUF ambacho kilisomba watu Dar-es-Salaam kwenda kuwahutubia Arusha ili kuepuka aibu ya kukosa watu.Pia inadaiwa wananchi wa Arusha wamedhamiria kuonyesha dunia uungaji mkono wao kwa chama cha CDM.
 
Asante kwa taarifa. Kamanda Crushwiser Do the needful plz!:poa
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha siku ya Jumamosi tarehe 06.10.2012 kuanzia saa 8 mchana.Pamoja na mambo mengine Kiongozi huyo wa CDM pia atatumia mkutano huo kuzindua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya daraja mbili.
Tayari kuna hekaheka kubwa katika jiji la Arusha kuhusiana na mkutano huo ambapo mazungumzo ya watu mbalimbali yanazungumzia mkutano huo unaotarajiwa kuwa gumzo.
Taarifa za awali zinasema mkutano huo pia utatumika kufuta nyayo za chama cha CUF ambacho kilisomba watu Dar-es-Salaam kwenda kuwahutubia Arusha ili kuepuka aibu ya kukosa watu.Pia inadaiwa wananchi wa Arusha wamedhamiria kuonyesha dunia uungaji mkono wao kwa chama cha CDM.

Mkusanyiko utakuwa uwanja upi kwenu ule tuliozoea wa NMC umeshageuzwa kuwa s o k o .
 
weraaaa weraaa....ngoja nikae mkao wa kutikisika.......
karibu sana kamanda.....tunakusubiri kwa hamu.....
wewe ndio Rais wetu tunaekutambua.......

hapo wamekufikisha wa kunyumba, but Molemo hajasema utafanyikia wapi exactly.
 
Huyu padri sijui ana matatizo gani?kuvunja ndoa za watu,kukiuka maadili ya kanisa wakati akiwa padri na wakina rose wake,ukifkia kufanya mapenz kwenye nyumba za ibada!!!!watu wa Arusha tumechoka vurugu zenu,hatuwataki jamani!!!!!!!!!!!!
Hayo ni mawazo yako sio ya watu wa Arusha. Haji Arusha kuendesha ibada, anakuja kwa mambo ya kisiasa. kwenye siasa kwa hayo uliyoyataja hapo hakuna msafi, hata wewe jichunguze vizuri.
 
Mkuu Ritz
Hivi watu wa Arusha hawana shughuli za kufanya za maendeleo? Haya maandamano na mikutano isiyokwisha taifa wanalijenga wakati gani?kweli tuliimaanisha Arusha iwe mji wa mikutano kwa kujenga AICC hatukumaanisha uwe mji wa mikutano hii ya kiwendawazimu isiyokwisha au ndio tuseme wana vichwa vigumu kuelewa?
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Umeambiwa anakuja kuzindua kampeni ya udiwani kata ya daraja mbili. Huo nao ni uendawaziwu!? You must be in toilet!
 
Umeambiwa anakuja kuzindua kampeni ya udiwani kata ya daraja mbili. Huo nao ni uendawaziwu!? You must be in toilet!
Tena uendawazimu mkubwa udiwani hata katibu wa wilaya angeiweza hiyo kazi
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ukweli husemwa:

Huko Arusha kuna nini?. Kila kukicha mikutano ya kisiasa. Mbona hata viongozi wa CDM wanaonekana kama hawana uhakika wa kisiasa na wananchi wa mkoa huu. Mimi nilifikili ni Ngome Kuu ya CDM au ndo yale ya Watanzania kuwa 'fickly' kisiasa.

Call it a political battlefield. Inaonekana kama vile Arusha hakieleweki.
 
Mkuu Ritz
Hivi watu wa Arusha hawana shughuli za kufanya za maendeleo? Haya maandamano na mikutano isiyokwisha taifa wanalijenga wakati gani?kweli tuliimaanisha Arusha iwe mji wa mikutano kwa kujenga AICC hatukumaanisha uwe mji wa mikutano hii ya kiwendawazimu isiyokwisha au ndio tuseme wana vichwa vigumu kuelewa?
Chama
Gongo la mboto DSM

Utasoma namba sana
 
Back
Top Bottom